Ukabila Ikulu, Ujenzi, Mambo ya nje, Mipango, TRA, BoT + Ofisi nyeti za serikali

Ukabila Ikulu, Ujenzi, Mambo ya nje, Mipango, TRA, BoT + Ofisi nyeti za serikali

Am amazed by the fact that in this century one narrow minded individual would bring up this tribal topic.. just look around the countries surrounding us and that will tell you the effects of tribalism. To jog your mind if ever you are currently informed, what happend in Rwanda and more recently in Kenya. Do you by any chance foresee that in our peasefull country?. Personaly i don't coz your kinds will forever be defeated.
My advice to you... take time and learn your country's history or ask Mwanakjj to share his knowledge which ofcourse he will do freely.
 
Hakika haiwezekani utafiti ukaishia kwenye ofisi za serikali na taasisi zake ni muhimu kuangalia nyanja zote za uchumi pamoja na kutafiti namna hawa watu walivyopata ajira,sidhani kama hoja hii ina maana yoyote kama hakuna utafiti kuthibitisha upendeleo (NEPOTISM). haiwezekani ukafika ofisi furani ukakuta wanyakyusa wengi kuliko wamakonde ukalipuka kusema kuna upendeleo,nafikiri inahitajika utafiti ufanywe na matokeo ya utafiti yawekwe wazi JF ndo yajadiliwe.Kuna mtoa mada amezungumzia juu ya wafanyabiashara kuwa Wengi ni Wachagga,ni kwa kiwango gani mimi sijui lakini kuna ukweli,wachagga wapo kwenye biashara ndogo na kubwa sijui huko nani anawapendelea,tuangalie pia idadi ya watumishi majumbani tukimaliza tutoe hitimisho la kwanini kabila fulani ni bingwa kwenye fani fulani then tujadili.Vinginevyo waacheni waendelee kupeta.
 
Good day.

Nadhani ni kwamba haya makabila matatu yanaongoza kwa elimu vichwani mwao. Ni sababu za kihistoria kwanini wamesoma kuliko makabila yaliyo mengi nchini. Angalia Mazingira yao ya ardhi na hali ya hewa, vyote hivi vilisababisha wazungu wapende kuishi maeneo hayo. Mimi si mchaga, natoka katikati ya Tanzania. Ila sioni ubaya wowote wa hawa wenzetu kuwa katika sehemu nyeti. Nadhani cha msingi ni kuangalia, wanafanya kazi vipi, wana deliver? nadhani tusiangalie tu kabila, tuangalie delivery. Waingereza walisema, "first deserve, then desire" nadhani haya makabila yana deserve kuwa walipo. Kwa sisi wengine, nadhani tukaze msuli tusome, ili nasi tufikie pale walipo wenzetu.
 
Mkjj,
Kwanza ninawapa pongezi wanajambo wote kwa kukata issue!.mimi nimsomaji wa siku nyingi toka bcs lakini si mchangiaji.Lakini hii maada imenikumba hata mimi katika harakati zangu za maisha ya kazi,nilipokuwa ndani ya mfumo wa serikali
Hili swala ni gumu kwa kuangalia kwa inje,nikiwa na maana ya kuwa kama mtu si mwajiriwa wa serikali au shirika la umma lolote.
unachokisema ni sahihi kwa wakati huo,lakini kwasasa hivi makabila mengi wamesoma,lakini kwa sababu waliotangulia ni wa makabila hayo,basi kazi zitakwenda kwa kuangalia kama muombaji anatoka kwenye kabila lake au laa.hapa ninamaana hakuna usawa,hata hizo nafasi za shule zitakwenda kwa mfumo huo.kwa hiyo labda tujadili nia mbadala lakini ukweli ndiyo huo kwa mtu ambaye yupo ndani ya mfumo wa serikali unaona hili,lakini kwa mtu ambaye haupo ndani ya mfumo huo unaweza usikubaliane na mtoa hoja.Ninaomba kutoa .01%

Duuuu,
Nimesoma mchango wa Mzee Mwanakijiji ukanikuna, lakini pia mchango wa Tuipendenchiyetu naona still unazidi kuifanya mada hii inoge. Je, ni kweli hadi leo hatuna watalaam kutoka makabila mengine ambao wanauwezo na uzoefu wa kushika nafasi katika wizara na Idara tajwa? Haya tuendelee kuelimishana.
 
