Mwanakijiji asante sana kwa maelezo yako marefu, mazuri na yenye kusisimua, but kwa kiasi fulani hapo niko kinyume kidogo na wewe kwa jinsi unavyojaribi kupinga kwa nguvu zote kuwa hakuna ukabila. Ukabila upo kwenye taasisi nyingi za serikali na unakuwa tena kwa kasi ya ajabu tukatae au tukubali lakini huo ndiyo ukweli.
Nakubaliana na wewe kuwa hayo makabila matatu ndiyo yaliyotangula kwenda shule na kuelimika, lakini kwa sasa kuna makabila mengi hata wazaramo wengi wameenda shule na kuelimika vizuri, lakini kilichopo sasa hivi ni kuwa haya makabila matatu kwa kuwa walitangulia kwenda shule na kushika nafasi nyingi kubwa na nyeti, imekuwa ni rahisi sana kwao kuwavuta wakwao hata kama wanasifa pungufu kuliko makabila mengine. Hiyo yote ni kwa kuwa wao ndiyo wenye mamlaka ya kuajiri pia.
Mwanakijiji wewe uko marekani japo kuwa uko karibu sana na media za bongo na kufanya utafiti mwingi but yanayoendelea ndani ya hizo taasisi sidhani kama unayafahamu kiundani zaidi. Nashauri tuache ushabiki bali twende na ukweli halisi.
Naungana na wewe rafiki yangu. Mtizamo wa miaka ya sabini kwamba haya makabila yameshika nyadhifa na nafasi kubwa katika maeneo mbalimbali ya kiutendaji kwa sababu wamesoma zaidi ni kutufumba macho ili kuendeleza ukabila. Watu wamesoma kutoka kila kabila, na nilichokiona ni kwamba watu wanaotoka kwenye makabila ambayo wengine wanadhani hawajaenda shule, wakisoma ni wanaelimika kweli na utendaji wao wa kazi ni smart, kwa kiwango kikubwa amini usiamini hawa ndio wenye uchungu na nchi na nakwambia ndio watakaoikomboa, hawana tabia ya wizi, udanganyifu, dhuluma na wanajaribu kufanya kazi katika misingi ya uwazi na ukweli. Greedy kwao sio kubwa ukilinganisha na makabila mengine. Kitu kizuri kinachonivutia zaidi kwa hawa watu wa makabila manyonge, hata elimu zao wanazipata kwa uaminifu - namaanisha sio watu wa kuiba mitihani, kununua vyeti au kudanganya viwango vya elimu. Mara nyingi wanapotafuta kazi hutafuta kwa haki sio kwa kutoa rushwa au kujuana, wale waliopata nafasi za kusoma ni vichwa vya kuotea mbali na uwezo wanao kweli. Kwa nini nasema hivyo? Kwa sababu watu wanaotoka hayo makabila jinsi hali ilivyokuwa ni kwamba ukifeli mtihani wa darasa la saba huwezi kusomeshwa private school kwa maana wazazi wasingeweza kumudu kutokana na kwamba hawana ajira, wanategemea labda zaidi kilimo, nyenzo duni na mvua ni za kubabaisha. Kwa hiyo unaona kwamba kuendelea sekondari ilikuwa ni lazima ufaulu kwa kiwango cha juu mno ili uweze kwenda government school. Wakati mwingine nilishuhudia wenzangu wengine waliokuwa na uwezo mzuri, lakini hali ya umaskini na kukosa mahitaji muhimu ya shule na ya kimwili iliwakatisha tamaa au iliwafanya pamoja na kujitahidi kote huko washindwe kufanya vizuri katika masomo yao. Hii jamii ya makabila yanyojiita yamesoma ambayo mie nimeyaona (ingawa sio jamii nzima) ila kwa kiwango kikubwa ni haya:
1. Kwa kuwa wakoloni walijenga shule katika mikoa yao kutokana na masilahi waliyokuwa wakiyafuata, nakubali kwamba kwa namna yoyote wangetangulia kusoma, maana kwingine watu walikuwa hawajui habari ya shule. Lakini isiwe ni kigezo mpaka sasa kwamba wao ni wamesoma ndio maana wapo wengi maofisini au serikalini au mahali pengine popote. Mfano: yaani ukute TRA au ikulu au wizara nyingine kwamba watu wa kabila fulani wao ni asilimia labda 80 halafu asilimia 20 ni makabila mengine kisa wamesoma kuliko wengine na kwenye hiyo fani ni wao tu! Nakataa. Shule zipo kila sehemu, watu wanasoma. Nimeshuhudia watu toka makabila mengine wakiburuza hadi kitaifa, wakiingia top ten, wakimaliza kwa kufaulu vizuri mno hizo fani vyuo vikuu hasa UDSM, halafu huwa wanaenda wapi kama hawawezi kupata hizo nafasi?
