Ukabila Ikulu, Ujenzi, Mambo ya nje, Mipango, TRA, BoT + Ofisi nyeti za serikali

Ukabila Ikulu, Ujenzi, Mambo ya nje, Mipango, TRA, BoT + Ofisi nyeti za serikali

YEBO YEBO.

bado sioni mantiki ya kulazimisha moshi kuwa na shule nyingi. nimesema shule nyingi huko ni boarding na hata kinchi si mji wa kwanza kuwa na shule uliza shule kama Tanga school, usagara n.k zilianza lini na huko kilimanjaro kulikuwa na shule gani?

kilichotokea baada ya uhuru katibu mkuu na waziri ya elimu wa kwanza walitoka kilimanjaro akina Elyofoo na mwenzake hao ndio wakafanya ukabila mkubwa na hiyana kuwabeba watu wao kwa msingi wa kikabila. kwa hiyo ubaguzi huu wa TRA, Hazina, BOT hakuanza jana wala juzi.

hoja ya kudai kilimanjaro kuna shule nyingi hivyo hata kalani wa TRA kutoka Kilimanjaro si sahihi kila kabila linaweza kuzalisha kalani kabila kama la wamasai waliokuwa nyuma kielimu limetuletea mawaziri wakuu mara 2 nini kalani?
.
JEE kwa vile uwanja wa ndege wa kimataifa uko wilaya ya temeke hiyo ina maana wakazi wa wilaya ya temeke wanasafiri sana kuliko wilaya zingine? au kampuni nyingi za shughuli za ndege kama wakala wa kuzaa tiketi wako temeke kwa vile wilaya hiyo ina Dar-international airport?.kama hivyo ndivyo basi Kilimanjaro kuwa na shule nyingi kutapelekea tuwe na makalani wengi TRA toka moshi.
 
Mzee Mwanakijiji,

Mzee ndio wewe tunayekuamini ktkt maswala kama haya na muda wote tulikuwa tunajaribu kukuvuta kwa hoja ili swala hili ulipe kipaumbele. Kutokubaliana ni wajibu ktk mjadala isipokuwa kama kweli Ume -Give up kwa nia nzuri yaani kuyakubali mawazo yetu wengi (demokrasia) nadhani itakuwa bora na vizuri sana kama utajaribu kuwasiliana na wahusika hasa huko TRA kupata ukweli zaidi. Muhimu ni kwamba swala limekuwa addressed!
Iwe ni Undugunization ama Ukabila, by the way nakubaliana na tafrsiri yako kuwa kiswahili safi cha kuweka fungu hili la watu ni Undugunization -Ukabila ni neno zito sana!...
Nduguyo sii lazima awe wa ubin ama tumbo moja na kama navyoelewa Watanga hasa Wabondei hujiita ndugu na mshikamano wao ni mkubwa sana bila kudharau makabila mengine. Kosa linakuja pale mtu unapotumia undugu huo kama kigezo kikubwa ktk utoaji ajira. watu hawa wapo dunia nzima na wanapigwa vita kila siku kama tunavyopigana na majambazi..
Sasa mzee tuifanyie kazi!... solution ndio muhimu zaidi maadam ujumbe ufike huko unakotakiwa!
 
The only thing I cannot resist is temptation...so I join the fray!

