Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

Ukara, Ukerewe: Kivuko cha MV Nyerere chazama, miili 229 ya waliopoteza maisha imeshaopolewa!

uwa wanazuiwa aseee umesahau lile tukio la daladala iliyopitiliza na kuzama kule kigongo ferry??wanainchi wanaojua kuogelea walizuiwa kabisa na waliomba wajitokeze wakaokoe watu wakawa hao wenyewe temesa sijui nini na walizidiwa. na hapo si mbali kabisa kwa watu wa kanda ya ziwa wanaojua kuogelea wengi wao,pia ona iyo mitumbwi ya wavuvi sasa lazima wasitize zoezi usiku hakuna hata boti lenye taa ili kuendelea na zoezi,pia shida ingine kubwa ni MABOYA YA UOKOZI jamani yanafungiwa kwenye grill na zinga la komeo na hamna shoka lililo karibu useme wakati kinapinduka mmoja aliekua hajataharuki agonge komeo atoe maboya..sielewi kabisa

Yale maboya yanatakiwa yawe free ili emergency inapotokea yawe yanaelea tu majini na watu waweze kujiokolea
 
Mnakosa vifaa vya kuokolea ndugu zetu sababu ya matumizi mabaya ya fedha ,kurudia mauchaguzi yasiyo na tija na kupoteza fedha za walipa kodi.Kwanini msingetumia hizo fedha kununua vifaa vya kisasa vya uokozi au kivuko chenye ubora?
 
kwani wamekufa watu wangapi hadi sasa kwa mujibu wa vyanzo vya kuaminika? Nimesoma skynews wanasema zaidi ya 200 wanahofiwa kufa.
Ila nilichojifunza
1:Wapinzani wasipuuzwe na wanatakiwa kuwepo ili wasaidie kuonyesha hatari ambazo zisingesemwa vizuri na CCM. Mbunge alionya kuwa haya yatatokea.
2:Nilitegemea Tangu MV BK izame tungekuwa na Disaster management plan ya uhakika humo ziwani. Nashangaa kuona watu wanaokolewa na mitumbwi na sio Boti za uhakika za uokoaji.
3: Kwa jinsi ilivyozama nakubaliana na huyo mkuu kupona mtu pale ni asilimia ndogo, ila excuse ya uchovu sijawahi kuisikia popote duniani.

Tujitahidi kutoa taarifa zenye faraja kwa Umma. Kusema tutaendelea kesho hata dunia inayofuatilia tukio hili inatuona hatujali watu wetu.
Maoni
Hii nchi we ione hivi hivi
Zima moto na uokoaji hata boti sidhani kama wanazo, achilia mbali kwamba hata mafunzo yao hawafundishwi kuogelea.
Ajali kama hizi utaona jwtz ndo wanaenda kubeba maiti ilihali zimamoto na uokoaji wanakula bata, nyumba yako ikiungua moto ukipiga sim unaambiwa gari halina maji
Hii rangi nyeusi najisikia aibu sana hata kua mtanzania
 
Ungejuaa telnolojia inavyofanya kazi hata kwa 5% usingeandika haya.
mi nisijue teknolojia inavyofanya kazi hahahaa jamii forum imenikuta mimi mtandaoni we umekuja lini?
huyo katukana wakubwa kesho wanamkuta na ip aliyotuma upuuzi wake,km ni simu au internet watampata tu,nachoongea hapa tuwe na mipaka ya kuandika,viongozi ni viongozi mtakufa mkiendelea kubishana nao
 
Kwa utawala wa kiongozi makini, mkali na mgumu kama jiwe, polisi makini na wakali wanaopiga raia kama mbwa koko, ma RC na ma DC makini na wakali wa kukamata raia masaa 48, usingetegemea watoe statement inayosema "mpaka sasa haijulikani kulikuwa na watu wangapi kwenye kivuko.”

Umakini, uweledi na ukali wao ni kwenye kutisha, kufunga, kupiga na kukandamiza raia tu!
 
Hii nchi we ione hivi hivi
Zima moto na uokoaji hata boti sidhani kama wanazo, achilia mbali kwamba hata mafunzo yao hawafundishwi kuogelea.
Ajali kama hizi utaona jwtz ndo wanaenda kubeba maiti ilihali zimamoto na uokoaji wanakula bata, nyumba yako ikiungua moto ukipiga sim unaambiwa gari halina maji
Hii rangi nyeusi najisikia aibu sana hata kua mtanzania
inauma sana mkuu.
Watanzania tunapaswa kumtegemea Mungu zaidi, kuwaamini hawa wanasiasa ni kuweka maisha yako rehani.
sasa utakosaje idadi ya watu wakati sijawahi kuona popote watu wanaingia kivuko bila tiketi. Pia utakosaje kujua idadi wakati ilikuwa siku ya mnada bugorora abiria lazima walikuwa wengi na umakini wa kuwamanage ulipaswa kuwa mkubwa kuliko siku za kawaida.
 
