Ukaguzi wa CAG usiozingatiwa ni wa nini?

Ukaguzi wa CAG usiozingatiwa ni wa nini?

Kwahio shida ipo kwenye KUKAGUA tusikague au kwenye Kufuatilia ? Wafuatiliaji hawafuatilii ?

Ieleweke kuwa lengo la mada hizi ni kutoa ujumbe na ujumbe huwafikia walengwa. Siyo hadithi za Kaluma Kenge.

Neuro, utakumbuka kama hivi tuliwasema ocean road. Tiba sasa saa tano asubuhi tayari. Wakati ule 2000 - 2200 mgonjwa yuko pale tangia 0700. Jambo la kheri kabisa.
 
Ingekuwa Kenya raila angeitisha maandamano ya kutaka mamlaka za uwajibishaji hapa kwetu uteuzi zichukue hatua dhidi ya wezi wa kodi za wananchi.

Bahati mbaya kwa sasa hatuna mpinzani wa kuweza kufanya ya Raila. Hivi ni nini mbadala wa upinzani hapa kwetu kinachoweza kuchukua nafasi ya upinzani kushinikiza serikali kuçhuku hatua?
Kwani mkuu wewe na mumeo hamuwezi kuwa wapinzani?
 
Demokrasia inahusu wengi kupewa. Hata hivyo ni busara zaidi walio sahihi kupewa:


Kaguzi za CAG zinazofanyika miaka nenda rudi bila hatua zozote za maana kuchukuliwa ni za nini?


Ya nini kupoteza pesa kwenye kuibiwa na kwenye kaguzi zisizozingatiwa?

Kwa mwendo huu wanaoona ofisi ya CAG ifutwe, wana hoja.

Wasikilizwe!
Kwakweli. !! Yaani anabweka tu haumi ! Duh 🙄!
 
Hizi ripoti huwa zinaenda bungeni na waliotajwa huitwa na kuhojiwa kwa kutoa maelezo ya ziada baada ya hapo bunge linakuja na maazimio. Sasa enzi zile PAC Iko chini ya Zitto mawaziri kibao walikua wanang'olewa na hakukuwa na maandamano.

Enzi hizo ripoti ya PAC ikisomwa wote tunakaa kwenye redio au Tv zetu maana tunajua Kuna vichwa vitaliwa. Ila tokea bunge la Ndugai tumeona PAC Haina makali, upinzani nao wakamweka Kaboyoka ambaye sio radical, so tokea hapo ikawa wezi wanasalimika tu Hadi leo.

So nadhani issue ni kubana wabunge tuliowachagua kama watakua mabubu basi imekula kwetu maana tuliwaingiza kwa kishindo!!
Bunge wanasema wanaisubiri ripoti ili waijadili !! Tusubiri tuone !! Tunalikumbuka Bunge la Mzee wa spidi na viwango !! R.i.p !
 
Ripot zake hufanyiwa kazi Kwa siri, baadhi ya mapendekezo
Ripoti inayotolewa hadharani na kutekelezwa kwa siri ina faida gani?Tutajuaje kama inatekelezwa kweli? Je niikukuuliza kuwa unajua siri gani ya ripoti iliyowahi kufanyiwa kazi?
 
Acha ujinga wako, sio kila anayekosoa Serikali ni chadema. Humu wamo wazalendo wa Kweli wanaoumia nchi yao kubakwa na hawa mafisadi!
Akikuelewa utupe mrejesho
 
Back
Top Bottom