Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Mwenye macho haambiwi tazama. Japo ukweli daima unauma na kwa kuwa sasa hivi tuna aina fulani ya siasa na mwelekeo mpya wa maigizo katika maisha. Twendelee tu kusema siasa isichukue nafasi ilihali matamko ya kisiasa yakichukua na mwelekeo wa kisiasa yakichukua nafasi ya kipekee na kutamalaki kwa sana
 
Mkuu,Nabii Nuhu alizingatia hesabu za idadi ya wanyama aliopaswa kubeba kwa mujibu wa kanuni alizopewa.Tatizo letu ni kupuuzia mambo ya msingi.
 
Amani ya bwana.

Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mh John Mongella akihojiwa na vyombo vya habari ametolea ufafanuzi ule upotoshaji mkubwa uliofanywa na wanasiasa watafuta kiki mara baada ya kutokea ajali ya kuzama kwa kivuko cha Mv Nyerere kwenye ziwa victoria.

RC Mongella amesema yeye ni mkuu wa mkoa tu na wala si mtalaamu wa maswala ya uokoaji, hivyo alichokifanya na anachokifanya sasa hivi ni kupokea na kufanyia kazi maoni ya watalaamu wa uokoaji majini (divers).
Kabla ya kusitisha zoezi la uokoaji siku ya kwanza aliambiwa hali ya maji ziwani imeanza kuwa mbaya na kutokana na usiku ,hivyo angetumia kofia yake ya ukuu wa mkoa kulazimisha divers waendelee na kazi angeweza kusababisha madhara zaidi na angeweza hata kuwapoteza hao wataalamu wa uokoaji.

Maelezo ya mkuu wa mkoa ni majibu safi kabisa kwa wanasiasa wakurupukaji wanaopenda kudandia mambo bila kuwa na ushahidi wa maelezo ya kutosha.
Mara baada ya kutokea ajali hiyo wanasiasa kama Zito, Mbowe na Mbatia walikuwa na uwezo wa kufika eneo la tukio na kushirikiana na wafiwa kwa haraka mno hata kwa kutumia ndege lakini hawakufanya hivyo badala yake wakaanza kuitisha waandishi wa habari wakiwa Dar kutoa matamko na kupotosha watu ,huku wakijifanya wanaijua sana hali ya ajali kuliko watu waliopo eneo la tukio!!

Hali hiyo ya kutafuta kiki za kisiasa kupitia ajali na matatizo ya watanzania ilikemewa vikali na Rais wetu mpendwa Dr Magufuli. View attachment 875133
Ujinga tu. Kwa hyo angekuwemo mule jemedali wetu john pombe wange ahirisha zoezi kwa sababu ya giza?tuache siasa yashapita.
 
Kuna upotoshaji mkubwa unafanywa kwa kutengeneza kauli/maneno yanayosemekana kutoka kwangu. Naomba kauli hizo zipuuzwe. Tokea kutokea kwa ajali ya kivuko cha MV Nyerere nimekuwa na mawasiliano ya karibu na viongozi wangu wa chama na nina support ya hali ya juu ya viongozi wangu kipindi chote na hakuna kipindi chochote nilichotofautiana na yeyote. Aidha, baadhi ya viongozi wangu wangu wa chama wapo eneo hili la tukio mda wote tokea siku ya tukio hili. Naomba wote walio nyuma ya upuuzi huu wawaheshimu wakerewe, wawaheshimu marehemu wetu tuliowapoteza. Nina majonzi, nina masikitiko na ninaomba mtambue hill.
Mhe. Joseph Mkundi (mb)
Ukerewe
 
1537703202888.png

Kwa wakerere, wakara, wajita, wakwaya na waruri kilichotokea ni kupinduka (KWIFUMA) na siyo kuzama (KUSIKA). Kama ingesika (kuzama) ni hakika wangetumia uzoefu wao wa kuogelea na wangeokoka wengi. Kwa vile imepinduka ikawafunika ndiyo maana wamekufa kibudu na wengi kiasi hicho. MUNGU AWAPE PUMZIKO LA AMANI
 
Wapuuzi ni walioshindwa kupeleka kivuko kinachokidhi mahitaji sababu mbunge wa eneo husika ni wa chadema.
 
Wewe mleta mada umeenda Mazishi au fashion show kuangalia watu wamevaa nini?
 
Kwa mara nyingine CCM imenunua msiba ambalo ulitarajiwa ufanyike kiserikali bila jezi za kijani. Kwenye eneo la maziko nguo za kijani zimeanza kutawala na ni za haohao wanaoshauri tuache tofauti za kiitikadi za kisiasa! Hali hii ndiyo inayotufarakanisha watanzania na lawama wanapewa wanaotengwa!
Kapicha kangenoga zaidi
 
Mwenyezi Mungu hamfichi mnafiki. Hawa ndo waliosema wanasiasa wasitafute kiki kupitia huu msiba lakini wamekuwa wa kwanza kwenda na vijora vya kijani msibani.

CCM huwa nawaona kama mchawi aliyechelewa kurudi toka makaburini alikokuwa anawanga!
 
Kweli tuna matatizo ya kuchambua mambo kwani wanaposema tusiweke mambo ya siasa na mambo ya vyama wana maana ya watu wasivae nguo za vyama vyao? Nadhani hapo kuna shida ya kutafakari mambo
Kwani wakienda na nguo za kawaida inawapunguzia nini? Matukio yakitokea wanakimbilia nyumbani kubsdili nguo na kuvaa ya kijani ili tuone hicho chama kinawapenda watu, mbona hamkwenda na uniform kufunga injini mpya za kivuko kuokoa maisha ya mamia ya Watanzania wenzetu waliozama majini?
 
Costa Concordi ilijikwaa kwenye jiwe na hii imepinduka tofautisha hapo!
 
Back
Top Bottom