Ukabila ndio umembeba Kenyatta, si sera!

Ukabila ndio umembeba Kenyatta, si sera!

Kama mambo yenyewe ndo hayo kulikua na haja gani ya kutumia pesa nyingi kuweka hiyo system wakati inaweza kuvurugwa na watu tena wachache tu. Hili ni tatizo kubwa kwa nchi za Afrika, kuamua kuingia kwenye mfumo ambao hawajajipanga vizuri kuweza ku control risks. Ha ha ha sijui Afrika tulilaniwa na nani. Eh mungu tunusuru waafrika katika janga baya hili. Nawaombea Amani wakenya wote na Wa Afrika kwa ujumla.
 
Kama mambo yenyewe ndo hayo kulikua na haja gani ya kutumia pesa nyingi kuweka hiyo system wakati inaweza kuvurugwa na watu tena wachache tu. Hili ni tatizo kubwa kwa nchi za Afrika, kuamua kuingia kwenye mfumo ambao hawajajipanga vizuri kuweza ku control risks. Ha ha ha sijui Afrika tulilaniwa na nani. Eh mungu tunusuru waafrika katika janga baya hili. Nawaombea Amani wakenya wote na Wa Afrika kwa ujumla.

Halafu cha kushangaza zaidi Bw. Raila Odinga ni Waziri Mkuu (au alikuwa sielewi Katiba yao inasemaje hapo) mwenye nguvu na mamlaka karibu sawa na Raisi, ndio analia kuibiwa kura, sasa unajiuliza yeye ndio mkubwa wa Serikali ataliaje kuibiwa kura? Na ni nani amuibie wakati yeye ndiyo bosi? Ni mambo ya kustaajabisha sana!
 
Kamata mwizi men..ya CHADEMA itafanya kazi kwa hackers na crackers wa 2014 na 2015? Yangu macho.
 
UCHAGUZI MKUU 2013 WAINGIA DOSARI MTINDO MMOJA NA HOFU KUTANDA KOTE HUKU TUME IKILAZIMISHWA KUENDELEA KUTANGAZA
KURA ZILIZOCHAKACHULIWA.


Kuna taarifa ya kwamba Tume ya Uchaguzi nchini Kenya hadi hivi sasa wamelazimishwa KUENDELEA KUTANGAZA KURA ZILE ZILE kutoka SafariCom zilizochakachuliwa na kuweka pembeni zile karatasi walizoleta wawakilishi wa tume toka mashinani.

Katika kufanya ujanja huo na udanganyifu ule ule, wawakilishi wote wa vyama waliotilia sahihi kutoka mashinani wote wamekataliwa kuingia ndani ya ukumbi wa BOMAS wala kupewa fursa ya kuhakiki takwimu wanazopewa tume ile kabla ya kuzitangaza kwa umma.

Ajabu nyingine ni kwamba sasa idadi ya kura kuzidi idadi ya kura zilizopigwa na hata idadi ya watu waliojiandikisha ni jambo ambalo hivi sasa imetawala kwingi.

Jambo lingine la kustaajabisha hadi hivi sasa ni kwamba ile idadi kubwa ya kile kilichoitwa 'KURA ZILIZOHARIBIKA' zikikauka ghafla mara baada ya kugundulika ya kwamba KATIBA ya nchi hiyo inasema kwamba kura zilizoharibika nazo zitatumika idadi yake hiyo hiyo kwenye kutafuta asilimia kwa kila m
gombea.

Yapo madai kwamba kuna maelekezo kwamba kati ya wagombea wote katika uchaguzi wa nchi hiyo, kuna mgombea mmojawapo ambaye ikulu ya nchi hiyo imetoa maelekezo kwamba iwe isiwe lazima tume hiyo itafute kila njia ya kumfanya mshindi.

Mpaka sasa kuna vyama ambavyo tayari vimetoa maoni kwa tume ile kusitisha matangazo ya kura chakachuzi mara moja na kuruhusu wawakilishi wa vyama waliosaini makaratasi za matokeo kule mashinani kuzihakiki kwanza kabla ya kutangazwa.
 