1. Kwa maana ya ujumla, na kwa kulinganisha na mahali/nchi nyingi za Afrika kwa mfano, Tanzania HAKUNA UKABILA. Maana ya ujumla ni ile ya kumbagua mtu kulingana na kabila lake, na hata kuonyesha chuki, dharau, na kejeli wazi wazi kuwa kabila lake si bora kulinganisha na kabila la mbaguzi. Ubaguzi huu wa kijamii, ukishika kasi, huelekea kwenye ubaguzi wa kisiasa na kiuchumi. Chimbuko au msingi mkubwa wa Ukabila ni tofauti ya lugha (makabila).
2. Tanzania kuna makabila machache, takriban matatu, ambayo yanatajwa sana KUWA NA UKABILA. Hayo ni pamoja na Wachagga, Wahaya na Wanyakyusa. Kwa ujumla, watu wengi kiasi wanadhani/wanaamini kuwa watu wa makabila haya hufanya upendeleo kwa wenzao (watu wa makabila yao) hasa katika fursa za elimu na ajira. Wakati watu wa makabila hayo tajwa hawawachukii dhahiri watu wa makabila mengine, na wanaweza kuishi nao bila ubaguzi kijamii, inaonekana huwapendelea zaidi watu wa makabila yao katika masuala ya uchumi na siasa.
3. Kuna ukweli wa kihistoria kuwa sehemu watokako watu wa makabila hayo matatu yalipata fursa za elimu mapema. Kutokana na ukweli huo watu wa huko waliweza kupata elimu bora na kwa wingi, na hatimaye fursa za ajira rasmi, serikalini na nje ya serikali, na wengine kujiajiri wenyewe katika sekta mbalimbali kwa kutumia elimu waliyopata kulinganisha na watu wa makabila mengine. Kwa ujumla, kimaendeleo watu wa makabila hayo wamepiga hatua zaidi na kadri wanavyoendelea ndivyo wanavyozidi kutamani maendeleo zaidi na wakati huo huo kujipenda na kujiendelea zaidi!
4. Tofauti ya kielimu kati ya mikoa hiyo ya ”Wamisionari” na mikoa mingine sasa inapungua kutokana na sera ya wazi na ya kimyakimya ya kuweka uwiano wa fursa kielimu iliyoasisiwa na Mwalimu kama njia mojawapo ya kupunguza ukweli na hisia za ukabila. Mwalimu (RIP) aliona mbali! Kuondoa machifu na majimbo, kuanzisha na kupeleka wanafunzi shule za bweni mbali na kwao, JKT nk ilikuwa ni mikakati iliyosaidia kupunguza ukweli na dhana ya ukabila. Hivi sasa pia kuna mwingiliano mkubwa zaidi kati ya makabila katika kuoana. Zamani haikuwa rahisi kukuta Mchagga kaolewa na asiye Mchagga, au Mhaya kuolewa na asiye Mhaya; sasa haya yamepungua sana.
5. Wakati huo huo, ndani ya UKABILA, au Kabila moja, kunaweza kuwa na UKABILA mwingine. Wachagga wa Marangu hujiona bora kuliko Wachagga wa Kibosho!
6. Kwa mfumo wetu wa maisha, mpaka sasa ni rahisi zaidi watu wa Kabila moja kufahamiana kuliko vinginevyo. Mwanzo wa kufahamiana ndiyo Undugu! Hii inafanya kuwe na mstari mwembamba sana kati ya UKABILA na UNDUGU ambao huweza kuleta UNDUGUNIZATION!
7. Ni rahisi zaidi pia kwa makabila hayo matatu, kutokana na sababu hizo hapo juu, kufanya UNDUGUNIZATION. Hilo likitokea inakuwa si rahisi kujua kilichotokea kuwa ni UKABILA au UNDUGUNIZATION!
8. Dalili na sababu za kukua kwa UKABILA na UNDUGUNIZATION zinatokana na ukweli kwamba hivi sasa hapa Tanzania fursa za elimu na ajira na biashara (uchumi) zimekuwa na ushindani mkubwa.

NOTA BENE:
Viongozi ”wengi” wastaafu na walioko serikali (BM, FS, Dr Salmin, Warioba, Bomani…Sefue, Ben Moses...) WAMEOA WACHAGGA! Inaweza pia kuwa kwa sababu za kihistoria; kuwa walikutana mashuleni/vyuoni na kwa vile ni hao hao Wachagga waliokuwa wamewahi kufika huko shuleni, vyuoni na hatimaye kuajiriwa serikalini na katika mashirika ya umma!
Kwa hali hiyo, ikiwa viongozi hao wasio Wachagga watapendelea wakwe na mashemeji nk kutokana na kujuana au UNDUGUNIZATION, utaona kitakachotokea kitakuwa UKABILA!
 
