Ukabila Ikulu, Ujenzi, Mambo ya nje, Mipango, TRA, BoT + Ofisi nyeti za serikali

Ukabila Ikulu, Ujenzi, Mambo ya nje, Mipango, TRA, BoT + Ofisi nyeti za serikali

Sasa unajua vigezo vyote? sasa wewe una Msc halafu unaajiriwa kama technician huoni qwazi kuwa hao wenye Msc hawajiamini? may be hata interview walifeli, wakatafute kazi ya size yao, kwanza ni mabwege kuajiriwa kama technician nawewe una masters, pambaf kabisa!!
 
..uamuzi wa mwisho wa nani aajriwe hufanywa na mtu mmoja. lakini process ya ku-interview na kuchuja waombaji kazi inatakiwa ifanywe na kamati ktk idara husika.

..pia elimu peke yake siyo kigezo cha kumpatia kazi muombaji. vigezo vingine vingi tu vinaweza kumkosesha kazi muombaji mwenye elimu kubwa kuliko wenzake.

..kwa mfano: unaweza kukuta muombaji ana qualify kielimu, lakini uzoefu wake wa kazi does not perfectly fit na nafasi ya kazi iliyotangazwa.

..pia unaweza ukakuta muombaji ana vigezo vyote, lakini ili ana-demand/ analipwa mshahara mkubwa hivyo kumkatisha tamaa muajiri mpya.

..wakati mwingine inaweza kutokea kwamba muombaji ni over-qualified. kwamba elimu yake, na uzoefu wake wa kazi, unamuweka juu zaidi ya majukumu ya kazi iliyotangazwa.
 
Jamani huyu mwanakijiji ni kiboko, yaani article hiyo alikuwa ameitunza kwa ajili gani? Sifa kwako mwanakijiji ingawa sijui ni kwa malengo gani uliitunza hiyo article ya mwalimu yenye facts hizo. Hata hivyo mimi mwenzenu nachukia mno mijadala isiyo na tija kwa taifa letu. mijadala ya ukabila na udini italiangamiza taifa hili. Watanzania sasa tumeishiwa na hoja na tumeanza kuangamizana wenyewe. Jee huu ndio uwazi na ukweli tunaoutangaza na kujivunia? Mimi nadhani huu ni ujinga na upumbavu.
 
ubaguzi wa ajira upo Bungeni unaratibiwa na DR.KASHILILLAH NA NOMBO.
 
Kwa kawaida ukishakuwa na Umri Mkubwa unakuwa umeona mambo mengi sana.
Mimi nina Umri wa kutosha sasa.
Naomba ni kanushe kuwa maeneo yote yaliyotajwa hayana Ukabila.
Wafanyakazi walioko pale wako kwa ajili ya elimu zao.
Kama umesoma na unafiti kwenye Fani lazima utapewa kazi.
Ukiuliza hapo utaambiwa wachaga wengi wako Ikulu, TRA, BOT n.k
Wote hao wamesoma Shule ndiyo Maana wako pale.
Watu wanaolalamikia Ukabila ni wale ambao hawakusoma na kama wamesoma sehemu kubwa wametawaliwa na majungu.
Kabila la Wahaya lilikuwa likisakamwa kwa kuwa na ukabila lakini si kweli, Wahaya ni watu wanaopenda sana kusoma na kujiendeleza Ndiyo maana Wanakuwa sehemu muhimu za kazi kwa ajili ya Uwezo walio nao.
Ukabila tanzania hauko kabisa.
 
Makabila mengine nayo yamesoma na wanaviwango vya elimu vinavyolingana na hao waliopo Bungeni, BOT, Hazina n.k. Tatizo utapataje nafasi huko bila kuwa na ndugu huko? Ni kweli wahaya na wachaga waliwahi kupata elimu kwa sababu za kihistoria, hivyo wakashika nafasi muhimu katika nchi hii mapema na wanawasidia ndugu zao kupata nafasi hizo. nyoka ni nyoka tu hata aking'oka meno
 
Yawezekana ndiyo makabila mengine ni wengi maeneo hayo ya kazi. Nionacho ni kwamba makabila yaliyo mengi hayana utamaduni wa kusaidiana, yamejaa majungu. Mimi si mchaga wa Mhaya, lakini hawa jamaa wanapenda kusaidiana na hata kuhabarishana. Mambo haya yanawainua sana.

