Ukabila Ikulu, Ujenzi, Mambo ya nje, Mipango, TRA, BoT + Ofisi nyeti za serikali

Ukabila Ikulu, Ujenzi, Mambo ya nje, Mipango, TRA, BoT + Ofisi nyeti za serikali

tuipendenchiyetu, karibu na tunafurahi kuwa umeweza hatimaye kuamua kuchangia badala ya kuwa mtazamaji tu.

a. Katika maendeleo yote ya elimu hadi hivi sasa, Makabila hayo yamerudi nyuma au yameendelea mbele?

b. Ili kuweza kufikia uwiano, je tuamue kuyafunga breki, kwa mfano kusitisha kwa miaka mitano kuchukua wanafunzi wa elimu ya juu toka makabila hayo?

c. Tukiamua kufanya hivyo, tuhakikishe kuwa hawaendi kusoma nje ya nchi pia kwa muda huo?

d. Je, tunapopokea CV ya mtu au kumchagua mtu tukiona jina la "Kagaruki", "Mwakipesile" au "Lyimo" tuwaengue moja kwa moja?

e. Kwenye ofisi ambazo zimejaa watu wa makabila hayo tuzipangue na kuwaaingiza watu wa makabila mengine ilimradi isionekane wamejaa watu wa kabila moja?

f. Tukishaanza kufanya hivyo na tukagundua kuwa watu warefu ndio wengi zaidi, tuanze kuhakikisha watu wafupi nao wanaingizwa? tukifanya hivyo tukagundua kuwa wengi wanaofanya kazi maofisini wanatumia mikono ya kulia, tuanze kutafuta watumiaji wa mikono ya kushoto? na tukimaliza hivyo na kugundua kuwa wengi waliojariwa ni wanaume, tuwapunguze ili tuongeze wanawake? Tukishamaliza hivyo na kugundua kuwa wanawake wengi waliojariwa ni waislamu, tuwaombe wastaafu ili wawapishe wakristu? tukifanya hivyo na kugundua kuwa wakristo hao wengi ni wakatoliki tuwatake wawamegee nafasi hizo waprotestanti?.. ni jinsi gani tutasitisha zoezi hilo la kibaguzi?


Niliwahi kwenda kuulizia kazi ktk ofisi moja mjini aeusha, nilishangaa mkuu wa ofisi akaniuliza 'wani wewe ni mhaya', nikamwambia hapana akasema basi kama sio mhaya ondoka tu ndugu yangu. Taratiiiibu nikasepa mtoto wa kiume.......... Ni ngumu kuamini lakini hii thread ina kaukweli ambako huwezi kukatetea kwa hali historia ilivyoshape mambo. Napitapita humuhumu tu wakuuu!
 
Mkuu Ndyoko hayo maneno uliambiwa kweli ama ni katika kutaka kuonyesha wahaya ni wakabila?
 
Ndyoko,
Ili uonekana mkweli zaidi, itaje kwa jina hiyo ofisi na mhusika huyo mkuu aliekuuliza
 
Aaaah jamani ukabila wapi?? sasa tutaanza kulalamika hata mtoto wa Mnyakyusa/Mhaya/Mchaga akiwa wa kwanza darasani na somo linafundishwa na mmoja wa kabila tajwa mtasema ukabila...jamani acheni hizo huo ni USONGOMBINGOO!!!!
 
Mada hii inahitaji karesearch sio nadharia za tangu miaka 70s kila kitu kinawezekana jamani!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
TUSIRUHUSU HATA MARA MOJA KUZUNGUMZIA RANGI NA UKABILA. UHURU WETU SIO WA RANGI WALA KABILA,RAIS MSTAAFU NELSON MANDELA WA S.A ALIWAH KUSEMA "NAWACHUKIA MAKABURU WEUPE NA WEUSI" SWALA LA MSING NIKUHAKIKISHA UMOJA WETU NA UHURU NA HAKI YA ELIMU INAENDA KWA KILA MTANZANIA.