Sina hakika na ambacho hii mada inataka kutufundisha. Watu mko biiize kuongelea ukabila sehemu za kazi. Mimi nafikiri cha msingi ni kuwa specific. Hii mambo ya kuja hapa na generalizations, haitusaidii kutatua tatizo. Sio nia ya hata mmoja wetu aliyeelimika (narudia aliyeelimika) kushabikia ukabila at this point. Serikali inazo taratibu za kazi (from recruitment to retirement) na naamini zinafuatwa na watendaji wake. Kama yupo mwenye evidence ya sehemu au mkuu wa sehemu inayokiuka maadili na taratibu hizo, basi ni vema akaweka bayana ili afuatiliwe na achukuliwe hatua. Kama tunazungumzia uteuzi wa rais, hadi leo hajawepo rais kutoka kabila mojawapo ya yaliyotajwa hapo. Hata kama ukidai kuwa rais anapelekewa wateule, sioni kwa nini mkerewe au mmachinga au mkwere ampendelee mhaya au mchaga. Na akifanya hivyo itakuwa sio ukabila!

Nilichokiona hivi karibuni ambacho nafikiri ndio tulitakiwa tukijadili kukiondoa nilidhani ni hii weakness ya kuwateua watu na kuwapa nafasi nyeti based on kujuana na undugu/urafiki na pengine hata udini. Hata uteuzi wa juzi wa wakuu wa wilaya, kuna vichwa mle tunajua ni maji kabisa. We can only speculate ni kwa nini wamepewa hizo nafasi ila kiutendaji tunajua ni sifuri. Labda ndio watanzania wanachotaka kuona? Kwamba mradi haya makabila yasiwemo kwenye utendaji whatever potato you put in there??

Kuna mawaziri mangapi na wakurugenzi wa mashirika nyeti tunaojua fika kwamba based on their previous posts ni maboga kabisa kiutendaji? Lakini wamewekwa kuongoza! Nafikiri hii ndiyo dhambi kubwa zaidi. The worst thing ni kuwa ukishamweka mtu dizaini hiyo, hata chini yake kukiwa na mpindishaji wa taratibu (mkabila, mrushwa,etc) huyu kiazi hapo juu hatakuwa na time ya kufuatilia, maana kawekwa tu pale. Hana sifa zinazotakiwa kiutendaji.

Tumeona pia siku za hivi karibuni presha ya wanawake kujazwa kwenye sehemu nyeti. Mimi sio mbaguzi lakini nasema, as much as we want women in positions, sio tu kila mwanamke. Kama hawapo wenye sifa tutangoja mpaka wakwalifai. Hali kadhalika wafanyakazi kimakabila, kabila sio ajenda ya kwanza, bali kwalifikeshen. Kwani elimu na experience peke yake ni nini? Kama elimu haijakukomboa utakaa hapo kazini ukikusanya miaka ya experience lakini mwisho wa siku delivery itakuwa sifuri, no matter what. Lazima tubadilishe attitude zetu jamani.

Jaribu kutazama mambo kisomi kidogo. Makampuni mengi ya kigeni (private) yaliyoko hapa nchini, hayakuletwa na moja ya hayo makabila matatu. Wala wazungu wenye makampuni hayo hawakujua kuna tofauti ya makabila nchi hii, eti nani mchaga au nani mmachinga. Lakini walipofika hapa wakaanza ku-recruit (obviously based on merits), uki-study leo utaniambia kama ni wazaramo ndio waliojaa mle maana walipewa nafasi sawa! Nakuachia hilo utajaza mwenyewe.

