silver_back
JF-Expert Member
- Jul 2, 2018
- 833
- 813
Tanzania sio nchi ya ulaya.Ingekuwa ni nchi za ulaya hadi sasa hivi kwa uzembe ulio fanyika, RC na wahuni wengine wote ungekuta wamesha jiuzulu
Wale madogo walio kwama chini ya pango ingekuwa Tanzania ungekuta walisha kufa wote
Sio suala la abiria kujua kuwa kivuko kina beba watu wangapi, hapo kinachoangaliwa ni uwezo wake wa kubeba ni tani ngapi!! Kama kina beba jumla ya watu 100,na tani 25 za mizigo, je kama siku hiyo kimebeba mizigo tani 10,abilia wanaweza panda hata 200,hilo ni wasimamizi wake ndio wanajua. Je wakataji tiketi wanapokata hawajui idadi inayotakiwa? Na tamesa wote wanajua kuwa huwa vinazidisha abiria kwani mapato yake ya siku c wanayaona? Dsm tu daladala ni nyingi na mtu unalazimisha kujibana humo humo wakati baada ya dk tano kuna nyingine inafika!! Sembuse usafiri wa visiwani ukiikosa leo hadi baada ya siku tatu tena?? Na kama huko ukara hi mala moja kwa wiki alhamisi tu!! Na wao tamesa wanafurahia tu kwani ni trip moja kwa wiki ila mtu wake ni nyomi ya kufa mtu!! Sema limetokea hili ndio watajifanya kuwa ni bahati mbaya!!
Police wanasimamia pale ..tra inajua capacity ya kivuko mana wanakatisha ticket kwann wasisemeHAPO WA KULAUMIWA NI @SUMATRA..Hao polisi TRA,hayo sio mamlaka yao,,kama polisi,kitengo cha Marine wao wanasubiri order tu kutoka Sumatra.
Hebu tuambie mlikuwa wangapi ndani ya Kivuko??"Ndugu zangu mimi nilikuwepo ndani ya kivuko kile cha MV NYERERE,tumepona tu kwa sababu tulikuwa nje,waliokaa ndani ni ngumu sana kupona kwakuwa kivuko kiligeuka gafla chini juu na kina uzito,
mtu ukifunikwa vile ata waokozi wakifika ndani ya robo saa kukuta bado mzima ni ngumu sana.
Kama hauamini na unazani masihara jaribu kuzama ndani ya pipa la maji kwa dakika 10 bila kupumua uone.
Mimi naomba wale waliozidisha abiria na uzito wakamatwe kama Mhe Rais alivyosema
na sisi abiria tujiongeze
Tukifika standi kwenye basi ama bandarini tuwe tunauliza, je hiki kivuko kina beba watu wangapi ?
na huo uzito ubandikwe kwenye mbao za matangazo,ukiona watu wamezidi usipande ila wa afrika sisi tunalazimisha na wengine tunatoa rushwa ili turuhusiwe kupanda madhara ndio haya,
ni ngumu sana kupona ukifunikwa vile ata kama baada ya dakika 10 kivuko kinge ondolewa majini lazima maiti zingekuwa nyingi sana,
watu waangalie ata Marekani boat ili wahi kuzama kwa kugeuka tu watu 17 wakaaga dunia,,waokozi wanafika wakakuta tayari na wenzetu wameendelea sana lakini kifo cha maji kinaua haraka hasa kama mtu unakuwa umefunikwa kama hawa walikuwa ndani.
Hiki kivuko kime karabatiwa mwaka jana na kote huko kimeenda vizuri tu tunakaribia kupaki watu wa ndani wanagombea kutoka nje
kwa kuwa watu walizidishwa uzito ukaenda sehemu moja kikageuka wajuu tukarushwa kwenye maji ndio pona yetu, wavuvi jirani wakaja kutuokoa,,walipoingia ndani ya kivuko kwa chini mda ule ule wakakuta watu washakufa kwa kukosa hewa sasa watu wasilaumu tu bila kujua.
nawaambia usiombe kufunikwa na kivuko, Sikia tu kwenye mitandao...fikisha salam mimi
John Kisekwa.
Da, watu wapo kwenye majonz wewe unaleta mambo yako ya uchama, da kuwa na huruma basi dada, chama umekikuta na utakiacha.Baada ya mbunge wa Ukerewe kuongea kuwa kivuko kilifanyiwa marekebisho baada ya yeye kuwasilisha hoja bungeni, Ufipa imewauma sana kwa huu USALITI wa mbunge wao.
Naona sasa watahamishia majeshi kwenye hoja hii ya jamaa kupona na serikali kusitisha zoezi la uokoaji.
Hivi kaokolewa ? Au kaibuka mahali au katapikwa kama yona Na samaki baada ya siku tatu?
Ana maswali mengi sana ya kujibu huyo jamaaMhuuuu.... Siku zote alikua wap mbona akuonekana....?
Au hakua kazini kuogopa ukubwa wa kesi ikabidi azamie aonekane alikuepo.....?
Ya Mungu mengi.
Tukifika standi kwenye basi ama bandarini tuwe tunauliza, je hiki kivuko kina beba watu wangapi ?
Mbwiga akili imekurudia!Post zako zinaonyesha jinsi ulivyo mweupe kichwani,yaani taifa linalia machozi kwa msiba wewe unaleta mambo ya itikadi?
Habari zinazoripotiwa kutoka eneo la tukio zinasema mtu mmoja ameokolewa akiwa hai asubuhi hii
Mtu huyo ambaye ni engineer wa ferry hiyo amekutwa akiwa hai
Chanzo: ITV
Kumbe serikali imefanya makosa sana kuzuia uokozi usiku ule,wangeokolewa wengi wakiwa hai
Bishoo huyo.Mtoto wa waziri sehemu kubwa ya uhai wake.It was time to sleep,mum said.Lazima aondoke kulala.Kwa kweli huyu jamaa jana kaniudhi sana kwa kukosa ubunifu. Boti iliyozama iko mita 50 toka nchi kavu. Huyu mkuu badala ya kuwasha genereta hata nne tano na kuziweka kwenye boti na kuwasha taa na kuendelea na uokoaji. Kirahisi tu huyu mkuu linasema kuna giza tukalale turudi kesho asubuhi. Kweli ? Really ? Leo baada ya kuhakikisha hakuna mtu aliye hai zoezi linaendelea usiku.
Huyu atumbuliwe kwa kukosa ubunifu akaongoze zizi
Acha roho mbaya mkuuBora afe maana hasira za malaika mkuu zitansulubu[emoji32][emoji32][emoji32][emoji177]
Nina uchungu na hawa nyang'au Mungu ndo anajua. Juzi Mkerewe mzima kisa tu Ukuu wa Mkoa anasitisha uokoaji eti kisa Giza.? Na vimada wa Lumumba humu JF wakaja na hoja nyepesi za kipuuzi. Niliwauliza usiku ule Nani aliyewapima wahanga mle ndani ya meli na kugundua WOTE wamekufa? Haya nyie kunguni mnaoishi kwa kujipendekeza njooni tena muunge mkono kauli za Mongela!!#ITVupdate:Mmoja wa Mainjinia wa Kivuko cha Mv.Nyerere kilichopata ajali ya kuzama ziwa Victoria ameokolewa muda mfupi uliopita akiwa hai.