Ukabila Ikulu, Ujenzi, Mambo ya nje, Mipango, TRA, BoT + Ofisi nyeti za serikali

Ukabila Ikulu, Ujenzi, Mambo ya nje, Mipango, TRA, BoT + Ofisi nyeti za serikali

Mswahili namna ulivyoweka tafsiri ya maneno ya Filemon Michael sijui atasemaje...maana kwa namna nilivyoelewa PM-michael akikaa watu kuhoji ukabila ndani ya TRA,BANK etc, basi nae akatae kuhoji serikali ya JK.
Uoni wangu: JF ipige mawe popote penye harufu mbaya ya Udini, Ukabila, Matumizi mabaya ya serikali na mengineyo.

kaka chuma huyo jamaa ni kichekesho...ameharibu kabisa maana ya ujumbe wangu...........mfano kaka yangu wewe una Msc ..ukiona tangazo la kazi linalohitaji hiyo sifa utaomba au utaacha kwa kuamini "nikiomba sintapata"...sasa kama mtu mwenye akili anahamasisha watu wasiombe kazi kwa kuwa hawatapata..wakiajiriwa wengine atapata la kulalamika.

kwa kifupi nimegundua watu wengi makoni wamembaini huyu na dawa akileta tafsiri zake potofu ni kumwacha...mara nyingine kukaa kimya inatosha!!
 
.....Raisi amemteua Jaji Mrosso kukaimu nafasi ya Jaji Mkuu. Kama sijakosea Mrosso ni "lichaga." Naona ndugu yetu mswahili pressure itampanda.
 
Wandugu! One way to address ukabila
1. Sasa mimi naona kuwe na Quota System katika kupata wanafunzi wa Vyuo Vikuu vya Umma- pengine kila Wilaya itoe 10 students who qualify to get Mikopo. This in the long run will address the current imbalances in a way. Ila kwa hali ilivyo sasa- Shule nzuri nyingi zipo Mbeya, Moshi, Iringa na Dar na ni private. Je mtoto wa mkulima wa Kibondo- atapataje nafasi kusoma higher learning? Is this fair? Ukabila ni rooted katika ependeleo (historical) wa baadhi ya maeneo kuwa favoured. So wandungu hili ni swala la to be fair and take affirmative actions!
2. One issue ni kama tu hakutakuwa na mzengwe katika kupata hawa wanfunzi huko Wilayani- na pia pia kama Wenzetu wengine will not migrate to other districts kosoma kupata hizo nafasi.
3. Kuna mtu ana uzoefu ktk nchi kuna utaratibu huu? Je unafanya kazi?
 
UK wana utaratibu wa ku monitor wanafunzi wanaoingia University hadi kwenye ajira ambapo unataja kama ni Asia au ni Pakistan au Bangladeshi n.k pia kama ni mweusi muafrika au chotara au Mjamaica.

si hivyo tu hadi kwenye Grants kuna maalum za kuwainua watu fulani wanapenga kutumia neno Minority au BME.

kwa kweli hili ni tatizo na serikali yetu inasema haiamini vitu hivi ni sawa na kusema uchawi haupo kwenye public huku kila mtu kivyake anahangaika na ushirikina. huu ni wakati muafaka kusema kuwa kuna Ukabila nchini na ni tatizo kubwa tuwahi kabla haijafikia hali kama ya nchi za Burundi na Rwanda. Mficha uchi hazai na mficha magonjwa kilio kitamuumbua.

Nakubali kabisa hata DPP kulikuwa na kampeni awepo mchagga.
 
Mtalii,
1. Yaani ofsini kwangu 95% ya wafanyakazi ni Wakristo- na Chuoni tulisoma na Waislam wengi tu tena walipasi vema. As a country- if we dont take affirmative actions now to reddress imbalances in Ukabila, Dini, Mkoa- inafika mahali- ndo inatokea watu wa kabila moja zaidi ni TRA, wanajeshi- ni Mara n.k. Ila kisiasa there is a denial of the truth! This is not healthy to our country!
2. Naona viongozi pia wamefunga maskio ya mawazo mapya- MSITU MPYA NYANI WALE WALE! Nani achukue hatua wandugu?
 
