Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
I think this is one of the fastest thread on JF. What does this mean?
Mwendapole,
Mimi sipendi hoja zinazoongezwa ama kupanuliwa na kuwa Ukabila. Mzee Mwanakijiji kasema kweli kabisa... Tanzania hakuna Ukabila! hiyo haina ubishi na wala hatuwezi kusema hivi vidimbwi vya watu wachache ktk kabila la Wachagga wanachukua jukumu la Wachagga wote!..Siamini kuna Ukabila nchini kama definiton ya Ukabila inavyosema ama MJJ alivyotupa.
Isipokuwa kama kweli magugu haya yapo - we have to look at the problem in hand!..
Tuondokane na mawazo ya Ukabila kabisa, pengine neno lililotumika ni zito zaidi lakini hizi pockets za washirikina hawa wachache inabidi kuzitazama vizuri kuliko kulitupilia mbali swala zima kwa sababu msemaji katamka Ukabila!
Kama Ukabila nilivyotoa maana haupo.. ni ukabila gani uliopo? Kwa maoni yangu na jinsi nilivyoelewa kama siyo ukabila niliouelezea ukabila uliopo Tanzania ni wa "idadi ya watu wa kabila moja mahali pamoja". Kama huu ndio tunauzungumzia, maswali yafuatayo hayana budi kujibiwa basi.
a. Je mtu kumuajiri mtu wa kabila lake ambaye ana uwezo na uzoefu wa kazi hiyo ni ukabila?
b. Je ni watu wangapi wa kabila moja wanaruhusiwa kuwepo kwenye wizara, idara, kitengo kimoja bila kuleta hisia za ukabila?
c. Je, mtu wa kabila lako ambaye hufahamiani naye akiomba kazi umnyime hata kama ana uwezo na uzoefu na ambaye vipaji vyake unaweza kuvitumia? je umuajiri hata kama tayari kuna mtu mwingine wa kabila lako hapo? Je umnyime nafasi hiyo kutokana na kabila lake na wewe mwenyewe kutojiona mbaguzi wa kikabila utawezaje kuing'ang'ania keko mkononi, wakati huo huo unataka uitafune?
d. Kwa vile inaonekana kuna watu wengi wa makabila haya matatu sehemu nyingi je tuwapunguze vipi idadi yao hata kama wana uwezo na uzoefu? Tusimamishe ajira zote zinazohusu Wahaya, Wanyakyusa, na Wachagga kwa muda (temporary freeze)? Je tuwape dili za kustaafu mapema ili nafasi ziwe wazi kwa watu wengine? Je tukianza kufanya hivyo tutakuwa tunatatua tatizo la ukabila au tunaliongeza?
e. Kama tulivyoonesha (na mifano ya Mswahili inashuhudia) tatizo kubwa katika ajira ni undugu na kufahamiana (nepotism na cronysm), je hili tutalitatua vipi ili ajira iwe on merit and merit alone?
Mwanakijiji,
Dhana unayotoa haina nguvu kabisa ikiwa leo hii mimi nitawachukua Wakerewe na kuweka visingizio kama hivyo!...na hakuna mtu anayebisha kuwepo kwa watu wa kabila moja sehemu moja ya kazi isipokuwa llazima tufahamu kuwa hata Ubaguzi wa rangi huko South na marekani walitumia sababu kama zako!...kinachotakiwa ni kulitazama swala lenyewe kama lilivyowekwa ubaoni sio kutumia dhana. South na Marekani walipowauliza waajiri wengi maneno machafu yaliwatoka! maneno kama weusi hawafanyi kazi, wazembe, hawana IQ na mengine kibao..hawa walikuwa waajiri walioyasema haya nje ya dhana ya baadhi viongozi na wananchi waliokuwa wakitetea hoja bila kuelewa undani wa issue nzima. Sisi hatujafika huko na wala tusiombee kufika huko kwa sababu ndio mwanzo tutakuja kugawanyika vibaya sana.
Nashukuru mkuu ES
Hawa watu mjini wametukuta na sasa wanataka kutufanya wajinga, mwinyi kama wewe kumbuka enzi hizo kuna timu ya mpira kama Nungu au cosmopolitan utamuona mikael kiongozi wa timu? hata Fat yetu kulikuwa na waswahili wenzetu utakutana na kina el-mamry,mnonji, abubakar mwilima, mohamed kassanda, n.k
sasa wamevamia hadi starehe zetu za mipira ndio utaona akina dismas ndumbalu wanagombea TFF. yaani wametuulia mashirika yetu ya umma na sasa hadi kwenye mipira wanatuvamia. huyu mikael anamjua mzee Tabu Mangara? shiraz shariff?
To deny the truth bila ushahidi wakati Mswahili katupa mifano ndani ya TRA ni kukwepa ukweli.
Penye haki siku zote ukweli hujitokeza!
Yebo yebo,
Mbali na yote haya ni uzushi kusema wakati wa Nyerere kulikuwa na Ukabila vile vile kutafuta viji sababu visivyokuwa na msingi. Haya yote yanatokana na sisi kuwa bado usingizini kiasi kwamba hata Rushwa tunapoambiwa na rais JK kuwa hata Japan, Canada na USA wana rushwa. Ni ujuha kuweka imani ya namna hiyo mbele wakati hao viongozi wa nchi hizo hawawezi kusimama na kudai nchi yao ina Rushwa kama nchini nyinginezo.. itakuwa scandal kubwa sana.
Ni hawa hawa Watanzania ambao leo tunaweka hizi sababu wakati tunalia kuajiriwa kwa wageni!... Je na wao wakituuliza kama ni kosa kumwajiri mzungu ama Mkenya mwenzake tutasema nini! Je, ni idadi gani ya wageni wanaotakiwa kuwepo kampuni moja!...
Tatizo sio kuwepo kwa Wachagga ama Wanyakyusa ktk sehemu moja ya kazi! tatizo ni kutumia kabila kama kigezo ama CV ya mtu kupata ajira!.. hakuna ushahidi wa wazi ila huwezi kuniambia ati TRA zaidi ya aslimia 50 ya waajiriwa wa TRA kupitia human resources ni Wachagga kwa sababu ndio waliokwenda omba kazi na wenye qualification.
Kuamini huku ni sawa na kuamini Wakenya ndio wanaoomba kazi maofisini kuliko Watanzania hali kazi zote zinaendeshwa na Watanzania hao hao ambao wanalalamika kuhusu utoaji wa ajira. How can they complain ikiwa hawajawahi ku apply kazi hizi?