Ukaguzi wa CAG usiozingatiwa ni wa nini?

Wapinzani wa bongo wanataka katiba mpya ili nao waonje madaraka
 
CAG kimekua chombo cha udhalilishaji.

Kama mtu anatajwa kufanya jambo halafu hakuna hatua inachukuliwa kujua ukweli wake hiyo ni sawa na kumtusi.

Baada ya ripoti ya CAG tuone vitendo vya kuwawajibisha walioguswa ili kama ni uongo mtu awe cleared.

Ila CAG anakuja anasema ooh kuna hela zimefichwa mahali , hatuoni efforts za kuzirudisha kama kweli zipo.

Inabakia kuwa uzushi.

Na ndicho anachofanya sasa CAG kuzuazua mambo tu ambayo hayana ukweli wowote.
 
CCM wajanja sana, baada ya kuona Upinzani unanunulika kupitia Mwendazake na zile slogan za kuunga juhudi,naona Mama yeye ana wanunua Wapinzani kupitia slogan ya Maridhiano!!
 

Ndugu pana mambo hapa ni vyema kuyaweka sawa.

Ni muhimu tutofautishe siasa na uhalisia:

Kwamba, "Pesa ya walipakodi ila sio ya serikali...."

Hilo ni siasa zisizomsaidia mtu yeyote. Labda tu, kama ni kwa ajili ya mabishano yasiyokuwa na kichwa wala miguu.

".. so ni kweli kwamba PAC ikiwa na mpinzani serious basi inakua na makali."

Hapa napo itakuwa labda una maana wananchi kupata haki ni kudra za mola. Kwamba awepo si mpinzani tu, bali awe serious vinginevyo imekula kwao?

Kufanikisha mawili hayo kwa pamoja huoni kuwa yahitaji matambiko ya aina yake ndugu?

".. hawakuchaguliwa na wananchi ndio maana nikasema whether iwe JPM au wananchi it doesn't matter ..."

Kumbuka mapema ulikuwa umetupa lawama kwa wananchi kuwa wao ndiyo waliowachagua wabunge hao.

Kwa mwendo huu hausomeki kwani uko kila mahali. Haieleweki unasimama wapi. Uko kama haikuhusu.

Kwamba labda wewe ni kama malaika fulani unayeelea juu kwa juu ukitumwagia nasaha kwa matumizi yetu ya baadaye?

Kazi kweli kweli.

Tambua hapa pana wezi wametajwa. Kuna yule polisi aliyekimbia na mabilioni. Hadi sasa hakuna jina wala picha yake. Anatafutwa kweli huyo? Iko mifano kadhaa ya hayo. Yote yanahitaji mpinzani serious na mijadala bungeni?

Wengi hawaoni hivyo. CCM hawaoni hivyo. Ila wewe mjomba?

Ama kwa hakika:

Haileweki unajaribu kusema nini hasa au hata kutokea wapi?



 

Huyo mwamba anaakisi watanzania tulio wengi tusivyokuwa na uzoefu wa mijadala.

Badala ya kutoa mawazo yake mtanzania hudhani anachosema yeye ni final and terminate.

Anawasilisha nadharia hata kama anajua uhalisia ukoje.

Anadhani muelimika ni yeye tu, wengine wote ni wajinga. Anakosa utulivu, busara au unyenyekevu kwenye mijadala. Kimsingi mtanzania ni mjuaji mno.

Ninajikusanya kuandika uzi mahsusi kumhusu mtanzania ambaye pia nami ni mjumbe.
 
Hi ofisi sasa hivi imekuwa haina mpango zamani ilikuwa inaheshimika sana.
Wanasiasa wameiharibu.Hata teuzi zake sasa hivi watu watakubali ili kupiga perdiem tu.
 
Kwahio shida ipo kwenye KUKAGUA tusikague au kwenye Kufuatilia ? Wafuatiliaji hawafuatilii ?
 
Kwamba, "Pesa ya walipakodi ila sio ya serikali...."

Hilo ni siasa zisizomsaidia mtu yeyote. Labda tu, kama ni kwa ajili ya mabishano yasiyokuwa na kichwa wala miguu.
Hoja hapo ni kwamba bajeti ya CAG Inapendekezwa na bunge ila bajeti zingine ZOTE zinapendekezwa na Serikali Sasa Kuna siasa Gani hapo wakati ni uhalisia. Huwezi mtuhumiwa ukaandaa bajeti ya anayekuja kukukagua itaondoa makali ya ukaguzi. Sasa siasa ikwapi hapo?