NIMEKUWA KIONGOZ NAKAMWE SIKUKUBAL UKABILA MIM NIMTANZANIA NA ASIL YANGU NI UTANZANIA NA WATOTO WANGU WATAKUWA WATANZANIA. TUSIWE WAPUMBAVU KWAKUKUBAL ONGELEA UKABILA NA UDINI HAKIKA TUTACHINJANA KAMA KUKU. MUNGU IBARIKI TANZANIA.

Amen
 
Big up mkjj! Maneno ya JKN yatabaki na yataishi. Because they talk the truth. We cannot invest on tribalism. Let's be aggressive on development issues. Ukweli utabaki kuwa pale pale, wahaya, wachagga, na wanyakyusa tumesoma na tunajua thamani ya elimu na walio wengi wako tayari na hakika wanajifunga mkanda kugharamia elimu kwa watoto. Na vijana hawanapiga kitabu kwa hasira. Akina samvulachole na tuipendenchi yetu wanachokiona ni matokeo ya kusoma/shule. Bila shule unategemea upewe kazi kisa uwiano? Hapani vigezo na vigezo ni shule; vidato au madigree. Lakini akina samvulachole wanatakiwa tu kutambua kuwa jamii nyingine mi sitaki kusema makabila, watu wanaamka! Akina mama wanauza magengeni, wanauza michicha, vitumbua, karanga n.k ili kupata fedha za kugharimia elimu kwa watoto wao. Hili ndilo jambo la maana kwamba aliyekuwa amelala sasa kaamka! Samvulachole, JIULIZE, ile jamii yenu kubakilivyo tatizo ni ukabila au? Sijui kwenu kule mtafanya nini, mnapinga kila kitu! Hamataki shule, hamtaki huduma ya maji ya bomba, hamtaki vyoo vya kisasa, hamtaki barabara sasa na hapo kuna ukabila?
 
Aaaah jamani ukabila wapi?? sasa tutaanza kulalamika hata mtoto wa Mnyakyusa/Mhaya/Mchaga akiwa wa kwanza darasani na somo linafundishwa na mmoja wa kabila tajwa mtasema ukabila...jamani acheni hizo huo ni USONGOMBINGOO!!!!
embombo jilipo.
 
Well done Mkkj,

Ndugu yangu samvulachole, umeanza kujihami ati topic haitawapendeza baadhi ya wachangaiji...wewe ulitaka kila mtu akubaliane na yasemwayo hata kama ni pumba?

Taonesha wewe mwenyewe ndo mkabila ma mdini, ndo maana ukachambua hobi uliyonayo..!!!

Hayo makabila ulotaja HAKIKA kumejaa wasomi...HATA UKINUNA...! sasa ulitegemea hapo kwenu samvulachole toka alfajiri umevalia msuli wachwza bao barazani ndo ulinganishe na kule kwa walima ndizi Bk?

Wenzio wamekwenda shule, wakapata nafasi nzuri kazini kwao, wewe utabaki mhudumu na mfagizi wa ofisi tuuu>! hadi utakapoelimisha kizazi kijacho cha huko samvulachole..!


tujaribu kujenga hoja bila lugha ya uchochezi, na isiyo harufu ya udini.
na pia kuna tatizo gani mtu kuwa na kazi ya mhudumu wa ofisi?. we hufagii kwako?. ofisi zisingekuwa zinafanyiwa usafi pangekalika?
heshimu kazi za watu.
 
Hakuna ukabila Tanzania bali kuna fursa ambazo watu wa aina fulani huzipata kutokana na juhudi za kuzitafuta na advantagewalizopata baada ya juhusi za babu zao . Leo hii ikitangazwa kazi basi hayo makabila munayotaja yatafanya asilimia sabini ya applicant na mengine mia yaliyobaki asilimia 30. Hisitoria inasema shule wapi zilianza na wapi zilikubalika na wapi walizikataa. Kwa yule anayefikiri anaeonewa aanza sasa, nenda kijijini kwenu kaelimishe watu walo baada ya miaka hamsini kutakuwa na wasomi wengi halafu mtapendeleana.
 