Watu wanaojituma wana-deliver na hawako limited na mahali pa kufanyia kazi wala aina ya kazi. Ajira iwe rasmi au isiyo rasmi wataweka strategy zao na utawakuta wanapaa tu. Usidanganyike kwamba eti tukiyaondoa haya matatu serikalini basi tumeyamaliza nguvu na wakwere na wazaramo watawapita (mtazamo mfu). Wataacha wanachokifanya wataanzisha kingine watapeta, na baada ya muda tutasema tena huko walikohamia wamependelewa!

Sitaki kupoteza muda wangu kwenye hili, all I can say is that kinachoendelea sasa hivi kwenye serikali ya mkwere kuweka ndugu zake kila mahali bila kujali uwezo wao ndio mwanzo wa kifo cha maendeleo ya nchi hii. Na ndio eneo linalohitaji hatua ya haraka. Hizo ishu za wahaya, wachaga, wanyakyusa ni ishu ya kihistoria na zaidi genetical. Taratibu ziwepo na zifuatwe, kama kuna ukiukaji uripotiwe watu wawajibishwe. These discussions must be objective.
 
Mzee mwanakijiji! Well said. Labda niongeze kwamba ukweli unabakia palepale kwamba kuna vipengele vingi vinavyopelekea kuwepo kwa khali hiyo. Mimi ni kati ya wale wanaoamini kwamba 'wakati utaamua' (time will tell?) Nikiangalia mie mndengeleko, nimeoa mnyakyusa, dadangu kaolewa na mchaga. Watoto wetu mabinamu wako mwaka wa nne UDSM. Watayofanya wao (upendeleo n.k) si yakikabila bali ya kindugu, ki-ukoo. Si sahihi lakini ni alama za nyakati hizo! Sitegemei kwamba nitaamka siku moja na kukuta vyote hivyo vimekwisha la hasha (kwani hata Stalin na ubabe wake yalimshinda), ila naamini kwamba tulikotoka ni bali kuliko twendako. Nawasilisha.
 
Imefika wakati na sisi tuwe na sort of affirmative action or plan, Mfano pale Standard Chartered Bongo kama wewe sio mlaki, Temba, Kavishe, Marealle etc huwezi kupata promotion. Hali kadhalika Vodacom pia kuna Uchaga sana ebu tuangalie sifa na sio uchaga na Ukenya. Kuna sula lina nipa tabu sana hasa katika hizi appointment pia zinazofanywa na raisi na wakubwa mbona tuna wasomi wengi ni lazima wapewe wale wale jamani tuna damu mpya zinakata mba kila kukicha.
 
Imefika wakati na sisi tuwe na sort of affirmative action or plan, Mfano pale Standard Chartered Bongo kama wewe sio mlaki, Temba, Kavishe, Marealle etc huwezi kupata promotion. Hali kadhalika Vodacom pia kuna Uchaga sana ebu tuangalie sifa na sio uchaga na Ukenya. Kuna sula lina nipa tabu sana hasa katika hizi appointment pia zinazofanywa na raisi na wakubwa mbona tuna wasomi wengi ni lazima wapewe wale wale jamani tuna damu mpya zinakata mba kila kukicha.

Penye ukabila ni kuuundoa tu..jitoe mhanga na umwandikie Barua Mkulu wa Nchi kumueleza!

Mbona Vodacom ni kampuni ya wageni?hawa wazungu ni wachaga?Suala la Standard charted naweza kulicshughulikia..Fanya kunitumia PM uniambie ni nani kapandishwa kwa ukabila..Mie nitaipeleka Makao makuu yao..I have close connection na wakuu wa hiyo BAnk
 
Imefika wakati na sisi tuwe na sort of affirmative action or plan, Mfano pale Standard Chartered Bongo kama wewe sio mlaki, Temba, Kavishe, Marealle etc huwezi kupata promotion. Hali kadhalika Vodacom pia kuna Uchaga sana ebu tuangalie sifa na sio uchaga na Ukenya. Kuna sula lina nipa tabu sana hasa katika hizi appointment pia zinazofanywa na raisi na wakubwa mbona tuna wasomi wengi ni lazima wapewe wale wale jamani tuna damu mpya zinakata mba kila kukicha.

