Ukabila Ikulu, Ujenzi, Mambo ya nje, Mipango, TRA, BoT + Ofisi nyeti za serikali

 
SIKU hizi watu wengi wanawabatiza na kuregistre watoto shule kwa kutumia majina ambayo hayana tribal indication mfano RICHARD SIMON au MASOOD KHAMIS kukwepa tribal vitimiztion ambayo kwa sasa tukubali tukate ipo tena sana,mtu akiona jina mfano Richard Kagaruki hata kwenye short list hawekwi au Moses Otieno-anajua Jaluo,Moses Masanja-anajua Msukuma,Edwin Atupele-Anajua Mnyakyusa,Moses Mkumbo-anajua Manyaturu,Moses Ngonyani-anajua Mungoni,Moses Chubwa anajua Muha,Moses Kapele-anajua Mfipa,Moses Tarimo anajua Mchaga etc etc,ili kuwanusuru watoto wenu na any future victimization avoid kutumia majina yenye tribal indication wakati unawa register shule
 

Nimefuatilia sana hizo wizara zilizotajwa kuwa zinaoongoza kwa ukabila, lakni sijaona Wizara ya mali asili, na utalii hususan TANAPA
Sijaona NSSF ikitajwa na BOT. Huko nako wamejaa wahaya, wachaga na wanyakusa?

Nawasilisha.


Before you judge others, start with yourself
 

Nakubali ndiyo hali halisi sasa!
 
Tangazo lilisomeka "HAKUNA KAZI"
By Utawala-
chini yake likasomeka "IMBOMBO ILIPO"
 
Tufichue hayo maovu ili yakome kwa wahusika kuona aibu wakiwekwa hadharani.
 

kama huamini kuwa kuna makabila yameenda skuli kuliko nyie hebu fanya utafiti wako kwa wachaga na wahaya.at least utajua ukweli
 
Ukabila upo sana kwenye kupiga simu wengine inasema not reachable hasa sisi
 
Hongera kwa ufafanuzi huo ili watu waelewe tulipotoka kihistoria na mabo jinsi yalivyo hiv sasa
 
kama huamini kuwa kuna makabila yameenda skuli kuliko nyie hebu fanya utafiti wako kwa wachaga na wahaya.at least utajua ukweli

not now,kwa karne iliyopita sawa!!Now days kuna muamko wa elimu every part of our country!!lazima tukubaliane tu ukweli ukabila upo sana,kibaya zaidi hadi kwenye sekta binafsi kama benki n.k
 
Mbona ni jambo la kawaida ndani ya nchi hii swala la ukabila kazini????????? ANGALIA IDARA YA MAHAKAMA....MAHAKIMU WAFAWIDHI NI WAHAYA NA WACHAGGA PIA UONGOZI WA JUU WAHAYA KIBAO.....WASAJILI NA HATA MA ACCOUNTANTS, MAMBO YA AJABU SANA TUACHE HAYA TUFUATE SIFA NA UWAJIBIKAJI......
 
Ni kweli we hv to admit hawa jamaa walitutangulia na wapo wengi wenye shule in comparison with Makabila mengine na ndo tayari wapo kw system hivyo ni ngumu kufikia uwiano ulio sawa ukizingatia yako makabila zaidi ya 120 hapa nyumbani,so lets take it az a challenge tuwapeleke wanetu shule ili huko mbeleni na wanetu wasiishie kulalamika.. Thats my take
 
Hayo makabila wamissionary walinvest uko na ndo maana wameenda shule vya kutosha!

Kuna mtu akanidokeza kula hao ni wala ndizi na kuna association kati ya ulaji wa ndizi na AKILI ingawa bado natafiti nkipata majibu ntashare na wana jamvi.

So habari ndo iyo alafu iyo mijitu ikiwa madarakani inajiamini na uwezo wa kufanya maamuzi magumu wanao wapo waliodiriki ata kupingana na JK enzi izo.IN UJASIRI WA HALI YA JUU maana JK alikuwa anatisha!
 
Unapozungumzia ukabila unatumia vigezo gani?

Kama utasema Wachaga ni wengi,na wakati huo wewe ni unatokea katika kabila ambalo ni dogo au unatokea katika kabila ambalo watu wake wamechelewa kupata elimu mapema.

