Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Yeyote aliyehusika kuruhusu ubebaji huo wa abiria awajibishwe.
Red: Wakazi wa kigamboni
Mtaonea watu bure! hii nchi hatukosmart kwa kiasi hicho, kama ni mkaazi wa Dar es salaam, angalia jinsi gari za mwendokasi zinavyojaza, angalia daradara za mjini hapa zinavyojaza harafu niambie kama ni ujazaji wa kiasi kinachotakiwa! je trafic hawapo kila kona na wanaona? na hata wakiona wanachakufanya kumanage hali hiyo? ok, kama ni msafiri wa tren za Dar hizi au tren za kwenda mikoani unajua zinavyojaza? ni kwa kiasi kinachotakiwa? tukubari tu we are all under risk! msiwaonee watu kwasababu ajari imetokea!!! maisha ya kujaza zaidi ya kiwango ndo maisha yetu wote, na serikali inajua hilo! wasijifanye walikuwa hawajui na kutaka kutoa kafara watu ili wao wawe safi!!!
 
Mkuu pia mim siizingatii kusema kua watu walisongea mbele ndio chombo kika capsize pia operational mistake zinaweza kua zimechangia kwa kiasi kikubwa.
Bro,mimi nakiri ili-overload kwa mujibu wa takwimu. Lkn niamini usiniamini,pale kuna kosa lingine kubwa litakuwa lilifanyika hapo. Haingewezekana kamwe isafiri umbali mrefu kiasi kile salama na ikamudu kuyavuka mawimbi makubwa ambayo yangetosha kuizamisha then ije iangukie kwane eneo ambalo maji yana utulivu km maji kwene ndoo. Kulikuwa na tatizo la kiuendeshaji pia na hasa hasa ndilo limetuulia ndugu zetu.
 
"Asenga mimi nilikuwepo ndani ya kivuko kile cha MV NYERERE,tumepona tu kwa sababu tulikuwa nje,waliokaa ndani ni ngumu sana kupona kwakuwa kivuko kiligeuka gafla chini juu na kina uzito,
mtu ukifunikwa vile ata waokozi wakifika ndani ya robo saa kukuta bado mzima ni ngumu sana.
Kama hauamini na unazani masihara jaribu kuzama ndani ya pipa la maji kwa dakika 10 bila kupumua uone.
Mimi naomba wale waliozidisha abiria na uzito wakamatwe kama Mhe Rais alivyosema
na sisi abiria tujiongeze
Tukifika standi kwenye basi ama bandarini tuwe tunauliza, je hiki kivuko kina beba watu wangapi ?
na huo uzito ubandikwe kwenye mbao za matangazo,ukiona watu wamezidi usipande ila wa afrika sisi tunalazimisha na wengine tunatoa rushwa ili turuhusiwe kupanda madhara ndio haya,
ni ngumu sana kupona ukifunikwa vile ata kama baada ya dakika 10 kivuko kinge ondolewa majini lazima maiti zingekuwa nyingi sana,
watu waangalie ata Marekani boat ili wahi kuzama kwa kugeuka tu watu 17 wakaaga dunia,,waokozi wanafika wakakuta tayari na wenzetu wameendelea sana lakini kifo cha maji kinaua haraka hasa kama mtu unakuwa umefunikwa kama hawa walikuwa ndani.

Hiki kivuko kime karabatiwa mwaka jana na kote huko kimeenda vizuri tu tunakaribia kupaki watu wa ndani wanagombea kutoka nje

kwa kuwa watu walizidishwa uzito ukaenda sehemu moja kikageuka wajuu tukarushwa kwenye maji ndio pona yetu, wavuvi jirani wakaja kutuokoa,,walipoingia ndani ya kivuko kwa chini mda ule ule wakakuta watu washakufa kwa kukosa hewa sasa watu wasilaumu tu bila kujua.
nawaambia usiombe kufunikwa na kivuko, Sikia tu kwenye mitandao...fikisha salam mimi John Kisekwa..."
 
Mimi sie huyo alieandika ila nimeipata mahali.
 
Hakuna chochote kinachoweza kuhalalisha watu 400 kufa kwa uzembe.

Wahusika walishindwaje kudhibiti idadi sahihi ya watu wanaoendana na capacity ya kivuko??

Sitashangaa siku moja kuona watu wanadandia mabawa ya bombadia au dreamliner kwasababu ya uswahili swahili tu.
 
Sio wakati wakulaumiana mimuda wakua kitu kimoja Kama taifa tuweke tofauti zetu za kisiasa pembeni ,
 
Amani iwe nanyi wapendwa.

Rais wetu mpendwa Dr Magufuli jana ametoa salamu za pole kwa wote waliofikwa na msiba kutokana na ajali ya Mv Nyerere, pia salamu hizo zimelengwa kwa watanzania wote kwa ujumla ndiyo maana akatangaza siku nne za maombolezo na bendera za taifa kupepea nusu mlingoti nchi nzima.

Jambo la pili amewashukia kama mwewe baadhi ya wanasiasa viherehere waliofilisika kichwani ,ambao kwao ajali ya Mv Nyerere wameigeuza kuwa fursa ya kupata kiki kisiasa.
Rais Magufuli amewataka wanasiasa hao kuviachia vyombo vinavyohusika vifanye uchunguzi wake bila kuingiliwa na mtu yoyote na amewashauri kama wana ushahidi wowote wasubiri watuhumiwa wa ajali hii wakifikishwa mahakamani wataenda kusema ushahidi wao huko badala ya sasa kupiga porojo za kisiasa ambazo zinaweza kuharibu ushahidi.

Ikumbukwe kuwa mara baada ya kutokea ajali hiyo mwenyekiti wa chadema Freeman Mbowe aliitisha vyombo vya habari na kuanza kutafuta kiki kwa kujigeuza mahakama na kuanza kushutumu na kuhukumu watu kwa mambo asiyoyajua vizuri.

Pia Zito Kabwe na James Mbatia hawakuwa nyuma katika kutumia msiba huu kama mitaji yao ya kiki za kisiasa .

Inasikitisha sana viongozi wa vyama vya upinzani badala ya kuwahi eneo la ajali kwenda kutoa msaada kwa wapiga kura wao ,wanabaki twiter kukejeli wafiwa na kujijenga binafsi kisiasa bila kutoa msaada wowote kwa waliopatwa na ajali hii!!!

Hongera sana Rais Magufuli kwa kuwavua nguo hawa wanasiasa uchwara ,wachumia tumbo na wanafiki ,ambao wao muda wote wanawaza siasa tu huku vyama vyao vikiwafia kwa kukimbiwa na wananchi..
Unamfananisha Rais na Mwewe!
R.I.P wahanga wa MV Nyerere.
Serikali haikwepi lawama
 
Mm sitoi tena. Nilitoa ile ya bukoba aikuwafikia walengwa.
 
Back
Top Bottom