Hakuna kitu kinachofurahia kama kuuchonga ukweli. Mswahili kwa kutumia takwimu na orodha ya majina ameonesha kuwa kuna Ukabila. Bahati mbaya watu wameanza kuamini sababu ya kuona majina ya watu wa kabila moja! Kinachosikitisha zaidi ni kuwa badala ya kujiuliza kama huo ni ukabila au kitu kingine tunakubali maelezo hayo na tunaanza kuamini kuwa kuna ukabila.
Nilivyoonesha kwenye jibu la kwanza kabisa kuwa madai ya ukabila hajajaanza leo. Miaka 30 iliyopita kuna watu walianza kusema maneno hayo hivyo kwanza tukubali kuwa kuna watu ambao hawajabadili maono yao licha ya muda kupita na hakuna kitu kinachoweza kufanyika kinaweza kuwabadili mawazo yao.
a. Hivi watu wote hao waliotajwa wangeamua kubadili majina yao na kuweka mwisho majina ya "Ndomba, Likuli, Bayo, Salum, Haji, Zoba" n.k itabadili madai hayo? Kwa mfano wachagga wote kuanzia sasa waanze kuomba kazi kwa kuficha ubini wao itaondoa wao kupewa nafasi za kazi?
b. Katika majina yote yaliyotajwa na Mswahili na wengine humu ni wangapi kati ya watu hao wanajuana? Je viongozi hao wachagga ambao wameajiri watu chini yao (huko Human Resource) ni wangapi walikuwa wanafahamiana na waajiriwa hao? Kabla sijarukia na kusema ukabila nataka nifahamu kwanza je wangapi kati yao wanafahamiana? Je Kittilya anafahamiana na Lymo, Macha, au Mrema? Je anafahimiana na Mkullo, Ngosha n.k ambao nao aliwaajiri? Nioneshe kwanza kuwa hawa wote hawafahamiani au kujuana kwanza ndio unioneshe ukabila!
c. Zaidi ya yote, naomba mtu anioneshe kuwa kwenye nafasi ambazo zinahitaji elimu kuna mchagga, mnyakyusa, au mhaya ambaye ameajiriwa ambaye hana elimu hiyo. Na hapa sizungumzii nafasi za kisiasa au kuteuliwa. Nazungumzia nafasi za kikazi. Kama kuna mchagga ambaye hana elimu naye amepewa kuongoza kitengo au idara ambayo hana ujuzi nayo badala ya kuuliza kama ni ukabila, kwanini tusiulize kwanini apewe nafasi hiyo, je anafahamiana na bosi?
d. Hivi tatizo kubwa Tanzania ni ukabila au undugunization? Mfano wa mama Mkapa je hao wote "waliopewa nafasi" ni kwa sababu ni wachagga au kwa vile ni ndugu? Hebu tuangalie maneno ya Mswahili:
"kamishina wa ushuru na forodha George Lauwo amempa kazi mdogo wake mr Lauwo "
alimpa hiyo nafasi kwa vile ni mchagga au ni ndugu yake?
chukulia mfano daktari wa mkapa alikuwa dr.Maro mchagga na ni ndugu wa mama Mkapa
Je alipewa nafasi hiyo kwa vile ni mchagga au kwa vile ni ndugu ya mama Mkapa? Kama kilichoangaliwa ni uchagga kwa nini wasimpe Dr. Minja ambaye anaqualification kama za dr. Maro?
mpiga picha wa Mkapa na sasa Rais Kikwete ni mchagga na ndugu wa mama mkapa freddy Maro
Je alipewa nafasi hiyo kwa vile ni mchagga au kwa sababu ni ndugu ya mama Mkapa? mbona wapo wapiga picha wengi tu kama Mroki Mroki?
TRA GENERAL COMMISSIONER ni Kittlya Harry huyu ni mchagga na ndio mkuu wa TRA NI mchagga aliyebebwa na Mramba basil mchagga mwenzake.
Je Kittlya alipewa nafasi hiyo kwa vile ni Mchagga au kwa vile anafahamiana na vigogo wengine wa serikali akiwemo Mramba? Mbona hawakumpa nafasi hiyo Tarimo ambaye ingawa ni mfanyabiashara mkubwa lakini hafahamiani sana na Vingunge?
nakupa zaidi RRO wa airport alikuwa Kimaro ambaye ni mchagga,
RRO long room alikuwa sabuni nae kilimanjaro, ukienda officer in charge majahazi alikuwepo Lyimo nae mchagga akaja Mushi nae mchagga, na ukienda RRO BANDARINI alikuwepo mzee Maleko mchagga bandari iko chini yake kabla yake alikuwepo Foyi nae mchagga,RRO wharf alikuwepo Kisaka mchagga ambaye sasa ni deputy commissioner,hawa ndio watendaji wanaopitisha ushuru.