Wasukuma sio wengi katika sehemu hizo kwa kuwa, sio kuwa hawakusoma kwa sasa, ila kwa kuwa hawakuwa katika nafasi za kuajiri tangu mwanzo.Sasa hivi wamesoma lakini nani atawaangalia wakati waliosoma tangu kabla ya uhuru ndo wanaoendeleza kuhakikisha watu wao ndo wanarithi hizo nafasi.KWA MAANA NYINGINE WASUKUMA NA MAKABILA MENGINE YAPO KATIKA SEHEMU AMBAZO HAZIAJIRI KWA MISINGI YA UKABILA. BALI UWEZO WA MTU.TRA KUNA ULAJI WA KUFA MAKABILA MENGINE HAYASTAHILI KUAJIRIWA HUKO!!
 
The only thing I cannot resist is temptation...so I join the fray!

1. Kwa maana ya ujumla, na kwa kulinganisha na mahali/nchi nyingi za Afrika kwa mfano, Tanzania HAKUNA UKABILA. Maana ya ujumla ni ile ya kumbagua mtu kulingana na kabila lake, na hata kuonyesha chuki, dharau, na kejeli wazi wazi kuwa kabila lake si bora kulinganisha na kabila la mbaguzi. Ubaguzi huu wa kijamii, ukishika kasi, huelekea kwenye ubaguzi wa kisiasa na kiuchumi. Chimbuko au msingi mkubwa wa Ukabila ni tofauti ya lugha (makabila).
2. Tanzania kuna makabila machache, takriban matatu, ambayo yanatajwa sana KUWA NA UKABILA. Hayo ni pamoja na Wachagga, Wahaya na Wanyakyusa. Kwa ujumla, watu wengi kiasi wanadhani/wanaamini kuwa watu wa makabila haya hufanya upendeleo kwa wenzao (watu wa makabila yao) hasa katika fursa za elimu na ajira. Wakati watu wa makabila hayo tajwa hawawachukii dhahiri watu wa makabila mengine, na wanaweza kuishi nao bila ubaguzi kijamii, inaonekana huwapendelea zaidi watu wa makabila yao katika masuala ya uchumi na siasa.
3. Kuna ukweli wa kihistoria kuwa sehemu watokako watu wa makabila hayo matatu yalipata fursa za elimu mapema. Kutokana na ukweli huo watu wa huko waliweza kupata elimu bora na kwa wingi, na hatimaye fursa za ajira rasmi, serikalini na nje ya serikali, na wengine kujiajiri wenyewe katika sekta mbalimbali kwa kutumia elimu waliyopata kulinganisha na watu wa makabila mengine. Kwa ujumla, kimaendeleo watu wa makabila hayo wamepiga hatua zaidi na kadri wanavyoendelea ndivyo wanavyozidi kutamani maendeleo zaidi na wakati huo huo kujipenda na kujiendelea zaidi!
4. Tofauti ya kielimu kati ya mikoa hiyo ya "Wamisionari" na mikoa mingine sasa inapungua kutokana na sera ya wazi na ya kimyakimya ya kuweka uwiano wa fursa kielimu iliyoasisiwa na Mwalimu kama njia mojawapo ya kupunguza ukweli na hisia za ukabila. Mwalimu (RIP) aliona mbali! Kuondoa machifu na majimbo, kuanzisha na kupeleka wanafunzi shule za bweni mbali na kwao, JKT nk ilikuwa ni mikakati iliyosaidia kupunguza ukweli na dhana ya ukabila. Hivi sasa pia kuna mwingiliano mkubwa zaidi kati ya makabila katika kuoana. Zamani haikuwa rahisi kukuta Mchagga kaolewa na asiye Mchagga, au Mhaya kuolewa na asiye Mhaya; sasa haya yamepungua sana.
5. Wakati huo huo, ndani ya UKABILA, au Kabila moja, kunaweza kuwa na UKABILA mwingine. Wachagga wa Marangu hujiona bora kuliko Wachagga wa Kibosho!
6. Kwa mfumo wetu wa maisha, mpaka sasa ni rahisi zaidi watu wa Kabila moja kufahamiana kuliko vinginevyo. Mwanzo wa kufahamiana ndiyo Undugu! Hii inafanya kuwe na mstari mwembamba sana kati ya UKABILA na UNDUGU ambao huweza kuleta UNDUGUNIZATION!
7. Ni rahisi zaidi pia kwa makabila hayo matatu, kutokana na sababu hizo hapo juu, kufanya UNDUGUNIZATION. Hilo likitokea inakuwa si rahisi kujua kilichotokea kuwa ni UKABILA au UNDUGUNIZATION!
8. Dalili na sababu za kukua kwa UKABILA na UNDUGUNIZATION zinatokana na ukweli kwamba hivi sasa hapa Tanzania fursa za elimu na ajira na biashara (uchumi) zimekuwa na ushindani mkubwa.

