Ukabila Ikulu, Ujenzi, Mambo ya nje, Mipango, TRA, BoT + Ofisi nyeti za serikali

Ukabila Ikulu, Ujenzi, Mambo ya nje, Mipango, TRA, BoT + Ofisi nyeti za serikali

Sikubaliani na mawazo yako jinsi ya kupunguza ukabila TRA na sehemu nyingine.

mie sipendi watu waonewe ninatachokampeni ni fair play hata kama akiwa mchagga apewe fair play. lakini kutumbia kujaa watu TRA kwa sababu za kihistoria hiyo sikubali na pia njia yako ya kulitatua tatizo hili sio muafaka. ninachosema ni usawa kwa wote na hili ndio chochoko ya kukosekana amani sehemu nyingi na hata kusababisha migongano kwenye jamii.
I would like to treat other people the way i should like to be treated.


Mswahili

Lengo ni kufikia hapo unaposema...hebu tuangalie sasa njia mbali mbali za kutufikisha hapo.


Mimi napendekeza haya:

1. Usaili wa kazi ufanywe na panel la watu wasiopungua 3 kutoka vitengo tofauti. Vitengi gani vitahusika then itategemeana na aina ya kazi inayotangazwa.

2. Kuwe na vyombo huru vya kutetea maslahi ya wafanyakazi (hivi vya sasa vimemwagiwa sumu za kisiasa) na hatimaye ni kama vipo lakini havipo.

3. Katika ujazaji wa form za kazi, kuwe na kipengele kitakachomfanya muombaji atamke wazi na mapema kuwa tayari ana ndugu au hana ndugu katika idara husika ya serikali.

4. Kama anaye ndugundani ya idara husika then ifanyike internal assesment kama mhusika (muombaji kazi) na yule ambaye tayari ni mfanyakazi wanaweza kutekeleza majukumu yako bila kuwepo na conflict of interest katika mazingira ya kazi kiujumla.

5. Wafanyakazi waelimishwe nini maana halisi ya ukandamizaji ambao una misingi ya udini, ukabila au ubaguzi wa aina yoyote ile.

6. Kuwepo na hatua za wazi; zinazoelezea adhabu ya kukutwa na hatia ya kumbagua mfanyakazi yoyote kwa namna hizo hapo juu.

7. Kuwepo na review ya mara kwa mara ya jinsi ajira fulani fulani (random selection) zilivyopatikana katika idara mbalimbali za serikali. Kwa dhumuni la kujifunza makosa au kugundua ukiukwaji wa taratibu kama hizo hapo juu.

Kwa leo ni hayo.

Alamsiki.
 
Yebo Yebo.. baada ya kufanya yote hayo na bado wachagga ndio wakaongezeka na watu hao wa makabila mengine kwanini msikubali mapendekezo yangu? DrWho, na wengine wanaoshangaa mapendekezo yangu tafuteni insha moja maarufu inayoitwa "A Modest Proposal"...
 
MMkjj thanks. However why should we only agree to your proposals? Personally, I think the best way to begin is to reflect on what has been discuussed by all those who have contributed to this discussion so far and see if we have learned anything out of it. Secondly, together let us review best practices in combating cronyism/ favouritism at work places from different parts of the globe. I believe these will help us decide what to do in oder to reduce unfair employment practices in Tanzanaia. Thirdly, let us decide on possible altenative methods which will help us achieve our goal. Fourtrhly, let us recommend those methods to individuals with authority at, for example, TRA for them to take action. And finally, as it has been shown in this discussion so far, let us consider and guard ourselves against things that may stand in our way.
 
pole sana mswahili,watanzania ambao ni wanachama wa vyama hawafiki milioni tano....so wengi wetu hapa tunashabikia maendeleo..angalia unaposhindwa kukubaliana na mwanakijiji kuwa kilimanjaro yenye shule 140 za sekondari itakuwa na wanafunzi wengi kutoka kilimanjaro..hii inaonyesha hutaki kukubaliana na ukweli ...shule kama marian bagamoyo huwa wanafanya interview watoto 1,000 na wanachukua 90...sasa kama hao unaosema hawakufaulu interview unategemea nini? shule za misheni hazipendelei la muhimu kwao ni kufaulu interview na nidhamu.
shule kama kibiti ,ni specialize ya kilimo [CBG.CBN.] sasa wao wanachukua watoto wa nchi nzima waliochagua kusomea kilimo...sasa kama hao unaosema hawakuchagua mchepuo wa kilimo form 5,watakua pale kufuata nini?
kuhusu rafiki yako beny ,.i feel sorry if you have a point ,mwambie aende mahakamani.