Najua hii topiki haitokuwa poplar na baadhi ya watu humu ndani na hata wenye website lakini potelea mbali

Je ni kweli wizara hizo zimejaa makabila ya Wachagga,Wanyakyusa na wahaya?

mimi nilikuwa siamini mpaka pale NILIPO ambiwa kuwa kuna UKABILA wa hali ya juuu kule Ikulu NA vile vile namba mbili kwa UKABILA ni TRA je kuna ukweli katika haya?

Japo kuna watu wanasema kuwa ni udini lakini sumu ambayo hatuko tayari hata kuijadili ni hii ya ukabila na ndio inayoturudisha nyuma je mnakubaliana nayo?





-JAMBO FORUMS WHERE WE DARE TALK OPENLY
Mbona hazungumzii ukabila JWTZ ambalo limejaa Wakurya?Kuzumgumzia ukabila ni UKABURU
 
Mada hii inahitaji karesearch sio nadharia za tangu miaka 70s kila kitu kinawezekana jamani!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

Fanya research ndogo hii hapa na kwa siku tatu tu, nenda pale nje ya Ikulu simama kwa mbali kidogo ili Camera zao zisikunase halafu angalia wanaoingia kwa kutumia mlango mdogo wa pembeni, fanya ku-tally waliovaa kibaragashia na wasiovaa kibaragashia ktk masaa ya kazi tu na baada ya siku tatu tuletee majibu,
 
Jamani nasisi wamakonde tunataka kazi nzuri zakisomi.tumechoka kuvuna korosho na kulinda mageti ya wazungu.
 
Bima ilijaa Wanyakyusa ilipokuwa inaongozwa na Nsekela na Mwaikambo. Matatizo ya Bima yalianza miaka hiyo. Kwahiyo usiwalaumu Wachaga.

Pia kuhusu hawa Wanyakyusa, tunazungumzia kabila gani? Tunazungumzia pia Waluguru na Wapogoro ambao ni ndugu zao? Wanyakyusa walitoka Morogoro na nimesikia kwamba wengi wao hata leo kule Rungwe na Mbeya wanajiita Walugulu. Wengine wanasema ni Wapogolo (nimeambiwa hakuna herufi ya "r" katika lugha ya Kinyakyusa). Lakini pia wanajiita Wanyakyusa ingawa wanasema ni Walugulu na Wapogolo. Ebu nifafanulie hapa. Hata leo kuna Wanyakyusa wengi sehemu za Morogoro ingawa wengi wao walihamia kusini magharibi sehemu za Rungwe na Malawi labda karne nyingi zilzopita.
Hakuna herufi ya V,(vyombo vinaitwa fyombo,)Wahaya (hawana' ng'ombe ,ngombe) kunyima ntu mie naona aibu somo
 
Big up mkjj! Maneno ya JKN yatabaki na yataishi. Because they talk the truth. We cannot invest on tribalism. Let's be aggressive on development issues. Ukweli utabaki kuwa pale pale, wahaya, wachagga, na wanyakyusa tumesoma na tunajua thamani ya elimu na walio wengi wako tayari na hakika wanajifunga mkanda kugharamia elimu kwa watoto. Na vijana hawanapiga kitabu kwa hasira. Akina samvulachole na tuipendenchi yetu wanachokiona ni matokeo ya kusoma/shule. Bila shule unategemea upewe kazi kisa uwiano? Hapani vigezo na vigezo ni shule; vidato au madigree. Lakini akina samvulachole wanatakiwa tu kutambua kuwa jamii nyingine mi sitaki kusema makabila, watu wanaamka! Akina mama wanauza magengeni, wanauza michicha, vitumbua, karanga n.k ili kupata fedha za kugharimia elimu kwa watoto wao. Hili ndilo jambo la maana kwamba aliyekuwa amelala sasa kaamka! Samvulachole, JIULIZE, ile jamii yenu kubakilivyo tatizo ni ukabila au? Sijui kwenu kule mtafanya nini, mnapinga kila kitu! Hamataki shule, hamtaki huduma ya maji ya bomba, hamtaki vyoo vya kisasa, hamtaki barabara sasa na hapo kuna ukabila?
<br /> <br />
Huu ni moja ya ubaguzi usiotakiwa,kudharau kazi za wengine wakati hata ulaya na marekani kuna wafagizi,wazibua vyoo na hata wazoa taka mitaani so brother acha dharau.
 
