Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Siasa mbona imejaa tele utambulisho tu siasa tupu
 
Mkuu RC yuko very right and your very wrong unaweza kuwa auditor kwa usalama wa kazini lakini sio kwenye marine sector ushauri aliyopewa RC na wataalamu ndio uko sahihi ila nakubaliana na wewe kuwa kama taifa kuna uzembe mkubwa umefanyika toka ajali ya Mv Bukoba na uzumbe huo unaanzia bungeni.
 
Ukerewe wanabaguliwa kimaendeleo kwa sababu ya siasa chafu za awamu hii.
 
Hawa jamaa wanafanya kampeni ya kisaikolojia yaani watu mwisho watasema wakati wa majanga tunawaona ccm tu. Lakini hatujawahi kuwaona upinzani, mfano upo kazini halafu kutwa unaimbwa wimbo ambao huupendi. Mwisho wa siku utaanza kuuimba na kuupenda, hili ndilo walifanyalo hichi chama cha majangili.


Ndukiiiii 🏃‍♂️🏃‍♂️🏃‍♂️
 
Mkuu ushauri mzuri sana. Lakini umepima viwango vya elimu tulivyopewa? Shida iko hapo ndugu.
 
Wamevaa body tight zao huko boss wao yuko dar hana habari nao
 
Mkuu inaonekana hata huna ufahamu wa kazi za sumatra na kwa taaarifa tu ni kuwa hivyo vivuko viko chini ya Temesa.
 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema baadhi ya pesa zitakazopatikana katika michango ya Watanzania zitatumika kujenga uzio na mnara katika makaburi ya watu waliokufa katika ajali ya kuzama kwa kivuko cha MV Nyerere.



Fedha hizo zinachangwa kupitia akaunti maalumu iliyofunguliwa katika benki ya NMB pamoja na namba maalumu ya Tigo kupitia simu ya mkononi.
Soma zaidi: RC Mongella awapongeza wananchi, wavuvi wa Ukara




Akizungumza katika shughuli ya mazishi leo Septemba 23,2018 visiwani Ukawa wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza amesema baadhi ya miili ya watu waliokufa katika ajali hiyo fedha hizo hazitatumika katika shughuli yoyote nje ya tukio hilo.



"Fedha hizi ni za wafiwa hivyo hatuna budi kuzitumia kulingana na mwenendo wa tukio," amesema Majaliwa.
Amesema ili kuhakikisha wananchi wa eneo hilo hawapati tabu Serikali iko katika mkakati wa kuleta kivuko cha muda.



"Tutafanya ukarabati wa kutosha katika baadhi ya vivuko ikiwemo Mv Misungwi, Sengerema ili kuimarisha usafiri wa majini katika maeneo yote," amesema Kassim.
Soma zaidi: Polepole: CCM kuisimamia Serikali ili kuimarisha usafiri Ziwa Victoria
Majaliwa amewaomba Watanzania kuwatia moyo wafiwa badala ya kuwaambia maneno yanayoweza kuwasababishia maumivu.



"Watu hawa wamepoteza ndugu zao wa muhimu hivyo ni vyema kuwapatia maneno mazuri yanayotia moyo badala ya kuwajaza maneno ya upotoshaji na tuiache Serikali ifanye jitihada zake," amesema Majaliwa.



Amesema muda wowote kuanzia sasa tume ya uchunguzi itaundwa ili kubaini chanzo cha ajali hiyo na Serikali ikiwa tayari iko katika mazungumzo juu ya matumizi ya Meli ya Mv Nyahunge.
Kivuko cha Mv Nyerere mpaka sasa takwimu zinaonyesha kilikuwa na watu 265 ambao kati yake 224 wamepatikana wakiwa tayari wamepoteza maisha huku 41 wakipatikana wazima.
 
Niliposema kwamba kuna viongozi wakubwa tu wanatakiwa kujiuzulu kwa hii kashfa kuna mjinga mjinga alinipandia juu!! Kujiuzulu hjuko hakumwachi salama kichaa wangu, naye anatakiwa kutema madaraka akapumzike amwachie msaidizi wake amalizie mwendo. Mkiambiwa CCM haina huruma na Wa-Tanzania mnabisha sasa mnaonaaaaa?? Kikosi cha polisi wa doria ziwa victoria hawana boats? Jeshi la wananchi hawana boats? Tukivamiwa sasa inakuwaje? Shit-hole country!!
 
Na sisi tunampongeza kwa kuwapongeza wakerewe.

Sisi tunawapa pole watani zake Nyerere "Wakara"
Kwa kuzamishwa kiutaniutani kwenye meli ya mtani wao!!

Sijui kuwajengea mnara ndio kuwafariji au kuwakebehi!!
 
Na kukarabati kivuko ili huduma za kuvusha ziendelee.
Fedha zingine za michango zitatumika kununua cctv ili tuone na kujua abiria wanaoingia kwenye kivuko kama ni wengi au wanene
Nb; serikali haijasababisha ajali, hivo hakuna bajeti ya kukarabati na haipaswi kulaumiwa
 

Mkuu hivi visiwa vipo wapi "visiwani Ukawa" au ndio mahaba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…