mwanakijiji hongera kwa kutoa facts...kama kuna watu nchi hii wanatakiwa kusaidiwa wapate huduma za elimu kwa wingi zaidi ni WASUKUMA,na WANYAMWEZI..tunayo bahati kuwa hawa watu ni wapole wangekuwa na maneno kama kina mswahili..tungekuwa hatuna la kusema,,.lakini wao wametulia WAPEWE ZAIDI kwa uwiano wao.unajua kuna watu wajinga wanafikiri TANZANIA ni DAR ES SALAAM...tanzania ni kubwa na wote wanastahili uzito sawa ...tusiangalie watoto wa mjini dar es salaam tu...
 
mswahili....
penye mti hakuna wajenzi...na unaweza kumpeleka n"gombe bwawani lakini kamwe huwezi kumlazimisha kunywa maji"
dodoma ni makao makuu ya ccm,bunge etc so kwa akili yako wagogo wengi watakuwa wanasiasa na /au wabunge.....
 
Philemon, ndio maana nimeachana na hoja.. sasa wanataka kuzungumzia undugunization wakati wamekataa hilo siyo tatizo kubwa kuliko huo Ukabila wanaoudhania upo. tumeomba ushahidi wa Kisayansi tunapewa kitengo na idara moja na kituo kimoja cha TRA.. tusipoona ukabila TRA kwa kuangalia idadi ya wachagga tunaambie hatutazami vizuri..! tunasema tatizo ni upendeleo unaotokana na kujuana, siyo TRA peke yake bali Polisi, Magereza, Jeshi, vyuoni, n.k .. Hawataki kuliangalia hilo kwani linahusu makabila mengine hata yale madogo madogo!!!

NImewauliza tutawapunguza vipi wachagga waliozidi hapo TRA naambiwa mapendekezo yangu siyo mazuri, msiniambie tufanye nini baadaye.. kama tatizo lipo sasa ni lazima tulishughulikie sasa!! Tutapunguzaje Wachagga waliozidi TRA, Wanyakyusa waliozidi Jeshini, n.k? Hakuna ugumu hapa
 
posted by DUA:

Umedandia gari hujui linakokwenda. Naomba usome issue ambazo ni raised kutoka mwanzo, swala la barabara za kaskazini kupewa 17 billion na za Mtwara na Lindi kupewa 1 billion lilijadiliwa bungeni na wako waliosema kama wewe kwamba wafadhili ndio wanachagua wapi waweke pesa ambalo vilevile limejadiliwa pitia kurasa za mwanzo utapata majibu. usikurupuke kufikiri kila mtu hapa anawachukia wachaga au wambulu au wamang'ati. Siwezi kurudia majibu yapo kwenye hii thread huko mwanzo ndio nikasema sasa kama huu si ukabila ni nini?

Dua,
shutuma unazozielekeza kwa wachaga hazina tofauti na makala za chuki gazeti kihutu, kanguru. kutokana na maandiko yako hapa kila mradi wa maendeleo uliopelekwa kilimanjaro umetokana na upendeleo wa kikabila.

hiyo barabara uliyoitaja hapo ni barabara ya kuelekea tarakea rombo. barabara hiyo ina urefu wa zaidi ya km 90 na ujenzi wake ulianza wakati wa waziri magufuli. zaidi barabara hiyo imekuwa ni kilio cha wananchi wa rombo kwa zaidi ya miaka 40--toka tupate uhuru.

siyo kweli kwamba barabara za lindi na mtwara hazipewi fedha kwa sababu ya hujuma na fitina za wachaga. barabara ya nangurukuru-mbwemkuru yenye urefu wa km 95 imewahi kutengewa t.shs 42 billion. kwa maana hiyo basi, serikali hapo imetumia pesa nyingi per km kwa barabara hiyo kuliko ile ya kuelekea tarakea jimboni kwa mramba. hujuma zinatoka wapi?

jamboforum sasa imetekwa nyara na kuwa genge la kushambulia watanzania wasio wazaliwa wa "mjini," hususan wananchi wa kilimanjaro. tunakoelekea siyo kwema, na kuna hatari ya forum hii kupoteza sifa ya pahala penye mijadala makini, na hoja zilizofanyiwa utafiti.
 