Maelezo haya yamejitosheleza vyema ,umenifilisi naunga mkono hoja yako
samvulechole... hakuna hoja ambayo ni ngeni hapa.. madai ya makabila hayo kupendelewa hayakuanza leo! tangu mara tu baada ya uhuru kulikuwa na tuhuma hizo hizo.. so.. there is nothing there..! Hata hivyo hatari unayoweza kuleta siyo ukabila bali ubaguzi, kuwa kama mtu anatoka kwenye makabila hayo basi asipewe nafasi fulani kwa vile watu fulani wanadhani kuna ukabila! Nitakupa mfano, kuna wanasheria watatu wote ni maprofesa... kuna Prof. Mwakalindile (Sheria, uzoefu miaka 30), Prof. Mtimba (mmakua, uzoefu miaka 10, sheria), na Prof. Chanda (Mzigua, sheria uzoefu miaka 5). Assuming maeneo ya fani zao ni sawa, ceteris paribus Rais anataka kumteua mshauri wa kisheria.. nani apewe kwa haki? Wengi watasema prof. Mwakalindile! Sasa kwa kufanya hivyo hata hivyo kuna wanyakyusa wawili tayari hapo ikulu ambao wameshapata nafasi zao, je tumnyime Mwakalindile kwa vile itaonesha ukabila?

Kabla hatujafikia hapo pa kudai ukabila tujiulize: "Kwanini inaonekana kuna wasomi wengi wa makabila hayo matatu Wachaga, Wahaya, na Wanyakyusa"? Je, tupunguze wanafunzi wanaotoka kwenye makabila hayo na kuwapa nafasi watu wa makabila mengine ili kuleta uwiano (parity)? Je tukiamua kufanya hivyo hatutakuwa tunaanza ubaguzi wa kikabila?

Tarehe 9 Disemba 1968 Nyerere alitumia siku ya Jamhuri kuzungumzia "Vitu ambavyo ni lazima Tuvisahihishe", vitu ambavyo baada ya uhuru havikwenda vilivyotarajiwa. Alizungumzia ukabila; kwanza alisema hivi:

"the man who talks about tribalism being practised without having any evidence for his statement is often a man who wants to stir up tribalism. Even if that is not his purpose, the result can be just the same. People will begin to think that there is tribalism, and, once people begin to think in these terms, then tribalism has begun to enter tinto our society"

Kuhusu Wahaya, Wanyakyusa, na Wachaga kupata nafasi nyingi katika serikali, Mwalimu alisema hivi miaka karibu 30 iliyopita:

"..the work of the civil servants and people in the parastatal organizations does require education..it so happened that the Tanzanians who had the opportunity for higher education under the colonialists were mostly Wahaya, Wachagga, and Wanyakyusa. And because most of the education was provided by missionaries, most of these people are also Christians. That was our inheritance. These conditions will change, but they have not changed yet. And for these reasons, when we get rid of the Europeans who were doing responsible jobs, and give these jobs to Tanzanians, the people who get them come mostly from one or other of these three tribes".