MzalendoHalisi,
wakati wa utawala wa Nyerere walianzisha quota-system ktk kuchagua wanafunzi wanaokwenda sekondari. kwa maoni yangu mfumo huo haujaweza kuondoa imbalances zilizokuwepo.

Wakoloni waliipendelea mikoa fulani fulani kutokana na sababu za kiuchumi. Nafurahi kwamba umelitambua hilo. Colonial legacy bado ipo mpaka leo.

Jeshi letu lina askari wengi kutoka maeneo ambayo wakoloni walipendelea ku-recruit askari wao. Hiyo ni miaka 46 baada ya Uhuru. Maeneo ambayo mkoloni aliruhusu Cash economy, not plantation economy, wenyeji wake wanaelekea kupendelea kujihusisha na biashara.

Ni vigumu sana kuwa na Quota-System Tanzania na wananchi wasishindwe kui-abuse. Mfano ni wanafunzi waliokuwa wakibadilisha majina na kwenda kurudia mitihani ktk mikoa iliyokuwa na "upendeleo." Hapa nazungumzia Quota-System ya kimaeneo.

Mimi nafikiri serikali ielekeze nguvu zaidi ktk kujenga mashule, na kuvutia waalimu[wataalamu wengine] kwenda kufanya kazi ktk maeneo yaliyoko nyuma kielimu, na kimaendeleo. Kwa mfano, wanaweza kutoa vivutio kama vya mishahara mikubwa, au nyumba za kuishi, kwa yeyote atakayekubali kwenda kufundisha/kufanya kazi ktk maeneo hayo.

Uzoefu wangu wa Affirmative action ni ule uliojikita ktk rangi na asili ya mtu. Hapa nazungumzia affirmative action kwa weusi na wahindi wekundu wa Marekani, na Abborigines wa Australia. Kwetu sisi watanzania mtu yeyote anaweza kuhama toka Mbeya akaenda Sumbawanga na aka-qualify for affirmative action.
 
Tatizo ni yale makabila yaliochomoza wakati ule ndio wanaendelea zaidi kwa sababu ya ku-hold key post hivyo wanakuwa wanauwezo zaidi ya kuwasaidia watu wao kimasomo na ina pia inapobidi kuwasaidia ktk ( interview) kazi, kwa sababu post zikitoka wao wanajua kwanza, pili ndio wapo kwenye panel na ndio mabosi wenyewe.
Kama pale TRA ilipoanza hiyo 10 years ago post zote zilikuwa zinashikiliwa na watu wa sehemu moja kasoro Luoga tu, ambaye labda Mkapa/Mbilinyi ndio walio muweka hapo.
Lakini vitengo vingine ni hao hao, kwenye Board napo nearly was the same, sasa matokeo yake ndio tunapata issue kama za kina Benny Lusago kupigwa transfer etc.
Nakumbuka kuna wakati moja enzi za Rabiel Swai TRDB (CRDB) yeye tuhuma zake zikipelekwa ikulu , kesho yake anakuja na copy ya hiyo barua kuwasemea ovyo waliomuandika.
Sasa ukiendeleza na zama za Bw Nkapa na Shemeji zake basi unakuta muendelezo ni huo huo , ukajumlisha na Sumaye na Mai Wife wake ni wa huko huko, basi na Ma Dc hivyo hivyo, Wakurugenzi wa Mikoa , yaani list ni ndefu saanaaa.
 