Tukizungumzia ukabila tutazame vitu 2. Kwanza ni ukubwa wa kabila husika. Pili ni elimu kama watu wengi katika kabila hilo wamepata.
Sasa ukizungumzia makabila kama Wachaga au Wanyakyusa na hata Wasukuma;utaona kuwa makabila hayo ndio makabila makubwa,kwa maana kuwa yana idadi kubwa ya watu.

Pili ukizungumzia upande wa elimu,utaona kuwa mkoa wa kilimanjaro hususani maeneo wanayotokea Wachaga utakuta elimu ilichukua nafasi tangu kipindi kirefu hususani kabla na hata baada ya kupata uhuru.
 

Wachangiaji umu jamvini, mmeshawahi kuchukua takwimu darasani hasa vyuoni, Law, bussiness, education, engineering na etc watu wa kwenu mnaobaguliwa mlikuwa wangapi?. Halafu njoo na ukabila ambao hata mzazi gani ampaye nyoka mwanaye aombaye samaki, na mwenye nacho huong.....
 
Ukabila upo sehemu nyingi na utaendelea kuwepo kwa vile watu wenye mitazamo chanya ya kuuondoa wanazidi kwisha. Kizazi hiki na vijavyo ndiyo vyenye majukumu ya kusema HAPANA kwa kila aina ya kubaguana kwa kipato,kidini, kikabila, rangi, jinsia n.k. Tukitaka tutaje kila sehemu na maovu yake ya kibaguzi Tanzania imechafuka kuanzia Serikalini, Taasisi za Umma na Sekta binafsi!
 
Ndugu mleta mada,ata mimi mwanzoni nilifikiria hivyo hadi nilipofanya utafiti na kugundua yafuatayo:
1.Hiyo mikoa yote uliyoitaja ni maarufu kwa kilimo cha kahawa,wakoloni walipokuja walikuwa wahitaji kahawa mno,lakini wenyeji wa mikoa hiyo hawakuwa tayari kulima kwa kiwango walichotaka wakoloni,matokeo yake wakoloni wakaweka vivutio vya kuwafanya natives wawe na mwamuko wa kulima cash crops ili wapate fedha,moja wapo ya kivutio ilikuwa ni kufungua shule za nguvu zitakazovutia wakulima kupeleka watoto wao na hivyo kuitaji fedha na kwingineko mkoa wa Kagera,mtot wa mkulima wa kahawa alikuwa analipa ada nafuu na wakati mwingine anasomeshwa na chama cha ushirika,matokeo ya hii attitude ya quid pro quo watu wa mikoa hii walikuwa na hamas ya kusoma sana na hata kufikia mashindo ya mzazi gani watoto wake wamesoma zaidi,hii ni tofauti na mikoa mingine kama Kigoma ambayo wakoloni walitaka iwe labour reserve -sehemu ya kupata vibarua na manamba na kwa makusudi kabisa hawakutaka wala ku encourage wenyeji wa mikoa ya labour reserve kwenda shule kwani kama wangesoma wasingekubali kuwa manamba.hali hii iliendelea hadi late 60s baba wa taifa alipoingila kati na kufanay juhudi za makusudi kudidimiza elimu na maendeleo kwenye mikoa iliyokuwa imetangulia na kuinua iliyokuwa nyuma,japo haikusaidia sana lakini ilipunguza gap ambalo ndilo unalozungumzia,mikoa iliyokuwa nyuma ilipewa pass mark ndogo sana na ufaulu kwenda sekondari ulikuwa raisi sana na mikoa iliyokuwa mbele iliwekewa pass mark kubwa ili wanafunzi wengi wasiende sekondari.Kama kuna mfuatiliaji iki ni kile kipindi amabcho watu wa mikoa hiyo iliyokuwa mbele waliokuwa wanaishi kwenye mikoa iliyokuwa na pass mark ndogo walikuwa wanachukua watoto hata wasio na undugu nao na kuwapeleka kumalizia daras la saba kwenye mikoa yenye pass mark ndogo na hivyo ku-defeat purpose ya Goverment kwa kiasi fulani.
 

Mkuu una maana gani kwa kusema wamejaa! Yaani wamewekwa pale bila SIFA zaidi ya UKABILA-Watanzania tumebobea katika fani za kutunga porojo na uzushi.
 

Mswahili umemaliza
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…