Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Taarifa iliyotolewa na Katibu wa Idara ya uhamasishaji na chipukizi UVCCM Taifa Ndugu Hassan Bomboko inasema Mwenyekiti wa UVCCM Ndugu Kheri Denis James (MCC) amesikitishwa na kuguswa na ajali mbaya ya kuzama kwa kivuko cha MV Nyerere katika ziwa Victoria iliyotokea leo ambapo wapo waliojeruhiwa na wengine kufariki dunia hivyo ametoa salamu za pole kwa wote walioguswa na kuathirika na tukio hili la kuhuzunisha na kusikitisha.

Taarifa hiyo imeendelea kusema Ndugu Kheri anawaombea majeruhi kupata nafuu, ndugu na wote waliopoteza jamaa zao wawe na subira katika kipindi hiki kigumu.
 
Huyo rubani aliruhusu vipi watu na mizigo kuingia kupita kiasi ? Imagine mama yake angekuwepo pale halafu anaambiwa zoezi la uokozi limesitishwa till tomorrow.
 
Serikali ndio wanamiliki na kuendesha hivyo vivuko wao ndio wanapaswa kulaumiwa,halafu ni aibu hakuna list ya majina /idadi ya wasafiri waliokuwa kwenye kivuko

Dah! Kumbe serikali ndiyo wamiliki!! Nashkuru kamanda nimekuelewa
 

Hoja yako nzuri ila inaelekea bado hatujajifunza kutokana na ajali zilizopita maana ajali kama hiyo ilitokea miaka 22 iliyopita ya Mv Bukoba kupinduka na ilichukua muda waokoaji kufika eneo la tukio na hata waliofika hawakuweza kuokoa

Kutokana na ajali hiyo ya Mv Bukoba. Ina maana hatujajipanga kweli huku mtu mmoja akizunguuka kuangalia kero za wananchi akiwa anahutubia helicopter ipo juu...walishindwa kusafirisha waokoaji kwa ndege faster eneo la tukio?
 
Pole Tanzania.....najuwa TLS na wapinzani watakuja hap na kusema serikali ndiyo inahusika na kuzama huku.
 
Badala ya wangenunua kipya wamenunua injini mpyaa hivi kuna haja gani ya kujenga reli ya umeme wakati kivuko kipya chatushinda...!!

Twafanya chaguzi daily pesa za kivuko hatunaa!!
Tukishauri hivi wanasema sisi ni BAVICHA hatuungi juhudi nzuri za ANKALI JIWE,Tumeenda kununua Drimulaina bovu kwa bei mara mbili ya kawaida,Tumenunua MV daresalamu bovu limefanya safari moja limekufa,Tumehamisha barabara chini tumeipeleka juu tazara huku tukijisifu,tumetumia mabilioni ya Shilingi kufanya uchaguzi hewa huku tayari kura za maruhani walikuwa wanazo kwenye ballot box,nashauri serikali tufanye vitu vinavyogusa wananchi wengi kwanza tuachane na miradi hewa white elephant,tuhimarishe vivuko hatarishi vyote,tujenge zahanati/vituo vya afya,tuimarishe miundombinu especially madaraja yanayounganisha vijiji/miji/kitaa/vitongoji etc tukishamaliza hayo mambo ndio twende kwenye vitu visivyo na msingi kama hayo MABOMBADIA na Miradi hewa ya UMEME.
 
Kwa hiyo kesho ndio tunaokoa watu au tunaenda kuvua maiti? Karne ya 21 tunashindwa kufanya uokoaji usiku na mchana kisa taa tu? That's a big joke! Sasa kama kivuko kingezama usiku tungesubiri mpaka asubuhi? Sometimes hawa viongozi wawe serious..mbona katika mbio za mwenge mnaweka taa na mnakesha? Kwa stahili hii viwanda tutaendelea navyo ni shoe shine na vyerehani
 
Mungu awatie nguvu wafiwa wote na wale walionusurika kifo.
 
Kabisa yaani TAA tu ndio imesababisha kusitisha uokoaji,Tumenunua meli bovu mv daresalamu kwa bilioni 8 lakini tumeshindwa kujidhatiti na majanga yaani TAA tu za uokoaji tumeshindwa kununua tunasubiri mpaka kesho jua liwake halafu tunasema tunaendelea na uokoaji,sasa unaenda kuokoa nini hiyo kesho?
 
NDIYO NANI HUYO?????
 
Unasitisha uokoaji kisa giza!?!?
Hao wanajeshi wetu wanafanya nini hamna chopper iwapeleke.
Huyo kada wa CCM anatoa kauli za kijinga tu.
Yani giza lisababishe kuokoa watu.!?!?
 
Unafikiri angekuwemo mama yake kichaa huo uokoaji ungeghairiswa?
 

Kama una vifaa, teknolojia na well equipped rescue team huwezi kuacha kuokoa watu eti sababu ya giza, wewe huoni ajali bado ni mbichi maana imetokea mchana wa leo kiasi cha baadhi ya watu bado kuwa hai..

Huu ni udhaifu lazima usemwe.
 
Viongozi wa Ajabu sana tulionao, sasa hyo kesho unaenda kuokoa au kuokota maiti.
 

Sio kila sehemu muweke siasa na hoja za kipumbavu kama hizi, mnajifanya kujua kila jambo end of the day mwaonekana ka mitaa.hiratu, unajua kinachosababisha marine vessel hasa melii nini?
Kunapokosekana uwiano wa uzito kati ya mzigo wa chini (watertanks) na ule wa juu (abiria na mizigo) hiyo ndo huwa sababu kubwa ya meli kuoverturn hata kama ni mpya.



Maafisa wa meli wanapozidisha mzigo hupunguza maji ya chini ili kudanganya wakaguzi...hiki ndicho kilichotokea hata kwa Mv Bukoba, unapopunguza mzigo wa chii na kuzidisha wa juu nadhani unajua nini kitatokea endapo ukiweka chupa ya dasani yenye maji nusu ndani ya besini na ukafunga kitu kizito juu ya chupa chenye uzito kuzidi hayo maji nusu. Ni Rais aliyewatuma kuover load? hizi kejeri na dhihaka dhidi ya Rais zinatoka wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…