Maana kama Kesi ya Benny ni sawa na kumpelekea ngedere kesi ya nyani maana hata Makatibu wa Kuu wengi ukiangalia wanatoka sehemu fulani, sasa wengine wanazidiwa nguvu wanakuwa wasindikizaji tuu, na wao wakipewa vijinafasi viwili vya ndugu zao basi wenzao kumi
 
Joka Kuu-
1. Nikuulize swali? Kama mfumo uliopo sasa wengi wa wanaotoa maamuzi ni wa kabila (dini) moja- na kuna ajira pmya na watu wa kabila/dini hiyo hiyo (due to historical/colonial reasons!) wanaqualify dont you see a likelyhood ya recruitment ya hao watu kuchukua jamaa zao? Ila kama kuna criteria- say given same qualifications if you need 20 new workers- 10 wawe Waislam na 10 wawe wakristo. This is a kind of proactive affirmative actions I ma talking about!
2. Over incentives to 'hardship areas' yes- this could be a long term solution- je hawa highly qualified workers wanakaa kweli Kasulu? Wakati hakuna infrustructure? kwa nini asikae Meru Arusha?
3. Nakubalina na mtalii- we need to learn from good country practices in the ways they have tried to re-ddress the imbalances! Tatzo langu kwa Bongo naona ni mzegwe tu na upendeleo ktk uekalezaji!
 
Tatizo ni yale makabila yaliochomoza wakati ule ndio wanaendelea zaidi kwa sababu ya ku-hold key post hivyo wanakuwa wanauwezo zaidi ya kuwasaidia watu wao kimasomo na ina pia inapobidi kuwasaidia ktk ( interview) kazi, kwa sababu post zikitoka wao wanajua kwanza, pili ndio wapo kwenye panel na ndio mabosi wenyewe.
Kama pale TRA ilipoanza hiyo 10 years ago post zote zilikuwa zinashikiliwa na watu wa sehemu moja kasoro Luoga tu, ambaye labda Mkapa/Mbilinyi ndio walio muweka hapo.
Lakini vitengo vingine ni hao hao, kwenye Board napo nearly was the same, sasa matokeo yake ndio tunapata issue kama za kina Benny Lusago kupigwa transfer etc.
Nakumbuka kuna wakati moja enzi za Rabiel Swai TRDB (CRDB) yeye tuhuma zake zikipelekwa ikulu , kesho yake anakuja na copy ya hiyo barua kuwasemea ovyo waliomuandika.
Sasa ukiendeleza na zama za Bw Nkapa na Shemeji zake basi unakuta muendelezo ni huo huo , ukajumlisha na Sumaye na Mai Wife wake ni wa huko huko, basi na Ma Dc hivyo hivyo, Wakurugenzi wa Mikoa , yaani list ni ndefu saanaaa.

August.

Unaweza kunipa habari zaidi za huyu Benny Lusago? Mswahili kamtaja sana lakini kwa vile jina lake Mswahili wana jf wanajua ni porojo naomba nipe zaidi. huko TRA kama hali ndio hiyo kunatisha sana na kusafishwa kuanzie huko.

Kumbe CRDB nao walikuwa na Base Ikulu? au ndio kina Freddy Maro na DR.Maro walikuwa na kazi maalum ya kufungua briefcase la shemeji yao.

Joka kuu.

Mkoa wa Lindi ulikuwa na sekondari mbili hadi Mwinyi anaingia. jee maofisa wa Elimu wa mkoa wanatoka wapi? hawakuwa na program za kuendeleza maeneno hayo au walikuwa na mkakati wa wakoloni?

Daraja la Rufiji nalo ilikuwa history hadi Mwinyi alipokuja na kufanya jitihada binafsi ndio likajengwa, jee wizara husika zinafanya kazi ya mkoloni?
 
Wandugu,
1. Tunaweza kusema kama kuna new positions priority to be given to 'unluck areas' if there are Tanzanians who qualify from such areas? Say TRA management must thrive to rectuit new staff from say Singida, Kigoma, Lindi etc if such regions do not have adequate proprtion of staff to TRA. Emphasis to be given to Muslims and women who qualify. In this way -tunaanza kuaddress imbalance katk ukabila TRA na kuifanya iwe na National Tanzanian face!
2. Wakati huo huo kuwa na Quota system ya say 10-20 students who qualify from each district to get places and Loans from higher learning.
3. Njia ya kusaidia to address imbalances (ukabila, udini, mkoa n.k)-is a combination of affirmative action and other long term strategies.
4. We may expect much resistance from those benefiting from the imbalances currently.
Je mwaonaje?
 
