Ikiundwa tume yenye umakini, yataibuka mengi sana! Nimetonywa na rafiki kwamba, tamaa ya kujaza abiria ilikuwa ni kawaida yao ili kuongeza kipato binafsi. Waendeshaji wa kivuko hicho walikuwa wakitoa ticketi halali chache, na sehemu kubwa ya pesa zilikuwa zinapigwa hadi Dar es Salaam. Mgao ulikuwa ni mkubwa!
Wakatishaji wa ticket walikuwa wakizunguka na kivuko kama daladala, wakikusanya pesa. TEMESA wanastahili wajieleze vizuri juu ya hilo la kujaza kuliko kiwango kilichopitishwa. Rais huyu ana kazi kubwa ya kunyoosha akili iliyoharibika. Tukubali alivyosema, lazima uwe na viongozi vichaa.