Ukabila ni jambo lisilo semwa sana nchini lakini lipo sana kazini/maofisini

Ukabila ni jambo lisilo semwa sana nchini lakini lipo sana kazini/maofisini

Kama utahitaji kupinga hili basi wewe ni mbishi tu tangu kuzaliwa.

Ukabila nchi hii upo nje nje kabisa ni rahisi sana kukuta watu wa kabila moja wako zaidi 96% kuliko makabila mengine ikiwa tu Boss ni wa kabila husika.

Utafiti wangu mfupi nimebaini hili jambo lipo katika kila sehemu halafu sio Tanzania tu hata kwa wenzetu.

Ikitokea Boss akatimliwa basi Boss ataye kuja lazima atakuja na safu yake na ataanza kufukuza watu alio wakuta kwa style fulani fulani au kuwashusha vyeo pamoja na kuwapunguzia mishahala ili mradi tu waichukie kazi na kuacha alete wa kwakwe.

Hapa kuna kitengo cha wakina shomire nimekuja kugundua kati ya wafanyakzi 44 wa kitengo hicho ni 11 tu ndo sio kabila husika na la boss.

Ukienda kwa wakina shirima na shayo usiseme ukigeuka wakina mwamposa na mwandosya wao hata aibu hawana wamepangana kaka mtu na wadogo mtu kitengo kimoja(hapa nazungumzia ingekuwa shuleni basi mkuu wa shule,second na mtaaluma wote wawe wa tumbo moja).

Basi ukija kwangu wakina malendeja na masanja hali ni ile ile na makabila mengine ni vilevile.

Hali hii hadi makanisani hasa haya makanisa ya wajasiria mali njaa. Mambo ni yaleyale.
Vijana wengi wameumizwa sana.

Mwishoni mwa mwaka jana kuna Boss alifukuzwa kazi kwa kuendekeza U simba na yanga.Ilikuwa ukiwa simba basi usijionyeshe hadharani wewe na ushabiki wako na kilichofanya afukuzwe kazi aliwapa ruhusa mashabaki wote wa yanga kwenda kuangalia mpira akabaki na mashabiki wa simba wa siku hiyo hiki kitendo kiliwakera mashabiki wa simba hadi kwenda nae HR Ukiambatanisha na kero na tuhuma za nyuma za mambo hayahaya akafukuzwa kazi.Na ndiko tuendako nawaambieni ipo siku hili litakuwa kubwa pia.

Nadhani mmekwisha kuona kwenye msiba au sherehekuna madaftari ya simba na yanga na mbwembwe zingine za kijinga.(Nimeunganisha hili pia maana linafanana na ubaguzi wa kikabila tu)

Pia kuna hii tabia ya kuangalia usoni na kupeana kazi hii hadi kwenye teuzi huko majuu wizarani hii tabia ishaota matawi na kuzaa watoto hadi vitukuu. Imefikia wakati sasa hadi ualimu wanaajiri kwa kujuana huyu ni mtoto wa mjomba,dada,shangazi ama wa baba mdogo.

Muda sio mrefu tutawafikia kenya na kuwazidi mpo hapa. Sasa hivi hata kama CV yako imeshiba namna gani bila connection wewe kauze mayai mtaani tu hakuna atakaye jari hata kidogo na pengine Cv yako utaikuta jararani huko imetupiliwa mbali.

Hii hali ndo imetufikisha hapa kupata wataalumu wasio na weredi wowote kwani kazi wamepeana kwa kujuana au kwa rushwa.Wengi sana waapo mtaani wenye sifa kuliko waliomo maofisini.

Mfano mdogo tu nenda mahospital kuanzia mapokezi utakavyokuwa unajibiwa kana kwamba huyo anayekupatia huduma kalazamishwa kuisomea hiyo kazi ni very careless.,

Niliwahi kulazwa hospital fln kubwa (VIP) Asubuhi ile kuna mdada mfanya usafi anadeki kwenye chumba changu nami nimelala basi akiwa anaendelea na usafi Dr wangu akaingia na kuchafua pale.Baada ya Dr kutoka yule binti mfanya usafi alimfyonza na kisha kutoa maneno makali.

Ni kamwambia ujue hii kazi yako inategemea watu wachafue ndo ufanye usafi imagine kama pangekuwa pa safi siku zote hapa wewe ungeipata hii ajira? Hujui kwamba huyu Dr pengine anahudumia wagonjwa zaidi ya 100 na hapo ukute ana kipindi anaenda kufundisha?(Dr alikuwa ni profesa maana mara kadhaa alikuwa anakuja na wanafunzi wake kuniuliza maswali)

Nilijikaza kumwelewesha yule binti na mwisho ni kamwambia haya ndiyo madhara ya kupeana kazi kwa kujuana. Siku ukifanikiwa ukawa na kampuni yako usifanye makosa haya .

Tusipokuwa na umoja na kutanguliza maslahi ya Taifa kwanza ipo siku hali itakuwa mbaya sana na tutakuwa tumechelewa mno kuliko sasa.
Upo kweli ila Sio mkubwa kama unavyo ukuza wewe... tena ni watu wa kanda fulani ndo wanahiyo tabia.. lakini mamlaka zikiamua kuwashughulukia, unaacha maramoja.....
 
