Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Duh haya ni majanga na aaibu kwa taifa la tz yaani serkal yenye misiraha na vikosi vya maaskar wote hao hatuna wataalam jmn wakat kila mwaka wa uchaguzi misiraha mipya inanunuliwa, ni rahisi kujiandaa na chaguzi na sio majanga tz buana[emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]
Bora wangeonesha ukakamavu kama ule walionesha wakati wa kuzuia ukuta, walituonesha uwezo mkubwa walionao ktk kulinda usalama na maisha ya watanzania, kumbe kuokoa maisha yetu wakati wa majanga hawawezi. Ombi kwao, wajenge haraka daraja la wami wasije kusingizia giza siku maafa yakitufika.
 
Hii comment ilitakiwa iwe Ndio uzi ili jamii ipate taarifa sahihi na sio huu upotoshaji unaofanywa na wanaojali matumbo.

Mkuu pole sana kwa kupoteza ndugu. Umetoa ushuhuda ambao wengi Naona hawajatilia maanani. Hakuna lisilo na mwisho wapotishaji na wazembe wakati wao wa hukumu utafika tu
Hawa vijana wa kijani ndio wanawasafisha mabosi wao mkuu wa mkoa na mkuru na count
 
Naomba mnijibu, nataka kujuwa hao divers are they professional trained and awarded certificates na wana utaalamu kiasi gani au ni divers wa mtaani tu wamejitolea kuokoa
Hamna wataalam anaependa kuona watu wanaangamia akasema tusitishe zoezi la uokozi hao ni wahuni kama wahuni wengine ambal hawana utu kabisa .
 
Amani ya bwana.

Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mh John Mongella akihojiwa na vyombo vya habari ametolea ufafanuzi ule upotoshaji mkubwa uliofanywa na wanasiasa watafuta kiki mara baada ya kutokea ajali ya kuzama kwa kivuko cha Mv Nyerere kwenye ziwa victoria.

RC Mongella amesema yeye ni mkuu wa mkoa tu na wala si mtalaamu wa maswala ya uokoaji, hivyo alichokifanya na anachokifanya sasa hivi ni kupokea na kufanyia kazi maoni ya watalaamu wa uokoaji majini (divers).
Kabla ya kusitisha zoezi la uokoaji siku ya kwanza aliambiwa hali ya maji ziwani imeanza kuwa mbaya na kutokana na usiku ,hivyo angetumia kofia yake ya ukuu wa mkoa kulazimisha divers waendelee na kazi angeweza kusababisha madhara zaidi na angeweza hata kuwapoteza hao wataalamu wa uokoaji.

Maelezo ya mkuu wa mkoa ni majibu safi kabisa kwa wanasiasa wakurupukaji wanaopenda kudandia mambo bila kuwa na ushahidi wa maelezo ya kutosha.
Mara baada ya kutokea ajali hiyo wanasiasa kama Zito, Mbowe na Mbatia walikuwa na uwezo wa kufika eneo la tukio na kushirikiana na wafiwa kwa haraka mno hata kwa kutumia ndege lakini hawakufanya hivyo badala yake wakaanza kuitisha waandishi wa habari wakiwa Dar kutoa matamko na kupotosha watu ,huku wakijifanya wanaijua sana hali ya ajali kuliko watu waliopo eneo la tukio!!

Hali hiyo ya kutafuta kiki za kisiasa kupitia ajali na matatizo ya watanzania ilikemewa vikali na Rais wetu mpendwa Dr Magufuli. View attachment 875133

Wewe badilisha id yako badala ya etwegw anza kutumia Ebwege maana huko upstairs ni empty set!
 
