Ukabila ndio umembeba Kenyatta, si sera!

Sasa ulitaka tamko lile watoe wakati gani??

Naona kamanda na wewe unasukumwa na misukumo ya hisia zilezile... Umelisikiliza tamko lenyewe?!! Toa hoja yako ndo uulize swali, kama hutoi hoja hutaeleweka uulizapo swali. Tunajadili kwa wema si kwa magomvi.... Toa mawazo yako pia
 
Sasa ulitaka tamko lile watoe wakati gani??

Mkodoleaji,
mimi mwenyewe hapa nilipo nina opinions zangu kibao kuhusu yanayoendelea kwenye uchaguzi wa Kenya lakini siwezi kuyaandika mpaka mshindi wa mwisho atangazwe. Sasa kama mtu asiyekuwa na umuhimu kama mimi ninajua na kuogopa madhara ya kutamka opinions kuhusu uchaguzi kabla haujawa concluded, je itakuwaje viongozi wa chama cha mgombea mkuu wasiheshimu?
Hata hivyo yule jamaa aliyetoa tamko wakati anaondoka alitabasamu, na kwa mimi ilinionyesha kuwa hali haijawa tense kihivyo baada ya kuona anatabasamu.
 
Naona kamanda na wewe unasukumwa na misukumo ya hisia zilezile... Umelisikiliza tamko lenyewe?!! Toa hoja yako ndo uulize swali, kama hutoi hoja hutaeleweka uulizapo swali. Tunajadili kwa wema si kwa magomvi.... Toa mawazo yako pia

Lubua wala sijasukumwa na hisia wale ni watu wanaotoa malalamiko, sasa sidhani kama unaweza kusema muda gani unafaa kwa malalamiko. Kwa sababu wanaweza kutoa baadaye mwingine akasema kwa nini hamkutoa wakati matokeo yameanza kutoka. Suala la kupigana litakuja kutokana na siasa za ukabila zilizojijenga kule kwao. Yaani kila mtu anaona mtu wao anafaa kuwa Rais
 

Nimekupata ZeMarcopolo
 
... Kenya Ukabila ... Tanzania Udini ... Which is worse?
 
... Kenya Ukabila ... Tanzania Udini ... Which is worse?
Tuombe Mungu udini uishie kwenye kuchinja tu, ukifikia kwenye uchaguzi mbona tutakuwa wakimbizi, sisi wenye majina ya asili ndo inaweza kuwa nafuu yetu.
 
Matokeo yanaonyesha tofauti. Sehemu zenye turn out kubwa zilikuwa ni around 25%. Mtu mmoja kumverify kupiga kura ilikuwa inachukua mpaka masaa mawili. Yule aliyetumia 40min ndiye aliyetumia muda mfupi, so watu wengi wameondoka bila kupiga kura.

mhh Marco.....dakika arobaini!!!!!!!
 
Kenya is for Kenyans, kwa vyovyote vile yatasemwa mengi!
 

Kamanda hilo usemalo ni la kweli wala silipingi. Lakini kwa mazingira ya uchaguzi wa Kenya wa mwaka huu wanasiasa wanatakiwa kuwa makini pale watoapo matamko yenye mwelekeo wa kupinga matokeo. Sidhani kama kwa hali halisi ya uchaguzi ule ilikuwa sahihi kwa CORD kuwa na press conference ikiwa tu vituo 5,000 kati ya 33,000 ndo vimetolewa matokeo.... Bado kulikuwa na vituo vipatavyo 28,000 ambavyo matokeo yake ni bado, kwa mujibu wa IEBC. Kumbuka 2007/2008 walishakufa watu zaidi ya 1,000 na wengine mamilioni wakaishia ukimbizini. Uchaguzi huu, kwa mujibu wa gazeti la mwananchi, wameshakufa watu wapatao 22. Kwa mazingira haya, si vyema kutoa matamshi ya namna ile, yaweza kuleta machafuko.
 
 

Uwezo mdogo wa kuchuja mambo,Jukwaa la Kenya politics huwezi hata changia kitu zaidi ni CDM na CCM!Jitahidi kufikiri nje ya BOX mkuu.Kila jambo na wakati wake.
 
Tuombe Mungu udini uishie kwenye kuchinja tu, ukifikia kwenye uchaguzi mbona tutakuwa wakimbizi, sisi wenye majina ya asili ndo inaweza kuwa nafuu yetu.

umeshasogea mkuu hadi kwenye kuchoma makanisa na zaidi ukiende Geita na buselesele hakuna mkiristo anayenunua kitu duka ya mwislamu na mwislam hanunui kwa mkristo.hapo ndipo jk katufikisha na chama chake!
 

Hauna akili wewe, na watu kama wewe ndo wachochezi
 
Huyu jamaa akiwa Raisi ile kesi yake ya mahakama ya kimataifa sijui itakuwaje,wataendelea kumfuatilia au watampotezea,yangu macho
 

Duuh! nahisi kuna ukweli kmenye kauli yako kuwa Odinga amegombea si tu kwa sababu anaamini anaweza kuongoza Wakenya, bali pia kwa sababu anadhani huu ni wakati muafaka wa Wajaluo kuongoza Kenya.
Radical Ethnicity is killing Kenya.!
 
Kenyatta Jomo amepanda mbegu moja mbaya sana Kenya. Aliwashawishi hata wazaliane ili waweze kushinda kwenye chaguzi zijazo. Naona sasa ndo yanatokea ila sidhani kama wakikuyu watashinda. Nna wasiwasi. Hii ngoma bado mbichi sana. Lets wait and see

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…