NOTA BENE:
Viongozi "wengi" wastaafu na walioko serikali (BM, FS, Dr Salmin, Warioba, Bomani…Sefue, Ben Moses...) WAMEOA WACHAGGA! Inaweza pia kuwa kwa sababu za kihistoria; kuwa walikutana mashuleni/vyuoni na kwa vile ni hao hao Wachagga waliokuwa wamewahi kufika huko shuleni, vyuoni na hatimaye kuajiriwa serikalini na katika mashirika ya umma!
Kwa hali hiyo, ikiwa viongozi hao wasio Wachagga watapendelea wakwe na mashemeji nk kutokana na kujuana au UNDUGUNIZATION, utaona kitakachotokea kitakuwa UKABILA!

kwa hiyo umekubali kuna ukabila?

na kama umekubali sasa lete proposals za namna ya kutatua tatizo hilo
 
Unakuta mtoto nyumbani anatetemeka kwa homa, ni mgonjwa watu wote wanakubali kuwa mtoto ni mgonjwa kwani wote wanaona anavyotetemeka na wanahisi joto la mwili wake. Sasa kila mtu anaanza kujaribu kuelezea mtoto anaumwa nini?

Mswahili et al, wanasema mtoto karogwa! wnaonesha ushahidi wa manyoya ya kuku, hirizi chini ya mlango na wanatukumbusha yule bibi kizee aliyepita jana hapo nyumbani na kurusha maneno ya laana. Anaelezea kwa kirefu kuwa angalia mtoto anavyoropoka ropoka, amechanganyikiwa, na inaonekana ametupiwa jini pia!! Wanaoamini mambo ya kishirikina wanakubali kwa haraka kwani ushahidi upo, mtoto wetu karogwa! Anataka tumpeleke kwa mganga wa kienyeji tujue ni nani mchawi wetu!

Mimi na wachache wetu, tunasema ndio mtoto anaumwa na tusipomfikisha hospitali atatuacha. Tunapuuza kabisa madai ya kurogwa kwani ni imani za kishirikina zisizo na msingi katika sayansi. Hata hivyo tunajuwa nguvu ya ushirikina na imani ya aina hiyo. Tunasema tunachoona ni dalili za malaria, na inawezekana na malaria ya kwenye ubongo (celebral malaria). Tunaonesha ushahidi kuwa mtoto alikolala hakuna chandarua, wala dawa ya mbu, na eneo tunaloishi kuna ugonjwa huu. Tunasema, badala ya kumchukua mtoto na kumpeleka kwa mganga wa kienyeji ili aaguliwe (tawire! tawire!) tunasema tumpeleke hospitali ili afanyiwe vipimo vyote ili kujua uzito wa tatizo lenyewe na kutafuta dawa muafaka. Washirikina hawataki hilo na kwa vile watu wenye imani hiyo ni wengi, basi wanashinda na kumchukua mtoto kwenda naye kwa mganga wa kienyeji. Si muda mrefu tunasikia kuwa mtoto amefia kwa mganga wa kienyezi baada ya kupoteza damu nyingi baada ya kuchanjwa!! Washirikina wetu hawamlaumu mganga, wanaendelea kumlaumu mchawi aliyemroga mtoto!!!

Baada ya kufanya uchunguzi baada ya kifo, tunagundua kuwa mtoto hakuwa amerogwa na hakuwa na malaria alikuwa na allergy ya manyoya ya kuku!!! Kumbe sote tulikosea!!!
 
