S. S. Phares
JF-Expert Member
- Nov 27, 2006
- 2,138
- 85
Sikubaliani na mawazo yako jinsi ya kupunguza ukabila TRA na sehemu nyingine.
mie sipendi watu waonewe ninatachokampeni ni fair play hata kama akiwa mchagga apewe fair play. lakini kutumbia kujaa watu TRA kwa sababu za kihistoria hiyo sikubali na pia njia yako ya kulitatua tatizo hili sio muafaka. ninachosema ni usawa kwa wote na hili ndio chochoko ya kukosekana amani sehemu nyingi na hata kusababisha migongano kwenye jamii.
I would like to treat other people the way i should like to be treated.
Mswahili
Lengo ni kufikia hapo unaposema...hebu tuangalie sasa njia mbali mbali za kutufikisha hapo.
Mimi napendekeza haya:
1. Usaili wa kazi ufanywe na panel la watu wasiopungua 3 kutoka vitengo tofauti. Vitengi gani vitahusika then itategemeana na aina ya kazi inayotangazwa.
2. Kuwe na vyombo huru vya kutetea maslahi ya wafanyakazi (hivi vya sasa vimemwagiwa sumu za kisiasa) na hatimaye ni kama vipo lakini havipo.
3. Katika ujazaji wa form za kazi, kuwe na kipengele kitakachomfanya muombaji atamke wazi na mapema kuwa tayari ana ndugu au hana ndugu katika idara husika ya serikali.
4. Kama anaye ndugundani ya idara husika then ifanyike internal assesment kama mhusika (muombaji kazi) na yule ambaye tayari ni mfanyakazi wanaweza kutekeleza majukumu yako bila kuwepo na conflict of interest katika mazingira ya kazi kiujumla.
5. Wafanyakazi waelimishwe nini maana halisi ya ukandamizaji ambao una misingi ya udini, ukabila au ubaguzi wa aina yoyote ile.
6. Kuwepo na hatua za wazi; zinazoelezea adhabu ya kukutwa na hatia ya kumbagua mfanyakazi yoyote kwa namna hizo hapo juu.
7. Kuwepo na review ya mara kwa mara ya jinsi ajira fulani fulani (random selection) zilivyopatikana katika idara mbalimbali za serikali. Kwa dhumuni la kujifunza makosa au kugundua ukiukwaji wa taratibu kama hizo hapo juu.
Kwa leo ni hayo.
Alamsiki.