Hapa napo itakuwa labda una maana wananchi kupata haki ni kudra za mola. Kwamba awepo si mpinzani tu, bali awe serious vinginevyo imekula kwao?

Kufanikisha mawili hayo huoni kuwa yahitaji matambiko ya aina yake?
Na ndio maana kamati za PAC na LAAC zinapaswa kuwa chini ya upinzani maana Hana maslahi ya Moja kwa Moja na chama tawala so anakagua kwa weledi. Na nimesema kwa ushahidi kwamba between 2009 na 2015 mawaziri sio chini ya 10 waliondolewa kwa ripoti za CAG baada ya mapendekezo ya PAC. So kumbe inawezekana kabisa hii kamati ikawa na makali kama ikiwa A. Chini ya Upinzani B. Mpinzani makini (maana sio Kila mpinzani ni makini).


hawakuchaguliwa na wananchi ndio maana nikasema whether iwe JPM au wananchi it doesn't matter ..."

Kumbuka mapema ulikuwa umetupa lawama kwa wananchi kuwa wao ndiyo waliowachagua wabunge hao.
Aisee mkuu usinilishe maneno... Kwanini umeikata hiyo sentesi yangu? Mimi naongelea uhalisia sio siasa, kiuhalisia wananchi huchagua wabunge ila mkuu hapo alipinga ndio nikasema WHETHER JPM or Wananchi (Ili kumpa benefit of doubt) waliwachagua it doesn't matter maana kisheria wao ni wabunge hivyo ndio pekee wenye mandate ya kushughulikia ripoti ya CAG. Sasa hapo uongo ni upi? Au unadhani hata tusipowatambua sheria itaacha kuwatambua?

Hata Mnyika juzi kasema sheria ya katiba mpya itapitishwa na hao hao wabunge!! Meaning hata kama hatuwataki au kutambua wao pekee kisheria ndio wanaweza pitisha muswada.
Wewe ndio huelewi mjadala umeanzia wapi, huyo mkuu alimlaumu CAG kula mshahara wa Bure ndio nikamjibu yeye sio kazi yake kuchukua hatua Bali BUNGE. Ndio nikamwambia bunge la Sasa LINACHUKUA hatua maana ripoti huwa lazima ijadiliwe tatizo ni MAPENDEKEZO huwa sio makali sababu limehodhiwa na CCM. Mbona hoja inaeleweka wazi kabisa kwamba shida ni dominance ya CCM bungeni ndio inafanya haya meaning solution ni kuongeza wapinzani makini Ili uwajibikaji uwepo kama tu US au UK.
Hapana wabunge hawawezi laumu serikali ndio maana Spika amesema ni uzembe wa bunge kutofanya kaguzi zao mapema mpaka ufisadi unatokea. Hivi mkipitisha azimio kuwa Mwigulu aondolewe au kukusanya Saini za kusema hamna Imani na waziri mkuu na wote wakasign unadhani serikali haianguki? Mbona huko nyuma mawaziri waliondolewa kwa staili hii why kwa Sasa bunge lisubiri serikali wakati mamlaka ya oversight ipo kwa bunge?

Kikwete alikua dhaifu kuliko Samia ila Bado bunge la Sitta lilinyoosha mafisadi sababu ripoti za CAG zilifanyiwa kazi kwa maazimio ya bunge kuondoa mawaziri.
 
Kama ulikuwa unajua hawakuchaguliwa na wananchi, kule mwanzo usingesema "tuliwachagua" mpaka ukafanya nikuulize nani aliyewachagua, kuwa makini na unachoandika, usiwe kigeugeu..
Wapi nimesema "hawakuchaguliwa na wananchi" unaweza nionyesha?? Nimesema WHETHER Ili kukupa benefit of doubt ya hoja yako kuwa HAWAKUCHAGULIWA na wananchi. Mimi naeleza kwa angle ya kisheria ndio maana hata Mnyika kasema sheria ya mabadiliko ya katiba itapitishwa na wabunge huku hapo hapo amedai waliiba kura. Meaning sheria ni sheria tu whether alipita kwa kura au wizi as you claim
Unazungumzia POAC ya Zitto, mbona huzungumzii za kabla na baada yake? jibu linarudi palepale, wanalindana, kumbe hata wakiamua kufanya kama walivyofanya kwa Zitto, bado wanafanya kwa mapenzi yao, ajabu mjuaji unadanganyika!.
POAC later PAC imeanza kuwa chini ya upinzani enzi za Zitto ila kabla ya hapo ilikua chini ya Chenge so naye aliowalinda CCM wenzie. Na pia hata ripoti za CAG kusomwa bungeni kumeanza na kina Dr Slaa na Zitto hiyo 2009 before that haikuwepo hii ripoti ya CAG!! I wonder hizi basics huzijui!!