Je, hawa wote, (i) hawana elimu inayowafanya wastahili nafasi hizo? (ii) wanafahamiana na nani? (iii)nioneshei kuwa watu hawa wote walirushwa nafasi hizo yaani hawakuanzia chini na hivyo waliwapita watu wa makabila na mengine na kupewa nafasi hizo
Human resource & adminstration yupo mtu wa kilimanjaro hapo ajira haendi kwingine. halafu fuatilia watendaji wa chini ya hawa policy makers.
fuatilia RRO/MANAGERS, fuatilia officers in charges wa long room(Dar),na boarders, then utapata jibu vipi kilimanjaro walivyothibiti idara hii nyeti.
nakupa zaidi RRO wa airport alikuwa Kimaro ambaye ni mchagga,
RRO long room alikuwa sabuni nae kilimanjaro, ukienda officer in charge majahazi alikuwepo Lyimo nae mchagga akaja Mushi nae mchagga, na ukienda RRO BANDARINI alikuwepo mzee Maleko mchagga bandari iko chini yake kabla yake alikuwepo Foyi nae mchagga,RRO wharf alikuwepo Kisaka mchagga ambaye sasa ni deputy commissioner,hawa ndio watendaji wanaopitisha ushuru.
na documents zote za bandari Dar lazima zinapitia kwa head declaration officer(HDO) MR. MCHIRA huyu nae kilimanjaro,
officer in charge wa container terminal bandari dar,ni mr. steven mchagga,
officer in charge border ya Tunduma ni mr, Niko ni mchagga na ukienda border ya Namanga kuna mr. Mosi nae mchagga,
Kwa mtu ambaye macho yake hayajafunzwa anaweza kushtuka akikabiliwa na data kama hizi, na kujikuta akikubali bila kuhoji kuwa kuna ukabila. Kabla miye sijashawishika naomba Bw. Mswahili atufanyie mambo yafuatayo.
a. Leta orodha ya vitengo vyote vya TRA na utupe viongozi wake wa juu wa vitengo hivyo makao makuu
b. Leta orodha ya mipaka yetu (Mipaka ya TZ na Uganda, TZ na Malawi, TZ na Rwanda, TZ na Burundi, TZ na Kenya na bandari zote ) na viongozi wake na makabila yao
Sasa, kabla hatujaenda mbali lazimi nikiri jambo moja kuwa nitakuwa mwongo na mzandiki kama sitakiri kuwa wapo Watanzania ambao wanatanguliza ukabila katika mambo fulani fulani na anga hizo siyo za Wachagga peke yao! kuna wasukuma wanaoependelea wasukuma wenzao, wandengereko wanaopendelea wandengereko wenzao n.k Watu wenye hisia hizo haiwajilishi kama ni wachagga au la, unless Mswahili aniambie kuwa katika ya binadamu wote waishio Tanzania wenye hisia ya Ukabila ni Wachagga peke yao!
Zaidi ya yote, wakati wengine wanaona ukabila katika hayo yote mimi bado naona kufahamiana na kujuana zaidi. Na ukiliangalia hili utaona kuwa watu wengi bila kujali makabila yao wameajiriwa kwa vile wanajuana na mzee fulani au familia fulani. Una nafasi kubwa ya kuajiriwa mahali fulani Tanzania ukiwa unajuana na watu wa humo kuliko ukiwa mtu wa kabila la mmoja wa wawili wa viongozi wa humo! Ni wangapi hapa tumepata nafasi kwa sababu wazee wetu au rafiki zetu wametuunganisha na marafiki zao!? Kwangu mimi tazio la undugunization ndio linalotishia maendeleo ya nchi yetu zaidi kuliko huu ukabila hewa!!! Bado sijashawishika kuwa kuna ukabila Tanzania kwa kiwango ambacho Mswahili na wengine wanataka tuamini!! Ni rahisi kudai ukabila kuliku undugunization, kwani ukabila unawahusu watu wa kundi fulani, na undugu unaweza kuwa unatuhusu sisi!!!!!!