Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Ninachofikiria kukimbilia ma kukisema ni 'Mungu atuepushe'!
Ila kweli hatuna akili ya kujikinga/ kujiokoa na janga lolote. Vyombo vya moto tunavitumia, vina manufaa mengi tu, ila bahati mbaya vina madhara pake tunapovitumia ndivyo sivyo. Ni wajibu wa serikali kutoa mafunzo kabla ya kukabidhi kwa watumishi/ watoa huduma katika vyombo hivi, na kuendelea kuwajibika kuhakikisha watumiaji nao (wamanchi) wanaelimishwa matumizi mazuri kila wanapoingia/ au wawamo ndani ya chombo.
Hii tabia ya kila chombo kinapokaribia ufukweni, basi abiria walio kwa miguu na walio na pikipiki au baiskeli kusogea karibu na sehemu ya kutokea bila ya kukemewa ndio inayoleta maafa.
 
Natafakari tu,
Kama PhD zimeokoa mtu mmoja, na wasio na elimu wameokoa 40,
Kuna haja ya PhD ?

Bado natafakari.
Ukimaanisha nini kwa mfano, kwani wasio na phd walishawahi kutengeneza dawa ya malaria, au dawa za kufumbaza virusi vya ukimwi, au wasio na phd washawahi kukuletea madawa hayo unayoyaona mahospitalini kutoka kwenye mashirika ya wasio na phd huko nchini kwao wasio na phd, wasio na phd walihudumia hao waliookolewa kwenye ajali wakawapa matibabu? Nijibu tu mkuu
 
Accident ya kivuko ndani ya maji na ugonjwa unao enezwa kwa ku contacts na victims ...... mi naona ebola tunaweza kuhandle ila maji mkuu hayana fundi
 
Ukimaanisha nini kwa mfano, kwani wasio na phd walishawahi kutengeneza dawa ya malaria, au dawa za kufumbaza virusi vya ukimwi, au wasio na phd washawahi kukuletea madawa hayo unayoyaona mahospitalini kutoka kwenye mashirika ya wasio na phd huko nchini kwao wasio na phd, wasio na phd walihudumia hao waliookolewa kwenye ajali wakawapa matibabu? Nijibu tu mkuu
Babu wa Loliondo ana Phd? Mbona wenye PhD zao walienda kupata dawa? Mbona tunatumia dawa za miti shamba na zinatibu vizuri kuliko hizo za wenye PhD ?
 
Lakini watanzania haya mapuuzi wanayaona? Nilitegemea Jiwe akipita mahali akute hakuna mtu yeyote barabarani, lakini majuha yamehazana
 
Ukipata fursa nenda wizara ya afya ukaulizie maandalizi dhidi ya mlipuko wa ugonjwa wa Ebola.


Ukipata fursa pitia maeneo ya mipakani kaulizie maandalizi ya kupambana na ebola.

Kumbuka kesi moja ya ebola inamasnisha ni mlipuko (yaani epidemic) na upo muongozo jinsi ya kukabiliana nayo....

Ufuatiliaji wa jinsi ya kupambana na ebola huhusisha shirika la afya duniani pamoja na vyombo vya usalama duniani...it is not a joke!

Pia chukua muda na kurejesha kumbukumbu zako za mlipuko wa Ebola nchi za Afrika Magharibi na utagundua kuna madaktari kutoka Tanzania walienda Afrika Magharibi kwa ajili ya kupambana na mlipuko mbaya wa ebola duniani...walifanikiwa na walirejea salama.

Mwisho kabisa msalimie aliyekutuma na umuambie atumie muda wake vyema kujielimisha!!
 
Tanzania ianze kupeleka wataalamu mapema kupata mafunzo ya hii kitu tusisubiri hadi foreigners waje! Tutakuwa tumeisha.
 
Natafakari tu,
Kama PhD zimeokoa mtu mmoja, na wasio na elimu wameokoa 40,
Kuna haja ya PhD ?

Bado natafakari.
Nadhani waliookoa watu 40 ni wavuvi ambao walikuwepo karibu na eneo la tukio. Mpaka hao unaowaita wa PhD kufika hakuna wa kuokoa.

Umbali wa kivuko kuzama siyo ishu, ishu kubwa ni kina cha maji. Watu wanazama kwenye swimming pool sembuse ziwani.

Ishu nadhani ni kujua kwa nini chombo kilizidisha abiria, na vyombo vyetu vya uokoaji havitoshi. Hii ni sambamba na zimamoto na ambulance. Lazima tuwekeze kwenye hii sector.
 
Wajati wewe unatafakari namna hiyo wenzako wanafikiria ni namna gani wataiba kura 2020!
2020 wala hawafikirii chochote,wanakunywa mvinyo wakiwa wamerelax,2020 mtuwekee tena mamvi muone shughuli.
 
Back
Top Bottom