Ukabila Ikulu, Ujenzi, Mambo ya nje, Mipango, TRA, BoT + Ofisi nyeti za serikali

Mswahili... I thought u'll go that way... ukishindwa hoja, unashambulia mtu...

"mbabaishaji", "hajui kupima habari", "anaingia kichwa kichwa", "anadandia safari", "aliabika"!!

Ukishindwa hoja za mtu, unamfanya mtu hoja!

Na hapana hujanitumia PM yenye kuonesha kabila langu...
 
Mwanakijij,Phillemon,Yebo Yebo,
Hii ni kampeni ya kuwachonganisha wachaga na makabila mengine ya Tanzania. Jamboforums imekuwa kama gazeti la kihutu kangura lilokuwa likihamisha chuki dhidi ya watutsi.
 
Jokakuu,
Kuifananisha JF na Kangura ni mawazo machafu sana!.. Kangura haikuwa na sura mbili hata kidogo,kisha kuwataja WAHUTU kama ndio mabaya ndio ukabila wenyewe huo! maanake huoni haki ya wahutu hata kidogo!..
Swala hapa sio gazeti ila ni haki ktk utoaji wa ajira!...
What's wrong kama tutaangalia tatizo hili kabla halijawa baya zaidi. What if Rwanda wangelitazama swala la Ukabila ndani na hasa AJIRA.. kungekuwa na matokeo gani!
Guys mbona mnapoteza mwelekeo wa JF?
 
mswahili sijakutajia dereva wala messenger yeyote isipokuwa jina la dereva mmoja pale holili,..nimekutumia majina ya examination/custom/na preventive officers ,,hizi kazi wanafanya graduates au equivalent ...so ni wasomi hao.ukitaka majina ya madereva na masenger sema tu na nitajie ni ya kituo kipi,mimi nitakumwagia tu hapa,
naona umeamua kuendelea kubisha tu!
 
Itakuwaje Tanzania kuwe hakuna ukabila wakati tuna makabila? nyie ambao mna mawazo potofu ndio mnataka kushabikia tu kuwa wahutu, watusi, wakikuyu, wajaluo nk ndio wanafanya ukabila, fungueni macho. Kwa nini tusijadili jinsi ya kuuondoa huo ukabila na kukaa kujadili ya kwamba hakuna ukabila. Mimi binafsi sitaki kujidanganya kwa sababu kila mtu ana kabila na Mwamba ngozi huvutia kwake. Hivyo ndio binadamu tumeumbwa labda nyie malaika wenzetu ambao ni miungu watu.

Hakuna mahali popote ulimwenguni ambako hakuna ukabila bali kuna nyenzo za kuuthibiti, Nyerere (RIP) alianzisha shule za mabweni na wanafunzi kwenda kusoma popote Tanzania kwa uwezo wao wa kufaulu pamoja na lugha ya kiswahili ili kupunguza ukabila lakini leo hii hiyo haitoshi inabidi tuweke dhana nyingine zaidi yaani tuende level nyingine ili tuutokomeze kabisa.
 
jokakuu

Mwanakijij,Phillemon,Yebo Yebo,
Hii ni kampeni ya kuwachonganisha wachaga na makabila mengine ya Tanzania. Jamboforums imekuwa kama gazeti la kihutu kangura lilokuwa likihamisha chuki dhidi ya watutsi.

Hutaki ukweli usemwe? kulifumbia macho hili swala sio msingi kwani litaibuka tena, la msingi ni kulitatua.
 
Mzee Mwanakijiji,

Siamini lolote lile toka pande zote mbili unless kuna mtu hapa ambaye ni mfanyakazi wa TRA na sii Mchagga ambaye anaweza kutupa ukweli.
Unajua Mwanakijiji hata maelezo ya Mmanda ukiyasoma kwa makini bado anadai kuwepo kwa wazee Wachagga ktk nafasi za juu kutokana na historia. tanzania haiendeshwi kwa historia ya elimu ila wale wenye uwezo leo hii. Na kasema mwenyewe kuwa vijana wa kichagga siku hizi hawasomi, wengi ni wafanya biashara. Meaning hawezi kuajiri watu wapya kwa sababu hakuna wachagga vijana waliosoma. hii ni sura nyingine ya maelezo yake huyu muungwana. Ikiwa wapo vijana wa makabila mengine wenye elimu leo hii kwa nini usiwape ajiri wao?.
List na ndugu PM inaweza kuwa kweli ama sii kweli kwa sababu JF watu wazushi sana kisha katumia sana initials. Madaktari na University tumewaona makabila mengine yakiwamo Wahaya wengi tu. Unajua mzee wangu unapo jenga Ukabila hata Mhaya na mnyakyusa utamwona hana nafasi hata kama wao wamesoma vilevile. Hii ndio nilivyoelewa mimi sio swala la kuwepo na watu wenye elimu kama kigezo cha ajira.
Now, nirudi nyuma niliposoima maelezo ya mwanzo ya Mswahili nilielewa kuwa hapa TRA hakuna cha msomi uwe Mhaya, Mnyakyusa, Mnyamwezi huna nafasi ya ajira kabisa kinachotazamwa kwanza ni kabila yako!..