Wana bodi.

Pande zote zimeweka mawazo yao kuhusu hii mada, na kwa upande wangu naamini yaliyowekwa yanatosha kumfanya mtu kuchagua aamini nini.

Napendekeza mada hii ifungwe kwani naamini haitaishia mahala pema. Tukubaliane tofauti zetu. Tukiwa divided kwa ukabila hatutaweza ku-focus kwa matatizo mengine yanayoikabili nchi nzima, kama RICHMONDULI, IPTL, SONGAS, RADAR n.k. in short RUSHWA za vigogo, na mambo mengine ya kutowajibika kitaifa.
 
Chief.

suala la mikataba mibovu sources zake ni ukabila pia. kwani suala la radar na ndege hujui wajanja wa kilimanjaro kupitia kwa dada yao mama mkapa walimuingiza kichwakichwa Mzee wa Masasi? mfuatilie mfanyabaishara mwenye initial Y.M huyu ndiye mshika ten percent ya Benny na mama Mkapa.

Mengi anadaiwa billion 5 kama kodi na vitu vingi anapitisha bure kama benzi aliyotumia kwa gea ya kuwa ni ya walemavu lakini TRA wanajua anaitumia yeye JEE Nani wakumkamata phillimon mikael au Mbowe ?
ndio maana tunasema ukabila ni kansa mbaya sana.

Mikael.

naona unajichanganya na huelewi unasema nini? kama bunge liko dodoma na unasema wagogo si wana siasa wengi kwa kauli hiyo unampinga mwanakijiji aliyedai kuwa kilimanjaro kuna shule nyingi hivyo lazima watu wa huko wamesoma.
Marian girls sera za shule hawachukui waislam zaidi ya watano kwa kila kidato. na shule iko bagamoyo kwa sera hizo wenye bagamoyo yao mtasema wana shule huku hawanufaiki kitu.

na umejikoroga mwenyewe kwa kusema bunge kuwa dodoma si kuwa wagogo ni wabunge zaidi kuliko makabila mengine kwa nukta hiyo wewe na mwanakjj mmejichanganya, na mimi nasema shule nyingi moshi ni bweni tunasoma watu wote, au kwa vile gereza liko ukonga basi watu wa ukonga wengi ni waharifu?
au unataka tujadili ukabila ndani ya chama chako ndio utaamini?

WANABODI.

mjadala huu lazima tuendelee nao wanaosema tuuache sioni mantiki lengo ni kurekebisha na kuwekana sawa na hata kazi ya hii forum ni kufichukua maovu ambayo hayawezi kuwekwa wazi na Nipashe, kulikoni, this day, Tanzania Daima, sayari, ITV au REDIO one kwa vile ni vyombo vya watuhumiwa wa ukabila ila hapa kila jambo linazungumzwa.

Joka kuu.

MR-Fupi katika bajeti ya mwaka jana alitenga bilion 17 kwa rombo jimboni kwake na dar-lindi bilioni 1 usimsingizie magufuli. huo ndio uchagga tunaoupigia kelele.

Mwanakijiji.

hivi huyu hapa na yule mwenye website ya mwanakijiji.podomatic.com ni watu wawili tofauti? kama mwandishi ukipewa habari kiasi kidogo tu basi wewe ni kazi yako kuifutilia kwa kina. nimekupa facts kibao bado unadai niletee na hiki na kile! kweli wewe mwandishi? kama mwandishi bado umekuwa mzito kuelewa somo kiasi hicho? au kwa vile fani ya uandishi imeingiliwa na kila mtu siku hizi mwandishi?
 
Duh!

mswahili this term umekuja kwa kasi nyingine kabisaaa!

Nilianza naona kama utaboronga lakini uandikayo kwa kiwango flani yana ukweli mkubwa tu. Mswahili hawa wa Kilimanjaro walikufanyia nini mzee? Yani unawakandia hadi naanza kuwaogopa. Ebana unawafahamu kwa kina haswa!

Mh!!!
 
Mzee Mwanakijiji,
Hivi tuchulie madai haya yameletwa hapa na mwanamke ambaye anadai kuwa TRA Inaajiri kwa kigezo cha gender!... wakatoa mifano kama ya mswahili ambayo inadadisi hata karani kuwa mwanaume, mpokea simu na kadhalika...
Wewe, kama mwanaume - Utawajibu nini?