Akaongeza pia,

"Therefore, if you ask me why Wahaya, Wachagga, and Wanyakyusa have most of the jobs which require higher education, the answer is very obvious. They were the ones who received higher education during colonial times. I'd say: investigate the position in politics where a man is not asked about his educational qualifications. Look at the Parliament, the National Executive and Central Committee of TANU, and at the Cabinet. How many Wanyakyusa, Wahaya, or Wachagga are members? You will find that perhaps there aren't any, or there are one or two. This is the truth"

kwa umahiri wake wa maneno JKN akatoboa ukweli huu

"Anyone who refuses to accept a very obvious truth like this, and says that the reason is tribalism, must provide us with the evidence for his statement. If he cannot provide any evidence, we must conclude either that he is a fool, or that he is strirring up tribalism deliberately. He is the sort of (a) person who begs work on a tribal basis, and when he is refused because he does not have the capabilities, he pretends he was refused on tribal grounds."

Akasema pia ni jukumu la serikali kusaidia sehemu ambazo bado ziko nyuma kielimu. Na alimaliza kwa kusema:

".. if a Mchagga, a Mhaya, or a Mnyakyusayoung man were refused work simply because of his tribe - when he is capable and there is no other Tanzanian with the qualifications - then we would be practising a very stupid and very evil kind of tribalism such as that which caused the establishment of Biafra. I beg you, my brothers, avoid ANYTHING WHICH COULD BRING OUR COUNTRY INTO THIS KIND OF DISGRACE" (emphasis mine)
(From: Uhuru na Maendeleo pp 76,77)

so what say you?
 
Mwanakijiji asante sana kwa maelezo yako marefu, mazuri na yenye kusisimua, but kwa kiasi fulani hapo niko kinyume kidogo na wewe kwa jinsi unavyojaribi kupinga kwa nguvu zote kuwa hakuna ukabila. Ukabila upo kwenye taasisi nyingi za serikali na unakuwa tena kwa kasi ya ajabu tukatae au tukubali lakini huo ndiyo ukweli.

Nakubaliana na wewe kuwa hayo makabila matatu ndiyo yaliyotangula kwenda shule na kuelimika, lakini kwa sasa kuna makabila mengi hata wazaramo wengi wameenda shule na kuelimika vizuri, lakini kilichopo sasa hivi ni kuwa haya makabila matatu kwa kuwa walitangulia kwenda shule na kushika nafasi nyingi kubwa na nyeti, imekuwa ni rahisi sana kwao kuwavuta wakwao hata kama wanasifa pungufu kuliko makabila mengine. Hiyo yote ni kwa kuwa wao ndiyo wenye mamlaka ya kuajiri pia.

Mwanakijiji wewe uko marekani japo kuwa uko karibu sana na media za bongo na kufanya utafiti mwingi but yanayoendelea ndani ya hizo taasisi sidhani kama unayafahamu kiundani zaidi. Nashauri tuache ushabiki bali twende na ukweli halisi.