Nikajiuliza kama hili lawezekana!.. kweli yawezekana kwani zipo taasisi nyingi zinahitaji kutazamwa kwa makini. Tumeanza na TRA budi tuitazame kwa undani kisha tutaingia ktk taasisi za kiotaifa zenye kuajiri Wakerewe, Wanyamwezi, Wahaya na hata Wanyakyusa.

What's wrong with!
 


kuwa na makabila nin lazima kuwe na ukabila? Naomba ujibu swali hili ili tuweza kukubaliana kama kuna ukabila au la. Ukabila jinsi unavyouelewa wewe ni nini?
 
kuwa na makabila nin lazima kuwe na ukabila? Naomba ujibu swali hili ili tuweza kukubaliana kama kuna ukabila au la. Ukabila jinsi unavyouelewa wewe ni nini?

Yes kuwa na makabila kuna changia kuwe na ukabila kama huna nyenzo za kuuthibiti kama ilivyojitokeza TRA.
 
MKJJ


Hebu angalia hii hapo juu halafu uniambie Mmanda anaposema tusishangae TRA twende jeshini kwanza. Ana maana gani? Ukabila uliokithiri!
 

Mkandara, Mswahili alipokuja na data zake ulikubali mara moja:


Dua, tulipozungumza mwanzoni wewe ulikubali hakuna ukabila:

mkjj We Are All Behind You. Mjadala Huu Umeishia Hapa Longolongo Za Ukabila Kwisha. Watu Waende Kusoma Kazi Zitatolewa Kwa Wale Wanaoweza Kutuongoza Bila Kujilimbikizia Mali.

Iweje leo ubadilike wakata data alizotoa Mswahili zimeoneshwa kuwa hazina mpango, tumempa changamoto ataje kituo chochote, idara yoyote tutampa majina atuambie ni ukabila upi ana uona.

Sote tunaangalia kitu kile kile lakini tafsiri zetu ndio zinagongana. Tumeona kuna wachagga, wanyakyusa, na wahaya wengi mahali mbalimbali pa ajira, wenzetu mnaita huo ukabila, sisi hatuoni ukabila tunasema aliyestahili amepewa nafasi.

Kwa kadiri ya kwamba makabila hayo bado yana uwingi na wanaendelea kusoma sioni mabadiliko yoyote huko mbeleni. Na si muda mrefu mtaona Wasukuma na Wanyamwezi wanatokea kwa wingi (kama ilivyoonza kuonekana) Siyo kwa sababu wanapendelewa, demographic yao dictates that! Mimi nikienda Mwanza na nikakuta kwenye ofisi moja ya serikali ikiwa na wasukuma asilimia 80 wanaofanya kazi zao kwa uadilifu sitalia ukabila, it make sense!!

Nimewauliza tena, je hao Wachagga wengi walioko TRA wanaliibia Taifa? Nimewawekeeni na ripoti huru iliyochunguza ufisadi ndani ya TRA, neno la Ukabila halipo!!

Mkandara, mwanzoni ulisema kitu ambacho mimi nimekubali na ndicho ninachosema na hicho siyo TRA peke yake bali kweny ajira nzima Tanzania.


Ulisema (kwa usahihi) kuwa tatizo letu katika Uchumi na katika eneo zima la ajira ni kujuana (cronyism) na undugunaizesheni (nepotism). Huu mjadala si mgumu kama watu wanavyotaka tuamini.

a. Mliotetea ukabila kubalini mmeshindwa kwa hoja, kwani hakuna ushahidi wa ukabila, siyo TRA peke bali kwenye maeneo mengine yote, kwani uwepo kwa wingi wa watu wa kabila moja mahali pa kazi unaweza kuelezeka kisayansi. Na huo sio ukabila. Kutokuwepo ukabila TRA siyo maneno yangu bali maneno ya hata huyo Mmanda!

b. Kubalini pia kuwa tatizo siyo ukabila bali ni kujuana na undugu (na hili siyo neno jingine la kuficha ukabila). Kwamba kuna watu wa makabila mbalimbali ambao wamepeana nafasi na kuajiriana.

c. Mkikubali tatizo ni undugunaizesheni na kujuanaizesheni, basi hapo tutaweza kukaa na kutafakari sisi kama Taifa tutaweza vipi kuondokana na magonjwa haya yanayodumaza uzalishaji, kulea uzembe, na kurudisha nyuma gurudumu la maendeleo yetu. Nina uhakika kuna watu wenye mawazo ya kina ya kuondokana na matatizo hayo. Kuendelea kutung'ang'aniza tuone ukabila wakati haupo, ni kupotezena muda kusiko kwa lazima. Kukubali kushindwa hoja siyo udhaifu wa mtu au unyonge! Ni ujasiri, kwani kwenye medani za hoja, hoja yenye nguvu hushinda!!

kwa ufupi those are the terms of surrender for those who have embraced this idea of institutional tribalism in TRA or any other government department. Agree that you were wrong, we'll still respect you and wait for your contributions on how we can remove the problem of undugunization and kujuanization at the work place.