2. Nilishudia hili mara nyingi nilipokuwa sekondari watoto toka makabila yanayojiita yamesoma zaidi (sio wote) ila kwa asilimia kubwa wakisema kauli kama hizi: mie hata nisipopiga book utanikuta ofisi kali; yaani hata nikipata zero mambo yangu yatakuwa supa, kwanza hapa nasubiria tu muda nikakabidhiwe ofisi maana baba, mjomba, mama, shangazi etc., ni bosi sehemu, wewe ukifeli utaenda kufia kijijini kwenu, nani anakujua? Au mara wewe si unasoma sana kwa sababu umetumwa na kijiji - hapa walikuwa wakimaanisha kwamba kabila lenu halijasoma, kwa hiyo ni wewe tu ndiye uliyetumwa kuja kusoma kwa niaba ya kabila/kijiji. Kwa maana nyingine ndio mtizamo ambao mpaka sasa watu wengine wanao kwamba makabila mengine hayana wasomi! Wakati mwingine ilibidi ucheke. Hizo zilikuwa kauli za kawaida kuzisikia wakati nasoma O-level na A-level, na kweli nyingi zimetimia. Kuna marafiki zangu niliosoma nao, unakuta labda hakufaulu vizuri, sasa baada ya kuachana sekondari kila mtu anaelekea anakojua, then baada ya miaka mnakutana unamwuuliza ndugu yangu uko wapi siku hizi? Anakutajia ofisi kubwa, lakini ukimwuuliza rafiki yangu hivi tangu tulipoachana sekondari ulienda wapi? Hapo atakupa maelezo yasiyojitosheleza, kwa maana hiyo, hapa katikati hutajua kama alisoma au alifanyaje, kwani hata akikueleza utaona kwamba hiyo CV yake isingeweza kumpeleka mahali alipo.
3. Jambo la tatu ni sumu mbaya mno kwao, nchi na kwa ujumla katika utendaji wao. Nimeshuhudia mimi mwenyewe misimu ya kuendea kufanya mitihani ya Taifa, O-level na A-level jinsi watoto wa ama wakubwa au toka makabila yaliyosoma wakihaha kutafuta mitihani. Mara nyingi nillisikia wanafunzi wenzangu wakisema (wale niliokuwa karibu nao zaidi) nimesikia fulani katumiwa paper ya namba, phy, chem toka Dar sijui na nani yake, wameisolve jana usiku mjini au mahali pengine popote. Au wakiwa katika mood ya kujiorganize ili kujua ni namna gani wangepata paper toka kwa mwenzao yeyote ambaye ni mtoto wa mkubwa - ujue mara nyingi katika harakati kama hizi - tajiri na tajiri na maskini na maskini, wewe huwezi kujua hizo dili zao kwanza sio rafiki yao ni mtu wa dhiki tu fulltime. Kundi hili siku zote litakuwa ni kundi la dhuluma, wizi, udanganyifu na kutojiamni katika utendaji lakini likishikilia msimamo kwamba ndio limesoma zaidi.
Sasa haya kama yalikwepo na ni ya kweli, ni hatari ndio maana unaona jinsi watu wanavyoboronga kutoka ofisi ya juu kabisa serikalini mpaka chini. Wengi ni mashahidi, mitihani ambayo huwa inavuja unategemea kwamba huo mtihani anaoweza kuutoa wizarani kirahisi ni mkulima wa jembe la mkono, au mtu aliyeko TRA, ikulu au wizara nyingine yeyote? Una jibu bila shaka. Nikipata watoto nitawaambia soma kwa akili na nguvu zako zote nikiwapa kila msaada unaotakiwa lakini nitawaambia, usithubutu kudanganya kwenye mitihani, never, never and never na unapotafuta nafasi yoyote ile hakikisha umeipata kwa vigezo sahihi!
Hiyo hali ya wizi wa mitihani na kudanganya haikuishia sekondari, iliendelea mpaka vyuo vikuu. Kwa masikio na macho nimeshuhudia UDSM jinsi watu wanavyodanganya kwenye mitihani (sio wote) - walikuwa wakiita "kudesa" na ni hali ya kawaida kabisa na wengi walikuwa wakiabudu na kuisifia! Tunaelekea wapi?
Sasa niwachekeshe hapa ingawa ni jambo la kweli: Nimemaliza UDSM 2008, kuna kundi ambalo nilikuwa napenda kudiscuss nalo, halikuwa kundi la marafiki sana lakini lilikuwa kama kundi la marafiki wa kusoma pamoja. Kuna siku moja baada ya kumaliza kudiscuss somo fulani ambalo tulikuwa tunajindaa kwa ajili ya test, hao ndugu zangu wakasema sasa tuset format ya jinsi ya kukaa ili tudesane. Nikawaambia jamani kwa nini mnakuwa na mawazo kama haya? Tuna muda wa kujisomea kwa nini tusijiandae tukaenda kufanya test kihalali? Ili hali bado tuna muda? Kumbuka niliwashauri kwa upole kabisa na kwa upendo. Ndugu yangu mmojawapo akanijibu: wewe si unajifanya kichwa? Tuone sasa kama utamaliza bila kushikwa! Kushikwa/kukamtwa hapa ni aidha kufeli somo moja au zaidi, hali ikiwa mbaya unadisco! Nilimjibu kwa ujasiri kwamba, sitadesa, na nitamaliza hapa mlimani nikifaulu tu, na kabla hujamaliza chuo usipobadili hiyo tabia nitakushuhudia ukikamatwa wewe! Hakubadili tabia, aliendelea kudesa, alikamatwa akawa anaona aibu hata kuniangalia. Baadaye alinijia na kuniomba ushauri ni jinsi gani asome ili asishikwe. Kwanza kabisa nilimwambia marufuku kudesa kuanzia leo kama unataka kufaulu. Sasa tunaheshimiana sana.
Ningeweza kuongea mengi sana kuhusu waliosoma na wasiosoma lakini naona niishie hapa kwa leo. Kuna madhara makubwa sana ya kiutendaji kwa watu waliodanganya kwenye mitihani, waliopewa nafasi ambazo hata mioyo yao inawashudia kuwa hawana sifa. Haya mambo yamewafanya aidha wasijiamini, au wafanye kazi bila taaluma, au kwa kushauriwa tu na watu na kuchukua maamuzi bila ya wao kufikiria kwa makini kwa sababu huenda huo uwezo hawana kwani hawakujijenga katika misingi ya namna hiyo.