Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Hivi RC, Msimamizi wa bandari Mwanza, RPC, DC, Kiongozi wa Zimamoto leo walipata usingizi kweli? huku roho za Watanzania zikiteketea ziwani? I cant imagine uongozi wa dizaini hii, na utasikia hakuna atakayewajibika.

Kumetokea nini mnashangaa ya leo na mnashindwa kushangaa ya nyuma au ndio kusahau?
 
Samahani kwa kusema hivi ila ninadhani kwa namna fulani waokozi walikua sahihi kusitisha zoezi kwenye mazingira yafuatayo:-

Kama teknolojia na njia zetu za uokozi si fanisi kwa wakati wa usiku, hivyo kuendelea na uokozi inakua si salama kwanza kwa waokoaji wenyewe na pia mafanikio yake ni madogo mno, ni afadhali kusitisha zoezi hadi kutakapokucha.

Hakuna anayenufaika na vifo vya ndugu zetu, sitaki kuamini kwamba zoezi lilisitisishwa "JUST FOR LEISURE", kwa sasa bado hatuna uwezo mkubwa sana wa kufanya uokozi wakati wa usiku, na isingekua habari njema leo hii kusikia kwamba tumefanikiwa kuokoa wawili na tumepoteza waokozi nane.

Mwenyezi Mungu atupe nguvu na roho ya ustahimilivu watanzania katika kipindi hiki kigumu. Amen
 
.."George Nyamaha, the head of Ukerewe district council, of which the island is a part, said: “There were more than a hundred passengers on board when the ferry sank. It is feared that a significant number have lost their lives.”

However, it was hard to establish the precise number of passengers since the person dispensing tickets had also drowned with the machine recording the data lost.."

-Boat imebeba waay more than capacity..
-Hawajui idadi ya walioingia..
-Na sababu ni kuwa mkata ticket amezama pamoja na machine ya kukatia, kwa hiyo hakuna data kamili.
Mkuu pale wanatumia mashine za EFD, hvi hakuna semu hizi data huwa zinakuwa backed up?
 
Aisee.... "tusisubiri siku ya kuja kuomba rambirambi" asante sana mbunge, na leo tutamwona RC kwenye kamera akisisitiza michango ya rambirambi...

...ni mwendelezo wa serikali kupuuza ushauri wa wapinzani.

Lkn Mungu ni mwema sana anajua kujibu na kukumbusha kwa wakati.
 
hakuna kauli iliyonisikitisha sio mimi tu bali na wale waliokuwa wananizunguka kama ya uokoaji utaendelea kesho.
imagine, umejibanza sehemu unasukuma Muda ili uokolewe, kwa bahati nzuri ukawa na karedio hata la simu unafuatilia updates za kuokolewa kwako, unamsikia mtu anasema tutaendelea kesho. Hapo lzima nguvu zikuishe ujifie tu.

Kauli ile ilijaa Ukatili, bora wangekwepa kimyakimya.

😂😂😂😂 mambo kama hayo anayaweza Le Mutuz tu le Bahariaz aliyezoea maji,yani umezama halaf unaweka pozi na kusikiliza radio kabisa😂😂😂
 
Akili za viongozi wa awamu hii ni Mungu tu ndiye anayezijua, hivi utasitishaje kuokoa mtu anayetapatapa kujiokoa kwenye maji, mtu ambaye ukichelewa hata kwa dakika moja tu anazama, halafu useme subiri nitakuja kesho asubuhi, inaingia akilini kweli?

Ningekuwa mimi Magufuli wote waliohusika na kusitisha kazi ya kuokoa leo wasingeingia ofisini.

RIP waliotangulia mbele ya haki, ugua pole majeruhi.