Baada ya Zitto ikawa chini ya Aeshi Hillary huyu wa CCM alikaimu kwa muda ndio akaja Mama Kaboyoka huyu alikua CCM ila akahamia Chadema 2015 so alikua moderate naye akawalinda Wana CCM wenzie. Na ndio maana nikasema WAPINZANI MAKINI maana hata Lipumba ni mpinzani ila sio makini.
Unadai pesa ya walipakodi sio ya serikali..., wakati serikali ikishakusanya ndio inaamua ipeleke wapi, ndio maana pesa nyingine wanazichezea kama tulivyoona this time kwenye ripoti ya CAG, open up your mind
Embu jaribu kunielewa mkuu, pesa anayopokea CAG naziita za umma sio serikali sababu SERIKALI wanapanga matumizi kwa pesa zilizopo hazina ila pesa za kwenda NAO alipo CAG inapangwa na kamati ya BUNGE PEKEE sio SERIKALI. Get the difference kwanza, pia hapo tunaongelea bajeti ya CAG sio bajeti ya afya, miundombinu n.k.
Naona unaendelea kupoteza muda tu, unasema zinafanyiwa kazi bunge la January blah blah.. wakati hapo juu umeshaandika iliyowahi kufanyiwa kazi seriously ni ya Zitto pekee
Mkuu mtiririko uko hivi ya "hatua kuchukuliwa"
1. Ripoti za CAG Ni kwa ajili ya bunge
2. Ripoti hutengewa muda kujadiliwa na kamati ya PAC na huwa wahusika wanaitwa ndani ya siku 60-90 watolee maelezo kashfa zao. Pia CAG huitwa kukazia mambo kadhaa.
3. Ripoti ya CAG ikishatolewa maelezo kwa kusikiliza pande zote mbili ndio hapo Sasa PAC wanakuja na FINAL draft ndio inapelekwa bungeni kujadiliwa.
4. Mpaka hapo ripoti zimefanyiwa kazi EXCEPT ni kwenye MAPENDEKEZO ndipo Kuna tofauti ya PAC enzi za Zitto na PAC ya Sasa kwenye bunge lenye chama kimoja. Kwa Sasa wanalindana maana hata PAC ipo chini ya CCM Sasa unategemea Nini.

Hoja ipo very clear so until bunge liwe balanced kwa uwakilishi wa upinzani kama 2009-2020 ndio tutaona ripoti inatolewa mapendekezo mazito.

NB; Tusiwe emotional kwenye mijadala maana sio vita ni kutofautiana hoja tu.
 
Ripoti kutolewa mapendekezo mazito, na hayo mapendekezo kuambatana na vitendo vizito ni vitu viwili tofauti, au kama wewe unadanganyika na maneno pekee it's ok.

Una maneno mengi mno yasiyoakisi uhalisia, mfano nakusoma nakuona unamuondolea lawama CAG kutokana na kile nilichoandika kule juu, halafu mbele unasema ni bunge ndio lilaumiwe kwa kutochukua hatua stahiki, unadai mapendekezo yao ni mepesi....

Sasa kama unakiri kazi ya CAG huwa haitiliwi maanani [kufanyiwa kazi kwa uzito stahiki] kuna ubaya gani niliposema mwanzo CAG anakula mshahara wa bure?? Think outside the box.

Unaandika maandishi mengi sana, ila kusema ukweli work done yako ni zero, hakuna popote nilipoandika ambacho hukuandika wewe, najielewa na nina hakika na nilichoandika kukuhusu, hiyo kazi ya kutafuta ifanye mwenyewe, pitia kule juu ulipoanza kuni-quote.