Ukabila upo wala tusikanushe. Kwa mfano, kule mbeya kuna sintofahamu na maelewano yasiyo mazuri kati ya wanyakyusa wa Kyela na wale wa Rungwe. Hawa wanajiona bora kuliko wengine na kuchukiana pia. Jambo hilo ndilo lililopelekea kugawanyika kwa kanisa la Moravian kule Mbeya na kutengeneza Kanisa la Moravian (lililobakia Rungwe) na Kanisa la Kiinjili la Moravian , lililobakia maeneo ya Kyela. Ukabila upo TZ ingawa si kwa kiwango kikubwa.

Si vyema kuendekeza ukabila kwa sababu hauna tija kwa ustawi wetu sote, yaani kati ya wanaoendekeza ukabila na wasioendekeza.
 
Unapotaka kujadili ukabila u must be very smart otherwise utapotosha maana halisi ya hii maada.I don't have any doubt kwamba Tanzania kuna ukabila tena wa hali ya juu sana hasa makazini, ukimkuta Mpare boss basi atataka kuajili watu wa kabila lake, lazima ifike sehemu tuachie ukweli ujihidhirishe, kama ni kusoma kwa sasa Tanzania kila kabila watu wamesoma tena wapo wengi tu,huu ukabila ndo unatak kutufikisha hapa tulipo, logic ya kuajilii watu wa kabila lako ni kwamba ukiharibu, muyaongee kinyumbani yaishe na kuufunika huo uchafu.Tuwe makini sana na hili suala japo halina tija kuendelea kujadiliwa na lakini ni bora limewekwa wazi.
 
Sidhani kama hawa watu wapo huko kwasababu za kabila zao..kuna sababu nyingine za misngi zilizwafanya wajazane huko..hicho ndo cha kujadili.
 
Mkjj,
Kwanza ninawapa pongezi wanajambo wote kwa kukata issue!.mimi nimsomaji wa siku nyingi toka bcs lakini si mchangiaji.Lakini hii maada imenikumba hata mimi katika harakati zangu za maisha ya kazi,nilipokuwa ndani ya mfumo wa serikali
Hili swala ni gumu kwa kuangalia kwa inje,nikiwa na maana ya kuwa kama mtu si mwajiriwa wa serikali au shirika la umma lolote.
unachokisema ni sahihi kwa wakati huo,lakini kwasasa hivi makabila mengi wamesoma,lakini kwa sababu waliotangulia ni wa makabila hayo,basi kazi zitakwenda kwa kuangalia kama muombaji anatoka kwenye kabila lake au laa.hapa ninamaana hakuna usawa,hata hizo nafasi za shule zitakwenda kwa mfumo huo.kwa hiyo labda tujadili nia mbadala lakini ukweli ndiyo huo kwa mtu ambaye yupo ndani ya mfumo wa serikali unaona hili,lakini kwa mtu ambaye haupo ndani ya mfumo huo unaweza usikubaliane na mtoa hoja.Ninaomba kutoa .01%

nami nakupa 10
 
samvulechole... hakuna hoja ambayo ni ngeni hapa.. madai ya makabila hayo kupendelewa hayakuanza leo! tangu mara tu baada ya uhuru kulikuwa na tuhuma hizo hizo.. so.. there is nothing there..! Hata hivyo hatari unayoweza kuleta siyo ukabila bali ubaguzi, kuwa kama mtu anatoka kwenye makabila hayo basi asipewe nafasi fulani kwa vile watu fulani wanadhani kuna ukabila! Nitakupa mfano, kuna wanasheria watatu wote ni maprofesa... kuna Prof. Mwakalindile (Sheria, uzoefu miaka 30), Prof. Mtimba (mmakua, uzoefu miaka 10, sheria), na Prof. Chanda (Mzigua, sheria uzoefu miaka 5). Assuming maeneo ya fani zao ni sawa, ceteris paribus Rais anataka kumteua mshauri wa kisheria.. nani apewe kwa haki? Wengi watasema prof. Mwakalindile! Sasa kwa kufanya hivyo hata hivyo kuna wanyakyusa wawili tayari hapo ikulu ambao wameshapata nafasi zao, je tumnyime Mwakalindile kwa vile itaonesha ukabila?

Kabla hatujafikia hapo pa kudai ukabila tujiulize: "Kwanini inaonekana kuna wasomi wengi wa makabila hayo matatu Wachaga, Wahaya, na Wanyakyusa"? Je, tupunguze wanafunzi wanaotoka kwenye makabila hayo na kuwapa nafasi watu wa makabila mengine ili kuleta uwiano (parity)? Je tukiamua kufanya hivyo hatutakuwa tunaanza ubaguzi wa kikabila?