Mie nilifanya Ziara Lindi Sekondari ya GOVERNMENT mwaka 2001, nikawauliza vijana wa F5 walochaguliwa, wangapi wanatoka lindi. out of 100 ni 5 ndio walokuwa wakazi wa Lindi. sikufanya utafiti wa 95 walikuwa wanatoka wapi?...
 
Chuma
May be ile sera ya majimbo will address such imbalances! When you you have a highly centralised system it is difficult for "unlucky areas" imbalances to be addressed fairly. Ndo maana Mkuu wa Mkoa wa Lindi haoni uchungu kwa nini 95% ya F5 students hawatoki Lindi- yeye is JK appointee- na anatoka Mbeya. Kwa nini asiwashauri watoto toka Mbeya kuja F5 pale Lindi? Afterall RC anweza kuhamishwa tu tena wakati wowote apelekwe hata Sumbawanga!
Mnaonaje?
 
MzalendoHalisi,
1.Nakubaliana na wewe kwamba favouritism ipo ktk ajira karibu kila sehemu. Nakubaliana na kuwepo kwa juhudi za lazima ku-recruit vipaji toka MAENEO yaliyoachwa nyuma kimaendeleo.

2.Binafsi suala la DINI naliogopa sana. Mara nyingi huwa linazua JAZBA zisizokuwa na ulazima. Nafikiria kwamba ukiwa na mpango maalum wa kuhamasisha/kusaidia/kuendeleza elimu ktk dis-advantaged areas basi matatizo ya ukabila na udini yataondoka yenyewe.

3.Kuhusu hilo la INCENTIVES ndivyo ambavyo mataifa mbalimbali yameweza kupeleka wataalamu kufanya kazi ktk dis-advataged/poor/rural/under-developed areas. Kwani unafikiri wazungu wanaoenda kufanya kazi ktk CRISIS AREAS wanavutiwa na nini kama siyo INCENTIVES?

MZEE KIFIMBO,
Umeniuliza kuhusu kiroja cha mkoa wa Lindi kuwa na shule mbili tu za sekondari. Kwa kweli sielewi undani wake. Labda umuulize Mzee Chuma ambaye alipata kutembelea huko.

Kuhusu daraja la mto Rufiji ilikuwaje halikujengwa mpaka wakati wa Mzee Ruksa hilo kidogo ninaelewa undani wake.

Habari za ndani kabisa zinasema barabara ya kusini ilikuwa ipitie juu ya bwawa la Stieglers Gorge[kidatu 3] kwa kuogopa gharama kubwa za ujenzi wa tuta na daraja maeneo ya bonde la mto Rufiji.

Barabara ilikuwa ipite Morogoro-Mikumi-Mdaula iingie Stieglers Gorge ieendelee kusini. Sote tunajua kwamba Kidatu 3 ilikufa, na hivyo serikali ikabidi irudie plan A-- kujenga barabara kukatiza bonde la mto Rufiji.

Nimeambiwa kwamba serikali ilitafuta wafadhili kila mahali, lakini kila mmoja alikuwa haionyeshi interest. Nimeambiwa wafadhili huangalia economic returns,mchango wa serikali, na gharama za mradi kabla ya kukubali kutoa ufadhili. Kipindi serikali inahangaikia mradi huo hali ya kifedha ya serikali ilikuwa mbaya sana.

Kutokana na hali hiyo nimeelezwa serikali iliamua kuomba msaada wa vifaa vya ujenzi toka Japan. Wakati huo JWTZ walijenga barabara ya kuelekea Songea hivyo serikali ikapata matumaini kwamba wangeweza kuwatumia haohao kujenga barabara ya kusini.

Serikali ya Japan ilileta vifaa vya kila aina vikawekwa kwenye kambi ya Ujenzi ya Nangurukuru. Haieleweki ni kwanini serikali haikuanza Ujenzi huo mara moja. Because of government inaction vifaa hivyo vikaanza kuchukuliwa kwa shughuli mbalimbali kwa amri za wakuu wa wilaya n.k. Katika mazingira hayo vifaa vingi sana viliharibika. Nimeambiwa anayepaswa kuwajibika kwa hilo ni RASHIDI KAWAWA ambaye alikuwa Waziri wa Ulinzi wakati huo.

Baada ya serikali kushindwa kutumia vifaa toka Japan sasa ndiyo ukatafutwa msaada toka KUWAIT FUND. Msaada huo ulipopatikana Kuwait akavamiwa na SADDAM HUSSEIN. Kwa hiyo fedha hazikupatikana na barabara haikujengwa.

Baada ya Kuwait kuwa na matatizo ikabidi sasa serikali iende kwa WASAUDIA. Sasa hapo ndiyo zikapatikana fedha za kuanza Ujenzi. Baadaye Kuwait ilipotengamaa, nao wakaongezea msaada.

Wakati serikali ikiendelea kutafuta msaada toka nje, mkandarasi Ladwa alipewa tender kujenga barabara to gravel stage toka mkuranga kuelekea rufiji darajani. Serikali ilikuwa inamlipa Ladwa kwa kutegemea fedha za ndani.

Nimeambiwa Wasaudia walipokuja kutembelea mradi walikuta kipande alichojenga Ladwa nacho kimeharibika wakaona wagharimie mradi mzima.

KWA MAELEZO HAYO HUWEZI KU-CONCLUDE KWAMBA BARABARA YA KUSINI HAIKUJENGWA KUTOKANA NA HUJUMA ZA WATU WA KASKAZINI.
 
inaweza hawakufanya Hujuma, lkn Uchungu wa hio barabara hawakuwa nao...as long as viongozi wanaenda na Ndege pamoja na yote Barabara bado haijamaliza kufikia LINDI...bado kutoka DSM hadi Mtwara masaa 14 au zaid...tumepunguziwa masaa ya kusubiri kivuko...Mkapa pamoja na kuwa Mtwara kwao pia hakuona uchung..Shemeji zake walimzonga MNO...sijui JK maana kule ni kwa Shemeji zake..lkn Rungu Analo shemeji yake Mkapa...sijui
 
Joka Kuu!!
Kama siyo affirmative action to address imbalances katika dini (Waislam wako sawa na Wakristo 50% by 50%?)- kwa sasa kuwapa Waislam walioachwa nyuma (kwa sababu za kihistoria/colonial reasons) strgies nyingine ni bom? tatuchukua mda mrefu sana kuwa na national face katika ajira in Tanzania govnt and institutions!
Let us call a spade a spade - tusiwe waoga- Mficha uchi hazai!
 
inaweza hawakufanya Hujuma, lkn Uchungu wa hio barabara hawakuwa nao...as long as viongozi wanaenda na Ndege pamoja na yote Barabara bado haijamaliza kufikia LINDI...bado kutoka DSM hadi Mtwara masaa 14 au zaid...tumepunguziwa masaa ya kusubiri kivuko...Mkapa pamoja na kuwa Mtwara kwao pia hakuona uchung..Shemeji zake walimzonga MNO...sijui JK maana kule ni kwa Shemeji zake..lkn Rungu Analo shemeji yake Mkapa...sijui

....utayasema yote na usipate jibu muafaka,la kwanini?

....kama joka lilivyosema,faida ya kiuchumi haiko wazi sana huko[labda sasa tunapoongelea gesi na mafuta].

....unakumbuka,iliwahi kujengwa reli toka ntwara kwenda,wapi vile?halafu ikaja ngolewa!

....nasikia kuna mawazo ya kujenga nyingine,kama chuma na makaa huko nyanda za juu kusini yatachimbwa.

....sasa,hapo hamna ukabila,bali hali halisi ya mambo ya dunia![ukiondoa ukabila]
 
....duh,hii renovation imekaa vizuri kinoma!

....hii si sehemu yake,lakini yakhe,mi nshatoa sifa tayari!
 
Back
Top Bottom