Siyo kweli kuwa wachaga wanaweza kujiajiri wote. hapa nilipowataja kama wakina shirima na shayo ndo wachaga wenyewe.Kuna idara wamejazana hadi wakati fulani kichaga imegeuka kuwa lugha ya mawasiliano mle.Nilijua tabia ya kuongea kilugha hadharani ni ya wasukuma na waha kumbe hata wachaga.
Kwa kweli Wachagga unawaonea tu ila hata wakiwa 100 ofisini na wewe pekee ni Mndengereko utapendwa nao sana na utoenjoy, shida ni Wahaya, Wasukuma na Wanyakyusa, itabidi uhame haraka hapo.
 
Hi
Shida hii ipo kubwa mno hasa ukiajiriwa ndo utaiona ukiwa mtaani unaweza usijue kwa maneno wanyotoa wahusika!
Yo kitaalamu inaitwa instructional discrimination na ndio mbaya kuliko apartheid hii nishaulizwa jhpiego wakati nimefika kwa top are you mshomile ohh are you muslim?? Yaani nitakufa nayo hii
 
Mm
Huwa najiuliza hata ukiwa kiongozi unaweza kupambana vipi na ukabila maofisini?
Maana kwenye usaili unaweza usiitwe kabila na mbaya zaidi majina yetu hasa surname ndo kielelezo cha makabila yetu.Boss akiona cv yako tu na kisha akaona cv ya kaijage basi mchezo umeisha inatupwa kabisa na haitaoneana.

Je wewe kama mdau unaweza pambana nalo vipi jambo hili?
Ningepinga jina lolote la kikabila mtu angekua na majina mawili ya kizungu au kiarabu la mwisho lazima aitwe tanzania mfano fatuma juma tanzania Peter Albert tanzania
 
Wao sio wabaya kama wengine na kwa sababu wapo ofisi nyingi watu hufikiri ni wakabila.
 
Pwani wako hivyo ukiwa mkristo na siyo kabila lao funga biashara yako
Hapa ndio umeharibu uzi wako woooote kwa kusema uwongo,

Labda useme udini unakusumbua, ila kwa ukabila hilo halipo pwani kabisaaaa bwashee, hakuna watu wakarimu na wanawapokea wageni hata kutoka inje ya invhi na kuishi nao vizuri na kwa wema kama wa pwani,

Na ndio maana leo dar es salaam inamilikiwa na wageni watupu, wenyeji wameenda inje ya mji,
Matokeo yake wanaambiwa eti wavivu

Uislamu ni uadilifu, na hili hutalikuta kwa wasio waislamu

Inchi hii ungesema imejaa udini kwenye ajira tungekuelewa vizuri zaidi, na ubaguzi mwingi upo baraaaaaa
 
Unazungumzia Dar mimi nimesema pwani. Dar unayoisemea wewe wenyeji hawapo Tena. Mimi nimeishi pwani kisarawe huko najua Kila rangi nasio nimeishi kisarawe mini vijijinj huko.

Pwani ni wabaguzi sana kidini sasa wala usiseme
 
Juzi kati hapa kuna boss mmoja ana kampuni yake binafsi aliniomba nikamsaidie kuwafanyia interview vijana flani wa kike na kiume,ktk ile panel tulimpitisha binti mmoja wa kike aliekua kavaa ushungi na ana jina la kiislamu kwa sababu ndie aliyeweza kujibu maswali vizuri na pia alikua na uzoefu wa ile kazi,tulivyompelekea yule boss jina la yule binti cha kushangaza akamkataa eti kisa ni muislamu,akasema yeye kwenye office yake hataki watu waislamu hivyo akasema tumchukue candidate number mbili aliyekua mkristo.
Kwa kweli nilihudhunika na kushangaa sana.
 
Haikuwa bahati yake .
 
Mijitu toka bara huko ndio inaendekeza udini na ukabila,mingine imekaribishwa dar sasa hivi inaanzisha kampeni dar es salaam ibadilishwe jina,wenye mji wao wanawachora tu
 
Juzi kati hapa kuna boss mmoja ana kampuni yake binafsi aliniomba nikamsaidie kuwafanyia interview vijana flani wa kike na kiume,ktk ile panel tulimpitisha binti mmoja wa kike aliekua kavaa ushungi na ana jina la kiislamu kwa sababu ndie aliyeweza kujibu maswali vizuri na pia alikua na uzoefu wa ile kazi,tulivyompelekea yule boss jina la yule binti cha kushangaza akamkataa eti kisa ni muislamu,akasema yeye kwenye office yake hataki watu waislamu hivyo akasema tumchukue candidate number mbili aliyekua mkristo.
Kwa kweli nilihudhunika na kushangaa sana.
Ona sasa, si nimesema mimi, udini tu basi, halafu wanajifichia kwenye ukabila
Udini unawasumbua
 
Unazungumzia Dar mimi nimesema pwani. Dar unayoisemea wewe wenyeji hawapo Tena. Mimi nimeishi pwani kisarawe huko najua Kila rangi nasio nimeishi kisarawe mini vijijinj huko.

Pwani ni wabaguzi sana kidini sasa wala usiseme
Soma hapo post #132

Kwa pwani udini na ubaguzi unawasingizia,
Jamaa wanaishi na kila mtu vyema sana, wako poa sana
 
Back
Top Bottom