Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Kuna kitu kwenye hizi updates sijakielewa. Kuna taarifa mbili kuwa, Nahodha anashikiliwa kwa kumpa deiwaka ambaye amesababisha ajali; taarifa ya pili inasema Nahodha Mkuu ni moja ya waliofariki! Hapa, sijaelewa.
Sio kwamba msimamizi Mkuu Wa kivuko ndio aliyefariki pamoja na huyo "deiwaka" ?
 
Ajali hutokea kutokana na makosa y'a kibinadamu ! Hivyo basi kinachotakiwa ni kuzitakia faraja familia zilizo patwa n'a maafa haya makubwa ! Ila kama taifa tujitafakari n'a kujua chanzo ili tatizo lisijirudie ! Kwa haraka mimi naona chanzo ni mizigo kutokupangwa vizuri ili chombo kiwe na balance hivyo centre of boyance ikahama ! Na yote hii ni lack of knowledge kwa attendants ! Kwa kawaida engine ikizima chombo hakiwezi zama maramoja ! Watu wanapata fursa ya kuchukua maboya ! Kwa tatizo kama Hili haliwezi kuisha bila kuweka utaratibu unaosimamiwa n'a qualified persons ndani ya viombo vya majini ! Mengine y'a kusamehana kwani tunajua mapungufu yetu n'a ignorance kama waafrica
Mkuu huko sawa kabisa. Kwa maoni yangu ni lacky of qualified skilled personnel ndiyo chanzo cha ajali kwani walishindwa kubalnce mzigo kulingana na centre of gravity ya hicho chombo. Kama issue ni watu kujiandaa kushuka ambapo ni mbele ya chombo basi kingelianza kuingiza maji mlangoni (kunywa maji)
 
Bado hiyo ni sababu ya kijinga tu! Chombo cha abiria 100 unapojaza zaidi ya mara mbili unatumia akili gani hiyo? yaani meli iliyobeba abiria wanaostahili inaweza kuzama kwa sababu ya watu kusogea mbele, Kweli?

Nimejaribu kujieleza kwamba taratibu za vyombo kama hivi hazistahili kusimamiwa na watu wapuuzi. Kuna watu hata kama wakisoma ujinga wa kupenda sifa kinyume na mafunzo yao hauwatoki.


Labda alichukulia mfano wa ungo unapoelea kwenye maji ukawekewa jiwe upande mmoja unabinuka kuelekea liliko jiwe
 
Yuko live.
-Anasema taarifa aliyopewa ni kuwa hiyo meli inaweza beba watu 100 na tani 25. Ila ilizidisha watu.

-Pia ilipakia mahindi magunia mengi na makreti ya bia na soda na vifaa vya umeme pamoja na gari/ magari.

-Ilikiwa ni siku ya soko alhamis hivyo na abiria walikuwa wamebeba mizigo, hivyo ni wazi ilizidisha uzito.

-Pia anasema inasemekana aliyekuwa anaendesha yawezekana sio kapteni mwenyewe, hivyo ameagiza wote wakamatwe. Pamoja na kapteni na watendaji wa kivuko wakamatwe na shughuli za upelelezi ziendelee.

-Pia amemuagiza waziri mkuu kuunda tume ya uchunguzi juu ya hii ajali.
Ataka wanasiasa wasichukulie hii kitu kisiasa.

Mwisho ametoa pole kwa wafiwa wote.
Only in Tanganyika,kivuko kinaendeshwa na kishoka,badala ya capten.
 
Mbowe kasha waambia hataki mumjue jue mbona hamuelewi?
 
Kwa mtazamo wangu,ajali ni ajali lakin katika hili tunaambiwa wazi kua kuna ukiukwaji wa idadi ya watu katika kivuko,ni wazi hilo swala sio la juzi tuu yani itakua Mara zote linafanyika ,swali je wahusika wako walikua wapi kuzuia ujwazaj wa abiria kupitiliza,adi Maafa yatokee??? Mkurugenzi wa TAMESA anapaswa kwajibika haraka sana,kushindwa kuwimamia kwa watu wake,RPC mkoa wa mwanza,,Na mkuu wa police wa ukerewe,mkuu wa kikosi cha maji cha mwanza,mkuu wa TRA mwanza,mkuu wa mkoa Na wa wilaya husika,hawa wote wanapaswa kuwajibika..Hawakua wakfatlia,haina Aja ya kukamata watu wadogowadogo,emu jiulize RPC hajawah kufatlia kuusu ukiukwaj with a Sheria???? Yani unauma sana..hawa wakuu wa wilaya inamana hajawah kufatlia juu ya kivuko hiki??? Swali la ziada je tungevamiwa na adui usiku wanajeshi wasingeenda vitani kwa sababu ya Giza???? Yani watu wanaona nchi kavu pale Na anakufa?? Kiukweli imeuma sana.hiv yy kwel mongela alienda kwake akalala wakati wananchi wake zaid ya 100 wamelala majini???
 
Ukitaka kujua kosa liko wapi, usianze kwa kutafuta sababu zisizo na ushahidi. Hadi sasa tuna taarifa zenye ushahidi, overloading. Uzuri ni kwamba TZ tuna mifano ya aina hii lakini kwa ujinga na huenda upumbav wa walioaminika kuendesha meli hizi bado hawakupata mafunzo. MV Bukoba, MV Spice..., MV Kipepeo meli zote hizi sababu ilikuwa ni overloading!

