Foxer
Member
- Sep 14, 2015
- 24
- 19
Hilo daraja litazuia meli zinazoingia bandaraniHee.., mbona unatutisha wa huku Kigamboni? ,ndio maana nasema pajengwe daraja pale, hamsikii..
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hilo daraja litazuia meli zinazoingia bandaraniHee.., mbona unatutisha wa huku Kigamboni? ,ndio maana nasema pajengwe daraja pale, hamsikii..
Sio kwamba msimamizi Mkuu Wa kivuko ndio aliyefariki pamoja na huyo "deiwaka" ?Kuna kitu kwenye hizi updates sijakielewa. Kuna taarifa mbili kuwa, Nahodha anashikiliwa kwa kumpa deiwaka ambaye amesababisha ajali; taarifa ya pili inasema Nahodha Mkuu ni moja ya waliofariki! Hapa, sijaelewa.
Mkuu huko sawa kabisa. Kwa maoni yangu ni lacky of qualified skilled personnel ndiyo chanzo cha ajali kwani walishindwa kubalnce mzigo kulingana na centre of gravity ya hicho chombo. Kama issue ni watu kujiandaa kushuka ambapo ni mbele ya chombo basi kingelianza kuingiza maji mlangoni (kunywa maji)Ajali hutokea kutokana na makosa y'a kibinadamu ! Hivyo basi kinachotakiwa ni kuzitakia faraja familia zilizo patwa n'a maafa haya makubwa ! Ila kama taifa tujitafakari n'a kujua chanzo ili tatizo lisijirudie ! Kwa haraka mimi naona chanzo ni mizigo kutokupangwa vizuri ili chombo kiwe na balance hivyo centre of boyance ikahama ! Na yote hii ni lack of knowledge kwa attendants ! Kwa kawaida engine ikizima chombo hakiwezi zama maramoja ! Watu wanapata fursa ya kuchukua maboya ! Kwa tatizo kama Hili haliwezi kuisha bila kuweka utaratibu unaosimamiwa n'a qualified persons ndani ya viombo vya majini ! Mengine y'a kusamehana kwani tunajua mapungufu yetu n'a ignorance kama waafrica
Bado hiyo ni sababu ya kijinga tu! Chombo cha abiria 100 unapojaza zaidi ya mara mbili unatumia akili gani hiyo? yaani meli iliyobeba abiria wanaostahili inaweza kuzama kwa sababu ya watu kusogea mbele, Kweli?
Nimejaribu kujieleza kwamba taratibu za vyombo kama hivi hazistahili kusimamiwa na watu wapuuzi. Kuna watu hata kama wakisoma ujinga wa kupenda sifa kinyume na mafunzo yao hauwatoki.
Only in Tanganyika,kivuko kinaendeshwa na kishoka,badala ya capten.Yuko live.
-Anasema taarifa aliyopewa ni kuwa hiyo meli inaweza beba watu 100 na tani 25. Ila ilizidisha watu.
-Pia ilipakia mahindi magunia mengi na makreti ya bia na soda na vifaa vya umeme pamoja na gari/ magari.
-Ilikiwa ni siku ya soko alhamis hivyo na abiria walikuwa wamebeba mizigo, hivyo ni wazi ilizidisha uzito.
-Pia anasema inasemekana aliyekuwa anaendesha yawezekana sio kapteni mwenyewe, hivyo ameagiza wote wakamatwe. Pamoja na kapteni na watendaji wa kivuko wakamatwe na shughuli za upelelezi ziendelee.
-Pia amemuagiza waziri mkuu kuunda tume ya uchunguzi juu ya hii ajali.
Ataka wanasiasa wasichukulie hii kitu kisiasa.
Mwisho ametoa pole kwa wafiwa wote.
Uliyoyaandika yanakuhusu.Avatar yako tu inaonesha kuwa wee ni zwazwa "you need some evolutions to be a real human being" Zinjanthropus mkubwa wewe!!!!
