Ukabila Ikulu, Ujenzi, Mambo ya nje, Mipango, TRA, BoT + Ofisi nyeti za serikali

Ukabila Ikulu, Ujenzi, Mambo ya nje, Mipango, TRA, BoT + Ofisi nyeti za serikali

PM

Naona sasa umeamua kwenda personal .............
 
Phillimon mikael.
hata ukinitukana kuniita kichwabata,dishwasher haniumizi kwani ukweli unauma na wewe unataka kuleta matusi ili mjadala ufungwe mnajulikana wana chadema.
sikusema Marian girls ni shule ya mchagga sehemu yeyote ile naomba nioneshe? nilichosema kuwa kila intake hawachukuwi zaidi ya wanafunzi watano hiyo ni sera ya shule yao na si wao shule nyingi tu za kikristu mmojawapo ni ST.anthony WAMEKWEKA wazi jambo hilo.

anayemiliki shule ya marian girls ni mtu wa sumbawanga kama humjui ni kardinar pengo hakuna nimemtaja mchagga.

naona unatoka kwenye hoja yenu ( na mwanakijiji) mliosema kilimanjaro kuna shule nyingi hivyo makarani wa TRA kuwa wachagga ni poa tu. nikawajibu kuwa na shule sehemu haina maana watu wa eneo husika wameelimika zaidi. jee hivi Tabora boys na girls au mirambo ingekuwa moshi mngesemaje? mngesema hata Nyerere, mkapa, walisoma TABORA hivyo watu wa huko wameendelea sana,

wewe umejichanganya kwa kusema kuwa marian girls watu wanaingia kwa kufaulu interview hivyo anayefaulu ndiye anapata nafasi. sasa jeee huko kilimanjaro mtu anaingia shule bila kufaulu interview? au kuna kigezo kingine kinatumika?au ukabila ndio interview tayari?
naamini shule kama weruweru. machame girls. kibosho ni bweni na wanasoma watu toka sehemu zote na utaratibu ni kufaulu na kama private school nako kuna interview au PM unataka kusema kwenye interview wachagga wanafaulu sana kwa vile kwao kuna shule nyingi?

jibu lolote unaonekana umejikanyaga. sisi waswahili tunasema ukubwa wa pua si wingi wa makamasi.

naona utanata kupeleka mjadala pabaya sintakujibu tena wewe kama Phillimon maana umeanza kuleta jazba na sisi waungwana karaha si nyumbani kwetu. umekuwa makengeza kama alivyokuwa mwenyekiti mstaafu wa chadema mzee Mtei, na mwenyekiti wa sasa wa Chadema. inaoneka huko chadema kuna ugonjwa wa makengeza.
 
kitabu cha list yenye staff wa TRA mbona hujaweka? hivi wewe PM na MMANDA nani yuko TRA? MMANDA amekiri kwa kusema "wachagga wapo tena sehemu nyeti za TRA" NA press release imewekwa humu. kunipinga mimi bila kumpinga MMANDA naona hunitendeki haki, NA ni kichekesho kumpinga msema wa TRA bwana MMANDA ambaye hakuja na hicho kitabu chenye list ya staff wa TRA. alikiri kuwa wapo wachagga kwa sababu za kihistoria na wataendelea kuwepo kwa sababu hizo hizo, kama kuna la kushangaa au kuhoji twende jeshini kwanza.
 
Phillimon mikael.
... nilichosema kuwa kila intake hawachukuwi zaidi ya wanafunzi watano hiyo ni sera ya shule yao na si wao shule nyingi tu za kikristu mmojawapo ni ST.anthony WAMEKWEKA wazi jambo hilo.

Unaweza ukawa na hoja kuhusu TRA, japo kama alivyokwambia Mwanakijiji si ukabila bali ni Undugunization. Lakini maneno yako hapo juu ni UONGO uliopindukia uso hata na chembe yeyote ya ukweli wowote.
 
Dua wrote:
Mbunge aliyelalamika upendeleo wa barabara bungeni ni mbunge wa nzega alikuwa ana mlalamikia mr. fupi(mramba) kwa kupendelea kwao. mfano halisi alitenga bilion 17 kwa barabara ya jimboni kwake huku barabara ya kusini dar- lindi imetengewa bilion 1 tena ni barabara muhimu. hao ndio wachagga au mikael barabara hii kwa vile ni ya waswahili? hivyo haijaenda shule?