MAPENDEKEZO YA KUONDOA WINGI WA MAKABILA KATIKA AJIRA TANZANIA

Kwa vile tatizo linalozungumziwa humu siyo "ukabila" in its classical meaning, bali ukabila kama wingi wa watu wa kabila moja kwenye maeneo fulani ya kazi, napendekeza hatua zifuatazo zichukuliwe ili kuhakikisha wingi huo unapungua.

a. Kusitisha mara moja ajira za wachagga, wahaya, wanyakyusa katika ofisi zinazotuhumiwa hata kama watu hao wana uwezo na uzoefu.

b. Kabla Mhaya, Mnyakyusa, Mchagga hajakubaliwa kuajiriwa huko aulizwe kwanza mtu wa kabila jingine kwanza.

c. Tufanye uhakiki wa Wachagga wote TRA na kuuliza vyeti na elimu yao tusiulize kama wanajuana na mabosi (kwani hilo siyo la msingi). Wachagga wote ambao haturidhiki na elimu, na uzoefu wao basi watemwe.

d. Tukishamaliza TRA, tuhamie idara nyingine zote ambazo zinawachagga wengi na tufanye hivyo hivyo.

e. Tukimaliza serikali tutagundua kuwa bado hata katika jamii yetu bado Wachagga wana nafasi kubwa, wanabiashara nyingi n.k Hii inawanyima nafasi watu wengine wengi hivyo tujaribu kwa namna yoyote ile kupunguza kumiliki kwao biashara. Tunaweza kufanya hivyo kwa kuwanyima vibali vya biashara hadi tutoe nafasi hiyo kwa watu wa makabila mengine kwanza.

f. Bila ya shaka kuna wachagga (Wahaya na Wanyakyusa pia) kwenye vyuo vyetu vingi, tuwaombe ndugu zetu hao waamue kwa angalau miaka mitano kusimamisha masomo ili nafasi zao zichukuliwe na makabila mengine ili nao waaelimike. Hii itaonesha ni jinsi gani ndugu zetu wameamua kupigana na tatizo la ukabila.

g. Hata hivyo baada ya kufanya hayo yote hawa jamaa wanaweza kuanzisha shule zao wenyewe na vyuo vyao na hivyo bado wakaendelea kuelimika, hatuna budi tutafute jinsi ya kupunguza uzao wao. Kwa mfano tunaweza kuwapangia kuwa Wahaya, Wachagga na Wanyakyusa wasizae zaidi ya watoto 4 na wakati huo huo tuwatie moyo watu wa pwani waoe wake wengi na kuzaa watoto wengi kwani nafasi za Elimu ziko nyingi na wazi.

h. Tukiona bado Wahaya, Wanyakyusa na Wachagga bado wako wengi na wanaendelea kuonekana kwenye vitengo mbalimbali tunaweza kuwatafutia sehemu nyingine Afrika (kama Botswana au Namibia) ambako tunaweza kuwasihi wahamie ili kutengeneza nafasi kwa watu wa makabila madogo madogo. Tunaweza kutumia fedha za madini kuwalipia tiketi.

Natumaini mapendekezo yangu yatatendewa kazi ili kujenga Taifa la watu wa moja, wenye mshikamano, na wasio na hisia za kibaguzi.
 
Duh!
lakini unajua mahojiano yako yanasikika dunia nzima?
 
Mzee Mwanakijiji,

Mswahili hana maana kabisa ya mtoto kulogwa! Objection, you're misleading the panel!
Hii babu umeitunga wewe kwa sababu Ukabila sio dhana ambayo haiwezi kufanyiwa utafiti wa kisayansi.
Mswahili kasema mtoto ana maleria kwa kutukia kuelewa kwake. Mswahili ni mzawa na mkazi wa nchi hii ya joto!... tatizo hapa ni wewe daktari wa darasa ambaye unatazama kwanza hizo simptons za maleria ambazo bado hazija add up kukupa jibu sahihi la vipimo ila unachoona ni homa tu!..
Mswahili anaomba mtoto apelekwe hospital(swala lishughulikiwe) wewe unasema hakuna haja ya hospital (No action to be taken) kwa huyu mtoto ila ni vizuri kulitazama swala la malaria kwa upana wake!..
Kibaya zaidi ni pale unapo suggest tuue jamii wote wa mbu (waliomo na wasiokuwemo)kuhakikisha hakuna tena maleria lakini huyu mtoto hana maleria....
 
