Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Poleni wote mlioguswa na hili janga kwa njia moja ama nyingine,


Tunanuomba mwenyezi Mungu awaokoe wote waliofikwa na haya maafa.
 
KIVUKO CHA MV. NYERERE CHAFUNGWA INJINI MPYA

Na Theresia Mwami - TEMESA
Kivuko cha MV. NYERERE kinachotoa huduma kati ya Bugorola na Ukara katika Wilaya ya Ukerewe Mkoani Mwanza, kinafungwa injini mpya tangu kununuliwa kwake na kuanza kutoa huduma mwaka 2004.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Bugorola, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA), Dkt. Mussa Mgwatu alisema kivuko cha MV. Nyerere kinafungwa injini mbili mpya zenye thamani ya shilingi milioni 191 ili kuongeza ufanisi wa kivuko katika kutoa huduma kwa wananchi wa Bugorola na Ukara. Dkt. Mgwatu amewaagiza mafundi wanaofunga injini hizo wafanye kazi usiku na mchana ili waweze kukamilisha ufungaji wa injini mapema iwezekanavyo ili kivuko kiendelee kutoa huduma ya usafrishaji wa abiria na mali zao.

Aidha, Dkt. Mgwatu amesema Serikali imedhamiria kuimarisha usafiri wa vivuko katika Ziwa Viktoria kwa kujenga vivuko vipya vitakavyotoa huduma katika maeneo mbalimbali yakiwemo ya Kigongo, Busisi, Kayenze, Bezi, Chato, Bwina, Bukondo, Senga, Muharamba, Kikumbaitale, Izumacheli na Nkome pamoja na kuvifanyia ukarabati vivuko vya MV. Nyerere, MV. Misungwi, MV. Sengerema na MV. Sabasaba.

Nae meneja wa vivuko TEMESA Mhandisi Hassan Karonda amebainisha kuwa mifumo ya injini ya kivuko cha MV. NYERERE imechoka sana kwa sasa kwa kuwa ni ya muda mrefu. Alisema, injini mbili mpya pamoja na giaboksi zinazofungwa katika kivuko cha MV. Nyerere ni za aina ya Perkins zenye nguvu ya kilowatt 161 kila moja na zinafungwa na mafundi wa TEMESA kwa kushirikiana na wale wa kampuni ya Delta Industrial Equipment Limited. Aliongeza kuwa kazi ya kufunga injini itaenda sambamba na kazi ya kukipaka rangi kivuko hicho na baada ya hapo kivuko kitaendelea kutoa huduma kama hapo awali lakini kwa kasi zaidi.

Kivuko cha MV. Nyerere kina uwezo wa kubeba tani 25 sawa na abiria 100 na magari 3 kwa wakati mmoja. TEMESA inasimamia uendeshaji wa vivuko 30 vya serikali vilivyoko kwenye jumla ya vituo 19 Tanzania bara.
 
Hichi kivuko nikipya, katika vivuko vya serikali, kimezama
 

Attachments

  • 1.JPG
    1.JPG
    8.5 KB · Views: 56
Loo! MV Bukoba ili binuka chali, badala ya kujua inaelea kwa sababu ya hewa ndani (elimu ya physics form 2), tukaitoboa ikazama!
 
...ivi samaki wanakula miili ya binadamuueeee.....nawaza vitoweoo SANGARA n SATO
 
Taarifa nilizozipata haraka sasa hivi ni kuwa watu wengi sana wanahisiwa kufa maji baada ya kivuko kubinuka juu chini, chini juu katika kisiwa cha UKALA wilayani Ukerewe.


====

Kivuko cha MV Nyerere kinachofanya safari zake kati ya Bugorara na kisiwa cha Ukala katika ziwa Victoria kimezama huku taarifa za idadi ya watu waliokuwemo ndani ya kivuko hazijajulikana.

Hivi ni Ukala au Ukara
 
Nimeiona video yake
Ndio kimezama watu wako juu ya maji
 
MBONA ANACHEKA KTK MAJANGA ILA NDIO KUSEMA KIFO HAKITISHI TENA WALE WANAHITAJI KUONEWA HURAMA MANA HATA AKILI ZAO HAZIPO HAPO TENA.....SO SAD
 
Back
Top Bottom