Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Kweli kabisa njiani wengine ukionekana dereva hujafunga mkanda tu balaa unaandika 30 wao wanasababisha majanga makuu hakuna hatua zozote zinazochukuliwa
 
Mamlaka ya kusimamia vyombo vya majini imeshajitenga na sumatra kwasasa inaitwa TASAC
 
acha unafki...
sumatra ipo ndan ya serikar n kama wa kuwajibishwa awe serikar n sio sumatra.
mbunge alishasem kivuko kifanyiwe marekebisho na serikari ikasem itakirekebisha, ad mwaka unaisha serikar ijafany chochote na kivuko kimezama..
asa unaweza vipi kuwalaumu sumatra apo..??
 

Tatizo hapo siyo mashine kwani zilifungwa mwezi wa nane mwaka huu!! tatizo hapa ni very clear, kama ni mali ya serikali yaani kama mashua/mtumbwi ni mali ya serikali na capacity yake kisheria ni kubeba abiria 101 na sasa ilibeba abiria 400 it means wafanyakazi walichukua cha juu yaaani nauli za abiria 299 ziliingia mifukoni mwao na nauli za abiria 101 ndo iliingia kwenye mfuko wa serikali!! The workers are not honest, they have all long been defrauding the government and have been leading a life not commensurate with their monthly income. They should all be sacked and face court of law - go to jail! I strongly believe the President Dr Magufuli will not stomach such incompetent, greedy, merciless employees!!if the boat was supposed to carry 101 travelers, why overload it to the tune of four times (400) over the total number is supposed to be on board?if it is a private business, the license should be revoked, all families be compensated, likewise if it is a government owned vessel, the families must be compensated, orphans be given free education up to University level!
 
Sitatoa hata senti tano kipande ! ujinga ni wakati wa kwenda tu .
 
vipaumbele vipi hivyo ambavyo serikali hii havijaguswa
Hili tukio halijakufunua bado macho kuona kwamba Kivuko kilikuwa kinahitajika, jaribu kuoanisha idadi ya watumiaji wa usafiri huo na uwezo wa chombo wenyewe.

Shule wanazosoma watoto na vijana wengi wale wa kawaida kabisa bado zinauhitaji mkubwa sana wa vifaa nyanja zote, sio michezo, kilimo, sanaa, sayansi, uje kwenye waalimu bora ambao of course mazingira yao lazima yawe mazuri.

Kuna mengi yamefanyika na yanaendelea kufanyika isipokuwa umakini uongezeke, elimu inahitajika sana pia na miundombinu iboreshwe zaidi na kwa kuzingatia masilahi ya wanyonge ambao ndio wengi na wenye nafasi finyu ya kuwa na njia mbadala.
 
Wakara sio kambale..wakina mama, wazee na watoto nao wangetoka?
 
huu ni msiba na hile ni ajali kila kitu utokea na kikishatokea uwa atukosi sababu cha msingi kama bado tupo hai basi tutashuhudia majanga,furaha,vicheko,udhuni,nk,lakini imeshatokea tumshukuru mungu tuifadhi marehemu wetu,tutoe nafasi ktk ili imetufanya tukomae na kujifunza zaidi sikubaliane na hoja ya kujiuzuru tunaweza poteza watu muhimu kwa makosa ya watendaji wadogo walioshindwa kufanya kazi ipasavyo,kujiudhulu sio mwisho wa majanga na vifo baina yetu..mungu walehemu marehemu wote wa hii ajali wape nguvu majeruhi wape moyo wa ustahamilivu ndugu na jamaa wa marehemu ameen[emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120]
 
Hivi hizi ajali za meli Tanzania huwa ni kafara au vipi? Yaani toka 8mchana mpaka Giza kinaingia hakuna hata helicopter ya kurandaranda

Helicopter zipo ajili ya kulinda usalama kwenye ziara za Magufuli,lakini kwenye hii ajali ni aibu sana jinsi Mamlaka zilivyolishughulikia hili tatizo.
 
RC wa mwanza bora angekaa kimya kuliko kutoa kauli ya kishenzi vile eti Giza limeingia tukalale tuendelee kesho.....huyu ni popoma kabisa yan tukalale wakati kuna ndugu zetu wanalala ndani ya maji kweli.....!!!

JPM huyu RC ukute anahusika na hii ajali si bure, labda aliona wakiokolewa watu wengi mission yake itafeli.....
 
Katika uokoaji Usalama wa waokoaji ni jambo la kwanza na la msingi.Hivi waokoaji wangeendelea na uokozi usiku wa jana na wao kupoteza maisha si tungeongeza janga juu ya janga.

Naamini uamuzi wa kusitishwa kwa zoezi hilo jana jioni uliangalia vitu vingi na kimojawapo ni uwezekano wa watu kuwa hai masaa karibu 6 chini ya maji na kuendelea kuwa hai.

Kwa waliozoea kuishi karibu na maji mtu anapozama na kumtafuta bila mafanikio mnaacha na kesho yake utamkuta anaelea.

Sidhani kama kuna manusura walikuwa wakionekana in the vicinity of 50m or up to 200m wakitapatapa na wakaachwa.

Wengi wetu tunasema kivuko kimezama karibu na bandari na kilikuwa kinashuhudiwa live sasa tunataka scope ya uokoaji itanuke hadi kenya?
Tupunguze ujuaji tuache siasa za mjitaka.

RIP MAREHEMU WOTE POLENI SANA WAFIWA
 
Wakuu tusimlaumu sana Mongella. Kuna mmoja kati yetu anayejua logistics za uokozi zilivyokuwa?
 
Watu wa kwanza kulaumiwa ni waathilika wenyewe sababu kama unaona chombo kimejaa pasina kuambiwa na Traffic wewe kama raia wa kawaida mwenye akili timamu lazima uchukue tahadhali kwani uhai hauuzwi kama tutaendelea kutegemea Matrafiki maana yake tutaendelea kupoteza maisha kizembe , Hata kama unaharaka kiasi gani Lazima ujihakikishie usalama wako kabla ya haraka zako uhai ukiondoka haurudi hapa ndo tunapata tafsiri ya msemo kuwa Haraka haraka haina Baraka.
Mamlaka husika Zinatakiwa pia zilaumiwe kwa kushindwa kudhibiti hili pia kushindwa kutoa Elimu mara kwa mara, kama hauamini mfano pale kariakoo likitokea tukio watu wataanza kuzuiwa upandaji na ushukaji ule wa mbwembwe kwenye dala² .Kinga ni bora kuliko Tiba
We need to change
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…