Sina hakika na ambacho hii mada inataka kutufundisha. Watu mko biiize kuongelea ukabila sehemu za kazi. Mimi nafikiri cha msingi ni kuwa specific. Hii mambo ya kuja hapa na generalizations, haitusaidii kutatua tatizo. Sio nia ya hata mmoja wetu aliyeelimika (narudia aliyeelimika) kushabikia ukabila at this point. Serikali inazo taratibu za kazi (from recruitment to retirement) na naamini zinafuatwa na watendaji wake. Kama yupo mwenye evidence ya sehemu au mkuu wa sehemu inayokiuka maadili na taratibu hizo, basi ni vema akaweka bayana ili afuatiliwe na achukuliwe hatua. Kama tunazungumzia uteuzi wa rais, hadi leo hajawepo rais kutoka kabila mojawapo ya yaliyotajwa hapo. Hata kama ukidai kuwa rais anapelekewa wateule, sioni kwa nini mkerewe au mmachinga au mkwere ampendelee mhaya au mchaga. Na akifanya hivyo itakuwa sio ukabila!
Nilichokiona hivi karibuni ambacho nafikiri ndio tulitakiwa tukijadili kukiondoa nilidhani ni hii weakness ya kuwateua watu na kuwapa nafasi nyeti based on kujuana na undugu/urafiki na pengine hata udini. Hata uteuzi wa juzi wa wakuu wa wilaya, kuna vichwa mle tunajua ni maji kabisa. We can only speculate ni kwa nini wamepewa hizo nafasi ila kiutendaji tunajua ni sifuri. Labda ndio watanzania wanachotaka kuona? Kwamba mradi haya makabila yasiwemo kwenye utendaji whatever potato you put in there??
Kuna mawaziri mangapi na wakurugenzi wa mashirika nyeti tunaojua fika kwamba based on their previous posts ni maboga kabisa kiutendaji? Lakini wamewekwa kuongoza! Nafikiri hii ndiyo dhambi kubwa zaidi. The worst thing ni kuwa ukishamweka mtu dizaini hiyo, hata chini yake kukiwa na mpindishaji wa taratibu (mkabila, mrushwa,etc) huyu kiazi hapo juu hatakuwa na time ya kufuatilia, maana kawekwa tu pale. Hana sifa zinazotakiwa kiutendaji.
Tumeona pia siku za hivi karibuni presha ya wanawake kujazwa kwenye sehemu nyeti. Mimi sio mbaguzi lakini nasema, as much as we want women in positions, sio tu kila mwanamke. Kama hawapo wenye sifa tutangoja mpaka wakwalifai. Hali kadhalika wafanyakazi kimakabila, kabila sio ajenda ya kwanza, bali kwalifikeshen. Kwani elimu na experience peke yake ni nini? Kama elimu haijakukomboa utakaa hapo kazini ukikusanya miaka ya experience lakini mwisho wa siku delivery itakuwa sifuri, no matter what. Lazima tubadilishe attitude zetu jamani.
Jaribu kutazama mambo kisomi kidogo. Makampuni mengi ya kigeni (private) yaliyoko hapa nchini, hayakuletwa na moja ya hayo makabila matatu. Wala wazungu wenye makampuni hayo hawakujua kuna tofauti ya makabila nchi hii, eti nani mchaga au nani mmachinga. Lakini walipofika hapa wakaanza ku-recruit (obviously based on merits), uki-study leo utaniambia kama ni wazaramo ndio waliojaa mle maana walipewa nafasi sawa! Nakuachia hilo utajaza mwenyewe.
Watu wanaojituma wana-deliver na hawako limited na mahali pa kufanyia kazi wala aina ya kazi. Ajira iwe rasmi au isiyo rasmi wataweka strategy zao na utawakuta wanapaa tu. Usidanganyike kwamba eti tukiyaondoa haya matatu serikalini basi tumeyamaliza nguvu na wakwere na wazaramo watawapita (mtazamo mfu). Wataacha wanachokifanya wataanzisha kingine watapeta, na baada ya muda tutasema tena huko walikohamia wamependelewa!
Sitaki kupoteza muda wangu kwenye hili, all I can say is that kinachoendelea sasa hivi kwenye serikali ya mkwere kuweka ndugu zake kila mahali bila kujali uwezo wao ndio mwanzo wa kifo cha maendeleo ya nchi hii. Na ndio eneo linalohitaji hatua ya haraka. Hizo ishu za wahaya, wachaga, wanyakyusa ni ishu ya kihistoria na zaidi genetical. Taratibu ziwepo na zifuatwe, kama kuna ukiukaji uripotiwe watu wawajibishwe. These discussions must be objective.