Naungana na wewe rafiki yangu. Mtizamo wa miaka ya sabini kwamba haya makabila yameshika nyadhifa na nafasi kubwa katika maeneo mbalimbali ya kiutendaji kwa sababu wamesoma zaidi ni kutufumba macho ili kuendeleza ukabila. Watu wamesoma kutoka kila kabila, na nilichokiona ni kwamba watu wanaotoka kwenye makabila ambayo wengine wanadhani hawajaenda shule, wakisoma ni wanaelimika kweli na utendaji wao wa kazi ni smart, kwa kiwango kikubwa amini usiamini hawa ndio wenye uchungu na nchi na nakwambia ndio watakaoikomboa, hawana tabia ya wizi, udanganyifu, dhuluma na wanajaribu kufanya kazi katika misingi ya uwazi na ukweli. Greedy kwao sio kubwa ukilinganisha na makabila mengine. Kitu kizuri kinachonivutia zaidi kwa hawa watu wa makabila manyonge, hata elimu zao wanazipata kwa uaminifu - namaanisha sio watu wa kuiba mitihani, kununua vyeti au kudanganya viwango vya elimu. Mara nyingi wanapotafuta kazi hutafuta kwa haki sio kwa kutoa rushwa au kujuana, wale waliopata nafasi za kusoma ni vichwa vya kuotea mbali na uwezo wanao kweli. Kwa nini nasema hivyo? Kwa sababu watu wanaotoka hayo makabila jinsi hali ilivyokuwa ni kwamba ukifeli mtihani wa darasa la saba huwezi kusomeshwa private school kwa maana wazazi wasingeweza kumudu kutokana na kwamba hawana ajira, wanategemea labda zaidi kilimo, nyenzo duni na mvua ni za kubabaisha. Kwa hiyo unaona kwamba kuendelea sekondari ilikuwa ni lazima ufaulu kwa kiwango cha juu mno ili uweze kwenda government school. Wakati mwingine nilishuhudia wenzangu wengine waliokuwa na uwezo mzuri, lakini hali ya umaskini na kukosa mahitaji muhimu ya shule na ya kimwili iliwakatisha tamaa au iliwafanya pamoja na kujitahidi kote huko washindwe kufanya vizuri katika masomo yao. Hii jamii ya makabila yanyojiita yamesoma ambayo mie nimeyaona (ingawa sio jamii nzima) ila kwa kiwango kikubwa ni haya:

1. Kwa kuwa wakoloni walijenga shule katika mikoa yao kutokana na masilahi waliyokuwa wakiyafuata, nakubali kwamba kwa namna yoyote wangetangulia kusoma, maana kwingine watu walikuwa hawajui habari ya shule. Lakini isiwe ni kigezo mpaka sasa kwamba wao ni wamesoma ndio maana wapo wengi maofisini au serikalini au mahali pengine popote. Mfano: yaani ukute TRA au ikulu au wizara nyingine kwamba watu wa kabila fulani wao ni asilimia labda 80 halafu asilimia 20 ni makabila mengine kisa wamesoma kuliko wengine na kwenye hiyo fani ni wao tu! Nakataa. Shule zipo kila sehemu, watu wanasoma. Nimeshuhudia watu toka makabila mengine wakiburuza hadi kitaifa, wakiingia top ten, wakimaliza kwa kufaulu vizuri mno hizo fani vyuo vikuu hasa UDSM, halafu huwa wanaenda wapi kama hawawezi kupata hizo nafasi?

2. Nilishudia hili mara nyingi nilipokuwa sekondari watoto toka makabila yanayojiita yamesoma zaidi (sio wote) ila kwa asilimia kubwa wakisema kauli kama hizi: mie hata nisipopiga book utanikuta ofisi kali; yaani hata nikipata zero mambo yangu yatakuwa supa, kwanza hapa nasubiria tu muda nikakabidhiwe ofisi maana baba, mjomba, mama, shangazi etc., ni bosi sehemu, wewe ukifeli utaenda kufia kijijini kwenu, nani anakujua? Au mara wewe si unasoma sana kwa sababu umetumwa na kijiji - hapa walikuwa wakimaanisha kwamba kabila lenu halijasoma, kwa hiyo ni wewe tu ndiye uliyetumwa kuja kusoma kwa niaba ya kabila/kijiji. Kwa maana nyingine ndio mtizamo ambao mpaka sasa watu wengine wanao kwamba makabila mengine hayana wasomi! Wakati mwingine ilibidi ucheke. Hizo zilikuwa kauli za kawaida kuzisikia wakati nasoma O-level na A-level, na kweli nyingi zimetimia. Kuna marafiki zangu niliosoma nao, unakuta labda hakufaulu vizuri, sasa baada ya kuachana sekondari kila mtu anaelekea anakojua, then baada ya miaka mnakutana unamwuuliza ndugu yangu uko wapi siku hizi? Anakutajia ofisi kubwa, lakini ukimwuuliza rafiki yangu hivi tangu tulipoachana sekondari ulienda wapi? Hapo atakupa maelezo yasiyojitosheleza, kwa maana hiyo, hapa katikati hutajua kama alisoma au alifanyaje, kwani hata akikueleza utaona kwamba hiyo CV yake isingeweza kumpeleka mahali alipo.