Hapa ndipo kama nchi tunapokuwa wapumbavu kwa ujumla wetu.
Siku ya alhamis SAA 1.22 jioni nikiwa eneo la tukio nilimuona na kumsikia Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela akitangaza kusitisha zoezi la uokozi kwa sababu ya giza. Na nikiri wazi sikumsikia akisema ameshauriwa na wataalamu au yalikuwa mawazo yake. Wakati anatoa tangazo lake kulikuwa na divers ndani ya kivuko ambao walitoka na miili kadhaa saa mbili kasoro hivi. Mara baada ya kutangaza kusitishwa kwa zoezi vilio vilisikika mwaloni toka kwa ndugu waliokuwa na matumaini labda kuna watu wako hai ndani. Baada ya kusoma mawazo ya waombolezaji Mkuu wa wilaya ya Ukerewe akalazimika kutuliza hali ya hewa kwa kusema, namnukuu; Ndugu zangu katika hali ya kawaida mtu hawezi kukaa ndani ya maji kwa masaa zaidi ya manne bado akawa hai kama hana vifaa vya kumsaidia kupumua, Sisi viongozi wenu tuna huzuni kama ninyi lakini kazi hii haiwezi kufanyika gizani, mwisho wa kunukuu". Kwa vile watanzania huwa tunaona kauli za viongozi ni kauli za mbingu wengi walitii lakini wachache wenye uchungu walitoa hoja wakaonekana wabishi mbele ya viongozi. Hilo ziwa lililochafuka SAA 1 jioni hapa Ukara ni lipi? Au waliondoka nalo sisi hatukuliona? Kivuko kimezama chini ya mita 100 toka ufukweni, wazoefu wa ziwa mnajua vizuri, hivi hata ziwa likichafuka kwa umbali huo na kwa watu wenye vifaa watashindwa kuendelea na kazi?
Kesho yake baada ya kelele za wananchi na mitandaoni zoezi lilifanyika hadi usiku siku ya Ijumaa. Hizi sababu za ziwa kuchafuka tumeanza kuzisikiaIjumaa jioni baada ya Waziri Mkuu kuwepo na walikuwa wanaongea kama kujikosha tu na Leo ndo zimeletwa hapa kama sababu rasmi.
Siasa zinatufanya watanzania tukose mawazo ya kuhoji hata vitu vya msingi. Nawashangaa vijana wa ccm mitandaoni mnavyokosa utu na kushabikia makosa ya kiutendaji kwa vile tu aliyekosea ni wa Chama chenu. Sidhani kama kuna mwanaccm mwenye uchungu na aliyepotelewa na ndugu/jamaaa/rafiki kama ilivyonitokea Mimi anayeweza kuunga mkono mawazo yenu. Mimi nilisafiri Jumanne na kivuko hicho hicho na alhamis kikapata ajali, lakini maneno ya usalama mdogo ndani ya kivuko yalikuwepo, na bado tulijaa ingawaje si kama siku ya gulio Bugolora. Siku za Gulio mpaka mitumbwi toka Chifule na Chibasi huwa inasadia kutokana na wingi wa watu.
Mbunge wa Ukerewe kawa mkweli kwamba kivuko kilifanyiwa ukarabati, napo ni kuwekewa injini mpya tu na hoja kuu hata kwenye baraza za madiwani ni kupatiwa kivuko kipya na kikubwa zaidi.
Acha nikae kimya Nina majonzi.
Pole mkuu umesema ukweli ambao wote tunausema maana wnatupa sababu zisizo mashiko kabisa
 
