Top Thinker
Senior Member
- Sep 8, 2011
- 183
- 125
Once Again, jutikumbushie
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
tuipendenchiyetu, karibu na tunafurahi kuwa umeweza hatimaye kuamua kuchangia badala ya kuwa mtazamaji tu.
a. Katika maendeleo yote ya elimu hadi hivi sasa, Makabila hayo yamerudi nyuma au yameendelea mbele?
b. Ili kuweza kufikia uwiano, je tuamue kuyafunga breki, kwa mfano kusitisha kwa miaka mitano kuchukua wanafunzi wa elimu ya juu toka makabila hayo?
c. Tukiamua kufanya hivyo, tuhakikishe kuwa hawaendi kusoma nje ya nchi pia kwa muda huo?
d. Je, tunapopokea CV ya mtu au kumchagua mtu tukiona jina la "Kagaruki", "Mwakipesile" au "Lyimo" tuwaengue moja kwa moja?
e. Kwenye ofisi ambazo zimejaa watu wa makabila hayo tuzipangue na kuwaaingiza watu wa makabila mengine ilimradi isionekane wamejaa watu wa kabila moja?
f. Tukishaanza kufanya hivyo na tukagundua kuwa watu warefu ndio wengi zaidi, tuanze kuhakikisha watu wafupi nao wanaingizwa? tukifanya hivyo tukagundua kuwa wengi wanaofanya kazi maofisini wanatumia mikono ya kulia, tuanze kutafuta watumiaji wa mikono ya kushoto? na tukimaliza hivyo na kugundua kuwa wengi waliojariwa ni wanaume, tuwapunguze ili tuongeze wanawake? Tukishamaliza hivyo na kugundua kuwa wanawake wengi waliojariwa ni waislamu, tuwaombe wastaafu ili wawapishe wakristu? tukifanya hivyo na kugundua kuwa wakristo hao wengi ni wakatoliki tuwatake wawamegee nafasi hizo waprotestanti?.. ni jinsi gani tutasitisha zoezi hilo la kibaguzi?
embombo jilipo.Aaaah jamani ukabila wapi?? sasa tutaanza kulalamika hata mtoto wa Mnyakyusa/Mhaya/Mchaga akiwa wa kwanza darasani na somo linafundishwa na mmoja wa kabila tajwa mtasema ukabila...jamani acheni hizo huo ni USONGOMBINGOO!!!!
Well done Mkkj,
Ndugu yangu samvulachole, umeanza kujihami ati topic haitawapendeza baadhi ya wachangaiji...wewe ulitaka kila mtu akubaliane na yasemwayo hata kama ni pumba?
Taonesha wewe mwenyewe ndo mkabila ma mdini, ndo maana ukachambua hobi uliyonayo..!!!
Hayo makabila ulotaja HAKIKA kumejaa wasomi...HATA UKINUNA...! sasa ulitegemea hapo kwenu samvulachole toka alfajiri umevalia msuli wachwza bao barazani ndo ulinganishe na kule kwa walima ndizi Bk?
Wenzio wamekwenda shule, wakapata nafasi nzuri kazini kwao, wewe utabaki mhudumu na mfagizi wa ofisi tuuu>! hadi utakapoelimisha kizazi kijacho cha huko samvulachole..!
Mbona hazungumzii ukabila JWTZ ambalo limejaa Wakurya?Kuzumgumzia ukabila ni UKABURUNajua hii topiki haitokuwa poplar na baadhi ya watu humu ndani na hata wenye website lakini potelea mbali
Je ni kweli wizara hizo zimejaa makabila ya Wachagga,Wanyakyusa na wahaya?
mimi nilikuwa siamini mpaka pale NILIPO ambiwa kuwa kuna UKABILA wa hali ya juuu kule Ikulu NA vile vile namba mbili kwa UKABILA ni TRA je kuna ukweli katika haya?
Japo kuna watu wanasema kuwa ni udini lakini sumu ambayo hatuko tayari hata kuijadili ni hii ya ukabila na ndio inayoturudisha nyuma je mnakubaliana nayo?
-JAMBO FORUMS WHERE WE DARE TALK OPENLY
Mada hii inahitaji karesearch sio nadharia za tangu miaka 70s kila kitu kinawezekana jamani!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
Hakuna herufi ya V,(vyombo vinaitwa fyombo,)Wahaya (hawana' ng'ombe ,ngombe) kunyima ntu mie naona aibu somoBima ilijaa Wanyakyusa ilipokuwa inaongozwa na Nsekela na Mwaikambo. Matatizo ya Bima yalianza miaka hiyo. Kwahiyo usiwalaumu Wachaga.
Pia kuhusu hawa Wanyakyusa, tunazungumzia kabila gani? Tunazungumzia pia Waluguru na Wapogoro ambao ni ndugu zao? Wanyakyusa walitoka Morogoro na nimesikia kwamba wengi wao hata leo kule Rungwe na Mbeya wanajiita Walugulu. Wengine wanasema ni Wapogolo (nimeambiwa hakuna herufi ya "r" katika lugha ya Kinyakyusa). Lakini pia wanajiita Wanyakyusa ingawa wanasema ni Walugulu na Wapogolo. Ebu nifafanulie hapa. Hata leo kuna Wanyakyusa wengi sehemu za Morogoro ingawa wengi wao walihamia kusini magharibi sehemu za Rungwe na Malawi labda karne nyingi zilzopita.
<br /> <br />Big up mkjj! Maneno ya JKN yatabaki na yataishi. Because they talk the truth. We cannot invest on tribalism. Let's be aggressive on development issues. Ukweli utabaki kuwa pale pale, wahaya, wachagga, na wanyakyusa tumesoma na tunajua thamani ya elimu na walio wengi wako tayari na hakika wanajifunga mkanda kugharamia elimu kwa watoto. Na vijana hawanapiga kitabu kwa hasira. Akina samvulachole na tuipendenchi yetu wanachokiona ni matokeo ya kusoma/shule. Bila shule unategemea upewe kazi kisa uwiano? Hapani vigezo na vigezo ni shule; vidato au madigree. Lakini akina samvulachole wanatakiwa tu kutambua kuwa jamii nyingine mi sitaki kusema makabila, watu wanaamka! Akina mama wanauza magengeni, wanauza michicha, vitumbua, karanga n.k ili kupata fedha za kugharimia elimu kwa watoto wao. Hili ndilo jambo la maana kwamba aliyekuwa amelala sasa kaamka! Samvulachole, JIULIZE, ile jamii yenu kubakilivyo tatizo ni ukabila au? Sijui kwenu kule mtafanya nini, mnapinga kila kitu! Hamataki shule, hamtaki huduma ya maji ya bomba, hamtaki vyoo vya kisasa, hamtaki barabara sasa na hapo kuna ukabila?
samvulechole... hakuna hoja ambayo ni ngeni hapa.. madai ya makabila hayo kupendelewa hayakuanza leo! tangu mara tu baada ya uhuru kulikuwa na tuhuma hizo hizo.. so.. there is nothing there..! Hata hivyo hatari unayoweza kuleta siyo ukabila bali ubaguzi, kuwa kama mtu anatoka kwenye makabila hayo basi asipewe nafasi fulani kwa vile watu fulani wanadhani kuna ukabila! Nitakupa mfano, kuna wanasheria watatu wote ni maprofesa... kuna Prof. Mwakalindile (Sheria, uzoefu miaka 30), Prof. Mtimba (mmakua, uzoefu miaka 10, sheria), na Prof. Chanda (Mzigua, sheria uzoefu miaka 5). Assuming maeneo ya fani zao ni sawa, ceteris paribus Rais anataka kumteua mshauri wa kisheria.. nani apewe kwa haki? Wengi watasema prof. Mwakalindile! Sasa kwa kufanya hivyo hata hivyo kuna wanyakyusa wawili tayari hapo ikulu ambao wameshapata nafasi zao, je tumnyime Mwakalindile kwa vile itaonesha ukabila?
Kabla hatujafikia hapo pa kudai ukabila tujiulize: "Kwanini inaonekana kuna wasomi wengi wa makabila hayo matatu Wachaga, Wahaya, na Wanyakyusa"? Je, tupunguze wanafunzi wanaotoka kwenye makabila hayo na kuwapa nafasi watu wa makabila mengine ili kuleta uwiano (parity)? Je tukiamua kufanya hivyo hatutakuwa tunaanza ubaguzi wa kikabila?
