chuma,
kama walivyoeleza wachangiaji wengine kuwepo kwa idadi kubwa ya kabila moja ktk sekta fulani siyo uthibitisho wa ukabila. ushahidi anaoleta mswahili hapa hautoshi kuthibitisha kwamba kuna ukabila ktk hizo taasisi anazozituhumu.
yuko mchangiaji aliyeleta mpaka majina ya watumishi wa baadhi ya vitengo vya TRA. ushahidi huo ulithibitisha kwamba kuna diversity nzuri tu huko TRA. majibu ya mswahili yalikuwa kwamba ameleta majina ya walinzi,wafagizi, na madereva wa TRA. leo hii mswahili anaibuka na kudai kwamba VETA kumejaa wachaga, hata wafagizi ni wa wachaga!!
mswahili huyuhuyu akadai kwamba waziri mramba amependelea jimbo lake ktk kutoa fedha za ujenzi wa barabara. uchunguzi ukabainisha kwamba Mramba siye aliyeanzisha ujenzi huo, bali waziri john magufuli.
mswahili akaibuka tena na kudai kuna mbunge amelalamikia jinsi fedha za miradi ya barabara zilivyogawiwa na Waziri Mramba. In particular, jimbo la mbunge husika lilipewa sh.billioni 1, na jimbo la Mramba lilipewa billioni 17. uchunguzi[data frm TANROADS & budget speech] ukabainisha kwamba tofauti hiyo ilitokana na ukweli kwamba barabara ya jimbo la Waziri Mramba iko ktk hatua ya ujenzi, wakati ile ya Mbunge aliyelalamika ipo ktk hatua ya fesiability study and design.
Unajua Mama Anna Abdalah mbunge wa kusini alipata kuwa waziri wa ujenzi. Katika uongozi wake barabara za Kusini zilipewa kipaumbele kuliko sehemu zingine za Tanzania. Sikusikia mtu yeyote akilalamika. Watanzania tuliolelewa katika umoja tulielewa shida ya wenzetu wa mikoa ya kusini.
yuko mchangiaji mwingine, sina uhakika kama ni mswahili, akaibuka na madai kwamba mamlaka ya elimu imejaa wachaga, na inapendelea uchagani. again, tulipoangalia bodi ya wakurugenzi, na management ya mamlaka ya elimu, tukakuta kwamba tuhuma kwamba pamejaa wachaga si za kweli. vilevile taarifa za mahesabu ya mamlaka ya elimu hazikuthibitisha upendeleo kwa shule za uchagani.
mswahili huyuhuyu alikuwa akimpamba sana Dr.Asha-Rose Migiro. Kumpamba huko inaelekea kulitokana na imani yake kwamba Mama Migiro ni mtu wa pwani/"mtoto wa mjini"/"mtoto wa kiswahili." Kwani Mama Migiro alipokwenda kijijini kwao Usangi, Kilimanjaro, na kuandaliwa sherehe ya kimila, basi mswahili akawa kama amemsusa--hatujaona akimpamba tena!!
Kurasa 118, Replies 1117, na views zaidi ya 20,500 hapa Jamboforums, zote zinalisakama kabila moja tu, WACHAGA!! Mbona Wambulu na Barabaig hawanyanyaswi kwa kudominate mbio ndefu Tanzania? Mbona hakuna anayehoji Jeshini ambako idadi kubwa ni watu wa Musoma? Mbona hakuna anayehoji kwamba matajiri wengi wa mabasi ni Wakinga?
Binafsi siamini kama Wambulu,Barabaig,Wakurya,Wakinga, wanaukabila. SIAMINI kama kuwepo kwa idadi kubwa ya makabila hayo ktk michezo, na taasisi nilizozitaja, kumetokana na UKABILA. Anayelia ukabila anajaribu kuleta majibu rahisi kwa maswali magumu.