Maagizo ya serikali hayawaruhusu viongozi wa upinzani kufanya shughuri zozote kwenye majimbo ambayo si yao, tukumbuke mhe. Zitto licha ya kuwa mwenyekiti wa taifa wa ACT lakini alikamatwa Morogoro kwa kufanya siasa eneo ambalo si mbunge!
Hapa ndipo kama nchi tunapokuwa wapumbavu kwa ujumla wetu.
Siku ya alhamis SAA 1.22 jioni nikiwa eneo la tukio nilimuona na kumsikia Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongela akitangaza kusitisha zoezi la uokozi kwa sababu ya giza. Na nikiri wazi sikumsikia akisema ameshauriwa na wataalamu au yalikuwa mawazo yake. Wakati anatoa tangazo lake kulikuwa na divers ndani ya kivuko ambao walitoka na miili kadhaa saa mbili kasoro hivi. Mara baada ya kutangaza kusitishwa kwa zoezi vilio vilisikika mwaloni toka kwa ndugu waliokuwa na matumaini labda kuna watu wako hai ndani. Baada ya kusoma mawazo ya waombolezaji Mkuu wa wilaya ya Ukerewe akalazimika kutuliza hali ya hewa kwa kusema, namnukuu; Ndugu zangu katika hali ya kawaida mtu hawezi kukaa ndani ya maji kwa masaa zaidi ya manne bado akawa hai kama hana vifaa vya kumsaidia kupumua, Sisi viongozi wenu tuna huzuni kama ninyi lakini kazi hii haiwezi kufanyika gizani, mwisho wa kunukuu". Kwa vile watanzania huwa tunaona kauli za viongozi ni kauli za mbingu wengi walitii lakini wachache wenye uchungu walitoa hoja wakaonekana wabishi mbele ya viongozi. Hilo ziwa lililochafuka SAA 1 jioni hapa Ukara ni lipi? Au waliondoka nalo sisi hatukuliona? Kivuko kimezama chini ya mita 100 toka ufukweni, wazoefu wa ziwa mnajua vizuri, hivi hata ziwa likichafuka kwa umbali huo na kwa watu wenye vifaa watashindwa kuendelea na kazi?
Kesho yake baada ya kelele za wananchi na mitandaoni zoezi lilifanyika hadi usiku siku ya Ijumaa. Hizi sababu za ziwa kuchafuka tumeanza kuzisikiaIjumaa jioni baada ya Waziri Mkuu kuwepo na walikuwa wanaongea kama kujikosha tu na Leo ndo zimeletwa hapa kama sababu rasmi.
Siasa zinatufanya watanzania tukose mawazo ya kuhoji hata vitu vya msingi. Nawashangaa vijana wa ccm mitandaoni mnavyokosa utu na kushabikia makosa ya kiutendaji kwa vile tu aliyekosea ni wa Chama chenu. Sidhani kama kuna mwanaccm mwenye uchungu na aliyepotelewa na ndugu/jamaaa/rafiki kama ilivyonitokea Mimi anayeweza kuunga mkono mawazo yenu. Mimi nilisafiri Jumanne na kivuko hicho hicho na alhamis kikapata ajali, lakini maneno ya usalama mdogo ndani ya kivuko yalikuwepo, na bado tulijaa ingawaje si kama siku ya gulio Bugolora. Siku za Gulio mpaka mitumbwi toka Chifule na Chibasi huwa inasadia kutokana na wingi wa watu.
Mbunge wa Ukerewe kawa mkweli kwamba kivuko kilifanyiwa ukarabati, napo ni kuwekewa injini mpya tu na hoja kuu hata kwenye baraza za madiwani ni kupatiwa kivuko kipya na kikubwa zaidi.
Acha nikae kimya Nina majonzi.
 
Mkuu hata OSHA,SUMATRA nao wana mkanganyiko baadhi ya majukumu na mamlaka.
 
Huyo RC na timu yake hawajali maisha ya wanyonge. Wavuvi wa dagaa wanavua usiku japo kuna giza inakuwaje kuvua watu (kuokoa) kusitishishwe kutokana na giza.
 
Amani ya bwana.

Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mh John Mongella akihojiwa na vyombo vya habari ametolea ufafanuzi ule upotoshaji mkubwa uliofanywa na wanasiasa watafuta kiki mara baada ya kutokea ajali ya kuzama kwa kivuko cha Mv Nyerere kwenye ziwa victoria.

RC Mongella amesema yeye ni mkuu wa mkoa tu na wala si mtalaamu wa maswala ya uokoaji, hivyo alichokifanya na anachokifanya sasa hivi ni kupokea na kufanyia kazi maoni ya watalaamu wa uokoaji majini (divers).
Kabla ya kusitisha zoezi la uokoaji siku ya kwanza aliambiwa hali ya maji ziwani imeanza kuwa mbaya na kutokana na usiku ,hivyo angetumia kofia yake ya ukuu wa mkoa kulazimisha divers waendelee na kazi angeweza kusababisha madhara zaidi na angeweza hata kuwapoteza hao wataalamu wa uokoaji.

Maelezo ya mkuu wa mkoa ni majibu safi kabisa kwa wanasiasa wakurupukaji wanaopenda kudandia mambo bila kuwa na ushahidi wa maelezo ya kutosha.
Mara baada ya kutokea ajali hiyo wanasiasa kama Zito, Mbowe na Mbatia walikuwa na uwezo wa kufika eneo la tukio na kushirikiana na wafiwa kwa haraka mno hata kwa kutumia ndege lakini hawakufanya hivyo badala yake wakaanza kuitisha waandishi wa habari wakiwa Dar kutoa matamko na kupotosha watu ,huku wakijifanya wanaijua sana hali ya ajali kuliko watu waliopo eneo la tukio!!