Tarehe 9 Disemba 1968 Nyerere alitumia siku ya Jamhuri kuzungumzia "Vitu ambavyo ni lazima Tuvisahihishe", vitu ambavyo baada ya uhuru havikwenda vilivyotarajiwa. Alizungumzia ukabila; kwanza alisema hivi:

"the man who talks about tribalism being practised without having any evidence for his statement is often a man who wants to stir up tribalism. Even if that is not his purpose, the result can be just the same. People will begin to think that there is tribalism, and, once people begin to think in these terms, then tribalism has begun to enter tinto our society"

Kuhusu Wahaya, Wanyakyusa, na Wachaga kupata nafasi nyingi katika serikali, Mwalimu alisema hivi miaka karibu 30 iliyopita:

"..the work of the civil servants and people in the parastatal organizations does require education..it so happened that the Tanzanians who had the opportunity for higher education under the colonialists were mostly Wahaya, Wachagga, and Wanyakyusa. And because most of the education was provided by missionaries, most of these people are also Christians. That was our inheritance. These conditions will change, but they have not changed yet. And for these reasons, when we get rid of the Europeans who were doing responsible jobs, and give these jobs to Tanzanians, the people who get them come mostly from one or other of these three tribes".

Akaongeza pia,

"Therefore, if you ask me why Wahaya, Wachagga, and Wanyakyusa have most of the jobs which require higher education, the answer is very obvious. They were the ones who received higher education during colonial times. I'd say: investigate the position in politics where a man is not asked about his educational qualifications. Look at the Parliament, the National Executive and Central Committee of TANU, and at the Cabinet. How many Wanyakyusa, Wahaya, or Wachagga are members? You will find that perhaps there aren't any, or there are one or two. This is the truth"

kwa umahiri wake wa maneno JKN akatoboa ukweli huu

"Anyone who refuses to accept a very obvious truth like this, and says that the reason is tribalism, must provide us with the evidence for his statement. If he cannot provide any evidence, we must conclude either that he is a fool, or that he is strirring up tribalism deliberately. He is the sort of (a) person who begs work on a tribal basis, and when he is refused because he does not have the capabilities, he pretends he was refused on tribal grounds."

Akasema pia ni jukumu la serikali kusaidia sehemu ambazo bado ziko nyuma kielimu. Na alimaliza kwa kusema:

".. if a Mchagga, a Mhaya, or a Mnyakyusayoung man were refused work simply because of his tribe - when he is capable and there is no other Tanzanian with the qualifications - then we would be practising a very stupid and very evil kind of tribalism such as that which caused the establishment of Biafra. I beg you, my brothers, avoid ANYTHING WHICH COULD BRING OUR COUNTRY INTO THIS KIND OF DISGRACE" (emphasis mine)
(From: Uhuru na Maendeleo pp 76,77)

so what say you?

Usengwili (Ahsante) Bambo Mwanakijiji, hatuna ukabila, sidhani, ukweli ndo huo, mimi kabla sijao, ma gifriend zangu takriban wote walikuwa ni wachagga (mimi si mchagga), hata shemeji yenu sasa ni mchagga, unajua kwa nini? kila nilipoishi au kusoma shule mademu waliokwepo wamekwenda shule atleast ni hao wa kichagga, nani atabisha? kila mtu afanye ka sensa kazini kwake au hata shuleni kila baada ya dada mmoja au wawili utakuta mchagga. WAZAZI wao walijua umuhimu wa shule mapema, sababu kubwa mwanakijiji keshaitoa hapo. sasa nikawa sina choice maana wa kwetu sikutani nao madarasani au kazini, wanaishia wapi, sijui! wanyakyusa vile vile wapo wengi sana makazini nani atabisha hilo? na kweli wana shule ya kutosha, wahaya nao vile vile wapo wengi tuu na shule zao si haba vile vile. Kama huamini chukua roster ya wanaojiunga na Vyuo mbali mbali vikuu au vinginevyo, utakuta akina Tarimo, Lyimo, Massawe, Urassa, Nkya, na wengineo wamejaa humo kibao, sasa kwa mantiki hiyo makabila mengine yatabaki nyuma siku zote. tupeleke watoto wetu shule jamani.
 
