well said mwanakijiji,you touch were i was thinking,...i like that..i support you kuwa TATIZO LA TANZANIA NI UNDUGUNIZATION aka USHKAJI...mimi nimeshuhudia unakuta bosi anaweza kuwa mchagga anaajiri watoto wa rafiki zake mhaya ,mgogo ets..au mara nyingi nimewaunganishia watu kazi kwa sababu nawafahamu ...lakini sio homeboys ...
tatizo lingine ni ABUSE OF POWER wengi wanawapa watu kazi watu wasio kuwa kabila lao BUT just because ana uhusiano wa kamapenzi na DADA hata kama ni nyumba ndogo....
nataka nikuhakikishie bw mswahili kuwa ukabila tanzania unapotea ..watu siku hizi hawaulizani kabila ila wanaulizana UNAMFAHAMU?...Sasa itategemea mnafahamiana vipi..siku hizi nataka nikuambie kuwa watanzania tumeoana sana kiasi unaweza ukasema mtu sio MCHAGGA Lakini ukifuatalia unakuta MAMA MCHAGGA..au unakuta binti wa kihaya anaitwa KOMBA ...siku hizi huwezi kujua kabila la mtu kwa kuangalia UBINI wake,nafikiri kwa hapo mwalimu alifahulu..
hata kina khamis abdul wapo kilimajaro na bukoba ...sio lazima wawe waswahili
HATA muheshimiwa rais alivyochagua baraza tukubali hakufanya undugu wala ukabila lakini ukweli ni kuwa ametumia KUJUANA au USHKAJI...