View attachment 872858
Nafikiri tusimlaumu mkuu wa mkoa pasi kujua vizuri sababu.kwanza tatizo limeanzia kwa wafanyakazi wa kivuko yamkini kupakia watu wengi kuzidi kiwango cha kivuko,shughuli ya uokozi inawatazama wataalamu wa majanga hayo na mkuu wa mkoa utakuta yeye hana taaluma hiyo,inawezekana giza lilipoingia wataalamu walimuomba kusitisha zoezi labda hata kwa kuepusha vifo vingine ambavyo ni vya waokozi wenyewe kwa uhaba wa vifaa yamkini vya kumulikia eneo husika na chini ya maji.zaweza kuwepo sababu nyingi hata wao na mkuu ni watu hawawezi kusitisha tu zoezi bila sababu na mle ndani kuna watu.sasa tukianza kumlazimisha Rais na kuweka uchochezi hapa wa kutamani kuona mkuu wa mkoa kafukuzwa kazi sioni kama ni sawa sana.
 
hakuna kauli iliyonisikitisha sio mimi tu bali na wale waliokuwa wananizunguka kama ya uokoaji utaendelea kesho.
imagine, umejibanza sehemu unasukuma Muda ili uokolewe, kwa bahati nzuri ukawa na karedio hata la simu unafuatilia updates za kuokolewa kwako, unamsikia mtu anasema tutaendelea kesho. Hapo lzima nguvu zikuishe ujifie tu.

Kauli ile ilijaa Ukatili, bora wangekwepa kimyakimya.
Hiyo ndio serikali ya CCM hiyo Mkuu..
Ungekuta suala la uchaguzi hapo wangekesha mpaka wafanikiwe kuiba kura lakini suala la kuokoa uhai wa binadamu tena Watanzania wenzako sio priority.
 
Hivi unawezaje kulala Ndugu yako au mtoto au mzazi wako akiwa amefunikwa na meli

Je angekuwepo waziri mkuu humo amezama au makamu au kiongozi yeyote maarufu, wangesitisha uokoaji ?

Hii nchi CCM na mamluki wake ni Certified zéro brain
HAKIKA WEWE NI JINGA KUU LA TANZANIA WALAHI
 
Samahani kwa kusema hivi ila ninadhani kwa namna fulani waokozi walikua sahihi kusitisha zoezi kwenye mazingira yafuatayo:-

Kama teknolojia na njia zetu za uokozi si fanisi kwa wakati wa usiku, hivyo kuendelea na uokozi inakua si salama kwanza kwa waokoaji wenyewe na pia mafanikio yake ni madogo mno, ni afadhali kusitisha zoezi hadi kutakapokucha.

Hakuna anayenufaika na vifo vya ndugu zetu, sitaki kuamini kwamba zoezi lilisitisishwa "JUST FOR LEISURE", kwa sasa bado hatuna uwezo mkubwa sana wa kufanya uokozi wakati wa usiku, na isingekua habari njema leo hii kusikia kwamba tumefanikiwa kuokoa wawili na tumepoteza waokozi nane.

Mwenyezi Mungu atupe nguvu na roho ya ustahimilivu watanzania katika kipindi hiki kigumu. Amen
Hivi boti za doria za polisi na JWTZ hazina taa, mbona zina tochi kubwa kwa juu zenye uwezo wa kumlika zaidi ya mita 200.

Hizo boti zipo ni juzi tu tulitangaziwa kuwa serikali imenunua boti za doria za kisasa na kupelekwa ziwa Vitoria na zanzibar.
 
hakuna kauli iliyonisikitisha sio mimi tu bali na wale waliokuwa wananizunguka kama ya uokoaji utaendelea kesho.
imagine, umejibanza sehemu unasukuma Muda ili uokolewe, kwa bahati nzuri ukawa na karedio hata la simu unafuatilia updates za kuokolewa kwako, unamsikia mtu anasema tutaendelea kesho. Hapo lzima nguvu zikuishe ujifie tu.

Kauli ile ilijaa Ukatili, bora wangekwepa kimyakimya.
Imagine doesn’t count!
Grow up kido!
 
Back
Top Bottom