Mswahili,
Hivi kama angekuwa Mchagga mwingine kabisa sio Mengi, tuseme Phillemon anayedaiwa millioni 5 na kuingiza hiyo benzi, bado matokeo yangekuwa hivyo hivyo?
 
jokaKuu
posted by DUA:

Umedandia gari hujui linakokwenda. Naomba usome issue ambazo ni raised kutoka mwanzo, swala la barabara za kaskazini kupewa 17 billion na za Mtwara na Lindi kupewa 1 billion lilijadiliwa bungeni na wako waliosema kama wewe kwamba wafadhili ndio wanachagua wapi waweke pesa ambalo vilevile limejadiliwa pitia kurasa za mwanzo utapata majibu. usikurupuke kufikiri kila mtu hapa anawachukia wachaga au wambulu au wamang'ati. Siwezi kurudia majibu yapo kwenye hii thread huko mwanzo ndio nikasema sasa kama huu si ukabila ni nini? Dua,
shutuma unazozielekeza kwa wachaga hazina tofauti na makala za chuki gazeti kihutu, kanguru. kutokana na maandiko yako hapa kila mradi wa maendeleo uliopelekwa kilimanjaro umetokana na upendeleo wa kikabila.

hiyo barabara uliyoitaja hapo ni barabara ya kuelekea tarakea rombo. barabara hiyo ina urefu wa zaidi ya km 90 na ujenzi wake ulianza wakati wa waziri magufuli. zaidi barabara hiyo imekuwa ni kilio cha wananchi wa rombo kwa zaidi ya miaka 40--toka tupate uhuru.

siyo kweli kwamba barabara za lindi na mtwara hazipewi fedha kwa sababu ya hujuma na fitina za wachaga. barabara ya nangurukuru-mbwemkuru yenye urefu wa km 95 imewahi kutengewa t.shs 42 billion. kwa maana hiyo basi, serikali hapo imetumia pesa nyingi per km kwa barabara hiyo kuliko ile ya kuelekea tarakea jimboni kwa mramba. hujuma zinatoka wapi?

jamboforum sasa imetekwa nyara na kuwa genge la kushambulia watanzania wasio wazaliwa wa "mjini," hususan wananchi wa kilimanjaro. tunakoelekea siyo kwema, na kuna hatari ya forum hii kupoteza sifa ya pahala penye mijadala makini, na hoja zilizofanyiwa utafiti.

Mswahili ameleta facts hizi:

Mbunge aliyelalamika upendeleo wa barabara bungeni ni mbunge wa nzega alikuwa ana mlalamikia mr. fupi(mramba) kwa kupendelea kwao. mfano halisi alitenga bilion 17 kwa barabara ya jimboni kwake huku barabara ya kusini dar- lindi imetengewa bilion 1 tena ni barabara muhimu. hao ndio wachagga au mikael barabara hii kwa vile ni ya waswahili? hivyo haijaenda shule?


Dua ans: Kama ni kweli hivyo mnavyosema mnaweza kunipa jibu muafaka kwa nini barabara ya kwenda Lindi Mtwara kama alivyosema Mswahili ilipewa bajeti ndogo na ile iendayo Kilimanjaro kupewa bajeti mara kumi na saba zaidi na kuleta utata bungeni. Utaita huu nao ni Kujuana au Undugu? NI UKABILA

Nafikiri umechanganya hapa angalia facts zako tena, nani ana-dictate programme etc. Kwa sababu EU mara nyingi wanafuata programme za nchi, japan vilevile.

phillemon michael :dua fungu la ule msaada wa barabara za kili ,ulikuwa ni msaada wa mfadhili ambaye alielekeza specifically pesa ziende wapi,..hata wafadhili wana priority zao..kwa mfano hizo pesa zili cover pia kuboresha barabara kuelekea hifadhi ya kilimanjaro kupitia njia ya machame na marangu...pia kipindi hicho hicho barabara ya arusha to ngoro ngoro ikajengwa kwa kiwango cha lami....nafikiri kama sikosei hata ile ya kupita serengeti imefanyiwa ENVIRONMENTAL IMPACT ASSESSMENT...unajua wazungu wako very sensitive kusaidia maeneo ambayo pia na wao wanayatumia ,sasa kwenye vivutio vya utalii ni kati ya sehemu hizo...na hata siku moja huwezi kukata pesa ya kupeleka maji nzega kutuka lake victoria upeleke masaini...hiyo ilikuwa zamani na ikatuletea sifa mbaya ,,sasa hivi project management zinashirikisha wafadhili kuanzia hazina....
NIKUPE MFANO WA MILLENIUM GOAL mfuko wa wamarekani kwa nchi masikini ,juzi tu wamekuja hapa na wanafungua ofisi pale hazina ili kusimamia pesa zao zitumike kwa malengo waliyoweka.