hahaaaa Mkandara.... that is exactly my point.. kutokana na maelezo ya Mswahili kweli unaweza kuconclude kuna ukabila kwa kutumia sample ndogo kiasi hicho!! suala la ukabila linaendelea kuwa nadharia tu na lisilo na ushahidi wowote wa Kisayansi! Nilichoomba toka mwanzo na imeshindikana kupata ni huo ushahidi wa kisayansi isipokuwa ushahidi wa pseudo-obviousness.. "kwani wewe huoni yote haya"?... naulizwa.. nikisema sioni wanadhani zimeniruka.. kwani natakiwa "kuona"!!
 
mara nyingi ndugu huwa wanatoka kabila moja

ni nadra sana ukawa nd aundugu kati ya tuseme Mzaramo na Mhaya au Mchagga na Mpemba
 
Mwanakijiji.

hakuna haja ya kubishana sana, nakubali umeshinda na kwa mantiki yako hata akina Malcom X, na martin luther KING walikuwa wapumbavu kudai haki za watu weusi marekani kwani kwa sababu za kihistoria wao walikuwa watumwa tu. na wageni wanataka nini tena zaidi kwenye nchi ya watu?

nashangaa hata akina condoleza rice wanapewa nafasi wakati sababu za kihistoria zinaonesha wenye asili ya nchi yao wamesoma sana.

napata kigugumizi kuona Adam Kimbisa kuwa meya wa jiji la Dsm kwani kihistoria wenye mji wao wapo iweje mrangi awe meya wa DAR?
na hata Obama nae atapata swali hili hili kwa sababu ya kihistoria hatakiwi kushiriki siasa marekani.

nakuuliza swali imekuwaje Augustino Mrema anakosa urais kila mwaka huku ni mchagga na ana sababu za kihistoria kumfanya afike IKULU? kwani kabila lake limekwenda shule miaka mingi.

ila kama wewe kweli mwandishi kama unavyodai mwenyewe fuatilia ujue wizara ya elimu baada tu ya uhuru nani alikuwa waziri na nani alikuwa katibu mkuu.
masuala ya ushirikina mie sijataja na hakuna nimesema kuna jini au tawire! naomba sema nilichosema usinizushie.
 
I think we need to find solutions on the issues raised on this thread.
 
mswahili, mawazo yako yanafurahisha sana... Unaonaje kuhusu mapendekezo yangu ya jinsi ya kuondoa na kupunguza hiyo idadi ya wachagga huko TRA na sehemu nyingine. Tumesema tuna tatizo, mimi nimetoa mapendekezo yangu nasubiri ya kwako.
 
Sikubaliani na mawazo yako jinsi ya kupunguza ukabila TRA na sehemu nyingine.

mie sipendi watu waonewe ninatachokampeni ni fair play hata kama akiwa mchagga apewe fair play. lakini kutumbia kujaa watu TRA kwa sababu za kihistoria hiyo sikubali na pia njia yako ya kulitatua tatizo hili sio muafaka. ninachosema ni usawa kwa wote na hili ndio chochoko ya kukosekana amani sehemu nyingi na hata kusababisha migongano kwenye jamii.
I would like to treat other people the way i should like to be treated.
 
mswahili, mawazo yako yanafurahisha sana... Unaonaje kuhusu mapendekezo yangu ya jinsi ya kuondoa na kupunguza hiyo idadi ya wachagga huko TRA na sehemu nyingine. Tumesema tuna tatizo, mimi nimetoa mapendekezo yangu nasubiri ya kwako.

tatizo yale yalikuwa siyo mapendekezo ya MWANAKIJIJI tunaye mjua sie

na mimi nilipatwa na wasi wasi kuwa kuna wewe unatumia jina la mwanakijiji kuposti humu au mnaishi pamoja

keshoo nitampigia simu nijue kama ni kweli mwanakijiji alieposti au mwingine
 
Bravo Mswahili,

Lovely, maneno mazito na keep it up, so far no competition, ninaona logic nyingi ambazo hazihusiani na tatizo, maneno yaliyopangwa kishule na ki-paper! lakini ndani yake empty! nothing!

Mzeee Mswahili, mkome nyani mwanangu ajali ya kuku impate mwewe tunakusubiri Shimo la udongo na basi la UDA mwanangu, wachola!

Bravo kwa kuliweka tatizo wazi na hadharani! sasa tusuke au tunyoe!
 
DrWHO
Na mimi nasubiri mchango wako katika "solution."
 
Back
Top Bottom