Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

IMG_20180922_212922.jpg
Tangulia mwanafunzi na sisi tupo nyuma yako, ndoto zako zimezimika ghafla.
 
Sipingani na utaratibu wa kawaida wa kuchangiana na kuwafairiji wenzetu waliopatwa na huu msiba mkubwa...
Ila serikali yetu badala ya kuongeza nguvu kwenye uokoaji wa watu wanakimbilia kuchangisha rambi rambi...
Hatujasahau
1.rambirambi za luck vicent iliyouaa watoto wetu
2. Rambirambi za tetemeko la ardhi
Je na hizi zitawafikia walengwa???
Zitaenda kununua meli mpya. Au kwa nini wasinunue helikopter ya kuzunguka visiwani?
 
wanabodi tafadhalini naomba msaada wa kufikiria maana mimi naona kama nafikia etc,
hivi kweli watu wachache wanaoweza kusogea kwaajili ya kuteremka wanaweza kusababisha imbalance ya chombo kikubwa kilichobeba magunia na magari yenye mzigo mzito?

kwani na magari yalisogea au ilikuaje na magunia je yalisogea ili yateremshwe?

nashimdwa kuelewa kama ni kiki au ni nini,, haingii akilini hata kidogo. magunia 100 yanaweza kuwa na kilo 10000 na kama kulikuwa na gari lenye vifaa vya ujenzi inaweza kuwa ni kama kilo 2000,..jumla ni kilo 12000,,, na kwa idadi ya watu 400 wanaweza kuwa na uzito wa kilo 20000,,,je inamaana kwamba watu wote walisogea kwenye kale kanafasi kadogo na kusababisha hiyo imbalances? maana haiwezekani... ile nafasi ya kuteremkia huwa si kubwa kiasi kwaba watu wote 400 wasogeepo!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!


we are in the left track indeed.
Mm mwenyewe APA wameniacha. Njia panda kabisa nkifikiria nashindwa elewa abiria wanasababishaje imbalance ya kiasi icho kuna wengine wanasema dereva alipiga kona kali na mzigo kulemea upande mmoja that's more sensible
 
Kuna mtu yeye linapotekea janga lolote hapa nchini atafanya mbinu yeyote ili afike na kupata kiki mtu huyo tulimuona kwa wahanga wa tetemeko ghafla akaibuka kwa wale wanafunzi wa kule arusha waliopata ajali kote huko alikwenda kwa dhumuni moja la kupata kiki ya kisiasa ili aonekane anajali sana lakini mpaka leo hii hajaonekana huko mwanza kwenye eneo la ajali na kuwapa pole wahanga na wafiwa haijulikani au hatujui labda anaogopa maneno ya rais tusitumie hili tukio kisiasa!
 
..kuna upuuzi mkubwa zaidi ya taarifa kwamba kivuko kilikuwa kinaendeshwa na "dei-waka."?

..taarifa hizo zimeichafua nchi.

Cc tindo, Pascal Mayalla, Richard
Pia nikashifa kwa mtu kusema eti ferry ilikuwa inaongozwa na "dei waka" , huyu ndiye mtu gani? Neno hili haliko kwenye lugha yeyote hapa Duniani. Kuweni makini kabla ya kupost chochote. Ni aibu
 
Back
Top Bottom