Kumbe upo Mkuu!!.......karibu tena
 
Najua hii topiki haitokuwa poplar na baadhi ya watu humu ndani na hata wenye website lakini potelea mbali

Je ni kweli wizara hizo zimejaa makabila ya Wachagga,Wanyakyusa na wahaya?

mimi nilikuwa siamini mpaka pale NILIPO ambiwa kuwa kuna UKABILA wa hali ya juuu kule Ikulu NA vile vile namba mbili kwa UKABILA ni TRA je kuna ukweli katika haya?

Japo kuna watu wanasema kuwa ni udini lakini sumu ambayo hatuko tayari hata kuijadili ni hii ya ukabila na ndio inayoturudisha nyuma je mnakubaliana nayo?

-JAMBO FORUMS WHERE WE DARE TALK OPENLY


Ndio wako wengi ila swali ujiulize ni je nafasi za kazi kigezo kikuu kimojawapo ni nini? Obviously ni elimu. Then je ni makabila gani matatu Tanzania watu wake wamesoma Tanzania? ukinijibu hilo utakuwa umemaliza mambo. Cha muhimu kawahimize nduguzo wazaramo waache kucheza bao na ngoma hela wapeleke watoto shule. NAUFUNGA MJADALA!
 
Ndio wako wengi ila swali ujiulize ni je nafasi za kazi kigezo kikuu kimojawapo ni nini? Obviously ni elimu. Then je ni makabila gani matatu Tanzania watu wake wamesoma Tanzania? ukinijibu hilo utakuwa umemaliza mambo. Cha muhimu kawahimize nduguzo wazaramo waache kucheza bao na ngoma hela wapeleke watoto shule. NAUFUNGA MJADALA!

Duh...shangazi ushakuwa Moderators siku hizi hadi uufunge Mjadala? ...au umekuwa Mke wa Moderator?....karibu JF...

Kwani wenye kucheza ngoma na bao ni wazaramo peke yao?...Unatoka wapi Mkuu ktk hii Tanganyika huru?
 
Samvulachole,
Ni vema umeanzisha mjadala huu. Wengi wa Watanzania hawapendi kusema juu ya hili ingawa ni kweli kabisa hapa kwetu Tanzania adui ukabila hajaisha hata kidogo. Hali hii hujitokeza hasa pale kunapojitokeza nafasi za kazi na wale wanaofanya "shortlisting" huzifanya kwa kuangalia ni yupi anatokea Mkoa alikotokea kutokana na kuzipitia CV. Kama wanoitwa kwenye usaili wameitwa na huyo aliyetumia Ukabila usishangae ukakuta kati ya wanaosailiwa watano basi ni mmoja tu amebandikwa kupoteza lengo juu ya kuwepo ukabila. Nani asiyejua kuwa Wachaga, Wanyakyusa na Wahaya ndiyo waliiowengi wameiona shule mapema, na huitumia nafasi hiyo kuendeleza utofauti huo kwa wengine waliochelewa kwenda shule. Kazi tunayo Watanzania na tunahitajikuyakemea waziwazi haya!!!
 
Hapo mwanakijiji umenena, hata leo ukienda vyuo vya uhasibu utakuta namba kubwa ya wanafunzi wa fani hiyo ni wachaga, kwa hiyo zikitangazwa nafasi za uhasibu uwezekano wa wachaga kupata ni mkubwa. Kwa hiyo tusilaumu sana tujibiidishe katika fani zote ili tuweze kupenyeza.Heko mwn. KJJ
 
Najua hii topiki haitokuwa poplar na baadhi ya watu humu ndani na hata wenye website lakini potelea mbali

Je ni kweli wizara hizo zimejaa makabila ya Wachagga,Wanyakyusa na wahaya?

mimi nilikuwa siamini mpaka pale NILIPO ambiwa kuwa kuna UKABILA wa hali ya juuu kule Ikulu NA vile vile namba mbili kwa UKABILA ni TRA je kuna ukweli katika haya?

Japo kuna watu wanasema kuwa ni udini lakini sumu ambayo hatuko tayari hata kuijadili ni hii ya ukabila na ndio inayoturudisha nyuma je mnakubaliana nayo?




-JAMBO FORUMS WHERE WE DARE TALK OPENLY

mkuu hapo kidogo kwenye kuambiwa ambiwa kisha nawe ukaja kuwaambia ambia watu, kwa hiyo watu watakua ni wakuambiwa ambiwa tu, mi ningeomba uje na data kamili na kama kuna nafasi walienda omba kabila zingine za kazi akapewa mchaga mwenye cheti cha darasa la saba akanyimwa kabila lingine mwenye profesional na hiyo kazi akanyimwa ndio utuwekee hapa jamvini, you sound like jealous mkuu, kuna kabila zina ishi systematically, hawako kama watanzania wengi tulivyo" tumezaliwa bahati mbaya lakini tunaishi kimakusudi'', mi nadhani tungesema israel wana ukabila kwa nini wao wanajeshi ni wengi? au marekani wanatenga watu kwa nini matajiri ni wengi kwao?, tungejaribu kuyaweka makabila hayo kama ndo kioo cha jamii,watu wajifunze namna gani wanapata maendeleo
 
hahahahaaaaaaa!! huyo jamaa kusney! mwn kjj kamata 50 kabisa!
 
Jamani ukweli wa upendeleo wa ukabila upo hii ni kwa sababu hao waliosoma yaani hayo makabila matatu ndio huwa ndio waamuzi wa nani aajiriwe, nitoe mfano halisi hapa SUA idara ya sayansi ya Udongo walitoa tangazo la kuhitaji mkufunzi msaidizi wakatoa na vigezo kuwa lazima mtu awe na shahada ya uzamili lakini hata wenye shahada wanaweza kufikiriwa.

Kwa uamuzi unaotatanisha waombaji wenye Msc walikuwa 6 na 1 mweye digrii 1 na ni mchaga na mkuu wa idara mchaga, akamteua huyo wa digrri 1, tena alikuwa anafanya kazi Tanga na chuo kigharimie usafiri wakati waombaji wengine walikuwa wanafanya kazi ndani ya idara hapahapa kama Technicians wakajiendeleza hawakuajiriwa. Je tuamini kuwa huyu mwenye digrii 1 alikuwa bora kuliko hawa wengine? Isitoshe kwa sheria huyu wa digrii 1 mpaka asomeshwe kwanza Msc ndio aanze kufundisha.

Huu ni mfano mmoja tu kati ya mingi. Ieleweke tu kuwa hata kama wanalingana kielimu waombaji sasa linakuja suala la nani anaamua yupi wa kuajiri, hapo ndipo penye matatizo, mfano ni wale wa watoto wa vigogo je ni kweli wale ndio wanafaa zaidi kuajiriwa benki kuu kuliko wengine?

Kazi kwenu!!!
 
Kama watu walikimbia shule na kwenda kuwinda watawezaje kushindana na watu walioenda shule miaka 1800?
 
Mwanakijiji tunashukuru kwa ufafanuzi, tunakushukuru kwa kutufungua ufahamu na tunashukuru kwa kumwelewesha kuwa hao wanaodaiwa kupendelewa ni watanzania si wageni ndabni ya TZ hivyo si mbaya hawawezi kuua kama wale wa north mara
 
Congrats Mwanakijiji.

Ulichokisema ni ukweli mtupu ila kuna wakati kulikuwa na kesi pale BOT ya watoto wa vigogo ambao walikuwa wame-forge vyeti na kupatiwa nafas za juu kuliko elimu zao....sina kumbukumbu nzuri ile kesi imeishia wapi... Nadhan baadhi ya maofis kuna haya matatizo
 
Back
Top Bottom