Mkandara,
nami nimekuwa naambiwa na hawa watu wa maliasili kuwa ktk game reserve activities za uwindaji hurusiwa na sio national park, watu wa utalii wanaweza kufafanua zaidi hilo.
pm + Dua
Barabara za kuzunguka Mlima i.e. Marangu-Tarakea-Kamwanga awali ulikuwa mradi mmoja, wafadhili wakaja na zao kulingana na pesa watazo tupa na kuchagua vipande, serikali ikalazima kuigawa na kuwa Marangu-Mkuu (Mwika Kilacha inclusive)-NORAD, Mkuu-Tarakea-BADEA na Tarakea Kamwanga ni GOT. mawasiliano yanaendelea kati ya EU na GOT kufadhili ile barabara toka Hai mpaka lango jingine la kupandia Mlima. CBA sna EIAs zote zilizofanyika zaonyesha kuwa miradi yote hiyo inalipa, credits to Meghji, Mramba na Magufuli. Pm umesema kweli barabara ya mwika kilacha automatically ilifaidika kuingizwa kwani nayo ilionekana ni kiunganishi kizuri na Holili (TZ)/Taveta(Kenya).
Back to the mada.
Ukabila unaozungunzwa hapani experience/perception binafsi za watu. mfano leo nikienda kuomba kazi, nikakutana na wenzangu watano (jumla tukawa sita), nafasi iliyo wazi ni moja. Bwana mkubwa wa ile sehemu tunayoomba kazi lets say ni Mhaya na miongoni wa wasailiwa yumo mhaya. impression nitayokuwa nayo mwanzoni ni kuwa wote tulioitwa ni competent, kwa hiyo yeyote aweza chukuliwa NOW akichukuliwa mhaya picha ya kwanza itayokuja akilini mwa wengi wetu itakuwa "kwa kuwa ni mhaya mwenzake".....regardless ya kwamba Bwana mkubwa mhaya anajuana naye au hamjui. sasa je tuuite huo UKABILA?? YES & NO!
NO, why
1. wote tuko competent na mmoja wetu lazima apate regardless of his/her kabila
2. There is a possibility ya ambaye si mhaya kuchukuliwa
3. Ni haramu kumtuhumu mtu aliyepata kihalali riziki yake
YES, why
1. %ge kubwa ya panel ikiwa ni wahaya, kutakuwa na ka-roho fulani ka'yule ni wa kwetu" trust me, makabila mengine hayana aibu
2. Nguvu/influence ya bwana mkubwa na uhaya wa huo bwana mkubwa
Serikalini haya mambo yako saana both KUJUANA na UKABILA, yote hii haina budi KUPIGWA VITA.
NB: nimetumia Wahaya kwa kuwa ni moja ya kabila lilosemwa. so ktk maelezo yangu waweza ku-substitute na Mchagga au Mnyakyusa vile vile. sina bifu na kabila lolote.
Ni rahisi sana kwa mtu ku-judge, inakuwaje watu waliosomea mambo ya tax wasipate ajira na mtu mwenye BSc/BA (Ed) apewe nafasi inayohusu taxes??, huyu bw/bi anatakiwa aende kufundisha, vinginevyo abadilishe fani aende akasomee kwanza ndio aajiriwe kama ajira itakuwepo wakati huo "under competitive selection" short of that ndio hizo speculations za ukabila na kujuana zina-emerge.
Naunga mkono, kuwe na kamati huru ya ajira, na ikiwezakana tutumie consultants e.g KPMG, PriceWaterHouse (wasiingiliwe though), especially katika hizi Authorities za serikali zilizo na uwezo wa kuajiri bila kupitia utumishi. Through my experience kamti ya uajiri ya UTUMISHI are doing a very good Job!!