Dua answered: PM Kama ni EU na Japan basi huu ni uongo wa hali ya juu kwa sababu hata siku moja EU hawachagui wanachotaka kwa vile sio taifa moja huwa wanaangalia Programme zenu. Japan ndio usiseme kabisa hawana interest hizo na wao sio wanaoongoza kwa Utalii bongo.

Mfano mzuri nikupe nchi zinazotoa pesa kama hizo i.e. KFW ya Ujerumani wao walitoa pesa za kujenga barabara ya Mombo - Lushoto kwa sababu wajerumani wa kwanza kuja Bongo walikupenda sana kule, kwa hiyo ndugu hizo pesa sio kweli zilitolewa kwa masharti. HUU NI MCHEZO UNAOFANYIKA HAPO BONGO. Mfano mwingine ni Mwanga water master Plan unafahamu nani anatoka huko. Usitufunge kamba hapa.


bugurunikwamnyamani added to the ans:

Mjomba mimi naweza kukusahihisha mambo mengi tu uliyosema hapo juu na yote ni katika kuweka FACTS sawa


Ninafanya kazi na organisation ambayo inatoamikopo katika nchi nyingi zinazoendelea na naweza kukuhakikishia kuwa huwa tuna tatizo kubwa sana katika baadhi ya nchi na hususwa za Africa kama kenya, Zimbabwe,Nigeria,Ghana,Zabaia,Uganda,Sudan na bila kuisahau Tanzania katika suala zima la kupunguza umasikini kuna UKABILA wa hali ya juuu katika proposals zao na hii inatokana na hao wanaowakilisha reports zao kuhusu miradi gani ifanyiwe kazi. Nitakupa mfano mdogo back in 90's Kenya kulikuwa na malalamiko makubwa kuhusu miradi mingi kwenda Rift Valley na Western Kenya kama Nyanza na Kakamega ili hali watu wanakufa na njaa Trukana na Marsabit vile vile mikoa ya Pwani iliachwa na ikapelekea movement ya jamaa wa COAST kutaka kujitenga na ikaundwa tume....kumbe baada ya uchunguzi kufanyika ikaja gundulika kuwa kulikuwa na Wakikuyu wanawapiga bao wajaluo ambako wao nao waliona isiwe tabu kwani wanao vigogo wao ambako walitaka investments ziende na kwao...

Si kweli kuwa wazungu ndio wenye kuweka priority bali ni nchi mwanachama kama Tanzania ambayo huwa tunahitaji tupate mikakati yao ya kupunguza umasikini na hapo ndipo jamaa wa Mipango wanawasilisha miyo Poverty Reduction Strategy Papers (PRSPs) na kusema ukweli ni kuwa mikoa mingi inayopewa kipaumbele mfano wa kurekebisha infrastructure Tanzania ni mikoa ya Kaskazini LAKINI SIYO KUTOKANA NA PRESHA ZA WAZUNGU kama ulivyosema bali

Vile vile umekosea kusema kuwa MILLENIUM DEVELOPMENT GOALS ni mfuko wa Wamerekani. Huuu ulikuwa ni mfuko ulioanzishwa na UNITED NATIONS kushirikisha member states zote za UN na kulikuwa na GOALS 8 ambazo walipeana kama njia za kumaliza umasikini na ofisi iliyofunguliwa DAR japo unaweza kufikiri iko independent lakini wako chini ya Country office ya UNDP


Nimeona bora nikuwekee hizo facts hapo juu na maneno yako kwamba JF imetekwa nyara hayana basis zozote. Tunajadili ukabila na sio mimi wala Mswahili tuliokwenda bungeni kuhoji. Umekuwa mgumu kusoma kilichotangulia na nimekuwekea tena hapa, ndio sababu ya kukwambia umedandia gari hujui linakokwenda. Sina chuki na kabila lolote Tanzania na sipendi ukabila unaoendekezwa na wewe pamoja na baadhi ya wachaga wenzio, kwa sababu hata hizi facts unazifumbia macho.
 