mi nisijue teknolojia inavyofanya kazi hahahaa jamii forum imenikuta mimi mtandaoni we umekuja lini?
huyo katukana wakubwa kesho wanamkuta na ip aliyotuma upuuzi wake,km ni simu au internet watampata tu,nachoongea hapa tuwe na mipaka ya kuandika,viongozi ni viongozi mtakufa mkiendelea kubishana nao
Nimezidi kujiridhisha kuwa kumbe ni kweli upo zero kwenye teknolojia ,ila nimependa ushauri wako wa mwisho kweli tusibishane nao.
 
This is more common than it should be, and not just with ferries. Please help raise awareness for the safety standards of all forms of transportation in Tanzania. We can do better.
 
mi nisijue teknolojia inavyofanya kazi hahahaa jamii forum imenikuta mimi mtandaoni we umekuja lini?
huyo katukana wakubwa kesho wanamkuta na ip aliyotuma upuuzi wake,km ni simu au internet watampata tu,nachoongea hapa tuwe na mipaka ya kuandika,viongozi ni viongozi mtakufa mkiendelea kubishana nao
Kukamatwa kwa ip itakuwa ni uzembe maana zipo njia nyingi tu za kuhide ip au kutumia free open source vpn. kucover hiyo ip
 
Mkuu kuzima kwa Engine kunaashiria kivuko kilikua kibovu na ndio maana kikiwa kimezima kinapoteza balance kupinduka hiyo idadi ya watu ndio walikua wanabeba kila siku ila ubovu wa machine umefanya ipinduke kwa navyojua matengenezo ya vivuko au meli kubwa yawe kama kupigwa X ray na kucheki balance ya line sidhani kama tuna dry dock ya kufanya haya yote ndio maana nasema hicho kivuko kilikua kibovu...
Engine mbili zilizokuwa mbovu zishabadilishwa. Na hawana hata mwezi toka kivuko kimeanza fanya kazi. Ndo maana nakwambia shida sio kivuko. Nisingependa andika mtandaoni kilichoonwa na mashuhuda wa ajari, lakini shortly ni human actions. Uzuri captains wa3 wa kivuko wamepona, hivyo wataeleza baadae nini kilisababisha. Ila jua tu kivuko kilikuwa full fit.
 
Daah afu linatokea lijitu ambalo vivu la kufikia na kusema wanaoishi Dsm wanapoteza muda wakati maisha ya mikoani yana risk sn hasa inapotokea maafa makubwa
Kwani Dar maafa hayawezi kutokea.... Akili zako haziko vizuri
 
so sad,mwenyezi mungu awapumzishe kwa amani walopoteza maisha na majeruhi wapate unafuu mapema,kweli imeniuma sana, imenitoa majozi,poleni sana wafiwa wote,ndugu, jamaa na marafiki wote.
 
Vifaa vya uokozi lazima ziwe standby hujui ajari itatokea lini na wapi, boti za doria zinafanya kazi 24hrs, nyingi ziko Mwanza jijini, kwa speed za boti hizo kutoka Mwanza hadi kisiwa cha Ukara sidhani itatumia hata nusu saa, afterall ajari imetokea saa 8 kulikuwa na uwezekano mkubwa wa kufika pale mapema na kuanza maandalizi ya kukabiliana na giza kwa kuandaa taa.

Mbali na boti za polisi za doria kuna helikopta za polisi na jeshi zisingeshindwa kufika pale na kumulika wakati zoezi likiendelea. Ni uzembe fulani tu umefanyika.
Hii nchi ni shida sana, serikali ya ccm ilinunua magari mengi sana ya washawasha mwaka 2015 ili kuwalinda wanapoiba kura, ni aibu kama alivyosema mdau hapo juu kwamba hawana hata miwani zenye tochi, eti wanasitisha zoezi la uokoaji kwa sababu ya giza, mbona sherehe za mwenge huwa zinakesha !?. Polisi wanzo Speed boart ambazo muda mwingi huwa zinakaa tu, wakisikia maandamo ya Ukawa wanatamani hata kuzitumia hizo boti nchi kavu.
 
Kwa utawala wa kiongozi makini, mkali na mgumu kama jiwe, polisi makini na wakali wanaopiga raia kama mbwa koko, ma RC na ma DC makini na wakali wa kukamata raia masaa 48, usingetemea watoe statement inayosema "mpaka sasa haijulikani kulikuwa na watu wangapi kwenye meli."

Umakini, uweledi na ukali wao ni kwenye kutisha, kufunga, kupiga na kukandamiza raia tu!
Na hasa wapinzani [emoji85]

Sent from my HUAWEI LUA-L21 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom