Ukabila Ikulu, Ujenzi, Mambo ya nje, Mipango, TRA, BoT + Ofisi nyeti za serikali

PM/Jokakuu

Msiwe wavivu wa kusoma hii issue kutoka mwanzo, Ukabila upo na kutokana na list aliyokuwa ametoa mwanzo Mswahili hilo halina ubishi, sasa kama kuna sehemu nyingine nazo kuna ukabila inabidi kuona data na kukubali au kukataa kwamba hapa au kule hakuna ukabila. Mswahili kitu alichosema ni kwamba hawezi kumwaga data mpya wakati nyinyi mnabisha kwamba hakuna ukabila bali ni chuki yake kwa wachaga kitu ambacho mimi sioni kama ni kweli, mpaka pale nitakapopata ushahidi huo.

Ndio sababu Mwanakijiji alisema bora tuite jina lingine, lakini hakuna uhalali huo wakati Mmanda wa TRA amekiri hivyo. PM data ulizoleta unasema hakuna ukabila, lakini ni lazima ufahamu kwamba hii issue ilianza mwaka jana Julai, Je ni muda gani huwa unatolewa kwa mtu kubadili jina Tanzania? huu ni mfano sina maana watu wamebadili majina, na Je kwa majina tu unaweza kusema huyu mtu ni kabila gani?

Hili tatizo haliwezi kuondoka lenyewe kwa sababu TRA ndio uti wa mgongo na sidhani kuna mtu ambaye hataki kufanya kazi kule kwenye mlo wa nje nje. Midhali mnakubali ukabila upo basi tutafute solution. Hii siyo chuki, hata Europe wanapotoa kazi huwa wanauliza maswali na kujali minorities (equal opportunities). Nategemea kuona michango yenu jinsi ya kuondoa hii cancer ya ukabila ambayo imejitokeza.
 
sikupenda kumjibu Mikael phillimon kutokana na lugha yake matusi na nilimuambia sintomjibu na nimemsamehe. kwa vile mada hii imewekewa vikao hivi sasa na watu wana kwenda mbio na huku nazidi kupata matusi kwenye private message yangu. hiyo hainitishi kwani naweka ukweli na kunawa mikono yangu historia itanikumbuka. hapa kuna wachagga kawaacha na vitengo alivyoteua viwili na ameweka hadi wafagiaji na madereva. muda wote nimekuwa nikimtaja mdogo wake Lauwo kapewa chakula pasipokuwa na sifa ya hiyo kazi. yeye analeta uongo na kusema ni majina tu yanafanana hapo tu sina haja ya kubishana na mtu anayeishi kwa mtaji wa ukabila, najua issue hii kwenu ni biashara mmeshampa habari kITTLYA kuwa kuna vita. hakuna vita ni maslahi ya nchi.
unatuletea dereva huyu anahusika nini na ukadiriaji wa kodi? mbona hujataja Holili YUKO nani? tunduma yuko nani na ni nani anafanya tathmini ya kodi?nani yuko container terminal? nani yuko TRA majahazi? nani anapita viwandani kukadilia kodi? acha uongo.
narudia tena PM muongo umewaruka wachagga wengi tu. wako wapi akina maleko? yuko wapi steven? yuko wapi Lyimo?
naomba kama unataka usilete matusi au ule mkasa wa kumchomea moto nyumba benny lusege, naomba usemi unataka mjadala wa nidhamu kama ni matusi yako hapa hakuna room ya matusi nenda huko chadema kwako au club bilicanas.
 
Mkandara,
PM has challenged each one of you kuomba majina ya watumishi kitengo chochote kile ndani ya TRA. Vilevile ameleta majina ya watumishi wa vile vitengo ambavyo mswahili alidai "kundi la kilimanjaro" limeviteka nyara.

Dua,
Mswahili hakutoa listi, bali majina machache hayazidi 10, na vitengo viwili/vitatu, halafu akadai TRA nzima inanuka ukabila. PM ameleta majina ya watumishi wa vitendo alivyotuhumu mswahili kwamba vimejaa wachaga na wakilimanjaro. Listi ya PM inadisprove madai ya Mswahili.

Msemaji wa TRA hajakiri kwamba kuna ukabila, ambao kwa definition yako,mswahili, na mkandara, ni hujuma ya waziwazi ya wachaga kuhodhi nafasi zote za kazi TRA. Msemaji wa TRA amekiri kwamba ni nafasi za juu tu, na specialised, ndizo zimejaa wachaga. vilevile ameeleza hilo halitokani na hujuma bali historia ya wachaga kuwa wa mwanzo-mwanzo katika kupata elimu.

Umekuja na madai mapya kwamba kuna waliobadili majina. nakuomba basi urudi kwenye hiyo listi ya PM utueleze majina unayoyatilia shaka halafu tuangalie tena kama ukabila bado upo.
 
Tabasamu
View Public Profile
Send a private message to Tabasamu
Find all posts by Tabasamu
Add Tabasamu to Your Buddy List

#9 15th February 2007, 10:32 PM
phillemon mikael
Senior Member Join Date: Sun Nov 2006
Posts: 363
Rep Power: 21




--------------------------------------------------------------------------------

tabasamu mada nzuri hiyoo ...hembu ifanyie utafiti...maana naona kati ya manahodha waanzilishi ,waliobakia wachache wengi wamejitosa baharini na huenda wameliwa na papa au nyangumi,manahodha waliobaki njaa inawasakama...kuwa mpinzani tanzania inabidi ukubali kuwa masikini..sijui mbowe anamudu vipi

WIMBO.

"..MV MAPENZI meli ya wapendanao.,
;;;'...kuchafuka kwa bahari sio mwisho wa safari nasema..
meli ilipokumbwa na dhoruba,manahodha wamejitosa baharini.."
 
page 33 bwana PM anasema yeye sio mchagaa wala chadema lakini hapo juu nimekopi maneno yake kujipigia chapuo. hapa mtajua maneno yake anayosema si ukweli uliopo. he is not a credible witness. I therefore exluding his statement as a part of evidence in subject before me.
 
jokaKuu

Usiende haraka mzee. Hebu soma ulichoandika halafu ulinganishe na nilichoandika. i.e.
Je ni muda gani huwa unatolewa kwa mtu kubadili jina Tanzania? huu ni mfano sina maana watu wamebadili majina
Na ya kwako ni hii
Umekuja na madai mapya kwamba kuna waliobadili majina.

Haya ya kwako ni madai lakini yangu si madai.

Unaposema msemaji wa TRA amekiri kwamba ni nafasi za juu una maana gani? Kwani huo si ukabila. Tunajadili ukabila uwe ngazi ya chini au juu hilo halina sababu ni ukabila tu. Sasa kama upo tuushughulikie.
 
phillemon mikael
Senior Member Join Date: Sun Nov 2006
Posts: 363
Rep Power: 21


mmefuta thread ya marealle ,:ni wakuja eeh!!!

--------------------------------------------------------------------------------

Quote:
Originally Posted by phillemon mikael
mbona ile thread MSIBA WA MANGI MAREALLE imefutwa? ilikuwa na ubaya gani...peple would like to know whts going on since all leaders would be there for the burial which starts today and end tommorow,and ccm in moshi is doing all what it can to make the burial a ccm affair ,i think so as to seal the mass support it is about to enjoy in kilimanjaro region...
sasa tunapoongelea UKABILA au CHUKI si ndio kama hivi,sasa ukiondoa thread ya yule mzee anayeendaa kupumzika kwa amani MANGI MAREALLE OBE tukueleweje? INA MAANA humu ndani mtu akiwa mchagga au wakuja ni kosa..thats whaat it sound like ...hata hivyo if you have decide to delete it its okay,you dont need to restore it..but we now undestand that some people here inside who we discuss there issues ,we may have be biased with there origin..yes stiff debate to WAKUJA or WAMLIMA,but for wa mjini are UNTOUCHABLELES..

Please lets look on issues in national and internatinal perspective way ,and not biased to our homestead boerders!!!! call spade a spade !!!!!@>//;.


phillemon mikael
View Public Profile
Send a private message to phillemon mikael
Find all posts by phillemon mikael
Add phillemon mikael to Your Buddy List

#24 23rd February 2007, 03:17 PM
Invisible
JF Admin Join Date: Sat Sep 2004
Location: Home
Posts: 3,455
Rep Power: 100000





--------------------------------------------------------------------------------

Sasa Phelemon ndo umefanya nini hivi? Hiyo ni Flooding ndugu.

Halafu kama hujaangalia vema usilaumu tu kuwa thread flani imefutwa. Nadhani hujaangalia vema au ku-search for it walau uone iko wapi.

Aidha sidhani kama suala la ukabila lina nafasi katika maamuzi ya thread ipi ifutwe ama ipi ikae.

Nadhani ukiiona thread yenyewe utajua umehukumu visivyo. Nitaandika kwenye thread husika ujue ipo ila haijachangiwa. Sijapenda reaction yako as long as najua hujajishughulisha kuitafta thread husika.

Anyway, you're welcome
__________________
Ficha upumbavu wako usiifiche hekima yako! - Yosh Bin Sira 20:31


Invisible
View Public Profile
Send a private message to Invisible
Send email to Invisible
Visit Invisible's homepage!
Find all posts by Invisible
Add Invisible to Your Buddy List

#25 23rd February 2007, 04:10 PM
Ogah
Senior Member & Expert Join Date: Fri Mar 2006
Posts: 362
Rep Power: 21




--------------------------------------------------------------------------------

pm

duuuhh sasa nawewe unaleta mpya hapa, hii sijawahikuona, yaani thread kufutwa kwa kufuata ukabila!!!!!!!!!!!!!!, NEVER ON JF or not to my experience either

punguza jazba ndugu, thats absolute-overreaction
 
phillemon mikael
Senior Member Join Date: Sun Nov 2006
Posts: 363
Rep Power: 21


TANZIA:Chief Thomas Lenana Mlang'a Marealle II, OBE Mangi wa wachagga AFARIKI

--------------------------------------------------------------------------------

MANGI mkuu wa kabila la wachagga 92 ,chief thomas marealle ,amefariki dunia katika hosipitali ya KCMC...pamoja na kuwa mangi marehemu aliwahi kufanya kazi umoja wa mataifa sehemu mbali mbali duniani..pia wakati wa vugu vugu la uhuru alikuwa mmoja wa wanaharakati na hata alipata kuhutubia mkutano wa umoja wa mataifa akitokea tanganyika..mara baada ya uhuru alikosana na nyerere ,kwani baada ya nyerere kufuta uchifu aliwapa mashifu wote waliokuwa na elimu kazi mf fundikira,sapi mkwawa ,kunambi ets isipokuwa chief marealle aliwekwa kando ,kwa bahati akaitwa UN kufanya kazi za un reprentative...nchi kama iran,italia,liberia,gambia ets hadi mwaka 1978 alipostaafu..wakati wa vuguvugu la upinzani aliunga mkono CHADEMA na NCCR MAGEUZI mwaka 1995..lakini baadaye alirudi kuunga mkono ccm mwaka 2005..marehemu ameacha watoto teddy.themi.,na aggrey marealle.

MUNGU AILAZE PEMA ROHO YAKE PEPONI ,AMEEN..BWANA AMETOA BWANA AMETWAA NA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE!!!!
 
Mwenye macho haambiwi ona. hapa juu nimiweka mada za Phillimon Mikael ambaye anadai si mchagga na ni mwanachama wa Tanu. phillimon alimshambulia hata administrator wa JF kwa minajili ya kikabila vipi mimi mswahili?

huyu ndiye phillimon mikael ambaye hataki wachagga warekebishwe hata kama wamekosea. na sasa amekuja hata na data za uongo kutetea kabila lake TRA.
 
phillemon mikael
Senior Member Join Date: Sun Nov 2006
Posts: 363
Rep Power: 21




--------------------------------------------------------------------------------

mama no body is in favor of chiefdom ,which were long abolished however this doesnt mean watu wasifuatilie historia na roots zao...so kwa wale watu wa kilimanjaro especially wachagga marealle ni part ya historia yao..

na afterall alifanya mengi katika ELIMU wakati bado akiwa mtawala ndio maana moshi kuna shule za DINI naa pia kuna shule za USHIRIKA ie LYAMUNGO zilizojengwa wakati wa utawala wake chini ya ofisi yake,ZAIDI ya hayo aliimarisha vyama vya ushirika na masoko ya zao la kahawa na afya..wazee wengi waliosoma kabla ya uhuru walifaidika na kulipiwa na council hadi makerere..council ya moshi ilijenga barabara ,mifereji ets hata kabla ya uhuru...

kwa hiyo wanaomkumbuka au kumuheshimu wana haki ya kufanya hivyo...ni kama reflections tu.


phillemon mikael
View Public Profile
Send a private message to phillemon mikael
Find all posts by phillemon mikael
Add phillemon mikael to Your Buddy List

#29 25th February 2007, 12:48 PM
phillemon mikael
Senior Member Join Date: Sun Nov 2006
Posts: 363
Rep Power: 21




--------------------------------------------------------------------------------



Waombolezaji wakiteremsha mwili wa Mangi Mkuu, Thomas Marealle katika mazishi yaliyofanyika nyumbani kwa marehemu, Mengeni Marangu, Kilimanjaro jana. Serikali iliwakilishwa na Waziri Mkuu, Edward Lowassa. (Picha na Hilary Bujiku wa Ofisi ya Waziri Mkuu)

PATA ZAIDI PICHA ZA MAZISHO YA MANGI MKUU THOMAS MAREALLE OBE ...BOFYA HAPO CHINI.

www.jakayakikwete.com/kikwete/displayimage.php?pos=-1776
 
Huyu ni PHILLIMON MIKAEL.

kutokana na msiba wa marealle alianzisha Thread maalum Tanzia ya Marealle lakini hatujawahi kuona akituambia kinjeketile, mkwawa, kibasila alikufa lini na yapi walifanya.

wanabodi msipoteze muda tena msiomjua sasa mmemjua bwana Phillimon MIkael NITAENDELEA kumuhifadhi sitamtaja humu hata anitukane vipi kutokana na heshima yake kwenye jamii.

sasa anadanganya watu ana orodha 1000 ya wana TRA? kwani TRA INA wafanya kazi 1000? tupe orodha ya wana chadema si TRA.
kumkoma nyani gladi kajisemea mzee ES! ZILONGWA MBALI ZITENDWA MBALI.kumekucha ukabila TRA wenye macho oneni.
 
Nilichukuamuda kidogo kupumzika maana kichwa kinauma. Ila baada ya kurudi kurasa zimejazana.. ikabidi nianzie nilipoachia.

Kwanza, hakuna anayekubali kuwa TRA kuna Ukabila period. Siyo mimi wala si Mmanda. Tunaambie mbona Mmanda kakubali really? Hebu tuone. (angalia ukurasa wa sita)

Mmanda atetea wingi wa Wachagga TRA

Written by Charles Mullinda
Friday , 21 July 2006

*Asema walipata elimu mapema

HATIMAYE Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imetoa tamko dhidi ya madai ya kuwapo ukabila katika mamlaka hiyo.....

"Hakuna suala la ukabila TRA, haya mambo yanazushwa tu na watu kwa sababu mbalimbali, zikiwamo za chuki binafsi na wengine ni hulka yao kuzua mambo." Mmanda amesema "HAKUNA" sasa sijui ndugu zangu walisoma wapi maneno ya "LIPO"

akaendelea...
"Kweli TRA ina watumishi wengi katika nafasi nyeti ambao ni Wachaga, lakini hili ni suala la historia, huwezi kulikwepa, kumbuka Wachanga ni kabila ambalo watu wake walipata elimu ya juu mapema kabla ya watu wa makabila mengine." - Amesema kitu ambacho wengi tunakisema hapa!

akaendelea....

"Na hapa sio TRA tu, angalia madaktari wengi hasa wa zamani kidogo ambao sasa ni mabingwa, wengi ni Wachaga, na kwa Tanzania nafasi za kazi hazitolewi kwa ukabila bali sifa za muhusika na uwezo alionao katika kuifanya kazi hiyo," - Tumelionesha hilo kwenye nafasi za mabingwa Chuo Kikuu Muhimbili na sehemu nyinyine.


akaendelea...

"Sisemi haya kwa sababu mimi ni Mchaga, hapana, bali hata wewe fuatilia ukweli, tunao Wachaga TRA, lakini wote ‘wanafiti’ katika nafasi zao, na hawa ni wale waliosoma zamani, leo vijana wa Kichaga wameishia biashara ya kuuza ndizi, wasomi ni wachache na makabila mengine ambayo yanazingatia elimu sasa yanaibuka," - Hili hakuna mtu (mtetezi wa ukabila) amelisema hapa. Mmanda amekiri Wachagga wengi hasa vijana wa sasa hawachangamkii sana elimu. Sisi tumewaambia wapo wachuuzi, wachoma mishkaki n.k Hakuna anayetaka kuangalia ukweli. Tunaambiwa angalieni "ukabila" TRA!

gazeti la TD likasema,

"Alisema iwapo wingi wa watu wa kabila moja ndani ya taasisi yoyote nchini utachukuliwa kama kukithiri kwa ukabila katika taasisi hiyo, ya kwanza kutuhumiwa kuhusu hilo ni jeshi ambalo lina watu wengi wa Musoma."

Pointi hii nimeiimba hadi nimepatwa na mafua!... wingi siyo ukabila!!

Je tunataka kutafuta suluhisho la tatizo?

Kama hilo ndilo lengo ni lazima tutambue tatizo la kweli na siyo la kusingizia. Hakuna mahali ambapo nimesema Ukabila = Undugunization. Nimeeleza maana ya Ukabila na maana ya undugunization. Ukabila ni hisia ya mtu kutukuza kabila lake na kuliona bora na lenye kustahili zaidi kuliko kabila jingine. Mtu mwenye ukabila atajaribu kwa nguvu zake zote kuyatenga makabila mengine, kuyakandamiza na kama angekuwa na uwezo kuyahamisha au kuyamaliza. Hisia hizi za ukabila zimeonekana Rwanda, Burundi, Kenya, Uganda, Nigeria n.k! Watanzania pamoja na matatizo yetu yote hatujafikia huko!!! Ni kweli mtu mmoja mmoja anaweza kuwa na hisia za kikabila kama tulivyoshuhudia hapa. Kwa vile Mswahili anachomoza na hisia za kikabila (akitukuza watu wa pwani na kudharau watu wa bara) siwezi kusema basi watu wote wa pwani ni wa kabila.

Tatizo jingine ni kuwa tukipingana kwa hoja na Mswahili tunaambiwa ni kwa vile sisi tumefaidika na "ukabila" huo. Nimemwomba anitajie amesema atanitumia kwenye PM.. nimesubiri weeeeee! Tukianza kupinga hoja tunageuzwa hoja (we become the subject).

Badala ya kung'ang'ania TRA na tunaendelea kukusanya ushahidi kuonesha kuwa Wachagga hawako wengi TRA peke yake, wapo wengi Muhimbili, Wahaya wako wengi UDSM, nk.. Kwanini TRA tunaambiwa ati ndio wakusanyaji wakubwa wa hela, wachagga=wapenda pesa!! Mbona sio leo utani dhidi ya wachagga na pesa umekuwepo!! Lakini twende BOT kuna Wachagga wangapi maana wao ndio watengeneza pesa. Pamoja na kuambiwa kuwa Wachagga wengi wapo TRA, hakuna hata mmoja ambaye amesema kuwa wachagga hawa wamekula njama kuliibia Taifa!!! Tunaambiwa kuwa ni hatari kwa usalama wa Taifa!!Kana kwamba ili kuiba ni lazima muwe watu wa kabila moja!! Mswahili, Dua, na wengine naomba mtuambie "Je Wachagga walioko TRA (watendaji) wamekuwa wakiliibia Taifa?" Kabla hamjajibu someni habari hii muone jinsi gani TRA imejitahidi kukabiliana na corruption ndani yake:






Of course, wanaotetea uwepo wa Ukabila watasema "look who is talking Luoga"! Nimeambatanisha hapa ripoti toka Transparency International:

Ndugu zangu, wote tunajua (I hope so) kuwa tatizo katika ajira Tanzania kufahamiana/kujuana na matumizi mabaya ya vyeti vya kitaaluma. Tukikubali matatizo haya kwa jamii nzima siyo TRA peke yake basi tushirikiane kupendekeza utatuzi. Ila kutung'ang'aniza tuone ukabila mahali ambapo haupo ni kama kumpigia mbuzi gitaa, hachezi!
 

Attachments

mswahili sasa unachotaka kufanya ni kututoa nje ya mada...mada ya marealle ni tukio kama mengine..mbona hujasema mimi muhaya kwa kumtetea mh magufuli,na nnimeanzisha mada zake mbili tatu[sio za majungu]...mimi nationalist mzee...

turudi kuleee ambako umeshashindwa kwa hoja na huna jipya zaidi ya kuamua tu KUBISHA....

umegusia holiili,tunduma,hororhoro ,sirari,.na nakupa kama ifuatavyo,,.....
angalia SIRARI,
examination and custom OFFICERS
1.A.SHEMNDOLWA
2.V.ASSENGA
3.NK LAWRENCE
4.MUSHOMI G.
5.ABDALAH .K
6.KAPESSA F.
7.MTUI.F
8.MONGO.
9.ASHURA H.
10.MDOE M.
angalia preventive officers ..TUNDUMA/MBEYA
1.MMEWA P.
2.NGOMA H.
3.BENJAMIN ANDOSYE
4.MASA.M
5.KESSY D.
Angalia custom officers HOLILI
1.CHALI A
2.MWAKASUNGULA L
3.KIANGIO S.
4.MANONI A.
5.MARTON L
6.MONYO W/DRIVER

SO mswahili that is the really picture ,if you have datas different to this bring them up....lakini ukweli ni kuwa TRA inaouwakilishi mzuri kwa watanzania wa pande zote ,huwafanyii haki kuwalaumu namna hiyo..sasa hao wachagga wanaoteuliwa na rais,waziri au bodi ...unaweza kupeleka malalamiko yako IKULU labda watakusikiliza
 
alisema lote huko kumejaa wachagga tupu....he is proved wrong with datas...so if he waana come up it must be with vivid datas!!!!!!!!!!!!!!!
 
hapana atakuja na kusema "sisi" wachagga tunawatetea wachagga wenzetu "wakati" Mmanda "amekiri" kuna ukabila!!! na gurudumu litaendelea kuzunguka...

Jamani kubalini hakuna ukabila yaishe!!!! Mliokubali hoja za Mswahili kwa data uchwara... kubalini data hizi tulizowapeni kutwa nzima. Msiwe mnabisha alimradi mmeshaamua kuna ukabila hata kama ushahidi haupo!!!
 

Sidhani kama unaamini mimi ndiye PM na Jokakuu! Situmii jina zaidi ya moja, sina sababu ya kutumia jina zaidi ya moja! Mzee natumia "Mwanakijiji" au "Mzee Mwanajiji". I hope umechanganya tu. Hamna tatizo.
 
I think this mdahalo is closed. Mwenye kuamini Ukabila upo ameamua kuamini hivyo, aliyeamini hakuna ukabila kama mimi nimeamua kuamini hivyo.
 
Mwanakijiji wewe si mchagga usijitie nimetukumia kwenye PM yako.

Phillimon MIKAEL.

nakushangaa kutujazia wafagizi, madereva na mataarishi, nimesema kuwa MANAGERS AU RRO ni wachagga na nikakuwekea majina yao. na wewe umesema una majina 1000 uliyoandika icluding madereva na wapika chai hayafiki 40. au ndio ule ugonjwa wa chadema (makengeza) unakusumbua?

nashindwa kuelewa wana chadema kutokuelewa somo labda kuwa makengeza huko chadema ni qualification nikitiza mzee Mtei alikuwa na matatizo hayo. na wewe pia una matatizo hayo. na hata ulipomuwakia admin wa JF ilikuwa unawaka mbona mmefuta thread ya kichagga na admin akakuweka sawa akasema vipi angalia vizuri! alikuwa na maana acha makengeza yako.

najua unaumia sana kwa TRA kwani ndio uchochoro unakuwekeni mjini na hili suala la ukabila TRA ni kama ulivyo kwenye chama chako lazima uumie.

nimekutajia officers incharge wenye dhamana wewe unaleta orodha ya madereva. nataka wenye authority ya maamuzi, dereva ana maamuzi gani TRA?

NAJUA kwako mada hii ni mtaji ili upate kusamehewa kodi na usiku kucha unahangaika na kittilya kuwa unapiga vita. hakuna vita tunaweka mambo sawa.

mie sikusema TRA madereva au wapika chai ni wachagga nioneshe wapi nilisema hivyo? nilisema watendaji kama RRO au officers in charge hawa ndio wakamua maziwa hatuzungumzii washika mapembe.

Mwanakijiji.

inajulikana wewe ni mbabaishaji na si responsible journalist ambaye hupima habari kwa kina. ndio maana unakuwa ukitumia jina mwanakjj tu. sawa na gazeti ambalo kila story utaona habari na mwandishi wetu, kila sehemu na mwandishi wetu sababu hawana uhakika na habari. ni sawa na mwanakjj.

habari si kukopi na kupaste statement kwenye magazeti wandiishi huwa na source zao na hata wakati mwingine kuzilipia.

Natoa mfano wa wazi kujua mwanakjj ni mbabaishaji wala hajui kupima habari huingia kichwakichwa tu kama anavyovamia mada hii,

kulitokea msiba wa vijana wawili-Brazil mwaka jana akina Tobi. WATU wote wakanyamaza wakijua kuwa sababu ya kifo cha wale vijana ni kushiriki katika biashara inayopigwa vita na Amina Chifupa na serikali yetu kwa sasa. na mtu akiwa brazil huhitaji kufanya utafiti mkubwa kwani huko ndio jikoni kwa biashara hiyo haramu. bwana Mwanakjj akakurupuka kukusanya michango ya hao marehemu huku akiongea na akina Kobi na hatimaye baadae akaja kuapata aibu.
mwandishi au mtu makini asingefika huko. nimelazimika kutoa mfano huu kuonesha kuwa huyu bwana ni mtu wa kudandia safari asizozijua. sitaki kwenda kwenye u wana habari wake na redio yake.
 
MKJJ

Nilipoandika PM/MKJJ/Jokakuu sikuwa na maana mbaya ya kwamba unatumia majina yote hayo; nilikuwa najibu hoja zenu kwa ujumla. (Sorry for that misunderstanding)

Back to the issue:

This is very interesting hata kule South Afrika miaka nenda miaka rudi wazungu walikuwa wanasema hakuna ubaguzi na kama unakumbuka vizuri ule mkutano wa Commowealth countries kule Zambia wakati Iron Lady Maggie Thatcher alivyokuwa anawatetea wazungu wenzake kule Rhodesia sasa Zimbabwe, kilichotokea kila mtu anajua. Ulaya vilevile walikuwa wanaimba hakuna ubaguzi lakini wametunga sheria ya kusaidia minorities. Unaweza ukaweka data nzuri sana kwa sababu wewe ni mfaidika kwa namna moja au nyingine huwezi kuliona hilo lakini ukweli utabaki pale pale. Wanaokataa ukabila wawaulize jirani zao ambao sio wachaga kama wao, Je ukabila upo hapa Tanzania? watalipata jibu. Hawana sababu ya kukiri ukabila upo kwa sababu za kihistoria wao ndio miungu watu ambao kila siku tunawapigia kelele hapa JF kwani ukabila hawauoni. Tuondoe matongotongo ili tuweze kuona sawa sawa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…