Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Wataka itumike kiuchumi au?kiongozi kuwajibika sini swala la kawaida sana kwenye uongozi
Labda angependa yawe mawazi ya kikabila zaidi, Ananikumbusha Mlowola aliposema ushahidi uliopelekwa kwake na akina Nassari na Lema kuhusu Rushwa ya Mnyeti kule arusha eti ulikuwa wa kisiasa, sasa inawezekanaje mwanasiasa akaongea jambo lisilo la kisiasa na wakati siasa ndio inaongoza nchi hii ?, na isitoshe kashfa yenyewe ilikuwa ya kisiasa.
 
Poleni sana wafiwa wote. Kama kungekuwa na rejesta ya abiria wote ingekuwa ni rahisi kwa ndugu kufuatilia ndungu zao kwani wengi hawajui kama ndugu zao walikuwa mule hasa wale wanaosafiri bila kuaga au vitambulisho. Majina yao yangechapiswa kwenye vyombo vya habari ingekuwa ni rahisi kufuatilia lakini kutokana na hali halisi itabidi wengi wazikwe na serikali
 
Pole sana mkuu!
 
Subiri siku ya ufunguzi wa tunnel bridge pale ferry ndio utakuja kunielewa, kila kitu huanzia mahali, hata ukiwaza tu, achilia mbali kuongea, ulimwengu unakusikiliza bila wewe kujua, na vitu hufuata channel ya mawazo yako. TUNATAKA UNDERGROUND TUNNEL BRIDGE AU DARAJA LA KUFUNGUKA, nitaendelea kulidai hadi lijengwe, na pia nitaendele kulalamika kwa chochote kile nitakachojisikia, mb ni zangu.
 
kwa wenyeji wa huko, hivi kutoka huko kivuko kilipotoka (bugolola) mpaka ukara kuna umbali gan?. na kivuko hutumia wastani wa masaa mangapi?. tujuzane wakuu.

taarifa za awali zilisema kivuko hicho kilianza safari yake kutoka bogololasaa 6 mchana na ilipofika saa 8 mchana ndio kikapinduka, kwa hiyo ni mwendo wa masaa mawili hivi, lakini leo waziri kamwele amesema Umbali kutoaka bugolola mpaka upande wa pili ni wa muda wa dakika 45, sasa hata haijulikani ukweli ni upi, mlioko huko mtujuze.
 
Nasikia mbunge kawaumbua wengi sana, kasema serikali baada ya yeye kuomba kivuko kirekebishwe, serikali ilifanya urekebishaji wa injini yake.
 
Kutokana na msiba uliolikumba Taifa na Mkuu katangaza Siku NNE za maombolezo.
Je tunaomboleza tukiwa job au home?
 
Hatuwezi kubali uchafuzi kwa wasio na hatia ,uzembe wa wachache serikalini ,usisababishe serikali nzima kulaumiwa,
Mbunge aweke wazi nini kilifanyika (hatua) baada ya kuiomba serikali kufanyia kazi ombi lake ,tusipepese macho,nongwa zimezidi mno
Hilo ni swali au unatania? Kungelifanyika kitu hiyo ajali ingetokea?
 
Maajabu ya dunia. Mbatia kapata habari ya msiba kaita waandishi. Na wengine wengi kazi yao Kutweet ujinga. Sasa ukiwapa madaraka Hawa wataongoza Watu Au nyani kwa Kukosa utu.
Luxurious dreamliner instead of badly needed ferry! You're alerted in advance!

Magufulai anaona aibu aibu aibu!!!!
 
Nijaribu kukisia tu ni km Km 50-60
 
Yote aliyoyasema kwenye press ya Jana ni uongo mtupu. Mbunge wa Ukerewe kuweka kula kitu hadharani soon kuhusu hoja take ya kivuko aliyoitoa bungeni. Stay tuned nitawajuza kupitia hapa hapa!
Kuondoa chama kwenye chaguzi za kipuuzi za marudio kutamgharimu sana
 
Imekuwa ni kawaida ya Serikali inapokuwa inafanya makosa ya kupelekea janga au majanga kukimbilia kubadilisha taariifa halisi za tukio huku ikilenga kujitetea na kujiondoa katika lawama. Hii imekuwa ikijitokeza kwa saana hasa katika serikali hii ya awamu ya "JIWE"...mfano mdogo tuchukulie lile tukio la mauaji ya polisi kwa dada yetu "Acquiline katika marudio ya uchaguzi wa Ubunge kinondoni".Tukirejea kwenye tukio hili la juzi la meli kuzama, jana JIWE katika kutoa salam za rambi rambi aliliambia Taifa kuwa "ana taarifa zisizo za uhakika kuwa pengine aliyekuwa anaendesha Meli hiyo siku ya tukio ni "Deiwaka"..Mimi nimejiuliza sana kwamba ni kwanini kaliongea hilo wakati huu tena yeye kama mtaalamu katika sekta hiyo akijua waziwazi hata kama angekuwa anaendesha "Deiwaka" hiyo sio kisababishi cha ajali hiyo kwani inawezekana huyo DEIWAKA amekuwa akiendesha mara kwa mara na wanafika salama kama wafanyavyo hata Deiwaka wa mabasi ya abiria na JIWE analielewa hilo fika kwani amekuwa katika sekta hiyo kwa mda mrefu na anajua sio "issue". Sasa ni kwanini jana kaliongelea hilo au "kachomekea" msemo wake wa kaiwada?, nia yake ni kujaribu kubadilisha fikra kwa wananchi kupunguza lawama kwa serikali kusudi lawama ziende kwa Kapteni wa meli hiyo..kama ilivyotokea kwa Kapten wa Mv Bukoba ilipozama 1995 na baadae alifungwa na kuachiwa ..lakini ile ilisaidia saana kuokoa ajira za watu wengi akiwemo waziri kwani wananchi woote walikimbilia kufuatilia kesi huku wakimlaumu kapteni wa Mv Bukoba na kutojishughulisha kabisa na chanzo cha ajali ile "source"..lakini cha kustaajabisha leo kwenye historia imeandikwa pamoja na serikali yenyewe kuwa ajali ile ilisababishwa na ubovu wa meli yenyewe jambo ambalo kwa wakati ule lilifichwa kuiokoa serikali na watendaji wake...Kwa hili la juzi hatudanganyiki tena! Jambo jingine lililonstaajabisha katika hotuba ya JIWE mwishoni kabisa "anajichanganya" akisema tusipoteze ushahidi kwa kutoa taarifa zisizokuwa za uahkika huku akihimiza tusubiri vyombo vinavyohusika vifanye uchunguzi, sasa sijui yeye ili la kumrushia kesi Kaptain wa Meli sio kuharibu ushahidi au alilenga nini hapo?..unajua siku zoote mtu unapoanza na uwongo jitahidi kumaliza vizuri na uwongo wako bila kujichanganya..Aise Jiwe wewe kiboko au noma msemo wa vijana wa zamani eti unatangaza siku nne (4) za maombolezo kuanzia jana ijumaa(tena usiku) maombolezo yameanza jana usiku...kwanini hukutangaza tokea asubuhi .......au kwanini siku nne zisingeanzia leo jumamosi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…