Na wananchi pia tuko wazembe sana. Kuna vitu tunachukulia poa tu au tunaona ni sehemu ya starehe. KUJIFUNZA KUOGELEA. Watumiaji wengi wa hivi vivuko asilimia kubwa ni wakazi wa hayo maeneo, yaani kutumia vivuko ni sehemu ya maisha yao ya kila siku kama sio kila wiki. Maji ya ziwa, bahari ni sehemu yao, wajifunze kuogelea. Kuogelea ni kama kujifunza baiskeli, ukijua umejua. Hausahau hata usipoogelea miaka mingi kisha ghafla ukatupwa majini.
Watu wangepona wengi hapa kama wangekuwa wanajua kuogelea, umbali huo ni mfupi sana kupoteza watu wengi kiasi hiki.