Mkuu nadhan ungejipa muda wa kuyasoma maelezo yangu vzr,huenda ingekusaidia unijibu vzr zaidi. Mimi sipo kupingana na overloading,na wala sijajielekea kudhania uchawi...but apart from overloading there was another cause. Hata hivyo nikuulize labda,Bugorola ilikoanzia safari hadi Bwisya ilikozamia pengine umewahi kuwahi kufika huko au? Ukiwa unapajua vzr,basi changia bila muhemko na ikiwa hupajui tafuta taarifa.Ukitaka kujua kosa liko wapi, usianze kwa kutafuta sababu zisizo na ushahidi. Hadi sasa tuna taarifa zenye ushahidi, overloading. Uzuri ni kwamba TZ tuna mifano ya aina hii lakini kwa ujinga na huenda upumbav wa walioaminika kuendesha meli hizi bado hawakupata mafunzo. MV Bukoba, MV Spice..., MV Kipepeo meli zote hizi sababu ilikuwa ni overloading!
Tukikataa sababu yenye ushahidi ndo mwanzo wa kukimbilia uchawi na mambo ya kusema ni mapenzi ya Mungu. Hatuhitaji mambo ya kichawi wala kiroho kwa jambo la wazi kama hili.
Jaribu kuwa mtulivu wakati mwingine unapotaka kuandika jambo, usiwe unasukumwa na ushabiki usio na maana.Kuitisha mkutano na waandishi ilpaswa kuwa hatua za mwanzo za serakali ili watuambie ni hatua gani za haraka zinatekelezwa kuokoa maisha ya walala hoi. Baadala yake zoezi lilisitishwa sababu ya giza, tambua hii ni karne ya 21, miaka 57 baada ya uhuru.Amani iwe nanyi wapendwa.
Rais wetu mpendwa Dr Magufuli jana ametoa salamu za pole kwa wote waliofikwa na msiba kutokana na ajali ya Mv Nyerere, pia salamu hizo zimelengwa kwa watanzania wote kwa ujumla ndiyo maana akatangaza siku nne za maombolezo na bendera za taifa kupepea nusu mlingoti nchi nzima.
Jambo la pili amewashukia kama mwewe baadhi ya wanasiasa viherehere waliofilisika kichwani ,ambao kwao ajali ya Mv Nyerere wameigeuza kuwa fursa ya kupata kiki kisiasa.
Rais Magufuli amewataka wanasiasa hao kuviachia vyombo vinavyohusika vifanye uchunguzi wake bila kuingiliwa na mtu yoyote na amewashauri kama wana ushahidi wowote wasubiri watuhumiwa wa ajali hii wakifikishwa mahakamani wataenda kusema ushahidi wao huko badala ya sasa kupiga porojo za kisiasa ambazo zinaweza kuharibu ushahidi.
Ikumbukwe kuwa mara baada ya kutokea ajali hiyo mwenyekiti wa chadema Freeman Mbowe aliitisha vyombo vya habari na kuanza kutafuta kiki kwa kujigeuza mahakama na kuanza kushutumu na kuhukumu watu kwa mambo asiyoyajua vizuri.
Pia Zito Kabwe na James Mbatia hawakuwa nyuma katika kutumia msiba huu kama mitaji yao ya kiki za kisiasa .
Inasikitisha sana viongozi wa vyama vya upinzani badala ya kuwahi eneo la ajali kwenda kutoa msaada kwa wapiga kura wao ,wanabaki twiter kukejeli wafiwa na kujijenga binafsi kisiasa bila kutoa msaada wowote kwa waliopatwa na ajali hii!!!
Hongera sana Rais Magufuli kwa kuwavua nguo hawa wanasiasa uchwara ,wachumia tumbo na wanafiki ,ambao wao muda wote wanawaza siasa tu huku vyama vyao vikiwafia kwa kukimbiwa na wananchi..
Kwa jinsi nilivyoelewa Captain hakuwa amesafiri na hiyo ferry na ndiyo maana kakamatwa. Aliyepoteza maisha ni huyo umempa jina "day waka"Sio kwamba msimamizi Mkuu Wa kivuko ndio aliyefariki pamoja na huyo "deiwaka" ?
Anapiga jalambaNaona Lukosi anajianda kupitisha bakuli U.K