Tukikataa sababu yenye ushahidi ndo mwanzo wa kukimbilia uchawi na mambo ya kusema ni mapenzi ya Mungu. Hatuhitaji mambo ya kichawi wala kiroho kwa jambo la wazi kama hili.
Mkuu nadhan ungejipa muda wa kuyasoma maelezo yangu vzr,huenda ingekusaidia unijibu vzr zaidi. Mimi sipo kupingana na overloading,na wala sijajielekea kudhania uchawi...but apart from overloading there was another cause. Hata hivyo nikuulize labda,Bugorola ilikoanzia safari hadi Bwisya ilikozamia pengine umewahi kuwahi kufika huko au? Ukiwa unapajua vzr,basi changia bila muhemko na ikiwa hupajui tafuta taarifa.
 
Amani iwe nanyi wapendwa.

Rais wetu mpendwa Dr Magufuli jana ametoa salamu za pole kwa wote waliofikwa na msiba kutokana na ajali ya Mv Nyerere, pia salamu hizo zimelengwa kwa watanzania wote kwa ujumla ndiyo maana akatangaza siku nne za maombolezo na bendera za taifa kupepea nusu mlingoti nchi nzima.

Jambo la pili amewashukia kama mwewe baadhi ya wanasiasa viherehere waliofilisika kichwani ,ambao kwao ajali ya Mv Nyerere wameigeuza kuwa fursa ya kupata kiki kisiasa.
Rais Magufuli amewataka wanasiasa hao kuviachia vyombo vinavyohusika vifanye uchunguzi wake bila kuingiliwa na mtu yoyote na amewashauri kama wana ushahidi wowote wasubiri watuhumiwa wa ajali hii wakifikishwa mahakamani wataenda kusema ushahidi wao huko badala ya sasa kupiga porojo za kisiasa ambazo zinaweza kuharibu ushahidi.

Ikumbukwe kuwa mara baada ya kutokea ajali hiyo mwenyekiti wa chadema Freeman Mbowe aliitisha vyombo vya habari na kuanza kutafuta kiki kwa kujigeuza mahakama na kuanza kushutumu na kuhukumu watu kwa mambo asiyoyajua vizuri.

Pia Zito Kabwe na James Mbatia hawakuwa nyuma katika kutumia msiba huu kama mitaji yao ya kiki za kisiasa .

Inasikitisha sana viongozi wa vyama vya upinzani badala ya kuwahi eneo la ajali kwenda kutoa msaada kwa wapiga kura wao ,wanabaki twiter kukejeli wafiwa na kujijenga binafsi kisiasa bila kutoa msaada wowote kwa waliopatwa na ajali hii!!!

Hongera sana Rais Magufuli kwa kuwavua nguo hawa wanasiasa uchwara ,wachumia tumbo na wanafiki ,ambao wao muda wote wanawaza siasa tu huku vyama vyao vikiwafia kwa kukimbiwa na wananchi..
Jaribu kuwa mtulivu wakati mwingine unapotaka kuandika jambo, usiwe unasukumwa na ushabiki usio na maana.Kuitisha mkutano na waandishi ilpaswa kuwa hatua za mwanzo za serakali ili watuambie ni hatua gani za haraka zinatekelezwa kuokoa maisha ya walala hoi. Baadala yake zoezi lilisitishwa sababu ya giza, tambua hii ni karne ya 21, miaka 57 baada ya uhuru.
 
kawa muungwana, si vizuri kutafuta kiki kwenye misiba, hayo ni mambo ya CCM!!
 
Sio kwamba msimamizi Mkuu Wa kivuko ndio aliyefariki pamoja na huyo "deiwaka" ?
Kwa jinsi nilivyoelewa Captain hakuwa amesafiri na hiyo ferry na ndiyo maana kakamatwa. Aliyepoteza maisha ni huyo umempa jina "day waka"
 
Alichosema mbowe ni wale wote wanaohusika wachkuliwe hatua kali
Kwani kuna kosa gani mtu ksema hvyo!

Ova
 
kwa wenyeji wa huko, hivi kutoka huko kivuko kilipotoka (bugolola) mpaka ukara kuna umbali gan?. na kivuko hutumia wastani wa masaa mangapi?. tujuzane wakuu.
 
Kama Mheshimiwa angepiga marufuku chaguzi zisizo na vichwa wala miguu za watu kujiudhuru kimakusudi halafu tena wanagombea haohao..nafikiri wangesave hata kiwango fulani cha fedha wakaongezea na kikingine wakasaidia maeneo kama haya...
Ona sasa watu wamerisk maisha kuwahi wakajirundika wengi matokeo yake vifo....mamlaka husika zinapaswa ziwe makini zaidi na maisha ya watu.....
Ni sawasawa na magari ya mwendo kasi manake jinsi yanavyoruhusiwa kushona watu..siku lilkitokea la kutokea haponi mtu....naongelea mwendo kasi maana ni rahisi kucontrol kuliko hizi daladala nyingine...
Pili kwa namna watu wanavyoongea kuhusu vyombo uokozi ulivyokua bado ni changamoto juu ya changamoto...
Nyie CCM nchi yetu bado ni changa sana na inahitaji pesa kwa ajili ya maendeleo ya wananchi maskini..kama kutengeneza vivuko vya maana na vikubwa,zana za uokozi etc....MUACHE KUPOTEZA PESA ZA UMMA KWA CHAGUZI AMBAZO watu wanaweka maslahi mbele....
 
Tuna vipaumbele vya hovyo. Kutumia mabilioni kujenga uwanja wa ndege na mpira Chato.

Kupanga ni kuchagua. Ukiwa na mipango ya hovyo na matokeo pia ni hovyo.

Ushamba ni mzigo.
 
Back
Top Bottom