3. Jambo la tatu ni sumu mbaya mno kwao, nchi na kwa ujumla katika utendaji wao. Nimeshuhudia mimi mwenyewe misimu ya kuendea kufanya mitihani ya Taifa, O-level na A-level jinsi watoto wa ama wakubwa au toka makabila yaliyosoma wakihaha kutafuta mitihani. Mara nyingi nillisikia wanafunzi wenzangu wakisema (wale niliokuwa karibu nao zaidi) nimesikia fulani katumiwa paper ya namba, phy, chem toka Dar sijui na nani yake, wameisolve jana usiku mjini au mahali pengine popote. Au wakiwa katika mood ya kujiorganize ili kujua ni namna gani wangepata paper toka kwa mwenzao yeyote ambaye ni mtoto wa mkubwa - ujue mara nyingi katika harakati kama hizi - tajiri na tajiri na maskini na maskini, wewe huwezi kujua hizo dili zao kwanza sio rafiki yao ni mtu wa dhiki tu fulltime. Kundi hili siku zote litakuwa ni kundi la dhuluma, wizi, udanganyifu na kutojiamni katika utendaji lakini likishikilia msimamo kwamba ndio limesoma zaidi.

Sasa haya kama yalikwepo na ni ya kweli, ni hatari ndio maana unaona jinsi watu wanavyoboronga kutoka ofisi ya juu kabisa serikalini mpaka chini. Wengi ni mashahidi, mitihani ambayo huwa inavuja unategemea kwamba huo mtihani anaoweza kuutoa wizarani kirahisi ni mkulima wa jembe la mkono, au mtu aliyeko TRA, ikulu au wizara nyingine yeyote? Una jibu bila shaka. Nikipata watoto nitawaambia soma kwa akili na nguvu zako zote nikiwapa kila msaada unaotakiwa lakini nitawaambia, usithubutu kudanganya kwenye mitihani, never, never and never na unapotafuta nafasi yoyote ile hakikisha umeipata kwa vigezo sahihi!

Hiyo hali ya wizi wa mitihani na kudanganya haikuishia sekondari, iliendelea mpaka vyuo vikuu. Kwa masikio na macho nimeshuhudia UDSM jinsi watu wanavyodanganya kwenye mitihani (sio wote) - walikuwa wakiita "kudesa" na ni hali ya kawaida kabisa na wengi walikuwa wakiabudu na kuisifia! Tunaelekea wapi?

Sasa niwachekeshe hapa ingawa ni jambo la kweli: Nimemaliza UDSM 2008, kuna kundi ambalo nilikuwa napenda kudiscuss nalo, halikuwa kundi la marafiki sana lakini lilikuwa kama kundi la marafiki wa kusoma pamoja. Kuna siku moja baada ya kumaliza kudiscuss somo fulani ambalo tulikuwa tunajindaa kwa ajili ya test, hao ndugu zangu wakasema sasa tuset format ya jinsi ya kukaa ili tudesane. Nikawaambia jamani kwa nini mnakuwa na mawazo kama haya? Tuna muda wa kujisomea kwa nini tusijiandae tukaenda kufanya test kihalali? Ili hali bado tuna muda? Kumbuka niliwashauri kwa upole kabisa na kwa upendo. Ndugu yangu mmojawapo akanijibu: wewe si unajifanya kichwa? Tuone sasa kama utamaliza bila kushikwa! Kushikwa/kukamtwa hapa ni aidha kufeli somo moja au zaidi, hali ikiwa mbaya unadisco! Nilimjibu kwa ujasiri kwamba, sitadesa, na nitamaliza hapa mlimani nikifaulu tu, na kabla hujamaliza chuo usipobadili hiyo tabia nitakushuhudia ukikamatwa wewe! Hakubadili tabia, aliendelea kudesa, alikamatwa akawa anaona aibu hata kuniangalia. Baadaye alinijia na kuniomba ushauri ni jinsi gani asome ili asishikwe. Kwanza kabisa nilimwambia marufuku kudesa kuanzia leo kama unataka kufaulu. Sasa tunaheshimiana sana.