asiependa shule ni mjinga kabisaa,,, ujue haya makabila matatu wameitumia nafasi yao kielimu vizuri. sasa kama wanaelimu wasiajiriwe kwa vile mkubwa wa eneo ni kabila lake??
tuwape kazi wasio na ujuzi waliokimbilia ngomani?? hebu mtazame hata kuelimisha watoto wa kike,makabila mengine waliona kumpeleka shule mtoto wa kike ni ujinga,akae angoje kuolewa,uchagani wakawapa watoto wa kike kipaumbele,wakaelimika sasa hawa wakiajiriwa tuseme nini tena? ukabila,ubaguzi na rushwa ya ngono?🙄
 
Usengwili (Ahsante) Bambo Mwanakijiji, hatuna ukabila, sidhani, ukweli ndo huo, mimi kabla sijao, ma gifriend zangu takriban wote walikuwa ni wachagga (mimi si mchagga), hata shemeji yenu sasa ni mchagga, unajua kwa nini? kila nilipoishi au kusoma shule mademu waliokwepo wamekwenda shule atleast ni hao wa kichagga, nani atabisha? kila mtu afanye ka sensa kazini kwake au hata shuleni kila baada ya dada mmoja au wawili utakuta mchagga. WAZAZI wao walijua umuhimu wa shule mapema, sababu kubwa mwanakijiji keshaitoa hapo. sasa nikawa sina choice maana wa kwetu sikutani nao madarasani au kazini, wanaishia wapi, sijui! wanyakyusa vile vile wapo wengi sana makazini nani atabisha hilo? na kweli wana shule ya kutosha, wahaya nao vile vile wapo wengi tuu na shule zao si haba vile vile. Kama huamini chukua roster ya wanaojiunga na Vyuo mbali mbali vikuu au vinginevyo, utakuta akina Tarimo, Lyimo, Massawe, Urassa, Nkya, na wengineo wamejaa humo kibao, sasa kwa mantiki hiyo makabila mengine yatabaki nyuma siku zote. tupeleke watoto wetu shule jamani.

hapo penye kijani sasa,,,, ni ngumu kuwakuta wadada wa kindengereko,kimakonde,kimbulu kwenye hiyo list. ukiwakuta ni mmoja kati ya 50.tena ujue huyo alikua anaishi karibu mojawapo wa haya makabila 3.
 
hapo penye kijani sasa,,,, ni ngumu kuwakuta wadada wa kindengereko,kimakonde,kimbulu kwenye hiyo list. ukiwakuta ni mmoja kati ya 50.tena ujue huyo alikua anaishi karibu mojawapo wa haya makabila 3.

Ila wapo wengi tu magerezani na kaka zao sababu ya kuwa vibaka...sijawahi kusikia kibaka mchagga ingawa najua wapo...
 
kusema tuache kujadili ukabila na udini eti hauna tija si kweli, hauna tija kwa maana si msingi wa maendeleo ila una tija kwa sababu unagusa jamii nzima, ni kweli kabisa nowdays kuna maeneo kama wewe si mtu wa kabila fulani au dini fulani huwezsi pata kazi, na situation imekua worse nowdays kwani hata hao wanaowekwa ni wana elimu kama yako(vyuo vingi nowdays) kwa iyo wanawafunga mdomo kwa kigezo hata waliopo wana elimu sawa na wengine, ila inakua sio sawa kwa sababu waliingia apo sio kwa fair interview!
kuna mashirika huwezi sikia matangazo ya kazi au matangazo ya kazi yanabandikwa kwenye notice board apo ofisini wakati sio internal advert! sasa mzaramo wa kule mwanerumango atajuaje bila kua na mtu anayefanya kazi pale?
tena kwa sasa kamzizi ka udini kanakua kwa kasi ya ajabu ila tunajifanya hatuambiani kwa kuogopa kuonekana wapumbavu kama ktk ile riwaya ya mfalme aliyekua uchi ila ukisemqa yuko uchi utaonekana mjinga so kila mtu hadi rais mwenyewe anajijua yuko uchi!
udini its a timed bomb na sasa limegusa pabaya hadi kwenye siasa na michezo, tumefikia hatua watu wanawasifia au kuwaponda baadhi ya viongozi wa siasa au wanamichezo kwa sababu ya dini zao hata waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali wameingia ktk mkumbo uo!
tufungue macho na tuone ukweli uu na uwe adresses mapema!
 
Back
Top Bottom