Ukaguzi viwango na uthibitishaji wa dawa za kuongeza maumbile mamlaka zinazingatia nini?

Ukaguzi viwango na uthibitishaji wa dawa za kuongeza maumbile mamlaka zinazingatia nini?

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
Habari Wakuu,

Kumekuwa na Ofisi mbalimbali zilizopewa vibali vya kuuza madawa ya kuongeza maumbile (Uume kwa Wanaume) na Shepu kwa wanawake. Ofisi hizo zimekuwa huru na zinajitangaza hadharani sambamba na kusifia huduma zao.

Nimewauliza wataalamu wa Afya kadhaa wanadai hakuna dawa iliyothibitishwa kitaalamu yenye kazi ya kukuza uume labda iwe kwa njia ya upasuaji. Sasa najiuliza kama madaktari na hospitali hakuna huduma kama hizo hizi Ofisi kama Ujana, Ujani zinazonadi dawa zao na kuwavutia watu kununua, inakuaji? Mamlaka zinazosimamia madawa zinapimaje ubora wa dawa zao na kutoa vibali zikauzwa kwa wananchi.

Vipi ikiwa kama wananchi wanashawishika kuzinunua dawa hizo wakati hazifanyi kazi iliyokusudiwa kama Wataalamu wa Afya wanavyodai?

Tunaomba ufafanuzi
 
Back
Top Bottom