Professor Malima alipopata skolaship ya kwenda marekani kusoma kati ya mwaka 1964 na 66 hivi wakati huo akiwa katibu mtendaji wa TANU wilaya fulani mkoa wa pwani, hakuna aliejua kuwa atakuja kuwa mzigo sana kwa nchi. Aliporudi alipewa kazi ya katibu Mkuu wizara ya mipango chini ya Waziri Professor Abdurlahmani Babu ambaye mara moja aliona weakness yake na kumkataa.
HEBU EXPAND HIII maana nilikuwa siijui hii
Ndipo Nyerere alipoamua kumpa kazi ya kufundisha Chuo kikuu ambapo alipata uprofessor kutokana na mshahara aliotoka nao serikalini wa katibu mkuu wa wizara. Huyu mtu hakuwa professor on merit. Niliwahi kusoma review iliyoandikwa na Professor Shivji kuhusu profesorial inaugural lecture ya Malima iliyokuwa ikiitwa kitu kama " The Political Economy of Devaluation in Developing Countries "; Shivji alionyesha kuwa this guy was really bogus.
Nimejaribu kuGOOGLE hiyo ya Shivji uliyoitaja hapo juu lakini sijaona kitu lakini that said naomba unielezee CRITIQUE ya Shivji kwa malima ilikuwa kwenye maeneo yepi ya kisomi, je ilikuwa Law au Developing economics ? Na ilikuwa based on which grounds ? na kama unayo basi imwage humu ili na sisi wengine tupate kuweka arguments zetu....na haswa upande wa developing economics
Unfortunately professor Malima hakuwahi kuandika technical paper yoyote kudhihirisha umahiri wake kama mtaalamu wa uchumi, alichoacha ni technical reports kadhaa zisizokuwa na maana yoyote na ambazo hakuna hata moja ilyowahi kuwa cited.
Hili nilikuwa silijui lakini hebu nipe mfano wa paper au reports ambazo aliandika Malima ambazo hazikuwa na maana yoyote ile
Nilifikiri kuwa Prof Rweikiza Mukandala aliwahi kufanya citation za Malima hapo nyuma lakini sina hakika ila naomba unipe mwangaza katika hili
hata hivyo nadhani Malima alitia fora kwa kuvurunda.
kivipi? hebu tupe emperical evidence jinsi gani alivyo vurunda...natumai kuwa you understand economics na niko tayari kufanya mjadala na wewe kuhusu hili