Yebo yebo,
Mbali na yote haya ni uzushi kusema wakati wa Nyerere kulikuwa na Ukabila vile vile kutafuta viji sababu visivyokuwa na msingi. Haya yote yanatokana na sisi kuwa bado usingizini kiasi kwamba hata Rushwa tunapoambiwa na rais JK kuwa hata Japan, Canada na USA wana rushwa. Ni ujuha kuweka imani ya namna hiyo mbele wakati hao viongozi wa nchi hizo hawawezi kusimama na kudai nchi yao ina Rushwa kama nchini nyinginezo.. itakuwa scandal kubwa sana.
Bob,
Napo sijakuelewa..tafadhali fananua kidogo uhusiano wa mfano wa rushwa na ukabila.
Ni hawa hawa Watanzania ambao leo tunaweka hizi sababu wakati tunalia kuajiriwa kwa wageni!... Je na wao wakituuliza kama ni kosa kumwajiri mzungu ama Mkenya mwenzake tutasema nini! Je, ni idadi gani ya wageni wanaotakiwa kuwepo kampuni moja!...
Hapa kwenye wageni ni upande mwingine tofauti kabisa maana hawa jamaa kwanza wanatakiwa kuomba kibali cha kufanya kazi Tz. Sasa iwapo kuna mfano wahindi 100 ambao wana elimu ya juu sana na uzoefu wa kazi za udaktari...serikali imekubali kuwapa vibali vya kufanya kazi Tanzania mimi sioni kwa nini wasipewe kazi kama watanzania wenye sifa hizo hawapo.
Dunia imebadilika leo hii sio tena wewe ni kabila, raia wa wapi au rangi yako...ni zaidi nini unacho...angalia Football ya Uingereza ilivyoawaliwa na wageni mfano mzuri timu ya Arsenal. Angalia pia USA kwenye fani ya udaktari jinsi wageni walivyoenda kwenye remote areas kuwa madaktari huko kwa sababu wazawa hawataki kukaa humo. Elimu na Uzoefu viwe vigezo vya kwanza, zaidi ya hapo ni siasa ambazo hazina nafasi katika dunia ya utandawazi.
Tatizo sio kuwepo kwa Wachagga ama Wanyakyusa ktk sehemu moja ya kazi! tatizo ni kutumia kabila kama kigezo ama CV ya mtu kupata ajira!.. hakuna ushahidi wa wazi ila huwezi kuniambia ati TRA zaidi ya aslimia 50 ya waajiriwa wa TRA kupitia human resources ni Wachagga kwa sababu ndio waliokwenda omba kazi na wenye qualification.
Ikifikia wakati idara moja ya umma kuwa na 50% ya wafanyakazi wa kabila moja basi tujijue tuko kwenye matatizo makubwa sana. Ningependa kuamini hatujafikia huo.
Kuamini huku ni sawa na kuamini Wakenya ndio wanaoomba kazi maofisini kuliko Watanzania hali kazi zote zinaendeshwa na Watanzania hao hao ambao wanalalamika kuhusu utoaji wa ajira. How can they complain ikiwa hawajawahi ku apply kazi hizi?
Mimi sitashangaa kwa watanzania kulalamika kwa hili...watanzania tuna desturi ya kulalamika. Huo ni ukweli wa wazi. Nitakupa mfano: kuna mkurugenzi mmoja alistaafu kazi, akaanza kufuatilia mafao yake...baada ya kupingwa danadana kama ilivyo desturi maofisi yetu ya serikali akaamua kwenda kuanza kulalamika. Wafanyakazi wenzake wa zamani wakabaki kumsema pembeni, "yeye si alikuwa mkurugenzi hapa mbona hakubadili hizi taratibu, leo ndio anaona taratibu ni nyingi na ndefu zisizo na maana..??!!!"
Nikija kwenye hoja yako Bob, utakubaliana na mimi kuwa asilimia kubwa sasa ya wahitimu wetu kutoka katika vyuo vyetu vya juu leo hii wanababaika kuandika Cv...?? Sasa tukija kwenye uzoefu...mfano fani ya Marketing...hebu niambie nchi yetu Tanzania miaka ya 1980 mpaka mid 1990's kulikuwa na Marketing gani. Hebu muweke mtanzania huyu na mkenya aliyesoma kwao miaka hiyo uone kama watakuwa level moja.
Haitoshi tu kusema tu kuwa tuajiri watanzania wenzetu. Ni lazima tuangalie chimbuko na mikakati ya muda mrefu ya kutafuta ufumbuzi ikiwa na pamoja kuinua elimu yetu. Kwa kiasi kikubwa kulinda masoko ya ndani kwenye dunia ya utandawazi ni vigumu sana, mtanzania ni lazima ajifue ili kushindana na mganda, mkenya n.k