Ningeweza kuongea mengi sana kuhusu waliosoma na wasiosoma lakini naona niishie hapa kwa leo. Kuna madhara makubwa sana ya kiutendaji kwa watu waliodanganya kwenye mitihani, waliopewa nafasi ambazo hata mioyo yao inawashudia kuwa hawana sifa. Haya mambo yamewafanya aidha wasijiamini, au wafanye kazi bila taaluma, au kwa kushauriwa tu na watu na kuchukua maamuzi bila ya wao kufikiria kwa makini kwa sababu huenda huo uwezo hawana kwani hawakujijenga katika misingi ya namna hiyo.
 
Maelezo haya yamejitosheleza vyema ,umenifilisi naunga mkono hoja yako

Mzee mwanakijiji na Mwakalinga. Msimtumie Nyerere kuhalalisha uovu na dhuluma. Mambo hayo aliyoongea Nyerere miaka mingi iliyopita, na kwa huo muda alikuwa sahihi tena huenda hata kwa asilimia 100.

Ni sawa ni hayo makabila ndio yaliyokuwa yamesoma kwa hisani ya ukoloni. Lakini usiichukue hiyo hoja miaka 30 au 40 iliyopita au zaidi ukatetea hali halisi tunayoiona sasa. Unanikumbusha, kuna watu walikumbwa na kashfa za wizi, dhuluma na uovu mwingine mwingi katika serikali yetu wengine walisimama kidete na kuwatetea kwamba ni wasafi lakini baadaye waliumbuka. Tanzania sasa hivi ukiwauliza viongozi wetu kuhusu nidhamu ya uongozi watakuambia wao ndio wanafanya vizuri kuliko nchi yoyote ile duniani - yaani hakuna rushwa, wizi, dhuluma na uonevu, nchi ina amani na demokrasia ya juu kabisa, yaani hayo majibu usishangae kuyasikia!

Makabila hayo yalitangulia kusoma, sikatai, yana wasomi wengi sikatai! Sasa hili la wizara fulani au taasisi fulani kabila moja tu ni asilimia 90, makabila mengine 0.1%, 0, -1 etc kwa kigezo hichohicho cha usomi, halafu mara zote tunawaona wanavurunda, ati makabila mengine sijui yanafika 150+ yasiwe kabisa hata na mtu mmoja! Hilo kama lipo nakataa, sio kigezo cha usomi tena ila ni vigezo vingine! Yaani unataka kuniambia hawa watu wanaograduate kuanzia miaka ya 1990 wote ni kutoka makabila matatu tu? Kuna thread yangu nyingine nimeiandika from experience kuhusu hoja hii, ukiisoma unaweza kuona evolution ya uovu ambao baadaye utaitandika Tanzania.

Sijui usomi nao watu wanauchukuliaje? Maana yake hasa ni nini, kwamba ulionekana ukiingia madarasani miaka fulani? Kuna uwezekano hapo ndiko tunapohitilafiana!

Potelea mbali, kama watu wa hayo makabila ni kweli wamesoma, na wameshika nyazifa kubwa kitaifa, wafanye mambo yanayotushawishi kweli ni wasomi, maana Tanzania hali yake ni mbaya kila eneo, sasa watumie usomi kuinusuru - sijui kama hilo linawezekana.

Sitegemei msomi kufanya mambo yanayoiumiza nchi yake.
 
Back
Top Bottom