Kwa ujumla, uchaguzi wa Kenya umegubikwa na ukabila na hili si la kumtupia lawama mgombea mmoja tu. Odinga naye yumo humo, katika mkumbo huo huo. Anagombea si tu kwa sababu anadhani anaweza kuiongoza Kenya, bali pia kwa sababu anadhani ni wakati wa Wajaluo kuongoza. Bado huo ni ukabila na huo ndio pia unaomfanya naye asipate kura.
Chama chake kimetoa tamko baya sana muda mchache uliopita. Japokuwa mambo waliyoyaongea mengine yana mashiko, nadhani kwa ajili ya amani na usalama usingekuwa wakati wa kutoa tamko kama lile. Lile tamko laweza kuwachochea watu wakaanza machafuko.
Siasa za ukabila zinaletwa sana Tanzania na Serikali ya CCM. Ngoja waendelee kuupalilia nchini kwetu tuone nasi watatufikisha wapi. Tumwombe Mungu, siasa za sasa zimekuwa chai ya moto, ukinywa lazima upulize. Zinachoma