Dua,
tungeweza kupata muhtasari na viambatanisho vya hotuba ya wizara ya miundombinu tungeweza kulijadili suala hili kwa kina. nimeisoma hotuba kama ilivyowasilishwa na mramba na inaonyesha kwamba barabara ya nzega iko ktk stage ya usanifu. barabara ya tarakea iko katika hatua ya ujenzi. kwa msingi huo inaleta mantiki kuwepo kwa tofauti ya viwango vya fedha zilizotengwa.

tatizo langu ni hii TONE iliyopo hapa ambapo makabila ya mkoa wa kilimanjaro yanazongwa kwa tuhuma zisizokuwa na msingi.

katika malalamiko ya mbunge kwanini hakuilinganisha barabara ya nzega na barabara nyingine zilizopewa fedha zaidi kama za kusini, au hata magharibi ya tanzania? nimeonyesha kwamba ziko barabara zilizopewa fedha zaidi ya barabara ya tarakea. barabara ya tarakea ilianza kujengwa wakati waziri akiwa ni magufuli. why single out wachaga, au mramba?
 
Wanabodi,
Sasa naona kweli hapa kuna hasira kwa sababu ya rangi za watu. ndgu Phillemon kwa maelezo yako hapo awali inaonyesha wazi wewe Mkabila!...
mswahili acha majungu...hata mzee mwinyi alihimiza waswahili msomi na muache tabia ya kukaa tu kupiga jungu kutwa,.kisa una kiunga chako cha minazi..wewe kalia kupiga jungu huku watu wanapiga kitabu..uzuri wa elimu hata mkibana ajira hapa watu wanaajiriwa proffesssionally botswana,marekani,uk,namibia ets uliza kuna maprofessa wangapi huko..na si waosha vyombo na wapiga soga kama wewe..kwanza inaonekana siku hizi kazi yako ya DISHWASHING umepumzika nini?
Hii ni dharau ambayo Mzee Mwanakijiji amekuwa akiizungumzia huko nyuma kama Ukabila na leo wewe umethibitisha hivyo!
Ndugu yangu hoja hujibiwa kwa hoja!
 
jokaKuu

Hii topic inahusu ukabila ambapo wengine wanasema hili ni neno kali sana bora tuite undugunisation. Sasa hilo sio la kwetu sisi bali ni la Baraza la kiswahili kama wanaweza kutuwekea neno lingine; lakini halipo na kama Mswahili alivyosema huko TRA MManda amekiri hivyo sasa mnataka sisi ambao hatuko jikoni tusikubaliane naye? Mmanda I believe ni mchaga na ndie msemaji rasmi wa TRA amekubali kweli ukabila upo pale.
 
Mkandara,
mbona unakemea upande mmoja tu? haya matusi na kejeli za kikabila hazikuanzishwa na Philemon. Philemon anamjibu mswahili in the same tone that he used. ungetenda haki kuwakemea wote wawili--mswahili kwa kuanzisha kashfa, na philemon kumrudishia kashfa.
 
Tabasamu.
usiinite muongo fuatilia kwanza kabla ya kukurupuka na kujibu kishabiki. nimweka post yangu dakika tano zilizopita jee umecheki na wenye shule kuthibitisha uongo wangu? au wewe ni muhusika katika hizo shule nilizotaja? naomba uliza kwanza halafu ndio uje kuniita muongo. tena ungesema neno labda hii si kawaida lakini kuniita muongo huku huja counter check na upande wa pili sio fair.
Mkandara.
mwache tu atukane MR.Phillimon hao wamesoma sana kwa sababu za kihistoria. waungwana hatugombani na mtu hapa ni darasani tunatoa elimu tu, sasa naona haja ya mimi kuingia kwenye mada ya radar na ndege ya rais, kwani kunyamaza tunaonekana wajinga.
 
Joka kuu.
naomba nioneshe sehemu nimemwita kichwabata? au dish washer? nimekuwa nikisisitiza kutokana na sababu za kihistoria nyinyi(wachagga) mmepiga hatua kubwa lakini jee hata ukarani makabila mengine kama sie waswahili hatuwezi kuifanya kazi hiyo? sijamtukana sehemu yeyote ile namheshimu kwa wadhifa aliona nao kwenye jamii. lakini ameshindwa kutunza heshima yake. muda mwingi nilikuwa na mwanakjj kama matusi angelalamika mwanakjj.
 
jokaKuu

Aliyeanzisha hii mada ni Samvulachole na wanabodi tulikubali kuwa hamna ukabila lakini baada ya kuwekewa data hapa na kuzifuatilia tumeona kwamba tulifanya makosa, ukabila upo tena sana tu.
 
Joka kuu.

jamaa yako anasema naleta majungu jee haya ninayoyasema hayapo? ningekuwa nazua mathalani kusema rais ni mchagga huku si mchaga hayo majungu. ninachozungumza kipo na majina ya wahusika nimeweka na wenye TRA yao wamekiri bado naambiwa majungu. yeye hana source yeyote anaonekana mkweli.

issue ya ghorofa za posta ilala amana kila mtu anaijua jee ni majungu? kama mimi naleta majungu humu basi hiki kijiwe cha JF hakina maana kuwepo wakijadili baadhi ya watu tunasema kunakata data/issue lakini tukija akina mswahili tunaambiwa majungu na wavivu tena vichwabata. jamani haki hii?
 