Worm.

SINA UGOMVI nao ila wameonesha kutokuwa waadilifu, kumbuka alipokuwa mama Mkapa Ikulu MAMBO mangapi yameharibika? kila mali ya serikali imechukuliwa kana kwamba waliopita mwanzo na kuziacha hizo mali kwa masilahi ya taifa ni wajinga.

nenda pale ILALA Amana kuna zile ghorofa za posta ambazo mama Mkapa na genge la kilimanjaro wamezipora. ina maana akina mzee kawawa walikuwa wajinga? au mama Maria Nyerere aliyeishi miaka mingi tu ikulu alikuwa mjinga na kuziacha mali za serikali? hawa watu hawana muamana.

kama msafiri mzuri ukisafiri na mnigeria ktk airport za ulaya basi immigration officers wa nchi za ulaya wanao deal na mnigeria huwa tofauti na anaye deal na mtu mwingine wanaodeal na wanigeria huwa ni special unit.

imejulikana kabila fulani si waadilifu si watenda haki kwanini tusiwatizame kwa macho mawili?
kuna mtu aliniambia kuwa Msumbiji ilipopata uhuru serikali yao ilisema haitaki wasomali na wachagga sijui kwanini kauli hiyo ilitoka.

Mwanakijiji.

nimekupa kila kitengo yuko nani? iweje unasema ni kituo kimoja tu au umekuwa makengeza kama Phillimon mikael? nimekupa Majina na sehemu walipo wachagga kwenye TRA nenda holili kuna bosi mchagga, border ya Tunduma kuna mchagga , border ya namanga kuna mchagga. long room Dar kuna wachagga, TRA mahajazi kuna wanachagga. tra wharf(bandari) kuna wachagga, container terminal ndio kabisa mdogo wake Lauwo NI MCHAGGA.
soma vizuri mwanzoni mwa michango yangu nimekuambia tatizo ni watendaji wengi ni wachagga sio policy maker ambao hawana impact yeyote TRA.

NA wewe FANYA utafiti ongea na mfanyakazi yeyote asiye mchagga TRA muulizie jeee kuna hali hiyo au laa? lakini wewe uko marekani na kuendelea kukanusha tu kitu bila kuwa na utafiti sioni kama unatutendea haki waTanzania.
TRA ina mchango mkubwa kwenye nchi mfano karibu asilimia 60 ya mapato ya nchi chanzo chake ni TRA SASA sehemu hiyo ikiwa chafu huoni tatizo?
hapo TRA kitengo nyeti ni kile cha ushuru na forodha ambacho kipo chini ya Lauwo mchagga na msaidizi wake ni kilimanjaro .
Mwanakijiji uliza tena umuhimu wa TRA kwa nchi labda hufahamu ndio maana unabisha tu. uozo mkubwa uko TRA na huko kukitengemaa basi faida kubwa kwa nchi.
 
Mswahili,
nenda pale ILALA Amana kuna zile ghorofa za posta ambazo mama Mkapa na genge la kilimanjaro wamezipora. ina maana akina mzee kawawa walikuwa wajinga? au mama Maria Nyerere aliyeishi miaka mingi tu ikulu alikuwa mjinga na kuziacha mali za serikali? hawa watu hawana muamana.
Ndugu yangu hapa umesema kitu ambacho kinasikitisha sana!...Binafsi sijali kama ni Ukabila ama Undugunization. Who cares kuhusu tafsiri anyway?.. vitu hivi lazima vikome na mali ya Umma yote lazima zirudishwe kwa wananchi hadi hapo utaratibu mzuri utakapo tumika!.
 
Mkandara.
vitarudi wapi? hizo nyumba zimekwenda na zile za sam Nujoma kachukua first lady huyo huyo toka KILIMANJARO sijui angekaa miaka aliyokaaa mama Maria nini kingebaki ungesikia hata makaburi ya kisutu ameokomba.miaka kumi tu vumbi lake zito.wenyewe waliotoka huko wanaogopana utasikia aisee yule ni wa machame yaani ogopa.
Mkandara kama tuna uchungu wa nchi basi turekebishe TRA hapo ndipo mapato ya nchi yanapopotea.
 
