Ukabila, ukanda, udini, ubinafsi na siasa vitaigawa Tanzania siku za usoni, tuvikemee

Ukabila, ukanda, udini, ubinafsi na siasa vitaigawa Tanzania siku za usoni, tuvikemee

Tman900

JF-Expert Member
Joined
May 30, 2017
Posts
589
Reaction score
1,897
Ukitazama Muundo wa Kupata kazi sehemu Nyingi za Serikali, kumekua na Ukabila, Ukanda, Udini, Ubinafsi na siasa, hivi vimetawala Sana katika akili za watu wengi, ninachokiona kupitia hivyo, siku zijazo vitatumika kuligawa hili Taifa.

Mfano wazanzibar walioko katika Vyombo vya usalama na sekta zingine za Serikali wanaonesha kujitenga waziwazi Ila ukimpa nafasi ya kumsoma Vizuri utaona hawa wanajitenga na Ubinafsi wa kujiona wao wako sahihi Kuliko wengine pia wanapeana kipaumbele wawapo katika sekta Moja hili linafanyika na watu wote Bara na Visiwani.

Ninachokiona kwa Mtazamo wa baadae watu wenye Nia mbaya Tanzania wanaweza tumia huo mwanya kuleta mgawanyo au kuchafua Amani ya Tanzania.

Kingine sisi sio wabunifu wa dhana na vifaa vya ki Technology ya Sasa. Maana Majeshi yote Duniani kwa Sasa yanawekeza katika Ubunifu, science, ukitazama mfano India wanauza Sana Vifaa vya Kijeshi AFRICA, China pia soko lao liko Africa kuuza dhana za Kijeshi.

Ila ukitazama kwa Upande mwingine Mifumo yetu hairuhusu watu kuwa wabunifu, ila wanategemea kununua dhana na vifaa kutoka mataifa Mengine ambayo wamewekeza ktk Ubunifu.

Kwa Africa (Tanzania) yaani ukiweza kufanya Ubunifu hata wa mlipuko au dhana inayoweza kutumika Kijeshi, utaonekana mtu wa ajabu na utapata taabu Sana kwa Ubunifu uliogundua.

Ninachokiona Kuna vipaji vingi na Ubunifu mwingi unapoteza kwa Watu wa wanaoishi Africa.
 
Hatuna watu wenye za kutosha kuligawa hili Taifa, siku zote 'nyumbu' huwa wanapenda umoja.
 
Back
Top Bottom