Hoja nyepesi kabisa hii Mkuu na usirudie tena kuisema hapa katika ulingo huu ' tukuka ' kabisa wa ' Great Thinkers ' wa JamiiForums. Siku ukipata muda nenda pale Kunduchi Beach waulizie hawa Wavuvi wawili maarufu wa enzi hizo ambao walipewa majina ya Samaki Kulwa ( Madenge ) na Samaki Dotto ( Kudura ) kutokana na Uhodari wao wa Kuogelea na Kuyakata maji utadhani walizaliwa Baharini au wana Undugu na akina Papa na Nyangumi.
Siku moja walienda Kuvua kama kawaida yao tena wakiwa na Wavuvi wenzao ambapo huko mbele Mtumbwi wao ulipatwa na dhoruba kali kidogo kutokana na eneo waliloenda ni la Mkondo wa Nungwi kama lilivyo eneo la Pwani ya Msasani jirani na Nyumba ya Nyerere na lilipo Soko la Samaki la Msasani. Cha Kushangaza baada ya kutokea hivyo dhoruba hao akina Samaki Kulwa na Samaki Dotto pamoja na Utundu na Utaalam wao wote wa Kuogolea ila Miili yao ndiyo iliyokuwa ya Kwanza Kuopolewa huku wakiwa wameshakufa na wale ambao ndiyo walikuwa kama GENTAMYCINE ' mangumbaru ' wa Kuyakata Maji ( Kuogolea ) walijitahidi kidogo hadi wenzao wa Mtumbwi mwingine kuja Kuwaokoa ila wakiwa wameshakunywa sana Vikombe na Matumbo yameumuka.
Wewe unadhani katika hao Abiria wote waliokuwemo katika MV Nyerere kulikuwa hakuna akina Samaki Kulwa na Samaki Dotto? Tena usishangae ukasikia kwamba 95% ya waliopoteza maisha ndiyo wale ' Wajuvi / Wataalam ' wa Kuogolea na hao waliookolewa ndiyo ' Mangumbaru ' wenzangu wa Kuogelea. Kujua Kuogolea hakukupi Wewe 100% ' Guarantee ' kwamba ikitokea dhoruba Majini na Chombo ama kwenda mrama au Kuzama kabisa basi utapona. Halafu tusisahau pia kwamba Siku ikipangwa imepangwa tu.