Mzee Mwanakijiji,
Siamini lolote lile toka pande zote mbili unless kuna mtu hapa ambaye ni mfanyakazi wa TRA na sii Mchagga ambaye anaweza kutupa ukweli.
Unajua Mwanakijiji hata maelezo ya Mmanda ukiyasoma kwa makini bado anadai kuwepo kwa wazee Wachagga ktk nafasi za juu kutokana na historia. tanzania haiendeshwi kwa historia ya elimu ila wale wenye uwezo leo hii. Na kasema mwenyewe kuwa vijana wa kichagga siku hizi hawasomi, wengi ni wafanya biashara. Meaning hawezi kuajiri watu wapya kwa sababu hakuna wachagga vijana waliosoma. hii ni sura nyingine ya maelezo yake huyu muungwana. Ikiwa wapo vijana wa makabila mengine wenye elimu leo hii kwa nini usiwape ajiri wao?.
Lisy na ndugu PM inaweza kuwa kweli ama sii kweli kwa sababu JF watu wazushi sana. Madaktari na University tumewaona makabila mengine yakiwamo Wahaya wengi tu. Unajua mzee wangu unapo jenga Ukabila hata Mhaya na mnyakyusa utamwona hana nafasi hata kama wao wamesoma vilevile. Hii ndio nilivyoelewa mimi sio swala la kuwepo na watu wenye elimu kama kigezo cha ajira.
Now, nirudi nyuma niliposoima maelezo ya mwanzo ya Mswahili nilielewa kuwa hapa TRA hakuna cha msomi uwe Mhaya, Mnyakyusa, Mnyamwezi huna nafasi ya ajira kabisa kinachotazamwa kwanza ni kabila yako!..
Nikajiuliza kama hili lawezekana!.. kweli yawezekana kwani zipo taasisi nyingi zinahitaji kutazamwa kwa makini. Tumeanza na TRA budi tuitazame kwa undani kisha tutaingia ktk taasisi za kiotaifa zenye kuajiri Wakerewe, Wanyamwezi, Wahaya na hata Wanyakyusa.
What's wrong with!
Mkandara, Mswahili alipokuja na data zake ulikubali mara moja:
Mswahili,
ndugu yangu nimekubali na hoja zako kwa sababu moja kubwa sana. Nimeitazama list nzima ya viongozi wa juu ambayo haina Ukabila lakini hawa watu hawakupata ajira zao through process ya TRA ila waliteuliwa na serikali moja kwa moja nje ya ofisi ya ajira ya TRA. Serikali haina Ukabila isipokuwa kila tunapotoa nafasi za kazi na hasa ile ya Human Resources hapo ndipo penye source ya Ukabila.
Nimekuelewa sana na kwa sababu Watanzania wengi walalhoi hawahitaji kuwa ma director au commissioner ila nafasi za kwaida (ajira) kulihudumia taifa, hapo ndipo tunapozungumzia.
Nimekubali pia kuna sehemu kibao nchini ambazo wapo watu wameweka kaka zao, dada zao, shemeji zao na kila aina ya KUJUANA kiasi kwamba haiwezi kutafsirika nje ya Ukabila hasa pale Wachagga na Wanyakyusa wanapoingiza mila zao. Mtanisamehe ndugu zangu wa Kili na Mbeya maanake palipo na ukweli inabidi tuseme na pengine mtaweza kulitazama swala hili kwa sura nyingine. Pia kuna kijimila dulani kuwa usipoajiri jamaa zako basi wewe zoba kama vile kutoiba ama kuchukua rushwa ukiwa ktk nafasi nyeti!...yaleyale ya Ujanja ni Kupata!
Wachagga na Wanyakyusa kila mtoto aliyezaliwa na damu yao iwe hata toka kwa Mwanamke huhesabika kama wao. Pamoja na kujichanganya kote kwa Makabila lakini hawa jamaa zetu wamekataa kabisa kutambua mtoto nje ya makabila yao na kujichanganya kwao ni ktk kuzidisha nguvu ya makabila yao.
Kuna kila haja ya kuendeleza mada hii tupate picha halisi ya mchezo huu ambao ulikuwepo wakati wa Nyerere na ulikuwa ukipigwa vita vibaya sana. nakumbuka kuna vijana marafiki zangu walikuwa mashushushu enzi zileee. Kazi yao ilikuwa kuwaibua viongozi ndani ya mashirika ambao huwapendelea ndugu na makabila yao ktk nafasi za kazi.. ndio maana mliona uhamisho wa baadhi viongozi wazuri wachapa kazi ktk baadhi ya sehemu kutokana na kosa ambalo lilionekana dogo tu... Ukabila!