Hali hiyo ya kutafuta kiki za kisiasa kupitia ajali na matatizo ya watanzania ilikemewa vikali na Rais wetu mpendwa Dr Magufuli. View attachment 875133
Hivi mbona mnatumia nguvu nyingi kukanusha uzembe huu, nadhani tunahitaji kujieleza kwa vitendo zaidi ya matamko yasiyo na tija
 
Kwanini hukwenda wewe kuokoa au hata kuvuta ndugu zako pia kama uliona ni vyema wangeendelea.. kwani leo umekatazwa pia.. jipange nenda usiku ukafanye yako.. wala hakuna atakaye kujali utakuwaje.. usisahau kujivalisha matairi mwilini maana hata kuogelea hujui na boti unaisikia kama usikiavyo baisikeli.
We jinga kweli ndio majibu gani ya kumjibu mtu aisee we huna hata huruma unchojali ni kuwasafisha mafiem wwnzako tu
 
Attachments

  • pic+polepole.jpg
    pic+polepole.jpg
    11 KB · Views: 15
Kwa hiyo waokoaji hawaruhusiwi hata kula?
unajua maana ya kiongozi kuhamasisha watu kufanya kazi pratically! umewahi kuzijua au kuzisoma principles za kiongozi makini...

umewahi kufanya kazi sehemu yenye kiongozi smart automatically ukajiona unafafanya kazi mpaka unasahau kula?

umewahi kupata uzalendo wa japo kujiuliza wale waliopo majini ni watanzania wenzangu na hawajala...mimi njaa kitu gani?

ukipata majibu ya hayo maswali utajielewa what is on your mind...
 
Wataalamu ndio wenye uwezo wa kujua , vipi wanaweza fanya, NA ushauri wao ni muhimu sana. Tukumbushane wale watoto 11 waliopotea ndani ya pango Thailand 2017, ili hukua karibia wiki nzima, mikakati kuwekwa sawa ili kuwaokoa, hata ile Submarine ndogo iliyotolewa na tajiri wa magari ya Tesla, ilikataliwa, NA waokowaji wakaonekana wana nia mbaya, mwishowe Bw Elon Musk aliabika kwa propaganda alizozifanya.

Mogela yuko sawa kama ayasemayo ni ya kweli.

Akina Mbowe NA Zitto hapa wamejiabisha, si tungeona hata kwenye hizo press conference zao wakianzisha michango .
 
Tena ni aibu kubwa, yaani unasitisha shughuli za uokozi kwa sababu ya giza!! Hebu tukumbuke changamoto walizokutana nazo askali wetu wakati wa vita na Idd Amin, kama viongozi wetu wangekuwa na akili ndogo kama ya hiyo ya kusingizia giza Idd angeingia hadi vyumbani mwetu, ndugu zangu, Tanzania ni yetu sote, mtu akikosea aombe radhi si kumtetea kama mnavyofanya. Kiukweli mkuu wa mkoa alikosea saana, naamini kuna watu tumewaua kwa kusitisha lile zoezi, na Mungu kathibitisha kupitia huyo Eng aliyekutwa hai huku akikaa ndani ya maji kwa masaa zaidi ya 48
Ndio mkuu uko sahihi kabisa Harafu wao wana kuja na hoja nyepesi eti mtu hawezu kuaa majini kw zaidi ya masaa 3 akawa hai mbona huyo yy amepona sasa aibu yao hao mafiem na roho zao mbaya.
 
Bora wangeonesha ukakamavu kama ule walionesha wakati wa kuzuia ukuta, walituonesha uwezo mkubwa walionao ktk kulinda usalama na maisha ya watanzania, kumbe kuokoa maisha yetu wakati wa majanga hawawezi. Ombi kwao, wajenge haraka daraja la wami wasije kusingizia giza siku maafa yakitufika.
Wanachoju ni ufisadi tu hamna lingine wanaleta masihara na maisha ya watu ingekuwa kuna ndugu zao mule wangestisha !!??[emoji26][emoji26]
 
Back
Top Bottom