TUME YA UCHAGUZI KENYA SASA YABARIKI ZA SAFARICOM NA KUSEMA NI KURA SAFI NA SALAMA

Mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi nchini Kenya sasa aleta mkanganyiko zaidi; aelezea ya kwamba zile kura za kule SafariCom alizolazimika kuzikataa hapo jana kwa kuwa yalikua yamechakachuliwa, leo asema zile zote ni kura safi na kwamba wala mitambo haikupata kuvamiwa wala matokeo kubadilishwa.

Muziki munene hapa.
 
KAMA SI MTAJI WA 'KURA 600,000 ZA KI-MALAIKA' RAILA ODINGA NDIYE ATAKUA AKIONGOZA KWENYE MATOKEO YA HIVI PUNDE KWA
KUMZIDI KENYATTA KURA 28,632

Naona ile fomula ya tofauti ya kura 600,000 (katika hesabu za yule anayesadikiwa kuongoza) iliotumika kule kwenye MATOKE YA KUPITIA KULE SAFARICOM yaliokataliwa na tume tena inaendelea kutumika hata sasa.

Kimsingi mtu ukitaka kujua matokeo sahihi kati ya wagombea hawa wa Kenya, kwanza kaondoe jumla ya kura laki 6 ndipo uanze kupiga mahesabu ya ki-ukweli.

Kwa mantiki hiyo, pale ambapo tumeambiwa ya kwamba vinara wawili hawa katika kinyang'anyiro cha kugombea urais hawa kura zao hadi sasa eti nikama ifuatavyo:

Licha ya kuripotiwa na Tume kwamba Uhuru Kenyatta amezoa 3,134,654 na Raila Odinga 2,563,286; mtu yeyote akijaribu tu kuondoa kwanza zile kura 600,000 zilizoingizwa ki-fomula ndipo utakapogundua kwamba kura za kikweli za Mhe Uhuru Kenyatta ni 2,534,654 dhidi ya zile za mpinzani wake wa karibu Raila Odinga zikisimama pale kwenye 2,563,286.

Naam, hadi hapo hii itakua na maana kwamba ni Raila Odinga ndiye atakayekua akiongoza kwa kumuacha nyuma kwa kura 28,632 hadi hivi sasa.


Great Thinkers, kidogo mtu akifanya udadisi makini utagundua ya kwamba kinachofanyika pale Bomas hadi hivi sasa ni ka-mchezo to mdogo tu kwenye Excel.

Sasa mtu ukijiuliza lengo hasa hapa utagundua ya kwamba Ikulu ya Rais Kibaki KATU HAITAKI KITU Marudio ya kupigiwa kura kati ya Kenyatta na Raila kwa kuwa wanakumbuka utafiti wa Synovet ilivyoelekeza ukweli mtupu.

Naam, mara baada ya mtu kujisumbua japo kidogo akilini kwa kuondoa tu zile kura 600,000 zilizopenyezwa hata kule kwenye MATOKEO YA KWENYE MAKARATASI KULE BOMAS hivi sasa utagundua ukweli ule ule waliouona watu wa Synoveta na watafiti wengine kibao nchini humo.

Ndio, kwa hesabu haka kadogo tu ya kuondoa kale ka 600,00 ya uongo ki-fomula mtu yeyote atagundua kwamba hadi hivi sasa anayestahili kuwa mbele katika hayo matokeo ya Nairobi hadi dakika hii ni Raila Odinga akiwa na kura 2,563,286 akifuatwa na Uhuru kwa kura 2,534,654 kukiwa kuna tofauti ndogo sana ya 28,632 peke yake.

Kimsingi ukiangalia hoja yangu hapo juu utagundua ya kwamba kule kuondoa kwanza zile 'KURA ZA KI-MALAIKA MICROSOFT EXCEL 600,000', hii njia ninayozungumzia hapa inakubaliana moja kwa moja na ukweli kwamba si Raila Odinga wala Uhuru Kenyatta atakayeweza kufikia asilimia 51% ya kura zote zilizopigwa nchini humo ila tu wawili hao wataalazimika kwenda kwenye ngwe ya pili ili rais wa kweli nchini humo aweze kupatikana.