Dua, tulipozungumza mwanzoni wewe ulikubali hakuna ukabila:
mkjj We Are All Behind You. Mjadala Huu Umeishia Hapa Longolongo Za Ukabila Kwisha. Watu Waende Kusoma Kazi Zitatolewa Kwa Wale Wanaoweza Kutuongoza Bila Kujilimbikizia Mali.
Iweje leo ubadilike wakata data alizotoa Mswahili zimeoneshwa kuwa hazina mpango, tumempa changamoto ataje kituo chochote, idara yoyote tutampa majina atuambie ni ukabila upi ana uona.
Sote tunaangalia kitu kile kile lakini tafsiri zetu ndio zinagongana. Tumeona kuna wachagga, wanyakyusa, na wahaya wengi mahali mbalimbali pa ajira, wenzetu mnaita huo ukabila, sisi hatuoni ukabila tunasema aliyestahili amepewa nafasi.
Kwa kadiri ya kwamba makabila hayo bado yana uwingi na wanaendelea kusoma sioni mabadiliko yoyote huko mbeleni. Na si muda mrefu mtaona Wasukuma na Wanyamwezi wanatokea kwa wingi (kama ilivyoonza kuonekana) Siyo kwa sababu wanapendelewa, demographic yao dictates that! Mimi nikienda Mwanza na nikakuta kwenye ofisi moja ya serikali ikiwa na wasukuma asilimia 80 wanaofanya kazi zao kwa uadilifu sitalia ukabila, it make sense!!
Nimewauliza tena, je hao Wachagga wengi walioko TRA wanaliibia Taifa? Nimewawekeeni na ripoti huru iliyochunguza ufisadi ndani ya TRA, neno la Ukabila halipo!!
Mkandara, mwanzoni ulisema kitu ambacho mimi nimekubali na ndicho ninachosema na hicho siyo TRA peke yake bali kweny ajira nzima Tanzania.
Kalamu,...
...Kila chaguzi sasa hivi linatazamwa kwa rangi zake iwe dini ama Ukabila wakati sote tunafahamu adui yetu mkubwa ktk uchumi wetu leo hii ni KUJUANA. Huna address shule itakuwa ngumu, ajira n.k.
Marafiki wengi wa JK wanatoka makabila mbalimbali na dini tofauti na ndio tunawaona wakishika nafasi kama ilivyokuwa toka wakati wa Nyerere. bahati mbaya hakuna mtu aliyethubutu kumuuliza Nyerere na pia wakati ule tukumbuke kulikuwepo na chama kimoja chini ya mfumo wa kisocialist. You are either with us or take the highway!
Ulisema (kwa usahihi) kuwa tatizo letu katika Uchumi na katika eneo zima la ajira ni kujuana (cronyism) na undugunaizesheni (nepotism). Huu mjadala si mgumu kama watu wanavyotaka tuamini.
a. Mliotetea ukabila kubalini mmeshindwa kwa hoja, kwani hakuna ushahidi wa ukabila, siyo TRA peke bali kwenye maeneo mengine yote, kwani uwepo kwa wingi wa watu wa kabila moja mahali pa kazi unaweza kuelezeka kisayansi. Na huo sio ukabila. Kutokuwepo ukabila TRA siyo maneno yangu bali maneno ya hata huyo Mmanda!
b. Kubalini pia kuwa tatizo siyo ukabila bali ni kujuana na undugu (na hili siyo neno jingine la kuficha ukabila). Kwamba kuna watu wa makabila mbalimbali ambao wamepeana nafasi na kuajiriana.
c. Mkikubali tatizo ni undugunaizesheni na kujuanaizesheni, basi hapo tutaweza kukaa na kutafakari sisi kama Taifa tutaweza vipi kuondokana na magonjwa haya yanayodumaza uzalishaji, kulea uzembe, na kurudisha nyuma gurudumu la maendeleo yetu. Nina uhakika kuna watu wenye mawazo ya kina ya kuondokana na matatizo hayo. Kuendelea kutung'ang'aniza tuone ukabila wakati haupo, ni kupotezena muda kusiko kwa lazima. Kukubali kushindwa hoja siyo udhaifu wa mtu au unyonge! Ni ujasiri, kwani kwenye medani za hoja, hoja yenye nguvu hushinda!!
kwa ufupi those are the terms of surrender for those who have embraced this idea of institutional tribalism in TRA or any other government department. Agree that you were wrong, we'll still respect you and wait for your contributions on how we can remove the problem of undugunization and kujuanization at the work place.
Would you agree?