Would you agree?
 

http://www.jamboforums.com/showthread.php?t=1867&page=34

MKJJ

Ni mimi niliyekuambia kwamba nimebadili mawazo yangu baada ya ukweli na facts kupatikana. Siwezi kung'ang'ania hakuna ukabila wakati upo. Nafikiri ni wewe ambaye unatakiwa kubadili mawazo yako
 
Dua ulipobadili mawazo mara ya kwanza ulikuwa na ushahidi nusu (maneno ya Mswahli) lakini sasa baada ya kupewa picha kamili hauna budi kuufuata ukweli. Na hilo halikupunguzii kitu kwani inaonesha ni jinsi gani unatafuta ukweli!
 
Sasa hayo ya TRA ni ya uongo? Au huelewi maana ya Forum? Pale unapokosea au wengine huita kuteleza unabadili msimamo. Ni sawa na vile wewe ambavyo hutaki kuuita ni ukabila wakati hakuna neno lingine na unataka tuuite undugunisation au kujuanaisation. LAKINI HILO LITAKUWA HALIONDOI TATIZO. WE NEED TO FACE THIS HEAD ON.
 
Ndugu zanguni mimi sipendi sana kuchangia tu, huwa nachangia kwa nadra sana pale inapobidi.

nimefuatilia huu mjadara na nina watu wangu TRA tatizo la ukabila ni kubwa kuliko mnavyolijadili humu, huko TRA watu wanataka kutoa roho kwa ukabila.

Sio siri ni jambo la wazi kabisa mnaobisha fanyeni taratibu za kujua hali halisi mnaweza kuwa mnatetea kitu bila kujua au wanajua wanafanya maksudi. huu si ubishi ni jambo la wazi hata serikali inalijua.

Philimon amesema kuwa hata Magufuri alimtetea, na kukanusha kuwa si mchaga hiyo si hoja.

ukitizama trend ya gazeti la Tanzania Daima la mheshimiwa Mbowe kwa muda mrefu limekuwa likimpigia debe waziri magufuri na makala zake za kumjenga zinatoka kila mara, na walikuwa wakijibizana na gazeti la Rai lililotoa kashfa nyingi tu za Magufuri hasa uuzaji wa nyumba kwa vimada zake.

kama Philimon aliweka thread ya kumtetea Magufuri inawezekana ni mwendelezo wa kazi ya Tanzania Daima (lina tenda) gazeti lenye mlengo wa Kilimanjaro na matangazo mengi ya TRA yanapelekwa huko Tanzania Daima.

mada hii ni nzito na si sahihi kujaribu kuififisha kwa utashi wa mtu au kikundi cha watu hapa ni maslahi ya taifa na ni mada nyeti kama ile ya Mzumbe university na UDSM.

TAFADHALI SHIRIKINI KWA NGUVU.
 
Mzee Nungwi.

Karibu mkuu usipotee sana tunakuhitaji mzee. naungana na wewe mzee wa Mzumbe kweli kabisa TRA noma kwa ukabila huo uchagga nani asioujua?

hayo majina yaliyoletwa hayajaja na makabila yake na ni idadi ndogo sana ya watumishi wa TRA na kuna kidato cha sita hapo alisema ni graduate muongo.

Mkandara,mswahili, Dua na wengine tuko nyuma yenu kitu muhimu sana mnaongea humu achaneni na Mwanakjj yeye yuko Marekani anajitia kujua mambo ya TZ atazidi kuumbuka tu. kweli alikuwa anachangisha mchango wa kusafirisha maiti ya muuza unga wa U.K aliyefia Brazil. asikutisheni hana kitu, hiyo redio ya uvunguni mara mtu anafungua mlango mara kapokea cm hana kitu ndio maana anakesha humu hana kazi. endelezeni libeneke mkitaka nguvu zetu tupo tumejaa tele. yeye mkurya ni mmoja wa wakabila wa kupingwa vita!!.
 
MSWAILI.
Ukowapi tunasubiri hizo hojja zao ulizo kusanya leo.
Naona kina mwanakijijji hawana hoja wanatuzuga tu hapa!!!
 
Mwanakijiji,
kama watu wazima, and so that we could move forward, hebu tukubaliane na hawa jamaa zenu kwamba huo "ukabila" upo. natumaini kwa kufanya hivyo watashawishika kuchangia mawazo juu ya utaratibu wa kuziba mianya ya "ukabila," TRA na taasisi nyingine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…