Tofauti sana na hii hoja yangu hapa juu, kuna hatari kubwa wapiga kura wa Kenya wakaishia kumuingiza 'RAIS WA MICROSOFT EXCEL' ikulu. Jambo hilo likiruhusiwa kutokea basi kimahesabu za haraka haraka 'SERIKALI YA MICROSOFT EXCEL' itakayozaliwa kwa mtaji wa kura za kipaumbele 600,000 italazimika KUTUMIA GHARAMA KUBWA MNO kutafuta kujihalalisha kwa wananchi ambapo utabiri wangu unaona dalili za akina Dr Ulimboka wetu huyu, Absalom Kibanda kuibuka kule Nairobi kwa kasi kubwa ajabu.

Kikubwa siku zote ni HAKI KWANZA kisha huu wimbo wa AMANI utafuaata tu mkondo wake bila hata ya mtu yeyote kulazimika kupanga polisi kibao barabarani kwenda kuwaua raia kama anavyofanya hivi sasa huyu 'RAIS WETU HUYU WA MICROSOFT EXCEL' pale Magogoni.
 
Mi naona hata hapa kwetu Tz tujifunze na tusikubali mfumo huo wa kujumlisha kura 2015, bali twende kwa hardcopy!
Afadhali tumeyaona Kenya kabla ya 2015.

Mnaonaje wadau?

si ajabu hata hao ma hackers walitoka bongo. TZ ni chuo cha wizi na kufix election africa mashariki na kati na kusini.
 
Kinachonishanga ni kwamba jumulisha kura za odinga na kura za wagombea wengine bado hawamfikii uhuru!inamaana wakenya wengi wanampenda uhuru tu.hapa kuna kitu.
 
Kura zinazoendelea kuhesabiwa kwenye uchaguzi wa Kenya inaonyesha jinsi Kabila moja halina haki ya kuchagua mgombea wa kabila jingine. Takwimu za kura toka central na Nyanza zinathibitisha.Mwl Nyerere aliwahi sema,Ukabila na sawa na mtu anaekula nyama ya watu.Hawezi acha. Napendekeza nchi ya kenya igawiwe kwa nchi za Africa mashariki na isiwepo tena. hii dhambi ya ukabila kidemocrasia iweze kuisha
 
SIRI YA USHINDI WA UHURUKENYATTA, MSHINDI WA UCHAGUZI WA URAISKENYA 2013
1. Ukubwa wakabila lake ambalo linaundwa zaidi ya asilimia 30 ya wakenya wote.
a. Kiambu amepata kura 442,042
b. Murang’a kura264, 758
c. Nakuru 232,805
d. Kericho190,287
Hii ni idadi kubwa kabisaya kura ambazo zinazidi maeneo yote yenye ushawishi kwa Raila
2. Kuungana naRuto
 
Wengine tupo mbali na TV, je ameshinda kweli? na ni asilimia ngapi? kama ni kweli hongera zake
 
Hakuna mshindi, uchaguzi unarudiwa. Kumbuka Uhuru amepata 49.5% na Raila amepata 44.5%. Hakuna aliyepata 50%+1vote kama katiba inavyosema. Ngoma bado.
 
Hakuna mshindi, uchaguzi unarudiwa. Kumbuka Uhuru amepata 49.5% na Raila amepata 44.5%. Hakuna aliyepata 50%+1vote kama katiba inavyosema. Ngoma bado.

bora urudiwe, na wakirudia wahesabu manually sio kwa kutumia walichokiita teknolojia mpya ambayo ilizingua wakati zoezi la uhesabuji kura likiendelea. Viva Odinga
 
Ukabila umezidi competence..
I still am sure that Uhuru is too young for that office.
I stand to be corrected.

Wewe ni m-TZ?

Mbona nyie mlimwamini Kikwete katika umri huo? Acheni wivu wakuu, mwache kijana akapige kazi maana mwenzetu amepiga shule ya uhakika siyo huyu wa kwetu tulidhani kasoma uchumi kumbe kasomewa uchumi!! Sasa hivi hapa kwetu kuna mkakati wa kushusha umri wa urais uwe chini ya miaka 40, inakuwaje kwa wenzetu tunawalalamikia kwa kumchagua mwenye miaka 52?

Go! Uhuru go my brother!!! Nchi imekuamini.
 
Back
Top Bottom