mswahili acha majungu...hata mzee mwinyi alihimiza waswahili msomi na muache tabia ya kukaa tu kupiga jungu kutwa,.kisa una kiunga chako cha minazi..wewe kalia kupiga jungu huku watu wanapiga kitabu..uzuri wa elimu hata mkibana ajira hapa watu wanaajiriwa proffesssionally botswana,marekani,uk,namibia ets uliza kuna maprofessa wangapi huko..na si waosha vyombo na wapiga soga kama wewe..kwanza inaonekana siku hizi kazi yako ya DISHWASHING umepumzika nini?
acha kupiga kungu,hiyo shule unayosema lini wamekuambia wana sera ya watoto 5.,ukweli ni kuwa wao wanachoangalia ni anayefaulu mtihani wao...hiyo ya mgao ndio nasikia kwako...au ulimpeleka yule mdogo wako akafeli ndio maana una hasira.
wewe kichwabata mimi sio mwanasiasa CHAMA CHANGU MIMI NI PESA TU..[YA HALALI],kama ni kadi za chama nilikua nayo ya youth league ,na ccm ,kwa misingi ya awali na imani za TANU basi,, sijawahi kuchukua nyingine...na mimi ni katika wale wasioamini ye mzee...naamini kuwa upinzani unatakiwa kuungwa mkono ili unawiri kwa manufaa ya UTAWALA BORA...lakini sio vile vyenye mrengo wa kidini kama chama chako...najua unajaribu kuhusisha mada hii na chama usichokipenda ..lakini hukitendei haki..huko ni ubakaji wa demokrasia...kama unapenda sana ukabila ni wewe,sio wote.

umepewa fact na wasomi kama mjj na wengine hapa ndani unakalia ubishi tu ..unataka kuvuna usikopanda...nakushauri uoteshe mbegu ..washauri hao wadogo zako watoto wa mjini waache mkole,mnanda na vingine..mjini unaposema leo hii dar ni ya kila mtu ...ndio maana tumeeondoa umeya wa jiji SAIGON sababu ya huu utoto wa mjini..kaka dito alikuwa akisema tuondoe tongo tongo..sasa tongo tongo hakuna watu wanafanya kazi na wanaleta maendeleo wewe unabakia kuumia ..huko mbezi,tabata,,hadi mbweni wanakaa wa kuja ...nyie mnaendelea kusogezwa MVUTI mnakuja kariakoo asubuhi kupiga soga.....sisitiza elimu kijana.
pamoja na dar kuwa mji mkubwa hadi karibuni ulikuwa mkoa wenye ratio ndogo kielimu kuondoa shule za tambaza .kibasila,azania,zanaki,ets zilizobinafsishwa hawakuwahi kujenga shule hadi pale keenja [wakuja] alipokuja kuwajengewa BEN MKAPA school..bado unasema wa njini wewe...na sasa serikali ya jk chini ya operatio inayosimamiwa na lowassa,mama sitta ,pinda,meya kimbisa na kandoro[wote wa kuja ]wanawajengea shule kila kata....kazi vitendo...hao saigon hawakujenga hata chekechea!!!!!!!

tufanye kazi kama taifa acha ukanda!!! ukabila ...!
 
Mswahili na Mzee Mwanakijiji nionvvyo mimi ninyi watu wawili siyo rahisi kukubaliana hoja kwa hoja. Na tatizo siyo kama Mswahili hajatoa data za kisayansi bali tatizo ni mgongano wa epistemological commitment and assumptions za jamaa hawa wawili kuhusu ukabila. Kwa hiyo jamani naona tu mkubaliane kutokukubaliana!!
 
nimepata kitabu chenye list ya majina ya staff TRA ,mswahili hatendi haki kuwachukia watu wa sehemu moja ya nchi yetu ,nimekipitia haraka haraka sioni ukabila anaohubiri ...nitajaribu kupioga hesabu ,nirudi...

mjj alikuletea mgawanyo wa makabila tanganyika ...kama kuna wa kulalamika ni wasukuma.wanyamwezi,warangi.wagogo,wangoni,benna,ha,ets kitendo chako cha kuegemea dar es salaama..kinaonyesha wewe una chuki binafsi na HUNA HOJA
 
Mlowezi,
Unaweza kutufafanulia "epistemological commitment?"
Wengine Kiingereza ni not reachable.
 
Samahani Jasusi, nitajaribu hapo ninamaanisha hivi: je vitu gani vinavyotushawishi tudai kama tunajua hicho tunachodai tunajua kama ni kweli? Kwa mfano hapa "ni nini kinachotufanya tuujue ukabila"
 
Back
Top Bottom