Ukaguzi wa CAG 2021: Halmashauri zilizopata Hati Mbaya zimepungua

Ukaguzi wa CAG 2021: Halmashauri zilizopata Hati Mbaya zimepungua

benzemah

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2014
Posts
1,533
Reaction score
3,187
Mwaka wa fedha 2020/21
Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG) kuhusu ukaguzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kwa mwaka wa fedha 2020/21 zinaonesha kuimarika ikiwa ni kielelezo kuimarika kwa usimamizi wa fedha katika ngazi hiyo.

Halmashauri zilizopata Hati Zinazoridhisha (Hati Safi) zimeongezeka kutoka Halmashauri 124 (67%) mwaka wa fedha 2019/20 hadi Halmashauri 178 (96%) mwaka 2020/21.

Halmashauri zilizopata Hati Zenye Shaka zimepungua kutoka Halmashauri 53 (29%) mwaka 2019/20 hadi Halmashauri 6 (3%) mwaka 2020/21.

Halmashauri zilizopata Hati Mbaya zimepungua kutoka Halmashauri 8 (4%) mwaka 2019/20 hadi Halmashauri 1 (1%) mwaka 2020/21.

 
Back
Top Bottom