Mswahili umenena mwanangu. Kinachogomba hapa ni woga wa neno ukabila. Kuna maneno watanzania tumekuwa socialised kutoyatumia yakiwemo Tanganyika, udini, ukabila, n.k. Hiyo ni vocabulary-phobia. Sasa kuyaogopa hayaondoi ukweli. Nyoka ni nyoka tu hata kama utamkimbia!
 
Jokakuu,
Unaweza kunionyesha matusi ya Mswahili yaliyotangulia?...
Jokakuu, ikiwa mtu mweusi leo atasema mabaya yote ya mzungu yataonekana kama matusi (kwa huyo mzungu ama wazungu wenzake) kwa sababu za kibinafsi ama rangi!..
Na kuna tofauti kubwa kama mzungu atarudisha kwa kutumia F....word na kuanza kuelezea kwa nini mtu mweusi yuko nyuma nje ya yale mweusi anayomtendea mzungu akiwa na maana tu kuwa yeye sio sababu ya mtu mweusi kuwa nyuma ama kubaguliwa. Pia yale yote anayoyafanya ni halali hayana Ubaya.Haya mabaya katendewa Mswahili na ndicho anachozungumzia..
 
mswahili,
nikuomba uwe mwangalifu na kauli na madai yako. siyo HAKI kuchanganya wachaga wote ktk hilo "kundi" la mama mkapa. wako waliopata kukuelimisha kwamba wachagga katika undani wao ni watu tofauti sana. hata katika lugha[warombo,wamachame,marangu,kibosho] hawaelewani 100%, wengine hawaoleani kabisa.

hisia unayoileta hapa ni kana kwamba kila mchaga ni tajiri mwenye uwezo, na amejaa dhuluma. tanzania ni nchi masikini, na umasikini huo haujachagua wala kubagua kabila pale tanzania.

naamini wewe umeishi dar na umeshuhudia jinsi vijana masikini wa kichaga wanavyohangaika kuchoma nyama, na kupiga viatu rangi. baadaye wanakusanya mitaji na kuanzisha viosk etc etc.

hali ya kuja mjini kutafuta maisha haipo kwa wachagaa tu. wapemba,wakinga,wahaya,wasambaa,wahaya,....wote hao wamekimbilia mjini kutafuta maisha kutokana na mabadiliko yaliyotokea vijijini kwao.

Ninachojaribu kueleza hapa ni kwamba wapo wachaga waadilifu wachapa kazi.
 
jokakuu

Ukifuatilia hii mada kutoka mwanzo ilifikia Mkandara kutoa mfano wa tenga la samaki ambalo lina baadhi ya samaki waliooza, na kupendekeza tuwatoe hao waliooza wakati MKJJ alisema samaki wote ni wazuri. Mswahili na wengineo tunakubali kwamba ukabila upo na sio wachaga wote wanaofanya hivyo. Je ni jinsi gani tutaondoa hili donda ndugu la wale waliooza?
 
Mkandara,
1.Tatizo langu lipo katika "TONE" ya jinsi haya madai yanavyowakilishwa hapa jamboforums. Labda wewe Mkandara unaifurahia au huioni, lakini wengine tunaiona.

2.Kuna hali ya kuwa-single out wachaga peke yao na siyo makabila mengine. kwanini kinachojadiliwa hapa ni TRA tu, na siyo taasisi nyingine? vipi kuhusu sekta binafsi je?

3.Kumekuwa na ongezeko la thread na postings zinazoashiria CHUKI dhidi ya wachaga na wanyeji wa kilimanjaro ktk ujumla wao. kuna "kitu" kinaendelea hapa, na mimi kinanitisha kidogo.
 
Mkandara,


2.Kuna hali ya kuwa-single out wachaga peke yao na siyo makabila mengine. kwanini kinachojadiliwa hapa ni TRA tu, na siyo taasisi nyingine? vipi kuhusu sekta binafsi je?
.
TRA inajadiliwa sana kwasababu ndiyo chanzo kikuu cha pato la TAIFA kwa sasa.Ndio injini ya Taifa.
 
Jokakuu

TRA Mmanda amekubali kwamba kuna ukabila (hili lilitoka kwenye vyombo vya habari Tanzania). Je hilo ni kosa? Pitia kurasa zote 30 uone jinsi watu wanavyojadili huu mjadala, hii Tone ya ku-personalise ndio hatukubaliani nayo. HOJA HUJIBIWA KWA HOJA. Kama ukifuatilia utaona Wahaya na Wanyakyusa wamejadiliwa hapa na MKJJ ameleta takwimu hata za idadi ya makabila mengi Tanzania. tunataka kuukata huu mzizi wa fitina wa Ukabila kwenye serikali.
 
Back
Top Bottom