Nikwambie ukweli, bila kujali POAC/PAC ipo mikononi mwa mpinzani au CCM, lakini linapokuja suala la kuwajibishana hata kama ikiwa chini ya upinzani, kama CCM wakiamua kuwalinda watu wao, hakuna chochote wapinzani watafanya, wataishia kulalamika tu bungeni...

And am not emotional, all am showing you is your weakness kwenye hoja zako unazoandika, unazunguka mnoo mpaka unaleta habari za basic za uchumi, I didn't asked you about that.. ujue tu wanasiasa huacha shule zao nyumbani wakiwa kazini.

Uwe na siku njema.
 
Fuatilieni kwa makini bungeni, hao wawakilishi wenu ndio wenye jukumu la kufanyia kazi ripoti ya CAG na kuipa maazimio serikali. Msiwalaumu wasiohusika.
Yan majizi ccm mnaiba halafu mnaulaumu upinzani eti kwa nini hauwakemie!!!!
 

Kuhusu pesa, serikali haina shamba. Pesa zote ilizo nazo ni pesa za wananchi yaani pesa za umma.

.. kwamba bajeti ya CAG Inapendekezwa na bunge ila bajeti ...

Kwa hiyo sasa?

Pesa ya walipakodi ila sio ya serikali...."

Hizi ni porojo tu. Hazina msaada wowote kwa yeyote ukiwamo wewe.

Mengine unayoongea ya PAC na LAAC ni nadharia nyingine. Tofautisha nadharia na uhalisia. Kwamba nani atakuwa na uchungu zaidi kuliko nani kuhusu mwizi?

Hapa si mahala pake tena ndiyo maana tunasema kama hakuna hatua za kuchukuliwa dhidi ya watu hawa hii bila kujali sababu, ofisi ya CAG ya nini? Huo ndiyo ulio msingi wa hoja.

Kwamba sielewi mjadala ulipoanzia? Haya sasa yatakuwa maajabu ya Mussa. Hapo labda rejea kwenye mada.

"Anzia Kwenye title kisha mada nzima kuoanisha maoni ya huyo mjumbe ambayo kwa hakika yanaendana na msingi kamili wa hoja. Ya nini kuandikia mate ndugu?" Au labda wewe ndiye mwasisi wa mada?

Kwamba nisikuwekee maneno mdomoni? Haya nayo ni maajabu mengine.

".. hawakuchaguliwa na wananchi ndio maana nikasema whether iwe JPM au wananchi it doesn't matter ..."

Kwani hayo siyo maneno yako? Hivi unaelewa maana ya hizo dots mwanzoni na mwishoni wa nukuu kutoka kwako hiyo?

Kwani wewe ulitaka nichukue bandiko lako lote zima zima kama lilivyo kuliweka tena hapa?

Kama hata maneno yako mwenyewe ni kukuwekea maneno mdomoni, huku si ndiko kukosa hoja kwenyewe sasa?

Wewe huoni hivyo ndugu?
 
Kwahio shida ipo kwenye KUKAGUA tusikague au kwenye Kufuatilia ? Wafuatiliaji hawafuatilii ?
Sasa unakagua unakuta madudu hayashughulikiwi so bora ukatafute kampuni yoyote tu ufanye kazi kwa raha zako.
 
Sasa unakagua unakuta madudu hayashughulikiwi so bora ukatafute kampuni yoyote tu ufanye kazi kwa raha zako.
Kwahio suluhisho ni kuacha kukagua na sio kwamba uyashughulikie yanayokaguliwa ?
 

Kilichopo kwenye bandiko lako hili ni nadharia nzuri kabisa. Yaani maneno matupu yasiyovunja mfupa.

Hakukosea aliyesema "the road to hell is paved with good intentions."

Tunachoongelea hapa ni wezi wetu. Kwamba kwa sababu zote nzuri kabisa zinaweza kuwepo, kama kaguzi za CAG hazitiliwi maanani hii ofisi bora isiwepo tu.

Kwa hakika ujumbe wetu huo utakuwa umewafikia kokote kule wote wenye meno waliko:



Maneno ya mkuu wao hayo si bure.

Yetu sasa ni macho. Wanaweza kuamua kupuuza ukaguzi huo wa CAG katika kuendelea kuanika kutokuwepo wa umuhimu wa ofisi yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…