Taarifa nilizozipata haraka sasa hivi ni kuwa watu wengi sana wanahisiwa kufa maji baada ya kivuko kubinuka juu chini, chini juu katika kisiwa cha UKALA wilayani Ukerewe.
====
Taarifa Kwa Umma Kutoka Wakala wa Ufundi na Umeme-TEMESA Kuhusu Kuzama Kwa Kivuko Cha MV.Nyerere
View attachment 872340
Kivuko cha MV Nyerere kinachofanya safari zake kati ya Bugorara na kisiwa cha Ukala katika ziwa Victoria kimezama huku taarifa za idadi ya watu waliokuwemo ndani ya kivuko hazijajulikana.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Jonathan Shana amesema kivuko hicho kimezama wakati kikielekea katika Kisiwa cha Ukara. Kiliondoka saa 6 mchana na ilipofika saa nane kamili mchana kilipinduka.
Amesema bado hawajapata idadi kamili ya waliokuwemo kwenye kivuko hicho.
Meneja wa Wakala wa Ufundi na Umeme (Temesa), Hassan Karonda amekiri kuzama kwa kivuko hicho na yuko njiani kulekea huko na watatoa taarifa baadaye.
Kivuko cha MV. NYERERE kilinunuliwa na kuanza kutoa huduma mwaka 2004. Kilifungwa injini mbili mpya zenye thamani ya shilingi milioni 191 JULY 2018. Kivuko cha MV. Nyerere kina uwezo wa kubeba tani 25 sawa na abiria 100 na magari 3 kwa wakati mmoja.
UPDATES: 1900HRS
=> Watu watano wamekufa na wengine 32 wameokolewa mpaka sasa ila hali zao ni mbaya kufuatia ajali ya kivuko cha MV Nyerere.
=>
"Mtu Hajalipwa Mshahara Halafu Anasikia Trilion 1 Imepotea Inauma" -Joseph Mkundi
Mbunge Joseph Mkundi akitahadharisha kuhusu kivuko cha MV Nyerere Apr 24, 2018
Alikuwa akichangia hoja ya bajeti ya Wizara ya Uchukuzi na Mawasiliano iliyopo chini ya Waziri wake, Profesa Makame Mbarawa.
UPDATES:
AJALI YA KIVUKO CHA MV NYERERE: WATU 44 WAMEFARIKI, ZOEZI LA UOKOAJI LASITISHWA HADI KESHO
Ambali na idadi hiyo ya waliofariki, Watu 37 wameokolewa katika ajali huku hali zao zikiwa mbaya
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella amesema zoezi la uokoaji limesitishwa kutokana na giza kuingia