Tarehe 9 Disemba 1968 Nyerere alitumia siku ya Jamhuri kuzungumzia "Vitu ambavyo ni lazima Tuvisahihishe", vitu ambavyo baada ya uhuru havikwenda vilivyotarajiwa. Alizungumzia ukabila; kwanza alisema hivi:
"the man who talks about tribalism being practised without having any evidence for his statement is often a man who wants to stir up tribalism. Even if that is not his purpose, the result can be just the same. People will begin to think that there is tribalism, and, once people begin to think in these terms, then tribalism has begun to enter tinto our society"
Kuhusu Wahaya, Wanyakyusa, na Wachaga kupata nafasi nyingi katika serikali, Mwalimu alisema hivi miaka karibu 30 iliyopita:
"..the work of the civil servants and people in the parastatal organizations does require education..it so happened that the Tanzanians who had the opportunity for higher education under the colonialists were mostly Wahaya, Wachagga, and Wanyakyusa. And because most of the education was provided by missionaries, most of these people are also Christians. That was our inheritance. These conditions will change, but they have not changed yet. And for these reasons, when we get rid of the Europeans who were doing responsible jobs, and give these jobs to Tanzanians, the people who get them come mostly from one or other of these three tribes".
Akaongeza pia,
"Therefore, if you ask me why Wahaya, Wachagga, and Wanyakyusa have most of the jobs which require higher education, the answer is very obvious. They were the ones who received higher education during colonial times. I'd say: investigate the position in politics where a man is not asked about his educational qualifications. Look at the Parliament, the National Executive and Central Committee of TANU, and at the Cabinet. How many Wanyakyusa, Wahaya, or Wachagga are members? You will find that perhaps there aren't any, or there are one or two. This is the truth"
kwa umahiri wake wa maneno JKN akatoboa ukweli huu
"Anyone who refuses to accept a very obvious truth like this, and says that the reason is tribalism, must provide us with the evidence for his statement. If he cannot provide any evidence, we must conclude either that he is a fool, or that he is strirring up tribalism deliberately. He is the sort of (a) person who begs work on a tribal basis, and when he is refused because he does not have the capabilities, he pretends he was refused on tribal grounds."
Akasema pia ni jukumu la serikali kusaidia sehemu ambazo bado ziko nyuma kielimu. Na alimaliza kwa kusema:
".. if a Mchagga, a Mhaya, or a Mnyakyusayoung man were refused work simply because of his tribe - when he is capable and there is no other Tanzanian with the qualifications - then we would be practising a very stupid and very evil kind of tribalism such as that which caused the establishment of Biafra. I beg you, my brothers, avoid ANYTHING WHICH COULD BRING OUR COUNTRY INTO THIS KIND OF DISGRACE" (emphasis mine)
(From: Uhuru na Maendeleo pp 76,77)
so what say you?
Mwanakijiji asante sana kwa maelezo yako marefu, mazuri na yenye kusisimua, but kwa kiasi fulani hapo niko kinyume kidogo na wewe kwa jinsi unavyojaribi kupinga kwa nguvu zote kuwa hakuna ukabila. Ukabila upo kwenye taasisi nyingi za serikali na unakuwa tena kwa kasi ya ajabu tukatae au tukubali lakini huo ndiyo ukweli.
Nakubaliana na wewe kuwa hayo makabila matatu ndiyo yaliyotangula kwenda shule na kuelimika, lakini kwa sasa kuna makabila mengi hata wazaramo wengi wameenda shule na kuelimika vizuri, lakini kilichopo sasa hivi ni kuwa haya makabila matatu kwa kuwa walitangulia kwenda shule na kushika nafasi nyingi kubwa na nyeti, imekuwa ni rahisi sana kwao kuwavuta wakwao hata kama wanasifa pungufu kuliko makabila mengine. Hiyo yote ni kwa kuwa wao ndiyo wenye mamlaka ya kuajiri pia.
Mwanakijiji wewe uko marekani japo kuwa uko karibu sana na media za bongo na kufanya utafiti mwingi but yanayoendelea ndani ya hizo taasisi sidhani kama unayafahamu kiundani zaidi. Nashauri tuache ushabiki bali twende na ukweli halisi.
Maelezo haya yamejitosheleza vyema ,umenifilisi naunga mkono hoja yako